Samia alituasa tukosoane kwa STAHA kwa mambo yaliyo dhahiri.Hiyo ndio demokrasia. Sasa hamtaki kukosolewa
Samia alituasa tukosoane kwa STAHA kwa mambo yaliyo dhahiri.Hiyo ndio demokrasia. Sasa hamtaki kukosolewa
Hata kama Covid 19 wakibebwa hadi 2025 Chadema haina cha kupoteza mbele ya jamii, imeonyesha inasimamia inachokiamini iko consistent, serikali ndio itakayojidhalilika kupitia vyombo vyake vya Bunge, NEC, ofisi ya Msajili na mahakama.Kuwatetea uviko19 kuwa ni wabunge halali wa CHADEMA kunahitaji kuwa na roho ngumu sana na kujitoa ufahamu kwa namna ya kipekee kabisa
Lissu amefafanua vizuri sana kwa kutoa mifano halisi michache
Yeye mwenyewe
Lema
Wabunge wa CUF
Kitendo cha CHADEMA kuweka wazi kwamba hakitapeleka wabunge wengine ni pigo kubwa kwa ccm kimapato, kimisaada na taswira ya bunge huko duniani... Kwahiyo ni lazima kwa hali yoyote ile uviko19 wabebwe hivyo hivyo mpaka 2025
Uliyemtaja Analia Na Kusaga Meno, Anatamani Muda Urudi Nyuma Afanye Masahihisho Lakini Haiwezekani Tena. Ananywea Kiiombe Kilicho Furika Na KusukwasukwaYuko wapi Musiba yule aliyekuwa na nguvu sana?
Kama anakisema vibaya CHADEMA, basi ninyi kisemeni kwa mazuri Watanzania tutaelewa tu.Ni mwandishi nguli na mwana JF maarufu CV yake haina mashaka popote na ana heshima yangu kubwa tu. Ni mmojawapo wa watu aliyenihamasisha kujiunga na JF hasa kule jukwaa la intelligence
Simhukumu vibaya lakini nadhani ana tatizo binafsi na CHADEMA kama ilivyokuwa kwa Prince Bagenda na Augustine Lyatonga Mrema mzee wa Kirachacha
Kuna mengi ya kusimuliwa kati ya wawili hawa.. Ya sirini na ya upenuni, Lakini yanayojulikana zaidi ni pale siasa za Mageuzi zilipoingia nchini mwaka 1992 na baadae Waziri wa mambo ya ndani kwa wakati huo Lyatonga Mrema alipojivua nyazifa zake zote na kukiacha chama chake na kujiunga na NCCR-Mageuzi kilichokuwa chama kikuu cha upinzani wakati huo
Kujitoa kwa Mrema ccm kulikuwa na mtikisiko mkubwa sana kwakuwa kwa wakati huo ndio waziri pekee aliyekuwa na uthubutu uliorejesha nidhamu serikalini na kuwa tishio kwa wazembe., wala rushwa majambazi na wapiga dili wengine
Mwaka 1995 wakati wa uchaguzi mkuu akasimama kugombea nafasi ya urais kupitia NCCR- Mageuzi chini ya timu ya Mabere Nyaucho Marando wakili msomi James Mbatia
Dr. Masumbuko Lamwai wakili msomi RIEP
Prince Bangeda mwandishi nguli na wengine wengi
Moto ule wa NCCR hiyo uliwatisha mno ccm na wakaona kitisho cha wazi kama wataiacha NCCR istawi, hivyo baada ya uchaguzi ule NCCR ilifitinishwa na kumeguka mapande mawili kila kundi likilishutumu lingine kwa usaliti
Baada ya hapo yalitokea mengi sana, lakini la kukumbukwa zaidi ni namna Prince Bangeda alivyotumika kumshambulia Mrema kupitia magazeti ya Rai na Mtanzani kwenye safu ya :Kalamu ya Bangeda' nadhani.. Yaani ilikuwa kama project maalum ya kumchafua mzee wa Kirachacha.. Prince Bagenda aliandika na kuandika na kuandika, aliandika mabaya tupu. Hakuna siku aliandika jema la Mrema na kwa baadhi ya mada akitoa ushauri wa kinafiki kabisa
Inawezekana pengine kuna siku Jenerali Ulimwengu atakuja kutuambia ule mradi ulikuwa wa nani na ulikuwa na lengo gani, lakini juu ya yote mwisho wa project hiyo ya Bangeda aliasisi gazeti lake na akiwa kwenye mchakato wa kuanzisha TV yake. Ofisi yake iliyokuwepo pale jengo la ushirika Lumumba iliwaka moto na kila kitu kikaishia pale.. Prince Bagenda hakuwahi kusimama tena na huku mzee wa Kirachacha ambaye hata mara moja hakuthubutu kumjibu Bagenda akidunda mpaka Leo hii na kigoli kaoa hivi karibuni
Nimeamua kutoa mfano huo baada ya kuona mwenendo wa mwandishi huyo kwa CHADEMA.. Hakauki kwa mada za kukisema vibaya hiki chama kinachotambulika kama kikuu cha upinzani Tanzania.. Ni mada za kukikosoa, kukisema vibaya kukiombea kifo tangu 2015 utadhani ndio chama pekee cha siasa Tanzania
Hakuna mtu aliwahi kupambana na sauti ya wengi akashinda.. Hakuna mtu aliyewahi kupambana na asiyejibu akashinda.. Kadiri unavyozidisha chuki na kukisema vibaya ndio kadiri unavyojimaliza.. Ukiweza BADILIKA SASA..La sivyo mwisho wako hauko mbali... Hakuna hata mmoja aliyewahi kutumika kisha akawa na mwisho mwema
Una jicho la tatu... Lifungue vema likuoneshe ya mbeleni
Mungu ibariki CHADEMA...!!!
Mahakama ilikubali maombi yangu siku ile Ile na nikapewa miezi 6 ya hukumu kutekelezwa. Miezi SITA haikufika..[emoji31][emoji848][emoji2827]Asante kwa kumuonya. However, I guess it is too late now. Mie nimeshawasilisha kesi rasmi mahakama ya mwisho. Nimeweka maandiko yake 2 ya kuishtumu CDM ambayo nimeomba mahakama iyapitie na kuona Kama ni ya haki ama la.Nimeomba mahakama baada ya kupitia nyaraka hizo itoe hukumu dhidi ya upande usio na haki kwa kadri inavyoona inafaa.
NB. Wakati wa magufuli pamoja magufuli kuwa na kesi nyingi sana nilichagua kuwasilisha mbele ya mahakama kesi moja tu ya Akwilina. Mahakama ilikubali maombi yangu siku ile Ile na nikapewa miezi 6 ya hukumu kutekelezwa. Miezi SITA haikufika.
Upotoshaji au usahihi wa jambo ni tafsiri ya kimapokeo au matokeo ya kimapokeo.....pamoja na yote kama usahihi unafahamika na wengi na yeye anapaswa kufahamishwa kama atasimamia kile anachokiamini anapaswa kuachwa na utashi wake na sio kutukanana na kudhalilishwa....... Demokrasia sio tu kuitamka bali na kuiishi....na kuiishi ni pamoja na kuvumilianaMkuu nadhani ujamwelewa vizuri mtoa mada, ebu fikiria unatambua kabisa Mji wa Abuja lipo Nigeria ila unawaambia watu kua lipo Namibia. He hiyo ndiyo demokrasia au upotoshaji? Tena baada ya masaa mchache unawambia watu mji wa Lagos lipo Mali na si Nigeria. Je unajua na tatizo binafsi na nchi Nigeria au ndiyo demokrasia yenyewe?
Umeambiwa abalance story aandike uhalisia kama CHADEMA wamekosea aseme na kama Tulia amekosea aseme.Sasa ikiwa wew ni Chadema kindakindaki unashangaa nini huyo mwandishi kuiponda chadema maana yake na yeye ana Imani yake
Mimi nadani tusidhani demokrasia ni kutendeka unachokitaka wew na ikiwa kinyume unaona nongwa
Jamaa yuko biased vibaya mno, ni kweli Chadema ina mapungufu yake hata mimi nimekuwa nikiikosoa hapa JF, lakini ukosoaji wa jamaa kwenye hili suala la wabunge 19 umekaa kama ana kisasi ama hasira flani hivi,
umekosa objectivity ambayo ungeweza kuitegemea kutoka kwa mtu kama yeye
Lakini ndio hivyo ni uhuru wa maon
Ukiangalia kwa makini sana mwandishi huyo unayemtuhumu ana kishambulia Chadema, Tena ukitumia jicho la Tatu(najua una macho zaidi ya Matatu), utagundua mwandishi huyu ana nia njema na Chadema wakati huo huo anaitakia mema Tanzania.Nimeamua kutoa mfano huo baada ya kuona mwenendo wa mwandishi huyo kwa CHADEMA.. Hakauki kwa mada za kukisema vibaya hiki chama kinachotambulika kama kikuu cha upinzani Tanzania.. Ni mada za kukikosoa, kukisema vibaya kukiombea kifo tangu 2015 utadhani ndio chama pekee cha siasa Tanzania
Dah, kamanda nenda katubu na ufunge kabisa kwa wiki nzima kupata radhi ya M/Mungu.Kwa vile Chadema ni Chama cha Mungu , shetani hujidhihirisha mwenyewe