Kaa la Moto
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 7,903
- 1,053
Nimepata sononeko ndugu zanguni.Nimekuwa nikufuatilia kwa makini threads na comments humu ndani, nimegundua kuna kaubaguzi humu ndani. Nasema kweli daima, uongo kwangu mwiko. Sijui ni kwa kutumia vigezo gani lakini baadhi ya comments zimekuwa zikifutwa bila sababu ya msingi.
Mathalani, jana katika thread inayosema Slaa na Kauli Tata, zimefutwa comments nyingi sana zikiwemo zangu kadhaa ambamo sijatumia lugha ya matusi wala kashfa. Halafu zimeachwa za wengine zenye lugha isiyo na staha kabisa sasa hapa ndiyo nashangaa kigezo ni nini? Au kwa kuwa anaongelewa SLAA au Mbowe?
Majuzi tena, nilianzisha thread iliyolaani baadhi ya wafuasi wa CHADEMA kuudhalilisha wimbo wa Taifa, few minutes later nashangaa eti imeunganishwa na thread ya mwaka jana sijui juzi inayosema Wimbo wa Taifa ufanyiwe marekebisho! Hivi ni vitu viwili tofauti. Kuufanyia marekebisho wimbo ni jambo moja, na kuudhalilisha wimbo wa Taifa ni lingine kabisa. Isitoshe hilo la marekebisho lilikuwa la mwaka juzi. Na leo kuhusu ya Membe.
Swali langu ni kwamba,, hivi humu ndani ukiigusa CHADEMA basi posts zako zinafutwa na kuunganishwa hovyo hovyo na zingine hata kama haziwiani? Hata kamahii FORUM ni ya CHADEMA, Chama kinachohubiri demokrasia,, basi Demokrasia hii ianzie humu. Tupeni demokrasia ya kutoa maoni pasina kuyafuta.
Kilio kama chako kimeshazoeleka humu. Kwa maneno mengine hujaleta tenzi mpya!