Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 374,212
- 866,477
- Thread starter
- #201
Thanks ngoja nifanye hivyo [emoji173]Mkuu
Rekebisha ni Kiraracha na si Kirachacha
Sent using Jamii Forums mobile app
Thanks ngoja nifanye hivyo [emoji173]Mkuu
Rekebisha ni Kiraracha na si Kirachacha
Hata mimi ni hivohivo ndugu yangu.Pamoja na mapungufu mengi kwa mitazamo ya walio wengi ya Pasco mayala lakini ukweli chadema ni kama sio tena sauti ya wengi, sio mkombozi tena kama tulivyodhania wakati ule, tunaweza kuandika mengi lakini chadema kimekua na mapungufu mengi sana nyakati hizi tokea 2015 kuja huku tulipo.
Niko na kadi ya chadema tokea 2004 na nimepiga kura kwa mbowe, slaa,. Lakini ile 2015 kwa kweli hapana, walao 2020 lakini nako walikuwa hawako serious.
Na kwa mwendo huu miaka kumi ijayo tutakuwa tukiona chadema kama tlp au caf kama sio udp kabisa.
Kwa mtazamo wangu, Mabere N Marando na Marehemu Augustino L. Mrema hawakuwa wanamageuzi sahihi.Ni mwandishi nguli na mwana JF maarufu CV yake haina mashaka popote na ana heshima yangu kubwa tu. Ni mmojawapo wa watu aliyenihamasisha kujiunga na JF hasa kule jukwaa la intelligence
Simhukumu vibaya lakini nadhani ana tatizo binafsi na CHADEMA kama ilivyokuwa kwa Prince Bagenda na Augustine Lyatonga Mrema mzee wa Kiraracha
Kuna mengi ya kusimuliwa kati ya wawili hawa.. Ya sirini na ya upenuni, Lakini yanayojulikana zaidi ni pale siasa za Mageuzi zilipoingia nchini mwaka 1992 na baadae Waziri wa mambo ya ndani kwa wakati huo Lyatonga Mrema alipojivua nyazifa zake zote na kukiacha chama chake na kujiunga na NCCR-Mageuzi kilichokuwa chama kikuu cha upinzani wakati huo
Kujitoa kwa Mrema ccm kulikuwa na mtikisiko mkubwa sana kwakuwa kwa wakati huo ndio waziri pekee aliyekuwa na uthubutu uliorejesha nidhamu serikalini na kuwa tishio kwa wazembe., wala rushwa majambazi na wapiga dili wengine
Mwaka 1995 wakati wa uchaguzi mkuu akasimama kugombea nafasi ya urais kupitia NCCR- Mageuzi chini ya timu ya Mabere Nyaucho Marando wakili msomi James Mbatia
Dr. Masumbuko Lamwai wakili msomi RIEP
Prince Bangeda mwandishi nguli na wengine wengi
Moto ule wa NCCR hiyo uliwatisha mno ccm na wakaona kitisho cha wazi kama wataiacha NCCR istawi, hivyo baada ya uchaguzi ule NCCR ilifitinishwa na kumeguka mapande mawili kila kundi likilishutumu lingine kwa usaliti
Baada ya hapo yalitokea mengi sana, lakini la kukumbukwa zaidi ni namna Prince Bangeda alivyotumika kumshambulia Mrema kupitia magazeti ya Rai na Mtanzani kwenye safu ya :Kalamu ya Bangeda' nadhani.. Yaani ilikuwa kama project maalum ya kumchafua mzee wa Kirachacha.. Prince Bagenda aliandika na kuandika na kuandika, aliandika mabaya tupu. Hakuna siku aliandika jema la Mrema na kwa baadhi ya mada akitoa ushauri wa kinafiki kabisa
Inawezekana pengine kuna siku Jenerali Ulimwengu atakuja kutuambia ule mradi ulikuwa wa nani na ulikuwa na lengo gani, lakini juu ya yote mwisho wa project hiyo ya Bangeda aliasisi gazeti lake na akiwa kwenye mchakato wa kuanzisha TV yake. Ofisi yake iliyokuwepo pale jengo la ushirika Lumumba iliwaka moto na kila kitu kikaishia pale.. Prince Bagenda hakuwahi kusimama tena na huku mzee wa Kirachacha ambaye hata mara moja hakuthubutu kumjibu Bagenda akidunda mpaka Leo hii na kigoli kaoa hivi karibuni
Nimeamua kutoa mfano huo baada ya kuona mwenendo wa mwandishi huyo kwa CHADEMA.. Hakauki kwa mada za kukisema vibaya hiki chama kinachotambulika kama kikuu cha upinzani Tanzania.. Ni mada za kukikosoa, kukisema vibaya kukiombea kifo tangu 2015 utadhani ndio chama pekee cha siasa Tanzania
Hakuna mtu aliwahi kupambana na sauti ya wengi akashinda.. Hakuna mtu aliyewahi kupambana na asiyejibu akashinda.. Kadiri unavyozidisha chuki na kukisema vibaya ndio kadiri unavyojimaliza.. Ukiweza BADILIKA SASA..La sivyo mwisho wako hauko mbali... Hakuna hata mmoja aliyewahi kutumika kisha akawa na mwisho mwema
Una jicho la tatu... Lifungue vema likuoneshe ya mbeleni
Mungu ibariki CHADEMA...!!!
Ila kweli jamaa alikuwa chawa mwandamizi wa Lowasa.Chadema ilizima ndoto zake baada ya kumchukua Lowassa
Lowasa angeshinda jamaa yetu angekuwa kwenye Kiti cha ZuhuraIla kweli jamaa alikuwa chawa mwandamizi wa Lowasa.
Na mwisho wa siku nani kaibuka mshindi? Chadema ipo Magufuli alikufa kibudu.Hapo ulipoandika hakuna aliewahi kupambana na asiejibu akashinda panafikirisha
Maana wafuasi wa Chadema mnaongoza kumtukana Magufuli huku mkijua hawezi kujibu kwasasa
All in all mengne watajibu wengine lakini la muhimu tukosoane kwa hoja sio vihoja.
Duh, yaani umepatia vema wasifu wa huyu mtu.Mimi huyo mwandishi nguli ambaye hakutajwa simjui, lakini katika kukadiria kwangu, kama mtu huyo hushiriki kwenye jukwaa hili la Siasa, JF; basi huyo ninayemjua mimi siwezi kamwe kumpa sifa ya "uandishi nguli."
Huyo tokea mwanzo kabisa kukutana naye hapa JF, na kusoma maandishi yake kadhaa nilihitimisha kuwa siyo mwandishi, ni kanjanja tu!
Kwa bahati mbaya sana ndani ya nchi yetu hii, nadhani tumeishiwa watu wenye upeo ambao tunaweza kuwatolea mifano ya sifa kama hizo ulizompa huyo mtu.
Mimi baada ya kumjua kuwa hana kitu kabisa, hasa baada ya kufahamu kuwa hana popote anaposimamia katika maandishi yake, nilimpa sifa ya kuwa "Popo"ambaye hana sifa za kuitwa mnyama moja kwa moja, ama kufahamika kuwa ni ndege.
Baada ya kumtambua hivyo, sikujishughulisha tena na kusoma mabandiko yake humu marefu, ambayo niliyapa sifa ya kuwa "magazeti".
Tofautisha. huyo si mwandishi. Mwanakijiji, pamoja na kukengeuka kwake, lakini anapopanga hoja zake, hata kama hukubaliani nazo unaona taaluma ya uandishi kutoka kwake. Huyu unayemleta hapa, makala zake hazina sifa za uandishi. Awe anasifu au anaponda, maandishi yake hayana vinasaba vya uandishi wa habari.
Na kuhusu mzee wa kirachacha, hiyo nayo ni habari nyingine kabisa. Mfano wa mwanasiasa asiyekuwa na 'bearing'. Sijawahi kumchukulia Mrema kuwa mwanasiasa wa kutolea mfano kwa wengine.
Well said.Mpuuzeni huyo njaa
Nimecheka sana hapo 'labda sijui itokee dharura gani huko au bahati mbaya gani....'Hahahaha mkuu hakuna kitu naheshimu kama MKE WA MTU labda sijui itokee dharura gani huko ama bahati gani mbaya..Lakini kwa hali ya kawaida kabisa kwangu hiyo ni haramu
Anaweza akawa ni mmoja Kati ya watu waliotapeliwa na kijana wa mboweNi mwandishi nguli na mwana JF maarufu CV yake haina mashaka popote na ana heshima yangu kubwa tu. Ni mmojawapo wa watu aliyenihamasisha kujiunga na JF hasa kule jukwaa la intelligence
Simhukumu vibaya lakini nadhani ana tatizo binafsi na CHADEMA kama ilivyokuwa kwa Prince Bagenda na Augustine Lyatonga Mrema mzee wa Kiraracha
Kuna mengi ya kusimuliwa kati ya wawili hawa.. Ya sirini na ya upenuni, Lakini yanayojulikana zaidi ni pale siasa za Mageuzi zilipoingia nchini mwaka 1992 na baadae Waziri wa mambo ya ndani kwa wakati huo Lyatonga Mrema alipojivua nyazifa zake zote na kukiacha chama chake na kujiunga na NCCR-Mageuzi kilichokuwa chama kikuu cha upinzani wakati huo
Kujitoa kwa Mrema ccm kulikuwa na mtikisiko mkubwa sana kwakuwa kwa wakati huo ndio waziri pekee aliyekuwa na uthubutu uliorejesha nidhamu serikalini na kuwa tishio kwa wazembe., wala rushwa majambazi na wapiga dili wengine
Mwaka 1995 wakati wa uchaguzi mkuu akasimama kugombea nafasi ya urais kupitia NCCR- Mageuzi chini ya timu ya Mabere Nyaucho Marando wakili msomi James Mbatia
Dr. Masumbuko Lamwai wakili msomi RIEP
Prince Bangeda mwandishi nguli na wengine wengi
Moto ule wa NCCR hiyo uliwatisha mno ccm na wakaona kitisho cha wazi kama wataiacha NCCR istawi, hivyo baada ya uchaguzi ule NCCR ilifitinishwa na kumeguka mapande mawili kila kundi likilishutumu lingine kwa usaliti
Baada ya hapo yalitokea mengi sana, lakini la kukumbukwa zaidi ni namna Prince Bangeda alivyotumika kumshambulia Mrema kupitia magazeti ya Rai na Mtanzani kwenye safu ya :Kalamu ya Bangeda' nadhani.. Yaani ilikuwa kama project maalum ya kumchafua mzee wa Kirachacha.. Prince Bagenda aliandika na kuandika na kuandika, aliandika mabaya tupu. Hakuna siku aliandika jema la Mrema na kwa baadhi ya mada akitoa ushauri wa kinafiki kabisa
Inawezekana pengine kuna siku Jenerali Ulimwengu atakuja kutuambia ule mradi ulikuwa wa nani na ulikuwa na lengo gani, lakini juu ya yote mwisho wa project hiyo ya Bangeda aliasisi gazeti lake na akiwa kwenye mchakato wa kuanzisha TV yake. Ofisi yake iliyokuwepo pale jengo la ushirika Lumumba iliwaka moto na kila kitu kikaishia pale.. Prince Bagenda hakuwahi kusimama tena na huku mzee wa Kirachacha ambaye hata mara moja hakuthubutu kumjibu Bagenda akidunda mpaka Leo hii na kigoli kaoa hivi karibuni
Nimeamua kutoa mfano huo baada ya kuona mwenendo wa mwandishi huyo kwa CHADEMA.. Hakauki kwa mada za kukisema vibaya hiki chama kinachotambulika kama kikuu cha upinzani Tanzania.. Ni mada za kukikosoa, kukisema vibaya kukiombea kifo tangu 2015 utadhani ndio chama pekee cha siasa Tanzania
Hakuna mtu aliwahi kupambana na sauti ya wengi akashinda.. Hakuna mtu aliyewahi kupambana na asiyejibu akashinda.. Kadiri unavyozidisha chuki na kukisema vibaya ndio kadiri unavyojimaliza.. Ukiweza BADILIKA SASA..La sivyo mwisho wako hauko mbali... Hakuna hata mmoja aliyewahi kutumika kisha akawa na mwisho mwema
Una jicho la tatu... Lifungue vema likuoneshe ya mbeleni
Mungu ibariki CHADEMA...!!!
Na huu ndiyo ukweli wenyeweMimi sina tatizo na Paskali kuiandika CDM vibaya maana ndio uhuru wa maoni. Na huenda kwenye kuisema vibaya huko baadhi ya mapungufu ya CDM yanaweza kurekebishwa. Ila ni kwanini Paskali anaisema vibaya CDM, hapo ndio kwenye mjadala.
- Paskali anaisema CDM kwakuwa ana wivu nayo kutokana na kuwa yeye ni mwanaccm, na CDM ina ushawishi mkubwa kwa umma bila kutumia vyombo vya dola. Inshort ana nongwa kubwa na CDM, hata akitoa ushauri sio wa nia njema, bali ni wa kinafiki zaidi.
- Paskali anapenda kutumia mitandao, na huku kwenye mitandao CCM haitambi kama ilivyo CDM, kwani huku mitandaoni hakuna vyombo vya dola vya kuibeba CCM na kuikomoa CDM. Hivyo Paskali anakutana na mashambulizi yanayomkera toka kwa wafuasi wa CDM, sasa anaandika kila mara kuhusu CDM maana anajua post yake itapata replies nyingi hata kama ni negative kwake, na ni sehemu ya kurelease stress zake kutokana na kejeli anazopewa na wafuasi wa CDM.
- Hili nadhani ni sehemu ya haya mabandiko yake ya sasa. Toka wakati wa Magufuli kuna mpango wa kuanzisha chama kingine ili kuchukua nafasi ya CDM, ndio hiki umoja party. Na namna pekee ilikuwa ni lazima CDM ife kwanza kisha kiingie chama kingine. CCM wanajua fika wameshapoteza mvuto, ila hawako tayari kuwaachia Cdm wachukue nchi kwa ajili ya usalama wa viongozi wake, hii ni kutokana na uhuni na wizi walioufanya. Sasa system wakatengeneza mpango wa kuanzisha chama kingine, lakini lazima CDM ife kwanza, kwani ndio yenye wafuasi wengi wa kweli kuliko ilivyo vyama vingine. Namna ya kuiua CDM ni pamoja na kutengeneza migogoro ndani ya CDM, kununua wanachama wake wenye ushawishi kwa nguvu au kwa ushawishi wa fedha na vyeo, kugoma kuwatangaza washindi kwenye chaguzi, kuwapora haki yako ya uchaguzi, kuwabambikia kesi, kuwaua, kuhujumu shughuli za kuwaingizia kipato viongozi wake, na hata kuchafua haiba yao kwenye jamii. Hii ya kuchafua haiba yao ndio akina Paskali wamepewa mchongo, ili wahakikishe CDM inachafuka, kisha itengenezwe justification ya kuwa kwanini CDM imekufa. Kwa sasa kuna mpango wa wazi wa kuifuta CDM, hivyo inatafutwa sababu ili umoja party iweze kuanzishwa na watanzania kushurutishwa kuikubali kwa faida ya CCM. CCM walifanikiwa huko nyuma kwa michezo hii michafu ya kuua vyama pendwa, je wataweza sasa kukiwa na kizazi kipya? Ngoja tuone hii kazi waliyopewa akina Paskali kama watatoboa.
Ohooooanakosoa kumshina Pascal Mayalla ?
Prince Mahinja Mlokozi Bagenda, kaz ya kulijenga Jimbo la Buhaya ianze sasa.Asante kwa masahihisho mkuu
Sasa sijui leo umeandika kitu gani hiki mkuu Mshana jr. Ulosi wote ule unaosifiwa nao, na umakini mwingi uliojidhihirisha nao katika jukwaa hili bado unafumbafumba mambo kama kigori asiyewahi kuonja?Hakuna mtu aliwahi kupambana na sauti ya wengi akashinda.. Hakuna mtu aliyewahi kupambana na asiyejibu akashinda.. Kadiri unavyozidisha chuki na kukisema vibaya ndio kadiri unavyojimaliza.. Ukiweza BADILIKA SASA..La sivyo mwisho wako hauko mbali... Hakuna hata mmoja aliyewahi kutumika kisha akawa na mwisho mwema
Una jicho la tatu... Lifungue vema likuoneshe ya mbeleni
Mungu ibariki CHADEMA...!!!
Kusema kweli leo nimemshangaa Mshana kupoteza muda wake kuleta mada kama hii hapa Jukwaani!Niliacha kusoma magazeti yake na kidhungu cha naniluuu... Maandishi yake yanachosha yanalegesha yanaudhi yana ukakasi
Mungu tujalie uzee mwema
Huyu asituchoshe
Kwema huko rafiki!!