CHADEMA imefanya nini kustahili dhamana ya Uongozi wa Taifa?

kama hapa Jamvini ndo sehemu ya GT then thinkers wenyewe hawaonyeshi wala kutoa jibu ya nini kifanyike kwa upinzani kushika nchi then CCM itaongoza milele....Anyway Swali nalirudisha kwa mwenye topic MKJJ.

"Kifanyike nini ili upatikane uongozi mbadala?"

Kitu fulani Kimekwisha fanyika. kwamfano mdogo tu,
Mtu 5 bungeni aliwapigisha magoti CCM mpaka PM kibarua kikaota Nyas Baraza la mwaziri likavunjwa.
Mkitaka Jambo lishukalo kutoka mbinguni itabidi muuache wosia kwa vilembwe wenu kwani si leo wala kesho.
 
Wapo wanaoamini kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ndiyo chama mbadala cha kisiasa chenye uwezo wa kushika hatamu ya Uongozi kwa kuunda serikali. Wenye imani hii wanaamini kabisa kuwa CCM imeshindwa kabisa na hivyo ni lazima iondolewe madarakani ili chama kinginge "kipewe nafasi" ya kuliongoza Taifa letu kuelekea kule tunakotaka.

Tukilinganisha uwezo wa watu, rasilimali, historia na mwelekeo kati ya CCM na CHADEMA chama cha CCM kinaiacha CHADEMA kwa mbali sana. Linapokuja swali la mahusiano ndani ya vyama hivyo ni wazi kuwa vyama hivyo vyote havina tofauti sana katika kusababisha migogoro ya ndani, kutumia michakato ya ndani kushughulikia matatizo yao na vile vile kuendesha propaganda dhidi ya kingine.

Hata hivyo tunapoelekea katika Uchaguzi Mkuu ujayo na tukiamua kupima rekodi ya CHADEMA kwa miaka hii karibu 15 iliyopita tunalazimika kujiuliza kama kweli CHADEMA ndicho chama kinachoweza kweli kuliongoza Taifa letu. Na tukiiangalia historia hiyo kwa ukaribu wa miaka hii minne iliyopita tunalazimika kujiuliza kama CHADEMA kimefanya mambo yoyote, kuonesha uongozi katika jambo lolote au kwa namna yoyote ile kuamsha Watanzania katika kujiletea mabadiliko kiasi cha kuweza kustahili mapenzi, imani, na ufuasi wa watu wengi sasa hivi.

Je, yawezekana watu wanaokimbilia CHADEMA sasa hivi au wanaoiamini CHADEMA wanafanya hivyo si kwa sababu ya mapenzi yao kwa CHADEMA ilivyo bali kutokana na chuki yao kwa CCM na utawala wake wa mfumo wa kifisadi kwa miaka 45 iliyopita?

Je, yawezekana katika kutoridhika huku watu wamefumbia mapungufu makubwa ya kimuundo, kiitikadi, kichama na kimwelekeo ya CHADEMA ambayo yanaweza kujitokeza kwa nguvu kubwa endapo chama hicho kitashika madaraka ya nchi na hivyo kuturudisha kwenye "madudu" yale yale ya CCM?

Je, yawezekana kwa kuweka imani pofu (blind faith) kwa kundi la watu ambao wamejithibitisha mara kadhaa kuwa hawajamudu fani na sanaa ya siasa na kuwa ni jopo la watu wenye mtazamo wa kisomi zaidi (elitist) kuliko wa kimwamko wa mabadiliko wanajiandaa kwa kukatishwa tamaa?

Je, yawezekana ndio sababu bado wasomi wengi na watu wengi katika taifa letu bado wanaikumbatia CCM na kuikubali kwa sababu tayari wanajua madudu yake (zimwi likujualo) na hawako tayari bado kuweka imani yao kwa chama hiki au kingine chochote cha upinzani?

Je, yawezekana uongozi wa CHADEMA ulivyo sasa hasa mvutano wa kipuuzi kati ya Freeman Mbowe na Zitto Kabwe ni kikwazo kikubwa zaidi kwa kumuamsha jitu huyu aliyelala (this sleeping giant) kiasi kwamba hawa wawili peke yao kinyume na inavyochukuliwa ndio kikwazo kikubwa zaidi kwa CHADEMA kupiga ile hatua ya lazima mbele? Je, itakuwa bora kama hawa wawili wakaachilia nafasi za juu za uongozi wa Chama ili kukipa chama ule msukumo unahojitajika?

Katika kutafuta majawabu ya maswali haya siyo vyema kwa kweli kuendelea kuikumbatia CCM na madudu yake na kujaribu kuiokoa kwani ndio njia ya haraka ya kuleta mabadiliko ya haraka kuliko kukumbatia upinzani ulivyo sasa?

Utajuaje kama Chadema wanaweza kushikilia dola bila wao kufanya hivyo? Hivi nani aliamini kuwa Tanzania bila Nyerere kuwa Rais ingewezekana? Ni nani aliamini kuwa Tanzania bila Nyerere kuwepo duniani ingewezekana?

Theses zako ni poor!
 
Lakini huoni matokeo ya juzi yanadhihirisha kuwa watu hawakitaki chadema? Ooh! yes unsema NEC ni ya CCM , ilikuwaje mkaingia kwenye uchaguzi wakati NEC ni ya CCM?
 
Hilo swali haliwezi kujibika bila kuwa na jibu la Kikwete alifanya nini ili akastahili kuwa kiongozi wa Tanzania? Tanzania tunatumia presidential sysetm unaposema CHADEMA imefanya nini ili kustahili kuongoza unatupeleka kwenye Parliamentary system of governing katika presidential system rais anaweza kuwa Hashim Rungwe wa NCCR mageuzi pamoja na viti 4 vya ubunge likiwise Dk wilbroad Slaa na viti vyake 22 vya ubunge lakini katika parliamentary system kiongozi atakuwa ni yule wa chama kilichotoa wabunge wengi ambacho ni CCM na hataitwa tena rais bali Waziri Mkuu.

Sasa tukilirudi kwenye swali lako ni kweli kuwa DK Slaa na chama chake cha CHADEMA wanastahili kuwaongoza watanzania tokana na kuwapigania walala hoi pale waliposimama kidete bungeni na kunyooshea kidole chama tawala kuwa kinafuja mali za wanachi na hakistahili kuongoza bila CHADEMA watanzania tusingejua EPA, Kagoda Farm, Meremeta, Richmond na scandal zingine kwa wao kuibua huo wizi wa CCM na kuahidi watakomesha wizi wa nanma ile ili kuwaletea maendele watanzania ni jambo bora na la maana linalowapa nafasi kubwa ya kupewa dhamana ya kuongoza taifa la Tanzania.

Hiyo yote ilikuwa ni Kazi ya DK slaa aliyesimama kidete bila woga wowote kuwatetea watanzania sasa swali langu kwako mwanakijiji Kikwete alifanya nini ili apewe dhamana ya kuwa mgombea wa CCM? Zaidi ya sura nzuri na kugawa mikono kwenye sherehe, tafrija na mechi za Simba na Yanga?. Tukifuata ukweli bila ushabiki sijawahi kuona mawaziri wa CCM waliochapa kazi kama Edward Moringe Sokoine, Augustin Lyatong Mrema, John Pombe Magufuri, Salim Ahmed Salim (alipokuwa ulinzi) na Edward Ngoyayi Lowassa alipokuwa waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu, pia ardhi nyumba na maendeleo mijini kabla hajageuka kuwa mwizi je Kikwete alifanya nini?
 
Kulikuwa na dada mmja aliyekuwa na wanaume wawili(A and B), kila mmja akitaka kumuoa dada huyo, wanaume hawa walikuwa na sifa tofauti, mmja"A" alishampangishia nyumba, na amekuwa nate mda mrefu tu , mwingine amekuwa nae c mda mrefu kulingana na yule wa kwanza, ila anampenda sana, na amejitolea ktk mambo yote yaliondani ya uwezo wake kufanya kama mwanaume hata huyo dada anamumkubali sana kwa kufight huyu njemba "B" ila uwezo wake ni hafifu kulingana na njemba "A", dada huyu alinifuata nimshauri afanye nini, nami baada ya kutafakari kama great thinker nikaona nimuulize swali hili "Hivi Salma unataka mwanaume aliyekufanyia nini, au mwanaume wa namna gani, au mwenye uwezo wa kukufanyia nini au atakaekufanyia nini? Wanajf nasi tutafakari kuwa tunachotaka ni serekari ya chama gani, au ya namna gani itakayokuwa inafanana na maisha yetu kama watanzania au tuendekeze itikadi za vyama na kuchagua viongozi wasiofaa kisa tu unapenda chama chake, Mwanakijiji amesema kweli, maana tunatoa kibanzi ktk jicho la CCM wakati kunajiti ndani ya Chadema pia na hatuko tayari kuyasema, Uongozi wa juu wa chama ndiyo serikali ya chama na ndiyo huunda serikari kama chama kitapewa hatamu, sasa kama hawaelewani tunategemea nini, Ombi langu jamani tuwe tunasoma mtoa hoja amekusudia kufikisha ujumbe gani mezani na tuchangiapo tutohoe yaliyomo ktk hoja hiyo na si kebehi za kiitikadi za vyama
 
Wapo wanaoamini kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ndiyo chama mbadala cha kisiasa chenye uwezo wa kushika hatamu ya Uongozi kwa kuunda serikali. Wenye imani hii wanaamini kabisa kuwa CCM imeshindwa kabisa na hivyo ni lazima iondolewe madarakani ili chama kinginge "kipewe nafasi" ya kuliongoza Taifa letu kuelekea kule tunakotaka.

Tukilinganisha uwezo wa watu, rasilimali, historia na mwelekeo kati ya CCM na CHADEMA chama cha CCM kinaiacha CHADEMA kwa mbali sana. Linapokuja swali la mahusiano ndani ya vyama hivyo ni wazi kuwa vyama hivyo vyote havina tofauti sana katika kusababisha migogoro ya ndani, kutumia michakato ya ndani kushughulikia matatizo yao na vile vile kuendesha propaganda dhidi ya kingine.

Hata hivyo tunapoelekea katika Uchaguzi Mkuu ujayo na tukiamua kupima rekodi ya CHADEMA kwa miaka hii karibu 15 iliyopita tunalazimika kujiuliza kama kweli CHADEMA ndicho chama kinachoweza kweli kuliongoza Taifa letu. Na tukiiangalia historia hiyo kwa ukaribu wa miaka hii minne iliyopita tunalazimika kujiuliza kama CHADEMA kimefanya mambo yoyote, kuonesha uongozi katika jambo lolote au kwa namna yoyote ile kuamsha Watanzania katika kujiletea mabadiliko kiasi cha kuweza kustahili mapenzi, imani, na ufuasi wa watu wengi sasa hivi.

Je, yawezekana watu wanaokimbilia CHADEMA sasa hivi au wanaoiamini CHADEMA wanafanya hivyo si kwa sababu ya mapenzi yao kwa CHADEMA ilivyo bali kutokana na chuki yao kwa CCM na utawala wake wa mfumo wa kifisadi kwa miaka 45 iliyopita?

Je, yawezekana katika kutoridhika huku watu wamefumbia mapungufu makubwa ya kimuundo, kiitikadi, kichama na kimwelekeo ya CHADEMA ambayo yanaweza kujitokeza kwa nguvu kubwa endapo chama hicho kitashika madaraka ya nchi na hivyo kuturudisha kwenye "madudu" yale yale ya CCM?

Je, yawezekana kwa kuweka imani pofu (blind faith) kwa kundi la watu ambao wamejithibitisha mara kadhaa kuwa hawajamudu fani na sanaa ya siasa na kuwa ni jopo la watu wenye mtazamo wa kisomi zaidi (elitist) kuliko wa kimwamko wa mabadiliko wanajiandaa kwa kukatishwa tamaa?

Je, yawezekana ndio sababu bado wasomi wengi na watu wengi katika taifa letu bado wanaikumbatia CCM na kuikubali kwa sababu tayari wanajua madudu yake (zimwi likujualo) na hawako tayari bado kuweka imani yao kwa chama hiki au kingine chochote cha upinzani?

Je, yawezekana uongozi wa CHADEMA ulivyo sasa hasa mvutano wa kipuuzi kati ya Freeman Mbowe na Zitto Kabwe ni kikwazo kikubwa zaidi kwa kumuamsha jitu huyu aliyelala (this sleeping giant) kiasi kwamba hawa wawili peke yao kinyume na inavyochukuliwa ndio kikwazo kikubwa zaidi kwa CHADEMA kupiga ile hatua ya lazima mbele? Je, itakuwa bora kama hawa wawili wakaachilia nafasi za juu za uongozi wa Chama ili kukipa chama ule msukumo unahojitajika?

Katika kutafuta majawabu ya maswali haya siyo vyema kwa kweli kuendelea kuikumbatia CCM na madudu yake na kujaribu kuiokoa kwani ndio njia ya haraka ya kuleta mabadiliko ya haraka kuliko kukumbatia upinzani ulivyo sasa?

Mkuu mwanakijiji kumbe mwenzetu uliliona hili tangu zamani make ungelisema hili leo, post za matusi zingeporomoshwa kama vile waziporomoshao hawana akili. Mara fisadi n.k.

CHADEMA wasichotaka kukubali ni ukweli kwamba walitaka kuvuna hata sehemu ambazo hawakupanda kisa tu walikuwa na BACK UP ya viongozi wa Dini. Kitu ambacho kinazidi kureflect tatizo la wasomi wa Kitanzania ambao wanatamani kwenda Peponi lakini hawataki kukubali kufa kwanza.
 
Kwani TANU wakati inachukua nchi ilikuwa na rasilimali gani? Haya leo CCM ina rasilimali wamezitoa wapi?

Natumaini kila mtu makini anajua. Je CCM na CHADEMA wapi kuna migogoro mingi? CCM hawatumii dola kutishiana na kunyamazina? Watu CCM hawajapotea kisa kuwa na msimamo tofauti nao? Angalia dira ya vyama vyote viwili, uongozi na maadili yao, makundi wanayokumbatia, sera zinamjali nani?

Ni wazi CCM imechafuka kila mahali mabavu ndio yanawasaidia kuendelea kuwepo, rasilimali walizonazo ni mali ya watanzania. Pia Slaa alisema kitu kizuri sana kwamba akipewa nchi kuna watu ccm wako makini na ndio atashirikiana nao kuendesha serekali, kwani kwa CCM ilivyo na mtazamo wa kifisadi zaidi haitoi nafasi kwa wale wanaolitakia taifa mema.

Nafikiri CHADEMA ni sulihisho, tuombe Mungu akiepushe na ule mkono mchafu wa CCM wa kuwawekea mapindikizi na kusababisha migogoro kama ilivyotokea NCCR na TLP.
 
Migogoro kwenye vyama ni jambo la kawaida. Hatuwezi kuwategemea CHADEMA wawe wamefanya kitu kando ya kuwa wapinzani, kabla ya kuwapa kazi ya kuiongoza nchi yetu. Uraisi ni taasisi inayoendeshwa kwa kanuni zilizo chini ya katiba. With proper handover and organizatio any party can run this country.

David Cameroon wa Liberal Democrats alifanya nini ili kuwa PM wa unigereza kando ya kuwa kionggozi wa upinzani. Sasa ana thubutu kufanya mageuzi makubwa ya kiuchumi uingereza. Hebu wanajamvi tuwe positive kwamba change can come but we can expect very little, if anythinng for CCM.

Zimwi litujualo sina imani nalo na sasa tumelipa nafasi nyingine! Tusipokuwa waangalifu zimwi hili litatumaliza!
 
Wapo wanaoamini kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ndiyo chama mbadala cha kisiasa chenye uwezo wa kushika hatamu ya Uongozi kwa kuunda serikali. Wenye imani hii wanaamini kabisa kuwa CCM imeshindwa kabisa na hivyo ni lazima iondolewe madarakani ili chama kinginge "kipewe nafasi" ya kuliongoza Taifa letu kuelekea kule tunakotaka.

Tukilinganisha uwezo wa watu, rasilimali, historia na mwelekeo kati ya CCM na CHADEMA chama cha CCM kinaiacha CHADEMA kwa mbali sana. Linapokuja swali la mahusiano ndani ya vyama hivyo ni wazi kuwa vyama hivyo vyote havina tofauti sana katika kusababisha migogoro ya ndani, kutumia michakato ya ndani kushughulikia matatizo yao na vile vile kuendesha propaganda dhidi ya kingine.

Hata hivyo tunapoelekea katika Uchaguzi Mkuu ujayo na tukiamua kupima rekodi ya CHADEMA kwa miaka hii karibu 15 iliyopita tunalazimika kujiuliza kama kweli CHADEMA ndicho chama kinachoweza kweli kuliongoza Taifa letu. Na tukiiangalia historia hiyo kwa ukaribu wa miaka hii minne iliyopita tunalazimika kujiuliza kama CHADEMA kimefanya mambo yoyote, kuonesha uongozi katika jambo lolote au kwa namna yoyote ile kuamsha Watanzania katika kujiletea mabadiliko kiasi cha kuweza kustahili mapenzi, imani, na ufuasi wa watu wengi sasa hivi.

Je, yawezekana watu wanaokimbilia CHADEMA sasa hivi au wanaoiamini CHADEMA wanafanya hivyo si kwa sababu ya mapenzi yao kwa CHADEMA ilivyo bali kutokana na chuki yao kwa CCM na utawala wake wa mfumo wa kifisadi kwa miaka 45 iliyopita?

Je, yawezekana katika kutoridhika huku watu wamefumbia mapungufu makubwa ya kimuundo, kiitikadi, kichama na kimwelekeo ya CHADEMA ambayo yanaweza kujitokeza kwa nguvu kubwa endapo chama hicho kitashika madaraka ya nchi na hivyo kuturudisha kwenye "madudu" yale yale ya CCM?

Je, yawezekana kwa kuweka imani pofu (blind faith) kwa kundi la watu ambao wamejithibitisha mara kadhaa kuwa hawajamudu fani na sanaa ya siasa na kuwa ni jopo la watu wenye mtazamo wa kisomi zaidi (elitist) kuliko wa kimwamko wa mabadiliko wanajiandaa kwa kukatishwa tamaa?

Je, yawezekana ndio sababu bado wasomi wengi na watu wengi katika taifa letu bado wanaikumbatia CCM na kuikubali kwa sababu tayari wanajua madudu yake (zimwi likujualo) na hawako tayari bado kuweka imani yao kwa chama hiki au kingine chochote cha upinzani?

Je, yawezekana uongozi wa CHADEMA ulivyo sasa hasa mvutano wa kipuuzi kati ya Freeman Mbowe na Zitto Kabwe ni kikwazo kikubwa zaidi kwa kumuamsha jitu huyu aliyelala (this sleeping giant) kiasi kwamba hawa wawili peke yao kinyume na inavyochukuliwa ndio kikwazo kikubwa zaidi kwa CHADEMA kupiga ile hatua ya lazima mbele? Je, itakuwa bora kama hawa wawili wakaachilia nafasi za juu za uongozi wa Chama ili kukipa chama ule msukumo unahojitajika?

Katika kutafuta majawabu ya maswali haya siyo vyema kwa kweli kuendelea kuikumbatia CCM na madudu yake na kujaribu kuiokoa kwani ndio njia ya haraka ya kuleta mabadiliko ya haraka kuliko kukumbatia upinzani ulivyo sasa?

wewe pamoja na waliokupa thank wote ni wehu ambao uwezo wenu wa ku analyza ni sifuri..ccm ina assets gani?? subiri chadema ikichukua madaraka na kuzirudisha zote kwa wananchi ndo utatuambia ccm ina assets gani..nani aliiba mke?? kwa taarifa yako kikwete ashaiba wake za watu kibao achilia mbali mademu wenu..au kwa kuwa wewe hujui au kwa kuwa wewe ni mmoja kati ya mnaofaidika na uozo wa jk?ivi nani alikwambia wasomi sijui wazee bado wanaikumbatia ccm??wewe ni mwehu, ccm ingekuwa bado inakumbatiwa ingeiba kura??huyo jk mwenyewe na ccm yake unaojaribu kuwakumbatia wenyewe wanajua kuwa waliiba kura..humuoni jk anavyokazana kutafuta public sympathy? angekuwa kashinda kihalali alivo mtu wa vijembe mkwere yule ungejua, ila kwa kuwa kaiba kura ndo maana kawa mpole, mwenyewe anajua..siendelei kupoteza muda wangu kuargue na mbumbumbu kama wewe..and am sure hauko tanzania ndo maana ur misinformed..tulio hapa home tanzania, wapambanaji wa kweli tusioogopa mabomu ya machozi wala maji ya kuwasha ndo tunajua ukweli..we endelea kubeba maboksi huko, subiri chadema wakishachukua nchi na kuwapa maisha bora wananchi wote na nyie mrudi mwehu wewe..
 
Mimi nina swali kwa vyama vya siasa, hasa vya upinzania; hii tabia ya kusema kuwa chama hakiwezi kuwafanyia lolote wananchi mpaka kiingie ikulu imetoka wapi? Hivi hizo pesa mnazopigia kampeni mnatoa wapi? Kama mna nguvu ya "kuchakalika" mkapata pesa nyingi za kupigia kampeni, kwa nini msiwe na ari hiyohiyo katika kushiriki kwenye kuboresha huduma za jamii?
Kwa nini vyama vya siasa havina "Social Action Funds"? wangeweza kutoa scholarships, kusaidia wahanga etc.

Wanaosema TANU haikufanya kitu kudeserve kuaminiwa na wananchi inabidi wasome vizuri historia. TANU ilianza kama TAA ambayo ilikuwa ni welfare association. Watu walisaidiwa/walisaidiana sana kwa kuwepo kwa TAA and later TANU. TANU haikuwa inachukua ruzuku toka kwa yeyote kama vinavyofanya vyama vya siasa vya siku hizi. Hivyo basi usifananishe vitu hivi viwili!

Palestine kwa mfano. Kuna chama kinaitwa HAMAS. Hawa hujulikana kama terrorists, lakini wamekuwa wakiungwa mkono na wapelestina wengi. Kwa nini? Kwa sababu wako mbele katika kutoa huduma za jamaa kwa watu wa Palestina. Hapa sisemi matendo yao ya kuua maadui zao ni sahihi, ila najaribu kutoa mfano wa jinsi vyama vinavyoweza kushiriki katika shughuli za maendeleo hata kama havina Dola.

Bottom Line: Vyama vya siasa vishiriki bega kwabega katika shughuli za kila siku za maendeleo kwa kadri ya uwezo wao.
 
Watanzania hasa vijana tuna imani kubwa na CHADEMA na ndiyo tumaini la vijana wa sasa na wabadae. Tumeona njinsi vijana walivyokibeba chama hiki kwenye uchaguzi uliopita. Mimi naamini chdema ina nafasi nzuri ya kupewa ridhaa ya kuongoza nchi hii kama itabaki ikiwa MOJA bila kukubali kugawanywa na CCM. Sote tunajua kazi iliyobaki ya CCM nikuhakikisha Chadema haipo mwaka 2015 kwa mbinu zozote. Naamini njia kubwa wanyoiamini CCM ni ile ye kukigawa chama kwa kutumia Mamululi na kuwanunua baadhi ya wanachama na Viongozi wenye ushawishi ndani ya chama.

VIongozi wa Chadema lazima watambue kuwa kuna wakati tulianza kuhisia kuwa kuna viongozi wameshaanza kuonyesha dalili za kununuliwa ili kukiua chama. Kiongozi wa namna hii si mwanamapinduzi wa kweli na wala hana tofauti na mafisadi maana anajali masilahi yake binafisi na hivyo anstahili kurudi kulekule kwa mafisadi. Kiongozi kama huyu atambue kuwa maisha yake ya kisiasa yanaishia si muda mrefu maana vijana hatuko tayari kumuunga mkono kibaraka wa mafisadi.

Zito VS Mbowe, mimi naamini kuwa Zito alipata heshima kubwa kwa watanzania kufuatia uwezo wake wa kujenga hoja bungeni, na kila mtu anaamini kuwa Zito ni mwanamapinduzi na anaweza kupewa hata nafasi ya juu kabisa kataka hii nchi. Kitu kimoja ambacho Zito anaweza kukosea na kujikuta akibaki kuwa mpiga deba tu ni pale anapotaka kukurupuka na kudhani kuwa muda ni mwafaka wa kuwa pale juu. Muda wa Zito kuwa pale juu kwa mtazamo wa wengi ulikuwa bado. Wengi tunampenda Zito na tunamweka kama Risasi ya badae ya CHADEMA ambayo haitaweza kukosea siku bundiki itakapolenga yule mnyama.

CHADEMA ni chama ambacho wananchi wengi na hasa vijana ambao ni endelevu wanamatumaini makubwa na wanahamu kubwa ya kuona kinawapeleka wanakotarajia. Viongozi wote wa CHADEMA akiwemo Zito wanayodhamana kubwa ya kuwatendea watanzania yale wanayotarajia na sikuwakatisha tamaa kwa migogoro ya ndani ya chama. Mimi na watanzania walio wengi tunaamini kuwa Credibility ya Kiongozi ndani ya chadema itatokana na utendaji wa kitimu utakao kifanya chama kiwakombowe watanzania pasipo kujali nani ni yuko juu zaidi au anajua zaidi kuliko mwingine. Viongozi wote wa CHADEMA pasipo kujali wadhifa watapokea taji na nishani zilizotukuka kama wakiongoza chama hiki kwa madhumuni ya kuwakomboa watanzania na si manufaa binafsi.

Napenda Viongozi wa CHADEMA watambue kuwa Watanzania wanakipenda chama cha chadema kwa sababu ya umakini wa viongozi wake kwa ujumla kama timu na siyo mmoja mmoja. Lakini watambue kuwa kama kuna mmoja kati yao andhani anaweza kuwa juu zaidi ya wengine ajue anajidanganya maana siasa inahitaji Team work.

Nakitakia Chama Cha CHADEMA Baraka njema ili kiweze kufikia matarajio ya vijana wa kitanzania. Mungu uwabariki viongozi wa Chadema na uwape busara na ustahimilivu na kuchukuliana na kufanya kazi kwa ajili ya manufaa ya watanzania walio wengi.
 
Wapo wanaoamini kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ndiyo chama mbadala cha kisiasa chenye uwezo wa kushika hatamu ya Uongozi kwa kuunda serikali. Wenye imani hii wanaamini kabisa kuwa CCM imeshindwa kabisa na hivyo ni lazima iondolewe madarakani ili chama kinginge "kipewe nafasi" ya kuliongoza Taifa letu kuelekea kule tunakotaka.

Tukilinganisha uwezo wa watu, rasilimali, historia na mwelekeo kati ya CCM na CHADEMA chama cha CCM kinaiacha CHADEMA kwa mbali sana. Linapokuja swali la mahusiano ndani ya vyama hivyo ni wazi kuwa vyama hivyo vyote havina tofauti sana katika kusababisha migogoro ya ndani, kutumia michakato ya ndani kushughulikia matatizo yao na vile vile kuendesha propaganda dhidi ya kingine.

Hata hivyo tunapoelekea katika Uchaguzi Mkuu ujayo na tukiamua kupima rekodi ya CHADEMA kwa miaka hii karibu 15 iliyopita tunalazimika kujiuliza kama kweli CHADEMA ndicho chama kinachoweza kweli kuliongoza Taifa letu. Na tukiiangalia historia hiyo kwa ukaribu wa miaka hii minne iliyopita tunalazimika kujiuliza kama CHADEMA kimefanya mambo yoyote, kuonesha uongozi katika jambo lolote au kwa namna yoyote ile kuamsha Watanzania katika kujiletea mabadiliko kiasi cha kuweza kustahili mapenzi, imani, na ufuasi wa watu wengi sasa hivi.

Je, yawezekana watu wanaokimbilia CHADEMA sasa hivi au wanaoiamini CHADEMA wanafanya hivyo si kwa sababu ya mapenzi yao kwa CHADEMA ilivyo bali kutokana na chuki yao kwa CCM na utawala wake wa mfumo wa kifisadi kwa miaka 45 iliyopita?

Je, yawezekana katika kutoridhika huku watu wamefumbia mapungufu makubwa ya kimuundo, kiitikadi, kichama na kimwelekeo ya CHADEMA ambayo yanaweza kujitokeza kwa nguvu kubwa endapo chama hicho kitashika madaraka ya nchi na hivyo kuturudisha kwenye "madudu" yale yale ya CCM?

Je, yawezekana kwa kuweka imani pofu (blind faith) kwa kundi la watu ambao wamejithibitisha mara kadhaa kuwa hawajamudu fani na sanaa ya siasa na kuwa ni jopo la watu wenye mtazamo wa kisomi zaidi (elitist) kuliko wa kimwamko wa mabadiliko wanajiandaa kwa kukatishwa tamaa?

Je, yawezekana ndio sababu bado wasomi wengi na watu wengi katika taifa letu bado wanaikumbatia CCM na kuikubali kwa sababu tayari wanajua madudu yake (zimwi likujualo) na hawako tayari bado kuweka imani yao kwa chama hiki au kingine chochote cha upinzani?

Je, yawezekana uongozi wa CHADEMA ulivyo sasa hasa mvutano wa kipuuzi kati ya Freeman Mbowe na Zitto Kabwe ni kikwazo kikubwa zaidi kwa kumuamsha jitu huyu aliyelala (this sleeping giant) kiasi kwamba hawa wawili peke yao kinyume na inavyochukuliwa ndio kikwazo kikubwa zaidi kwa CHADEMA kupiga ile hatua ya lazima mbele? Je, itakuwa bora kama hawa wawili wakaachilia nafasi za juu za uongozi wa Chama ili kukipa chama ule msukumo unahojitajika?

Katika kutafuta majawabu ya maswali haya siyo vyema kwa kweli kuendelea kuikumbatia CCM na madudu yake na kujaribu kuiokoa kwani ndio njia ya haraka ya kuleta mabadiliko ya haraka kuliko kukumbatia upinzani ulivyo sasa?

tupeni ,majibu
 
CCM wamefanya nini zaidi ya kuneemesha wachache kupitia epa ,escrow,ndege mbovu,mabehewa ya tren nk?
 
Back
Top Bottom