CHADEMA imefanya nini kustahili dhamana ya Uongozi wa Taifa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA imefanya nini kustahili dhamana ya Uongozi wa Taifa?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mzee Mwanakijiji, Nov 17, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Nov 17, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Wapo wanaoamini kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ndiyo chama mbadala cha kisiasa chenye uwezo wa kushika hatamu ya Uongozi kwa kuunda serikali. Wenye imani hii wanaamini kabisa kuwa CCM imeshindwa kabisa na hivyo ni lazima iondolewe madarakani ili chama kinginge "kipewe nafasi" ya kuliongoza Taifa letu kuelekea kule tunakotaka.

  Tukilinganisha uwezo wa watu, rasilimali, historia na mwelekeo kati ya CCM na CHADEMA chama cha CCM kinaiacha CHADEMA kwa mbali sana. Linapokuja swali la mahusiano ndani ya vyama hivyo ni wazi kuwa vyama hivyo vyote havina tofauti sana katika kusababisha migogoro ya ndani, kutumia michakato ya ndani kushughulikia matatizo yao na vile vile kuendesha propaganda dhidi ya kingine.

  Hata hivyo tunapoelekea katika Uchaguzi Mkuu ujayo na tukiamua kupima rekodi ya CHADEMA kwa miaka hii karibu 15 iliyopita tunalazimika kujiuliza kama kweli CHADEMA ndicho chama kinachoweza kweli kuliongoza Taifa letu. Na tukiiangalia historia hiyo kwa ukaribu wa miaka hii minne iliyopita tunalazimika kujiuliza kama CHADEMA kimefanya mambo yoyote, kuonesha uongozi katika jambo lolote au kwa namna yoyote ile kuamsha Watanzania katika kujiletea mabadiliko kiasi cha kuweza kustahili mapenzi, imani, na ufuasi wa watu wengi sasa hivi.

  Je, yawezekana watu wanaokimbilia CHADEMA sasa hivi au wanaoiamini CHADEMA wanafanya hivyo si kwa sababu ya mapenzi yao kwa CHADEMA ilivyo bali kutokana na chuki yao kwa CCM na utawala wake wa mfumo wa kifisadi kwa miaka 45 iliyopita?

  Je, yawezekana katika kutoridhika huku watu wamefumbia mapungufu makubwa ya kimuundo, kiitikadi, kichama na kimwelekeo ya CHADEMA ambayo yanaweza kujitokeza kwa nguvu kubwa endapo chama hicho kitashika madaraka ya nchi na hivyo kuturudisha kwenye "madudu" yale yale ya CCM?

  Je, yawezekana kwa kuweka imani pofu (blind faith) kwa kundi la watu ambao wamejithibitisha mara kadhaa kuwa hawajamudu fani na sanaa ya siasa na kuwa ni jopo la watu wenye mtazamo wa kisomi zaidi (elitist) kuliko wa kimwamko wa mabadiliko wanajiandaa kwa kukatishwa tamaa?

  Je, yawezekana ndio sababu bado wasomi wengi na watu wengi katika taifa letu bado wanaikumbatia CCM na kuikubali kwa sababu tayari wanajua madudu yake (zimwi likujualo) na hawako tayari bado kuweka imani yao kwa chama hiki au kingine chochote cha upinzani?

  Je, yawezekana uongozi wa CHADEMA ulivyo sasa hasa mvutano wa kipuuzi kati ya Freeman Mbowe na Zitto Kabwe ni kikwazo kikubwa zaidi kwa kumuamsha jitu huyu aliyelala (this sleeping giant) kiasi kwamba hawa wawili peke yao kinyume na inavyochukuliwa ndio kikwazo kikubwa zaidi kwa CHADEMA kupiga ile hatua ya lazima mbele? Je, itakuwa bora kama hawa wawili wakaachilia nafasi za juu za uongozi wa Chama ili kukipa chama ule msukumo unahojitajika?

  Katika kutafuta majawabu ya maswali haya siyo vyema kwa kweli kuendelea kuikumbatia CCM na madudu yake na kujaribu kuiokoa kwani ndio njia ya haraka ya kuleta mabadiliko ya haraka kuliko kukumbatia upinzani ulivyo sasa?
   
 2. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #2
  Nov 17, 2009
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Chadema haijafanya chochote kile kustahili uongozi.
   
 3. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #3
  Nov 17, 2009
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  Migogoro inayoendelea sasa inaashiria nini kwa mfumo mzima wa vyama vyetu vya siasa?
   
 4. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #4
  Nov 17, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  CHADEMA imefanya nini?

  Ndugu...kwani ulitaka ufanye nini na kwa nani? kwa miaka michache na kwa system ambayo imejaa unfair competition and huge external propaganda naamini wamejitahidi walau sasa the voices of wananchi are hear to some extent..some streotype kwamba upinzani ni vita umepungua kwa wananchi wa kawaida...grassroots

  Chadema internal problems

  Too many but yes wengi wanaamini chadema with blind eyes kwasababu ya chuki yao na CCM leadership style

  Inabidi CHADEMA i-face realiatic ya Ukabila na kwangu mimi ..very very skeptical and worry of former (priest) kuwa rais..must prove kwamba hatumikii kanisa..

  The opportunity is there...kuungana na CUF for the sake national interest will change the whole political equation to the best..can they?..seems to be very remote idea..to kind of current CHADEMA leadership.. whom we describe them in very simple terms "business networks"
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Nov 17, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ni vigumu sana kupima chama cha Upinzani kwa kutafuta mambo ambayo wameyafanya kinyume cha Upinzani wake. Sijaona nchi wala chama cha Upinzani wakifanya kitu ambacho mimi naweza kukipa nguvu ya kuongoza nchi zaidi ya sera zake.

  Hivi sasa hata Marekani wanatawaliwa na Demokratic, na ukiniuliza mimi Republican wamefanya nini toka Obama kuingia madarakani kusema kweli SIJUI zaidi ya hizo safari za kujitangaza kwa wananchi.Chini ya Mzee Bush pia siwezi kusema Demokratic walifanya kipi kustahili heshima ya kuiongoza Marekani kama sio kuonyesha Upinzani wao kwa maamuzi ambayo hayakuwa na maslahi kwa wananchi wake. zaidi ya hapo kusema kweli mimi sijui hata moja! nifungueni macho.

  Hivyo, ni vizuri tukijadili yale tuloyataka Chadema iyafanye kama chama cha Upinzani.
   
 6. S

  Semjato JF-Expert Member

  #6
  Nov 17, 2009
  Joined: Jun 26, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  maswali ya kimsingi sana...natamani majibu yake kila siku!..vingi ya vigezo tunavyojaribu kuvitumia kujua wanaostahili kuwa viongozi wa nchi yetu haviiungi mkono Chadema dhidi ya CCM...mara zote inapoungwa mkono Chadema kwenye vigezo hivyo ni double standards tu hutumika(yale tunayoikosoa nayo CCM hatuoni kama Chadema nayo aidha inazungukwa nayo na kuna uwezekano itayavagaa)...
   
 7. l

  lukule2009 Senior Member

  #7
  Nov 17, 2009
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CHADEMA waache Migogoro na hasa Zitto Kabwe ndio chanzo. Ana ubinafsi na umimi mwingi sana, hana uongozi wa pamoja, anapingana na uongozi halali wa chama kwenye vyombo vya habari na kwa kusema ukweli hicho kinachoitwa mgogoro .. chanzo kikubwa ni ubinafsi na kupenda sifa kulikokithiri kwa Zitto.

  Mambo aliyoandika hapa JF juu ya vikao vya ndani vya chama yanaonyesha wazi kuwa hafai na hajui maana ya uongozi. kwa maoni yangu ikibidi Chadema wanaweza kumchukulia hatua hata yeye hata hivyo naona wanamvumilia sana.. in fact I have a feeling kwamba he is overrated .... Haiwezekani Naibu katibu mkuu unabishana na katibu wako magazetini .. no way ...kwa sababu kimsingi hiyo ni ofisi moja. sasa yeye anafanya kazi na magazeti wapi na wapi.

  Kesho akiwa serikalini say waziri mkuu si ndio itakuwa Raisi anasema hivi na yeye anasema vile .,. vurugu tupu. Mwalimu alikuwa na influence kwenye nchi na kila siku kwenye hotuba anasema... tulifanya hiki , tulifanye kile .. sio mimi nilifanya hivi ... hata kama ni yeye kweli aliyefanya.. sasa Zitto leo anasema yeye ndio alifanya hata wabunge waliokuwa hawaongei waongeee sasa mtu gani huyo..

  Credibility yake kwa sasa inatia mashaka sana. kila kitu mimi kila kitu mimi .. principle ndogo kabisa ya uongozi anashindwa kuifuata .. kuwa uongozi ni team work..... na inaonekana anaendelea.. wewe katibu kamsimamisha mtu kazi kwa mamlaka aliyonayo kikatiba ... unasema mimi sikubali na wewe ndio Naibu wangu jamani utawala gani huo?Vinginevyo ajiuzulu..kama hakubaliani ndio kanuni za uongozi zinavyosema..

  Ila ushauri kwa CHADEMA (kwa maoni yangu) waachane na sera ya majimbo kwa sasa. Itawapotezea muda kuielezea wakati wenzao wanapiga kampeni wao wanaelezea jinsi utawala wao wa majimbo utavyoendeshwa.. na pia ni rahisi kwa CCM kutumia sera hiyo hiyo ya majimbo kuwabomoa.. tatizo la nchi yetu sio majimbo ni uongozi bora kwisha...

  Na pia kuanza kuover all Adnimistration system upya kwa sasa itazidi kutuchelesha .. issue ni viongozi serious wenye vision .. sheria zinazofanya kazi .. wafanya wa serikali wanaoheshimu kazi zao, mafisadi kushughulikiwa kiasi watu waogope kuibwa.. wezi wakiona watu wanafungwa ufisadi utaisha.. the thing kwa sasa ni kwamba watu wananjua they can get away with ufisadi as far as they got money......

  Sasa, Je CHADEMA wanastahili kuongoza kwa sasa ... kwa maoni inabidi wafanye kazi zaidi .. waonekane wametulia .. vinginevyo ni kheri zimwi ulijualo....
   
 8. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #8
  Nov 17, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,579
  Likes Received: 3,881
  Trophy Points: 280
  MKJJ -those above are certain Million Dollar Questions.

  ''Je, yawezekana katika kutoridhika huku watu wamefumbia mapungufu makubwa ya kimuundo, kiitikadi, kichama na kimwelekeo ya Chadema ambayo yanaweza kujitokeza kwa nguvu kubwa endapo chama hicho kitashika madaraka ya nchi na hivyo kuturudisha kwenye "madudu" yale yale ya CCM?'' -MKJJ

  Chadema hawajafanya chochote mpaka sasa, ila wameonyesha mwanga wa nini viongozi wanatakiwa kufanya, kujenga hoja, mabadiliko aliyoyafanya Slaa,Zitto bungeni are things that give them credit

  Mimi Chadema natamani washike nchi kwa IMANI, I believe that they can do something.What I am real struggling ni hili swali nililo-li-quote kutoka kwako.

  Ni swali gumu, lakini ni assignment ambazo zinaweza kuwa solved

  Mbowe vs Zito thing is small issue if and only if democracy will be practised openly.

  Kama nilivyosema hapo juu Imani yangu kwa chadem inatokana na waliyoyafanya tayari, na imani ya mashaka ni juu ya wao kuitekeleza demokrasia kwa vitendo ndani ya chama

  Nikibalance btn imani yangu kwao na mashaka yangu kwao, naona imani inazidi zaidi ya mashaka. Hata hivyo haya mashaka for the sake of the country needs to be questioned, discussed and solved. Is possible.

  wana CCM waliomchagua JK kuwa rais walijua alifanya nini? je wangerudi nyuma na kujiuliza nini alichowahi kufanya JK, wangejiuliza kuwa yeye ndiye archtect wa almost miradi yote michafu na umeme nchi hii ''wangejiuliza tu haya au wangeyafahamu JK hakutakiwa kuwa pale'' anachofanya sasa ni yanaelezea performance yake ever since''

  Cha ajabu mwakani wana CCM watampa tena JK!!!(God forbid) why? mapenzi ya wanachama kwa vyama vyao mara nyingi yanategemea wanafaidika nini na wanapata sh. ngapi, hawafikirii nchi as a whole, hawafikirii vizazi vijavyo.

  Maswali uliyouliza ni foundations siyo ya Chadema bali ya taifa letu, yakijibiwa vizuri kwa rate ya 100% for each.Lisifanyike kosa la CCM


  Ugomvi wa wanachama is so common, katiba , vikao na taratibu halali za chama zikufuata basi kila mmoja anakuwa safe.

  Wapewe nchi just for what they have arleady done outside the government
   
 9. J

  JokaKuu Platinum Member

  #9
  Nov 17, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,747
  Likes Received: 4,967
  Trophy Points: 280
  ..kwani CCM wamefanya nini cha maana?
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Nov 17, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Umeniwahi aisee....

  Ila kwani kuna ulazima opposition wawe wamefanya chochote kuweza kuongoza nchi? Kama ndio hivyo basi CCM waachwe tu waendelee kutawala.
   
 11. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #11
  Nov 17, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Shukrani ya Punda ni mateke!
   
 12. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #12
  Nov 17, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,579
  Likes Received: 3,881
  Trophy Points: 280
  You have missed the point!

  Author amesema CCM hamna kitu ''zimwi likujualo' ila tunawajua kuwa hamna kitu, tumewaprove na kuhakikisha kuwa hawana kitu.

  ana compare kati ya hawa wasio na kitu tunaowajua na hawa tusiowajua, haja confirm ameuliza, mpe majibu!
   
 13. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #13
  Nov 17, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Zitto angekuwa mbinafsi asingemwachia dikteta wenu Mbowe nafasi ya uenyekiti.
   
 14. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #14
  Nov 17, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  CHADEMA sio chama mbadala. CUF wamekomaa na wana demokrasia kubwa sana kwenye chama chao.
  bora ya Nccr kuliko CHADEMA. Unless Mbowe na baba yake wakae pembeni.
   
 15. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #15
  Nov 17, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Huu ubinafsi na umimi wa zitto ni upi? bana acheni hizoooo.leteni hoja za maana kupinga watu siyo blah blah zenu.kwanini hamsemi "Ubinafsi na umimi wa mbowe na baba mkwe wake; kwanini hamsemi ubinafsi na ubabe wa slaa agh...mnaboa sana nyinyi....another reason to go for CUF come 2010
   
 16. 911

  911 Platinum Member

  #16
  Nov 17, 2009
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 761
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Hapa mimi ndo nimeona pana dhumuni hasa la habari yooote hiyo ilioandikwa...Kujaribu kuiokoa CCM.Nikiunganisha nukta na matamshi ya mleta mada(si katika thread hii) kuwa anataka kurudi Jembe na Nyundo(of which Im not sure kama hakuweko huko anyway!).Man,you of all people should have known better that CCM has rotten to its core...Nenda kajiunge nao,na utakuwa mmoja wao na overtime possibly ukawa kama wao!!Kila la heri katika 'kyama'!Wenyewe wanasema kijani majani Chichiem ina wenyewe...
  Wengne hatuamini katika zimwi likujualo...
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  Nov 17, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,307
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji, hili naamini unalijua wazi kuwa Chadema bado haina uwezo wa kushika dola, Mbowe analijua hili, Dr. Slaa analijua hili, Zitto analijua hili na kila serious practical man analijua hili.

  Pamoja na kutokuwa na uwezo wa kushika dola, Chadema angalau wameonyesha mwelekeo, wakisaidiwa na mchango wa mawazo ya watu kama nyie, wakakubali kupunguza mapungufu yao ya ubinafsi, wakajoin forces na CUF kusimamisha mgombea mmoja kila mahali, 2010 wataonyesha njia, 2015 watanzania watawaamini, CCM Chini!

  Kuna post fulani niliwahi kukushukuru Mzee Mwanakijiji kwa kuisaidia CCM kuondoa mapungufu yake. Nashukuru sasa uneonyesha angalau mwelekeo kuibua mdajada wa mapungufu ya Chadema ili kuuimarisha.

  Bahati nzuri mimi sina chama, wala sina chuki na CCM bali mpanda demokrasia wa kweli, lazima atatamani upinzani wenye nguvu for the sake of balance of power ndani ya Bunge. The only light for now ni CUF na Chadema, unless tusubiri mpaka yatimie yele maneno ya unabii wa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, kuwa 'upinzani wa kweli utatoka CCM pekee'.

  Na tutaendelea kusubiri mpaka Masiya atakaporudi mara pili kutukomboa na kuukomboa ulimwengu.
   
 18. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #18
  Nov 17, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180

  Karibu PPPT!
   
 19. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #19
  Nov 17, 2009
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  kutofautiana katika vyama ni jambo la kawaida sana, tatizo ni namna ambavyo tofauti hizo zinavyoshughulikiwa. Bado hatujapata wataalamu ktk vyama vyetu (CCM, Chadema et la) wenye uwezo wa kushughulikia migogoro ya ndani.

  Siamini kwamba ndani ya Chadema tatizo ni Zitto, tatizo ni mfumo wa demokrasia kongwe ulioigwa kutoka CCM, kwamba hata kama hafai maadam ni M'kiti/Rais amalizie muda wake. akitokea mshindani anaitwa msaliti. Siamini pia kwamba Zitto ni mbinafsi labda haya yanatoka kutoka kwa wapinzani wake kisiasa ndani ya Chadema. Chadema wanatakiwa wafanye hima sasa tena bila kupoteza muda kabla ya 2010 ili kurudisha imani kubwa waliokuwa nayo wananchi kwao kabla hawajaanza madudu yao tunayoshuhudia sasa ili angalao tukiite chama mbadala wakati wa uchaguzi mkuu ujao.
   
 20. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #20
  Nov 17, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Chama gani kinatumikia kanisa? Na vipi unaposhabikia mdudu CUF ambaye ni purely Islamic Party?
   
Loading...