CHADEMA ilipotosha umma taarifa ya Membe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA ilipotosha umma taarifa ya Membe?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mujumba, Mar 18, 2011.

 1. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  chama cha demokrasia na maendeleo pamoja na baadhi ya vyombo vya habari vinalaumiwa kupotosha taharifa ya waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa mh Benard Membe

  Taharifa kamili
  WIZARA ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, imesema baadhi ya vyombo vya habari pamoja na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), vilipotosha taarifa ya Wizara hiyo kuhusiana na chama kinachofadhiliwa ili kuleta machafuko nchini.

  Imesema Waziri Bernard Membe hakutaja jina la chama wala nchi kinachofadhiliwa na nchi za Jumuiya ya Ulaya ili kuleta machafuko nchini.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, John Haule amesema, Serikali itachukua hatua za kidiplomasia chini ya Mkataba wa Kimataifa wa Vienna kuhusu Mahusiano ya Kidiplomasia wa mwaka 1961, ikiwa itathibitisha nchi na chama hicho.

  Haule amesema , Wizara imepokea taarifa za ujumbe wa simu za mkononi unaosambazwa kuwa baadhi ya nchi za Jumuiya ya Ulaya zinatuhumiwa kukifadhili chama cha siasa nchini ili kuleta machafuko na kwamba, raia wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo wanakuwa na wasiwasi juu ya usalama wao.

  “Tumepokea taarifa hizo na tumezipeleka kwenye vyombo vinavyohusika kwa uchunguzi na ikithibitika, Wizara itatoa taarifa,” amesema Haule leo.

  Amesema, katika mkutano wa Waziri Membe alioufanya wiki iliyopita na waandishi wa habari, alijibu suala hilo bila kutaja jina la chama wala nchi inayofadhili, lakini Chadema kiliibuka na kumtaka Membe kuzitaja balozi hizo zinazofadhili chama hicho na kiasi cha fedha kinachotolewa
   
 2. M

  Marytina JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Yakhe ghahawa ina levya?
  Mbona hivyo au hujapata kashata.Wapi kuna mnanda kutajiburudishe hata asubuhi hii?
   
 3. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  TAHARIFA??????????? Ndio mdudu gani?
   
 4. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sijapata ufafanuzi. Ni nini alichosema Membe na waliopotosha walisemaje? Unawezaje kufanya masahihisho bila kutaja kosa lilikuwa lipi na lipi jibu sahihi?
   
 5. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,278
  Trophy Points: 280
  Wameshachanganyikiwa hao, na huyo mwenyekiti wao Mkwere mpaka ikifika December lazima awe mwehu kamili, hiyo ndio laana ya wananchi ilivyo na nguvu, sasa hivi wanaongea kama wehu, haya Mkwere leo anawalaumu maprofesa, wakati ni yeye huyo huyo ndio anawapa vyeo kwenye siasa, unadhani maprofesa wakilipwa vizuri kama wabunge hawawezi kufanya kazi kwa bidii na kwa roho moja?
   
 6. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Jamani tuwe tunaangalia heading zetu kabla ya kupost.
   
 7. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  tumekusikia,tutakufikia
   
 8. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #8
  Mar 18, 2011
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hawa jamaa kweli wamechanganyikiwa. Tulimshuhudia wenyewe kwenye Kioo Mheshimiwa Membe akisema kuwa wana taarifa kuwa kuna nchi moja ya magharaibi inafadhili chama kimoja cha siasa nchini ili kuleta machafuko.
  CDM wametaka Membe ataje hizo Nchi zinazotuhumiwa kufadhili machafuko. Tatizo liko wapi?
  Huwezi ukaamka tu na kudai kuwa kuna tuhuma ya baadhi ya nchi za magharibi kufadhili machafuko bila kutaja nchi zenyewe. Kama ulikuwa unataka kufanya uchunguzi kwanza UNGEKAA KIMYA na kufanya uchunguzi wako kimya kimya kabla hujazomoka hadharani.
  Ilichotaka CDM ni Membe kutoa ufafanuzi wa hizo nchi zinazosemekana kufadhili machafuko. Upotoshaji uko wapi hapo??
  Na mbona hawakuzungumzia kauli ya Mheshimiwa Sophia Simba ambaye aliitaja wazi CDM? Ama na yeye atamtuma Katibu Mkuu wa Wizara yake kuja kumfutia makosa?? Ama kweli Serikali hii kila sasa mtu na lwake!!!
   
 9. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #9
  Mar 18, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Chadema wamezoea sana kuzidisha na kupotosha umma. hao hao walidanganya kuwa Mkuu wa Mkoa Shinyanga amefariki, na hao hao tena jana tu wamezua kuwa magufuri kajiuzulu. Na kesho watasema mengine.

  hakika Chama hiki kimejaa wanafiki na waongo wakubwa sana katika kutaka kuleta balaa nchini.
   
 10. K

  Kikambala Senior Member

  #10
  Mar 18, 2011
  Joined: Jun 28, 2008
  Messages: 163
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wewe usiwe kama pwagu,uzushi huwa unakuwa kama hakuna wa kutoa ufafanuzi wa jambo
   
 11. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #11
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,654
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Wapambe mna nguvu kuliko wenye mali, endeleeni tu kuwatumikia mafisadi lakini mwisho wa siku mtalipa kwa usaliti wenu.
   
 12. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #12
  Mar 18, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  umeona eeh? Sijui source yao ya habari huwa ni ipi? Slaa kipindi cha uchaguzi ashawahi kuzusha kuna contena lenye shahada za kupigia kura limekamatwa mahali,polisi kwenda wakakuta ni uzushi hakuna cha shahada wala nini! Hivi kwanini cdm wanamfeed kiongozi wao habari za uzushi? Hii inafanya watu kukosa imani nao
   
 13. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #13
  Mar 18, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,130
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  duhhhhhhhhhhh kweli watz ni vipofu na viziw
   
 14. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #14
  Mar 18, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hahahaha,we marytina kila nikisoma post yako lazima nikute neno hilo duh
   
 15. M

  Marytina JF-Expert Member

  #15
  Mar 18, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  hilo neno ni aina flani ya dharau huku tabora.Huku ukiitwa yakhe ghahawa vipi humaanisha huna uwezo wa kufikiri unaitaji msaada wa kuzindua fikra zako.
  Mtaani watu wakichoka mwili na akili hutumia kahawa vijiweni hapo husema CUF ni chama cha kisomi zaidi kwani mwenyekiti wake ni professor.Pia husema Pengo Kadinali alikuwa akiingia bungeni kama mbunge maalum alikuwa na kura ya veto ila kwa sasa JK kamzuia.Hoja gani jamaniiiiii upuuzi mtupu
   
 16. h

  hoyce JF-Expert Member

  #16
  Mar 18, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,119
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Uzushi? Kwani kikwete alishinda kwa kura zipi? Mbona mawakala wa vyama na waangalizi hawakuruhusiwa wakati wa kujumlisha kura kitaifa (rejea ripoti ya waangalizi wa EU), pia jiulize kwa nini ilitungwa sheria ya kutopinga matokeo kortini, maana kura bandia walizozizoea zingechambuliwa na uhuni wao kubainika.
   
 17. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #17
  Mar 18, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,508
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Wewe Shanga...... Shangazi or Kashangazi una matatizo gani?? Unawasiwasi kuwa Chadema wanatia kitumbua cha baba mchanga nini??? Try to urgue with your mind to your head!!!
   
 18. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #18
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Umenena, sasa kweli sirikali imechanganyikiwa.
   
 19. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #19
  Mar 18, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Yakhe ghahawa ina levya?
   
 20. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #20
  Mar 18, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,644
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  kama umma haujapotoshwa basi waziri atuambie ni chama gani kinapata hela toka nje...

  tuende kwa evidence
   
Loading...