kingukitano
JF-Expert Member
- Jul 18, 2011
- 1,971
- 497
Uchaguzi wa Ubunge wa Kalenga umekwisha na mshindi ameshapatikana. Ni Godfrey Mgimwa wa CCM. Waswahili walisema: yaliyopita si ndwele,tugange yajayo. Ndivyo inavyotakiwa kwa vyama vyote vilivyoshiriki ucaguzi wa Kalenga.Ni kwakuwa,wananchi wa Kalenga wamechagua waliyemchagua kwa matakwa yao na sababu zao. Kama alivyosema Mbunge Godbless Lema kwenye ukurasa wake wa facebook kuwa CHADEMA inayaheshimu maamuzi ya watu wa Kalenga. Lema alinena vyema sana na kidemokrasia.
Kufuatia ushindi wa Kalenga, wanachama na wapenzi wa CCM wamekuwa wakiibeza na kuikejeli sana CHADEMA. Wanafanya hivi katika upofu wa kidemokrasia.Hawajui ya kuwa uamuzi wa wananchi hautabiriki.Wananchi wanaweza kuamua chochote na muda wowote. Hizi mechi kali kati ya CCM na CHADEMA hazijaishia Kalenga.Mtanange bado unaendelea.
Wapo wanathubutu hata kusema kuwa sasa ni wakati wa uongozi wa CHADEMA kuachia ngazi. Eti kwakuwa CHADEMA imeshindwa Kalenga na katika kata 23 za Udiwani. Siamini kuwa Chaguzi Ndogo ni kipimo cha mwisho cha kufanikiwa au kushindwa kwa chama. Ni matayarisho tu ya mwaka 2015. Ingekuwa kwenye uchaguzi mkuu,hoja hii angalau ingekuwa na mshiko. Kwasasa,mambo bado haya jamani.
Kwanza, uongozi wa chama si kama kocha wa timu ya kandanda. Uongozi hutegemea watu na mawazo yao ya kujenga. Uongozi wa CHADEMA hadi hivi sasa unafanya kazi ya kutukuka na kupigiwa mfano. Umeweza kuwafanya CCM walale na mawazo kila uchao na katika kila uchaguzi wa sasa. Mapambano bado yanaendelea tena kwa kasi kubwa.
Kuna hoja ya kwamba kushindwa kwa CHADEMA Kalenga kumesababishwa na Zitto Z. Kabwe. Iko wazi kuwa Zitto hausiki na wala hakuna muda tena wa kumzungumzia ndani ya chama kwakuwa taratibu za kisheria na za kichama zinaendelea na hakuna haja ya 'majungu' katika hili. Zitto ni Zitto na CHADEMA ni CHADEMA.
CHADEMA itabezwa na kukejeliwa vya kutosha.Lakini,inazidi kuimarika na inasonga mbele. Subirini Jaji Damian Lubuva arekebishe Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, wananchi wajiandikishe na kujihakiki kwa wingi, wananchi wawe na uchungu na shahada zao za kupigia kura na kutokubali kurubuniwa. Hapo ndipo demokrasia ya nchi hii itakapoonja ladha mpya. Na siku husika wala haipo mbali sana.
Itoshe kusema kuwa,CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, inaimarika na kusonga mbele. Mapambano yanaendelea hadi kieleweke. Demokrasia haina sifa ya hichohicho kuwa pale pale.
Utetezi huu wa kipumbavu,hautawaokoa hivi unadhani ccm,haina watu ktk wapya mnotaka waandikishwe,,naporojo nyingi kwenu bila kujua uimara wa ccm