Hii habari imetolewa na wafanyakazi wa ikulu kwani kuna CDM kwenye ofisi ya rais.Vipi Dr Magufuli kajiuzulu? uzushi mwingine huo.
Hii habari imetolewa na wafanyakazi wa ikulu kwani kuna CDM kwenye ofisi ya rais.Vipi Dr Magufuli kajiuzulu? uzushi mwingine huo.
Jaribuni kutumia akili mlizopewa bure na mwenyezi Mungu. Siku mbili ama tatu kabla ya Membe kuema KUNA CHAMA FULANI kinafadhiliwa na nchi moja ya magharibi, Waziri mwenzake katika Baraza la Mawaziri na mwana CCM mwenzake alitamka wazi kuwa CHADEMA inafadhiliwa na nchi moja ya magharibi ili kuleta machafuko nchini. Kutumia akili uliyopewa na MUNGU ni pamoja na kujumlisha moja na moja ili kupata mbili badala ya kumi na moja! Mawaziri wawili wa Chama tawala wanatuambia kuwa kuna Chama kinafadhiliwa ili kuleta machafuko nchini, mmoja anataja wazi jina la Chama hicho na mwingine anadai kuwa taarifa imepelekwa kwenye vyombo vya usalama ili kupata udhibitisho wa taarifa hizo, akili yako inakuambiaje??? Umeishatafuniwa, basi hata kumeza tu mpaka umezewe??? Za mbayuwayu jumlisha na za kwako!
Mnyika alisema kauli ya membe ina utata maana haijatajwa chama gani kinafadhiliwa. Kwa ilo jamaa,membe,anachanganyikiwa!
Chadema wamezoea sana kuzidisha na kupotosha umma. hao hao walidanganya kuwa Mkuu wa Mkoa Shinyanga amefariki, na hao hao tena jana tu wamezua kuwa magufuri kajiuzulu. Na kesho watasema mengine.
hakika Chama hiki kimejaa wanafiki na waongo wakubwa sana katika kutaka kuleta balaa nchini.
hapo kwenye blue CCMumeona eeh? Sijui source yao ya habari huwa ni ipi? Slaa kipindi cha uchaguzi ashawahi kuzusha kuna contena lenye shahada za kupigia kura limekamatwa mahali,polisi kwenda wakakuta ni uzushi hakuna cha shahada wala nini! Hivi kwanini cdm wanamfeed kiongozi wao habari za uzushi? Hii inafanya watu kukosa imani nao
Sikiliza vizuri kama una upofu wa masikio kauli ya Membe. Ametaja kuna chama kinafadhiliwa ........ lakini hakukitaja jina na mwisho alimalizia tumewaachia vyombo vya usalama kufuatilia hilo na kutoa taarifa kamili.
Kimsingi hakutaja jina na vile vyombo vya usalama vinalifanyia kazi na watatoa taarifa na hatua. Sasa Chadema Pupa za nini, Je hamjui kuwa mnajikanyaga wenyewe, kwanini mna react kama sio nyie.
Acheni ujinga huo, Tuache vyombo vya usalama vifanye kazi yake kiumakini na ufasaha.
Vipi Dr Magufuli kajiuzulu? uzushi mwingine huo.
Sikiliza vizuri kama una upofu wa masikio kauli ya Membe. Ametaja kuna chama kinafadhiliwa ........ lakini hakukitaja jina na mwisho alimalizia tumewaachia vyombo vya usalama kufuatilia hilo na kutoa taarifa kamili.
Kimsingi hakutaja jina na vile vyombo vya usalama vinalifanyia kazi na watatoa taarifa na hatua. Sasa Chadema Pupa za nini, Je hamjui kuwa mnajikanyaga wenyewe, kwanini mna react kama sio nyie.
Acheni ujinga huo, Tuache vyombo vya usalama vifanye kazi yake kiumakini na ufasaha.
Vipi Dr Magufuli kajiuzulu? uzushi mwingine huo.
unajua mkuu kuna msemo unaosema'ukirusha jiwe gizani atakayesema yalaaah ujue limempata" Membe hakutaja chama sasa kwnini cdm wakurupuke?? kwanini TLP,DP ama SAU wasilalamike? au wanajihisi nini? mwaka huu wataglue kweli
sasa kama hakutaja chama nyie mlitakaje? membe kama mwanadiplomasia aliyebobea hawezi kumention jina la chama publically na cdm hawana audacity ya kumfanya ataje jina la chama! wanausalama wanalifanyia kazi hilo na hatua zitchukuliwa! cdm walipasawa wapambane na bi sophia simba aliyewataja hadharani
chama cha demokrasia na maendeleo pamoja na baadhi ya vyombo vya habari vinalaumiwa kupotosha taharifa ya waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa mh Benard Membe
Taharifa kamili
WIZARA ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, imesema baadhi ya vyombo vya habari pamoja na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), vilipotosha taarifa ya Wizara hiyo kuhusiana na chama kinachofadhiliwa ili kuleta machafuko nchini.
Imesema Waziri Bernard Membe hakutaja jina la chama wala nchi kinachofadhiliwa na nchi za Jumuiya ya Ulaya ili kuleta machafuko nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, John Haule amesema, Serikali itachukua hatua za kidiplomasia chini ya Mkataba wa Kimataifa wa Vienna kuhusu Mahusiano ya Kidiplomasia wa mwaka 1961, ikiwa itathibitisha nchi na chama hicho.
Haule amesema , Wizara imepokea taarifa za ujumbe wa simu za mkononi unaosambazwa kuwa baadhi ya nchi za Jumuiya ya Ulaya zinatuhumiwa kukifadhili chama cha siasa nchini ili kuleta machafuko na kwamba, raia wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo wanakuwa na wasiwasi juu ya usalama wao.
Tumepokea taarifa hizo na tumezipeleka kwenye vyombo vinavyohusika kwa uchunguzi na ikithibitika, Wizara itatoa taarifa, amesema Haule leo.
Amesema, katika mkutano wa Waziri Membe alioufanya wiki iliyopita na waandishi wa habari, alijibu suala hilo bila kutaja jina la chama wala nchi inayofadhili, lakini Chadema kiliibuka na kumtaka Membe kuzitaja balozi hizo zinazofadhili chama hicho na kiasi cha fedha kinachotolewa
CCM kuwa waongo hakujustify CDM kupapatika na kudanganya!!!!
au unataka kusema uongo wa CDM una upako?
conclusion ya Membe ni kuwa vyombo vya usalama vinafuatilia na mwisho vitatoa majibu. kwa maoni yangu hakukuwa na haja ya CDM kulalama labda wangeishia tu kupambana na Sophy na kuacha habari ya Membe kuwa hawahusiki period
Viongozi wa CCM akiwamo Sophia Simba na Lipumba ndio walioitaja Chadema moja kwa moja na maswali ya waandishi yalilenga kwa Waziri Mhusika na Mambo ya Nje kutaka kujua kama ni sahihi kwa viongozi wa serikali kama Sophia Simba kuzungumzia mataifa ya nje kufadhili machafuko kupitia chama cha siasa alichokitaja, sasa Membe kwa kuwa aliyesema ni Waziri asingeweza kusema Waziri mwenzangu ni mwongo, bali alijibu kidiplomasia kwamba tutachunguza na ikithibitika tutatumia mikataba ya kimataifa kulishughulikia. Kwa upande wa Chadema kama chama cha siasa ambacho ndicho kunahusishwa na vurugu (rejea hotuba ya Rais) ndio wanaoamini (ni kweli) kwamba walengwa ni wao na hivyo kumtaka Waziri MWenye dhamana na mambo ya nje, ambaye ni Membe kutaja chama na nchi maana wanamuona Sophia Simba, kama mropokaji ambaye maneno yake hayawezi kubeba uzito unaostahili. Kwa mantiki hiyo, Membe hajakosea (Kwa maoni yangu) kwa kuwa yuko serikalini (Ambayo JK ni bosi wake na Sophia ni mwenzake) na Chadema nao hawajakosea maana ni chama cha siasa ambacho kimeonyesha kupambana hadi kuonekana kama chama cha fujo (kama ilivyokuwa CUF enzi zake).
- Kama Membe ni Waziri basi ni Decision Maker, maana yake jambo lolote linamfikia katika hatua ya mwisho kabisa ili kufanyike maamuzi kutoka na uchambuzi uliofanywa na wataalam wa Serikalini, kwa swala hili alipaswa kujitokeza kuongea baaada ya kupata taarifa sahihi kutoka katika vyombo vyote na hapo kama Decision Maker alikuwa anakuja kutoa maamuzi juu ya hili jambo na jinsi walivyolifanyia kazi na ushahidi uliopo na nini Serikali imeamu yaani Msimamo wa Serikali.
Chadema wamezoea sana kuzidisha na kupotosha umma. hao hao walidanganya kuwa Mkuu wa Mkoa Shinyanga amefariki, na hao hao tena jana tu wamezua kuwa magufuri kajiuzulu. Na kesho watasema mengine.
hakika Chama hiki kimejaa wanafiki na waongo wakubwa sana katika kutaka kuleta balaa nchini.