CHADEMA inaimarika na inasonga mbele

CHADEMA inaimarika na inasonga mbele

Mwaka 2015 siyo mbali sasa nyinyi watu badala ya kuchambua chanzo cha CHADEMA kufanya vibaya kwenye uchaguzi kisomi mnakimbilia kwenye weak and unsubstantiated arguments kama vile daftari la wapiga kura,nk.Hamtakisaidia chama namna hii.
 
Mwaka 2015 siyo mbali sasa nyinyi watu badala ya kuchambua chanzo cha CHADEMA kufanya vibaya kwenye uchaguzi kisomi mnakimbilia kwenye weak and unsubstantiated arguments kama vile daftari la wapiga kura,nk.Hamtakisaidia chama namna hii.

Daftari la Wapigakura ni suala la kimbumbumbu Mkuu TEKNOLOJIA? Uchambuzi huu pia ni wa kisomi kwakuwa hata mimi ni Msomi
 
Last edited by a moderator:
sasa mboni kabla ya uchaguzi mlijiaminisha mtashinda?....mwanakijiji aliwashauri kama mnaamini sheria mbovu, police na tume watawabeba ccm msishiriki!! mboni mlishiriki uchaguzi?

baadaye kidogo sana utakuja kujua manufaa ya cdm kushiriki uchaguzi huo , STAY TUNED , MWL NYERERE ALIWAHI KUNUKULIWA AKIDOKEZA kwamBA , CHAMA CHA SIASA NI MABARABARANI NA MAJUKWAANI ! Ulielewa alichokimaanisha ?
 
Ukweli ni kwamba Watanzania wengi bado wana imani na serikali ya ccm pamoja na siasa yake ya ujamaa na kujitegemea, ushahidi ni huu kuwa wanawapa zaidi ya 75%!!
Nimekuta Zitto kandika sehemu na ndio nikajua kuwa bado tuna safari ndefu pamoja na cdm kutumia mbinu, nguvu, gharama na muda mwingi kuwafumbua watu macho lakini wapi, hayafumbuki!
Cha kusikitisha hata huyu mwenye kuiponda cdm anaongea kama kwamba yeye sio Mtanzania au ni aina ya wale ambao wameshapata walichokuwa wanakitafuta. Sio busara kufuata mkumbo.
 
Uchaguzi wa Ubunge wa Kalenga umekwisha na mshindi ameshapatikana. Ni Godfrey Mgimwa wa CCM. Waswahili walisema: yaliyopita si ndwele,tugange yajayo. Ndivyo inavyotakiwa kwa vyama vyote vilivyoshiriki ucaguzi wa Kalenga.Ni kwakuwa,wananchi wa Kalenga wamechagua waliyemchagua kwa matakwa yao na sababu zao. Kama alivyosema Mbunge Godbless Lema kwenye ukurasa wake wa facebook kuwa CHADEMA inayaheshimu maamuzi ya watu wa Kalenga. Lema alinena vyema sana na kidemokrasia.

Kufuatia ushindi wa Kalenga, wanachama na wapenzi wa CCM wamekuwa wakiibeza na kuikejeli sana CHADEMA. Wanafanya hivi katika upofu wa kidemokrasia.Hawajui ya kuwa uamuzi wa wananchi hautabiriki.Wananchi wanaweza kuamua chochote na muda wowote. Hizi mechi kali kati ya CCM na CHADEMA hazijaishia Kalenga.Mtanange bado unaendelea.

Wapo wanathubutu hata kusema kuwa sasa ni wakati wa uongozi wa CHADEMA kuachia ngazi. Eti kwakuwa CHADEMA imeshindwa Kalenga na katika kata 23 za Udiwani. Siamini kuwa Chaguzi Ndogo ni kipimo cha mwisho cha kufanikiwa au kushindwa kwa chama. Ni matayarisho tu ya mwaka 2015. Ingekuwa kwenye uchaguzi mkuu,hoja hii angalau ingekuwa na mshiko. Kwasasa,mambo bado haya jamani.

Kwanza, uongozi wa chama si kama kocha wa timu ya kandanda. Uongozi hutegemea watu na mawazo yao ya kujenga. Uongozi wa CHADEMA hadi hivi sasa unafanya kazi ya kutukuka na kupigiwa mfano. Umeweza kuwafanya CCM walale na mawazo kila uchao na katika kila uchaguzi wa sasa. Mapambano bado yanaendelea tena kwa kasi kubwa.

Kuna hoja ya kwamba kushindwa kwa CHADEMA Kalenga kumesababishwa na Zitto Z. Kabwe. Iko wazi kuwa Zitto hausiki na wala hakuna muda tena wa kumzungumzia ndani ya chama kwakuwa taratibu za kisheria na za kichama zinaendelea na hakuna haja ya 'majungu' katika hili. Zitto ni Zitto na CHADEMA ni CHADEMA.

CHADEMA itabezwa na kukejeliwa vya kutosha.Lakini,inazidi kuimarika na inasonga mbele. Subirini Jaji Damian Lubuva arekebishe Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, wananchi wajiandikishe na kujihakiki kwa wingi, wananchi wawe na uchungu na shahada zao za kupigia kura na kutokubali kurubuniwa. Hapo ndipo demokrasia ya nchi hii itakapoonja ladha mpya. Na siku husika wala haipo mbali sana.

Itoshe kusema kuwa,CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, inaimarika na kusonga mbele. Mapambano yanaendelea hadi kieleweke. Demokrasia haina sifa ya hichohicho kuwa pale pale.

Bandiko lako linajikanganya na kujipinga "big time". Hakuna ushahidi wowote kuwa daftari likiboreshwa CDM itashinda kila uchaguzi. Mbona Arumeru CDM ilishinda kwa daftari hili hili?

CDM kwa sasa imegubikwa na matatizo mengi ambayo wanazi wa chama wanayafumbia macho kwa kuamini Mbowe & Co. watayatatua (wakati huenda hii "status quo" inawafaidisha wao wenyewe!). Busara ikitumika CDM isiende Chalinze kwa sababu zilizo wazi kabisa.
 
Kwani dalili ya chama kustawi ni nini.ustawi wa chama chochote ni kuungwa mkono na jamii inayoifanyia kazi,na kipimo rahisi ni kupigiwa kua nyigi sasa nyie kila kukicha mnazidi kutoungwa mkono halafu unajipa moyo.upende au ufiche uso zitto ni muhimu kwa chadema.heri uwatoe slaa na mbowe chama kitaendelea lakini zitto itachukua muda kustabilize.

Zitto unaemsema hapa yupi? Zitto huyu wa siku zote au kuna Zitto mwingine kazaliwa? kama ni Zitto wa siku zote tunaemjua wote basi kamshauri aludishe hela zote alizopewa na TISS ndiyo umlete apewe uenyekiti wa CHADEMA.
 
Daftari la Wapigakura ni suala la kimbumbumbu Mkuu TEKNOLOJIA? Uchambuzi huu pia ni wa kisomi kwakuwa hata mimi ni Msomi

Nimesema ni weak and unsubstantiated arguments yaani namaamisha ni hoja dhaifu na isiyo na ushaidi kwasababu sote hatuna uhakika kama hao wapiga kura walioachwa nje ya daftari la wapigara wanaunda idadi ya kutosha kusaidia chama kushinda au hata kama wakiandikishwa je watapiga kura?na wakipiga kura je wote wataipigia kura CHADEMA?Na ndiyo maana nikasema hiyo ni hoja dhaifu,Hapa suala ni kwa CHADEMA kubadili mbinu na mikakati tu basi!Nadhani waraka wa Dr Kitila umeweka kila kitu bayana,Ni juu ya CHADEMW kuyafanyia kazi mawazo yale.
 
Last edited by a moderator:
Kinachonipa nguvu zaidi ni pale ninapojiuliza "Hivi magamba watahitaji kuwa na pesa kiasi gani ambacho kitatosha kununua shahada za wapiga kura wapya zaidi ya mil.20 mara baada ya maboresho mapya ya daftari la wapiga kura sambamba watu kupewa vitambulisho vipya vingine? Maana hata mimi ninampango wa kuwa na vitambulisho vya kura zaidi ya kimoja ili wakinijia MAGAMBA niwauzie feki alafu nabaki na kile original natimba nacho kwenye kupiga kura kama kawaida! Mbona wataisoma huko mbeleni na watakoma awamu hii ya maboresho ya daftari hili! Na mimi naiomba tume icheleweshe hivyohivyo kwani vijana lazima tupige hela kwelikweli kupitia vitambulisho hivi vipya na kura tunapiga kiulainiiiii.Hiyo ndo plan ya vijana kuelekea 2015 na lazima kieleweke.
 
Jidanganyeni tu na kujipa moyo hivyohivyo kweli mbadala wa ccm haujazaliwa nchi. Hii

we ndo unaedanganyika au baba yako ni mmoja wa mafisadi na majangili? Una maslahi gani na chama chakavu
 
Kinachonipa nguvu zaidi ni pale ninapojiuliza "Hivi magamba watahitaji kuwa na pesa kiasi gani ambacho kitatosha kununua shahada za wapiga kura wapya zaidi ya mil.20 mara baada ya maboresho mapya ya daftari la wapiga kura sambamba watu kupewa vitambulisho vipya vingine? Maana hata mimi ninampango wa kuwa na vitambulisho vya kura zaidi ya kimoja ili wakinijia MAGAMBA niwauzie feki alafu nabaki na kile original natimba nacho kwenye kupiga kura kama kawaida! Mbona wataisoma huko mbeleni na watakoma awamu hii ya maboresho ya daftari hili! Na mimi naiomba tume icheleweshe hivyohivyo kwani vijana lazima tupige hela kwelikweli kupitia vitambulisho hivi vipya na kura tunapiga kiulainiiiii.Hiyo ndo plan ya vijana kuelekea 2015 na lazima kieleweke.

Nimelipenda sana swali lako. Ndio maana waswahili husema mbio za sakafuni huishia ukingoni. Muda si mrefu ccm watakwama na hata wenyewe wanalijua hilo
 
Nimesema ni weak and unsubstantiated arguments yaani namaamisha ni hoja dhaifu na isiyo na ushaidi kwasababu sote hatuna uhakika kama hao wapiga kura walioachwa nje ya daftari la wapigara wanaunda idadi ya kutosha kusaidia chama kushinda au hata kama wakiandikishwa je watapiga kura?na wakipiga kura je wote wataipigia kura CHADEMA?Na ndiyo maana nikasema hiyo ni hoja dhaifu,Hapa suala ni kwa CHADEMA kubadili mbinu na mikakati tu basi!Nadhani waraka wa Dr Kitila umeweka kila kitu bayana,Ni juu ya CHADEMW kuyafanyia kazi mawazo yale.
1.Watu wamepoteza/kuibiwa vitambulisho vyao vya kupigia kura
2.Watu walishauza vitambulisho vyao na hawajarudishiwa tena
3.Watu wanabadilishana na pesa kwa makubaliano walejeshewe baada ya kumalizika zoezi la kupiga kura
4.Watu hawana vitambulisho na hawamo kwenye daftari hii ni ukweli kwamba kipindi daftari linaboreshwa hakuwa na sifa
5.Kinachonipa moyo ni kuona wapigaji kura wanaoipa ushindi ccm kwa sasa ni wazee! Wakati takwimu zilizokabidhiwa juzi kwa raisi zinasema kindi kubwa la watu kwa sasa ni vijana
 
MAJIBU SAHIHI
--------------------
Jibu ni kuboreshwa kwa Daftali la wapiga kura tuu.

Karenga ni mabibi ndio yamepiga kura kalenga sasa unafikili maCCM yangefeli kweli....

Makamanda piganieni maboresho ya daftali sasa chaguzi hizi, kwa mjini kama chalinze tutashinda tu ata kwa daftali hili.

Hongera chadema kwakushinda (ingawa hakutangazwa), kama TISS wote walikuwa pale, police nao, kauli ya mkuu wa kaaya lazima kushinda, vitisho vywa green guard na CCM mkoa, na nguvu kubwa ya kutisha vijana na watu makini kutopiga kura.... Nasema tena hongereni sanaa, SASA TUELEKE CHALINZE HAKUNA KUKATA TAMAAAAAAA...

Mungu bariki Tanzania
Mungu bariki Tendega for 2015


Dr Slaaa anadai 2010 alishinda uchaguzi wa raisi, je dafatari lililotumika ni lipi?
 
CHADEMA inatakiwa ijiangalie upya,mimi ni mwana CHADEMA sitarudi nyuma nina imani na chama changu,hapa wanatakiwa wafanye utaratatibu wa ku recruit vijana ambao wana moyo wa dhati kukitumikia chama wawe katika makundi manne wa!wezeshwe na chama wazunguke kila jimbo na kila wilaya,ikiwezekana kila kata na kijiji ili kutoa elimu ya uraia na kuwahamsisha wapenda mabadiliko huko kote kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura na wajue umhimu wa kufanya mabadiliko

.kuna vijana safi kama Alphonce Mawazo,kuna mtu kama Nicholous Ngowi hawa ni mfano tu wa vijana wanaoweza kupewa jukum hilo ili viongozi wao waganye kazo ya uratibu wamipango hiyo chama kina nguvu kazi ya kutosha ila haitumiwi.
Chama kinatumia gharama nyingi kipindi cha chaguzi ndogo kwa kukodi helcopter lakini tukijiandaa mapema kwa kupitisha hawa vijana mi nawaita swepers kitaturahosishia kazi askari wa miguu siku zote ndio huleta ushindi.
Asante
 
Kura 5,800 siyo haba hasa ukichukulia kuwa wapiga kura wengi ni wazee, vitisho toka Polisi, Green na TISS na kutojitambua kwa walalahoi aka wapiga kura wa eneo husika imesababisha CCM kushinda maeneo mengi yenye ufukara kama Kalenga na kwngineko kote ambapo watu bado wamelala
 
Nakumbuka kuna mwanafalsafa mmoja alikuwa anatembea na karabai inayowaka gulioni,alipoulizwa mbona umewasha taa mchana?alijibu ni mchana lakini watu hawaoni!haya ndiyo ya watz
 
Bado naamini CDM ina nguvu kuliko CCM.

CCM nguvu yake iko katika dola na umwagaji damu, na ujinga wa wenyeji mahali.

Walichofanya wenyeji wa Kalenga hakiwezi kufanyika kaskazini kwani huku tunajitambua ndio maana kuna maendeleo ukilinganisha na kusini.
 
Back
Top Bottom