CHADEMA imemkosea nini huyu mwandishi?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,782
Ni mwandishi nguli na mwana JF maarufu CV yake haina mashaka popote na ana heshima yangu kubwa tu. Ni mmojawapo wa watu aliyenihamasisha kujiunga na JF hasa kule jukwaa la intelligence

Simhukumu vibaya lakini nadhani ana tatizo binafsi na CHADEMA kama ilivyokuwa kwa Prince Bagenda na Augustine Lyatonga Mrema mzee wa Kiraracha

Kuna mengi ya kusimuliwa kati ya wawili hawa.. Ya sirini na ya upenuni, Lakini yanayojulikana zaidi ni pale siasa za Mageuzi zilipoingia nchini mwaka 1992 na baadae Waziri wa mambo ya ndani kwa wakati huo Lyatonga Mrema alipojivua nyazifa zake zote na kukiacha chama chake na kujiunga na NCCR-Mageuzi kilichokuwa chama kikuu cha upinzani wakati huo

Kujitoa kwa Mrema ccm kulikuwa na mtikisiko mkubwa sana kwakuwa kwa wakati huo ndio waziri pekee aliyekuwa na uthubutu uliorejesha nidhamu serikalini na kuwa tishio kwa wazembe., wala rushwa majambazi na wapiga dili wengine

Mwaka 1995 wakati wa uchaguzi mkuu akasimama kugombea nafasi ya urais kupitia NCCR- Mageuzi chini ya timu ya Mabere Nyaucho Marando wakili msomi James Mbatia
Dr. Masumbuko Lamwai wakili msomi RIEP
Prince Bangeda mwandishi nguli na wengine wengi

Moto ule wa NCCR hiyo uliwatisha mno ccm na wakaona kitisho cha wazi kama wataiacha NCCR istawi, hivyo baada ya uchaguzi ule NCCR ilifitinishwa na kumeguka mapande mawili kila kundi likilishutumu lingine kwa usaliti

Baada ya hapo yalitokea mengi sana, lakini la kukumbukwa zaidi ni namna Prince Bangeda alivyotumika kumshambulia Mrema kupitia magazeti ya Rai na Mtanzani kwenye safu ya :Kalamu ya Bangeda' nadhani.. Yaani ilikuwa kama project maalum ya kumchafua mzee wa Kirachacha.. Prince Bagenda aliandika na kuandika na kuandika, aliandika mabaya tupu. Hakuna siku aliandika jema la Mrema na kwa baadhi ya mada akitoa ushauri wa kinafiki kabisa

Inawezekana pengine kuna siku Jenerali Ulimwengu atakuja kutuambia ule mradi ulikuwa wa nani na ulikuwa na lengo gani, lakini juu ya yote mwisho wa project hiyo ya Bangeda aliasisi gazeti lake na akiwa kwenye mchakato wa kuanzisha TV yake. Ofisi yake iliyokuwepo pale jengo la ushirika Lumumba iliwaka moto na kila kitu kikaishia pale.. Prince Bagenda hakuwahi kusimama tena na huku mzee wa Kirachacha ambaye hata mara moja hakuthubutu kumjibu Bagenda akidunda mpaka Leo hii na kigoli kaoa hivi karibuni

Nimeamua kutoa mfano huo baada ya kuona mwenendo wa mwandishi huyo kwa CHADEMA.. Hakauki kwa mada za kukisema vibaya hiki chama kinachotambulika kama kikuu cha upinzani Tanzania.. Ni mada za kukikosoa, kukisema vibaya kukiombea kifo tangu 2015 utadhani ndio chama pekee cha siasa Tanzania

Hakuna mtu aliwahi kupambana na sauti ya wengi akashinda.. Hakuna mtu aliyewahi kupambana na asiyejibu akashinda.. Kadiri unavyozidisha chuki na kukisema vibaya ndio kadiri unavyojimaliza.. Ukiweza BADILIKA SASA..La sivyo mwisho wako hauko mbali... Hakuna hata mmoja aliyewahi kutumika kisha akawa na mwisho mwema

Una jicho la tatu... Lifungue vema likuoneshe ya mbeleni

Mungu ibariki CHADEMA...!!!
 
Mkuu Mshana Jr jina sahihi ni Prince Bagenda na si Prince Bangeda kama ulivyoandika.

Kuhusu mada yako, kaka yangu na mtani wangu ameshahama kwenye mada chokonozi tangu alipojiunga na CCM na kutia nia na kuwemo kwenye mchakato wa ndani wa kugombea ubunge Kawe.

Mada zake siku hizi hazishangazi kwakuwa zina mwelekeo unaofahamika. Anatumikia chama chake. Maybe he is in a planned political agenda and strategy!
 
Mkuu Mshana Jr jina sahihi ni Prince Bagenda na si Prince Bangeda kama ulivyoandika.

Kuhusu mada yako, kaka yangu na mtani wangu ameshahama kwenye mada chokonozi tangu alipojiunga na CCM na kugombea ubunge Kawe.

Mada zake siku hizi hazishangazi kwakuwa zina mwelekeo unaofahamika. Anatumikia chama chake. Maybe he is in a planned political agenda and strategy!
Asante kwa masahihisho mkuu
 
Jamaa yuko biased vibaya mno, ni kweli Chadema ina mapungufu yake hata mimi nimekuwa nikiikosoa hapa JF, lakini ukosoaji wa jamaa kwenye hili suala la wabunge 19 umekaa kama ana kisasi ama hasira flani hivi,

umekosa objectivity ambayo ungeweza kuitegemea kutoka kwa mtu kama yeye
Lakini ndio hivyo ni uhuru wa maoni,
 
Kama hujaelewa kitu unakaa kimya ama unauliza kwa waliokuzidi ufahamu
Ujumbe upo kamili mwenyekiti keshasema mzee. Huu ujumbe alioutoa ulikuwa mpana na ndio maana hata msigwa ameuweka kwenye akaunti yake kule insta. Najua unaelewa mshana jr.
tempFileForShare_20220517-221401.jpg
 
Sasa ikiwa wew ni Chadema kindakindaki unashangaa nini huyo mwandishi kuiponda chadema maana yake na yeye ana Imani yake
Mimi nadani tusidhani demokrasia ni kutendeka unachokitaka wew na ikiwa kinyume unaona nongwa
Jaribu kusoma swali na kulielewa ..jaribu kusoma mfano wa utangulizi nilioweka.. Tuna tofautiana itakadi ni kweli lakini hatuwezi kuzusha hata yasiyo ya kweli kwa kisingizio cha uhuru wa demokrasia.. Huo utakuwa ni upuuzi ujue
Tunakosoa penye shida
Tunasifu panapostahili hizo ndio siasa za ushindani
 
Mshana,kwanza nakupongeza kwa andiko, pili Mimi ulinivutia kujiunga jf, mm na mke wangu, ila moja ya kosa nalo lifanya ni kutokukutanisha na mke wangu popote pale mpaka nife,maana yee uwa akisoma maandishi Yako uwa anavutiwa mpaka namwona Sito fanya kosa la kumwachia nafasi hyo,

Cjawai vutiwa na Mwandishi uliyemsema kwanza, wakat Mimi nasomea uandishi yeye alikuwa mtumishi wa kipaji a sio elimu.

Ila kama general ulimwengu alifanya project hii Mungu akbariki
 
Ni mwandishi nguli na mwana JF maarufu CV yake haina mashaka popote na ana heshima yangu kubwa tu .. Ni mmojawapo wa watu aliyenihamasisha kujiunga na JF hasa kule jukwaa la intelligence

Simhukumu vibaya lakini nadhani ana tatizo binafsi na CHADEMA kama ilivyokuwa kwa Prince Bagenda (RIEP) na Augustine Lyatonga Mrema mzee wa Kirachacha

Kuna mengi ya kusimuliwa kati ya wawili hawa.. Ya sirini na ya upenuni, Lakini yanayojulikana zaidi ni pale siasa za Mageuzi zilipoingia nchini mwaka 1992 na baadae Waziri wa mambo ya ndani kwa wakati huo Lyatonga Mrema alipojivua nyazifa zake zote na kukiacha chama chake na kujiunga na NCCR-Mageuzi kilichokuwa chama kikuu cha upinzani wakati huo
Kujitoa kwa Mrema ccm kulikuwa na mtikisiko mkubwa sana kwakuwa kwa wakati huo ndio waziri pekee aliyekuwa na uthubutu uliorejesha nidhamu serikalini na kuwa tishio kwa wazembe., wala rushwa majambazi na wapiga dili wengine

Mwaka 1995 wakati wa uchaguzi mkuu akasimama kugombea nafasi ya urais kupitia NCCR- Mageuzi chini ya timu ya
Mabere Nyaucho Marando wakili msomi
James Mbatia
Dr. Masumbuko Lamwai wakili msomi RIEP
Prince Bangeda mwandishi nguli na wengine wengi

Moto ule wa NCCR hiyo uliwatisha mno ccm na wakaona kitisho cha wazi kama wataiacha NCCR istawi, hivyo baada ya uchaguzi ule NCCR ilifitinishwa na kumeguka mapande mawili kila kundi likilishutumu lingine kwa usaliti

Baada ya hapo yalitokea mengi sana, lakini la kukumbukwa zaidi ni namna Prince Bangeda alivyotumika kumshambulia Mrema kupitia magazeti ya Rai na Mtanzani kwenye safu ya :Kalamu ya Bangeda' nadhani.. Yaani ilikuwa kama project maalum ya kumchafua mzee wa Kirachacha.. Prince Bagenda aliandika na kuandika na kuandika, aliandika mabaya tupu. Hakuna siku aliandika jema la Mrema na kwa baadhi ya mada akitoa ushauri wa kinafiki kabisa
Inawezekana pengine kuna siku Jenerali Ulimwengu atakuja kutuambia ule mradi ulikuwa wa nani na ulikuwa na lengo gani, lakini juu ya yote mwisho wa project hiyo ya Bangeda aliasisi gazeti lake na akiwa kwenye mchakato wa kuanzisha TV yake. Ofisi yake iliyokuwepo pale jengo la ushirika Lumumba iliwaka moto na kila kitu kikaishia pale.. Prince Bagenda hakuwahi kusimama tena na miaka michache akafariki dunia huku mzee wa Kirachacha ambaye hata mara moja hakuthubutu kumjibu Bagenda akidunda mpaka Leo hii na kigoli kaoa hivi karibuni

Nimeamua kutoa mfano huo baada ya kuona mwenendo wa mwandishi huyo kwa CHADEMA.. Hakauki kwa mada za kukisema vibaya hiki chama kinachotambulika kama kikuu cha upinzani Tanzania.. Ni mada za kukikosoa, kukisema vibaya kukiombea kifo tangu 2015 utadhani ndio chama pekee cha siasa Tanzania

Hakuna mtu aliwahi kupambana na sauti ya wengi akashinda.. Hakuna mtu aliyewahi kupambana na asiyejibu akashinda.. Kadiri unavyozidisha chuki na kukisema vibaya ndio kadiri unavyojimaliza.. Ukiweza BADILIKA SASA..La sivyo mwisho wako hauko mbali... Hakuna hata mmoja aliyewahi kutumika kisha akawa na mwisho mwema

Una jicho la tatu... Lifungue vema likuoneshe ya mbeleni

Mungu ibariki CHADEMA...!!!
Niliacha kusoma magazeti yake na kidhungu cha naniluuu... Maandishi yake yanachosha yanalegesha yanaudhi yana ukakasi
Mungu tujalie uzee mwema
Huyu asituchoshe

Kwema huko rafiki!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom