Kubwajinga
JF-Expert Member
- Jan 23, 2008
- 2,194
- 297
Wakuu zangu,
Haya maswala ya kujiuliza kama Chadema inaweza kuongoza ni maswali yasiyokuwa na msingi kabisa.
Kina mama na wana JF wote mtanisamehe sana kwa mfano mdogo naotaka kuuweka hapa:-
Uongozi wa nchi ni sawa na uongozi wa nyumba (kwa udogo wake). Huwezi kumpima bwana mmoja na mwanamme mwingine kama anaweza wakati wote ni wanaume. Ati sababu unazotumia ni kwamba mume mmoja hajawahi kuoa..
Kama kuna sababu zinazowasukuma kuamini kwamba Chadema haiwezi kuongoza nchi bora mziorodheshe wazi na zenye maana lakini sii habari hii ya kupima uume wa Chadema wakati miguu yenu mmeifunga!
Mkuu Mkandara,
Sidhani kama kuna anayesema kuwa hawawezi kuongoza, bali swali ni kuwa je Watanzania wakipewa sasa hivi kuchagua kuongozwa na mmojawapo wa viongozi wa CHADEMA wanaofahamika, say Mbowe, Zitto au Slaa ili wawaondoe CCM ambao ndani yake wana watu kama Salim A. Salim, Dr. Mwakyembe, Prof. Mwandosya, S. Sitta n.k. watawakubali? Jibu hatulijui lakini tunapoongea na waliokaribu yetu, majibu yao ni overwhelmingly NO.
Viongozi wa CHADEMA lazima waonyeshe kuwa ni tofauti na bora kuliko wa CCM bila ya hivyo haitakuwa rahisi kubadilisha CCM na CCM-b.