chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 12,009
- 20,684
CHADEMA wamezindua operesheni yao Kigoma, na katika malengo ya operesheni, mojawapo ni Katiba, lakini inaonekana wameingia katika Kambi ya ACT Wazalendo iliyo chini ya Zitto Kabwe-Mkoa wa Kigoma.
Watu walikuwa wachache sana japo makumi ya mamilioni yametumika kuandaa mkutano huo. Wana Kigoma hawakuwa na mshituko wowote wala hamasa ya kumuona Lissu na Mbowe, ambao walikakamaa kwa masaa kadhaa kujieleza.
Wana mkakati wa CHADEMA waje na mbinu mpya, vinginevyo chama kinaelekea kufa katika jamii.
Waha walikuwa bize na shughuli zao za kuvua migebuka na kutafuta mafuta ya samli, na baadhi yao walisema hawatarajii Katiba iwaletee hela mfukoni au kuwainua kimaisha, waliomba serikali iongeze ruzuku ya kilimo na elimu badala ya kuzipoteza katika michakato isiyo na umuhimu kwa wananchi ila wanasiasa waroho wa madaraka.