MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,565
- 836
Tunasukumiziwa katika makoo yetu chama kimoja tu kuwa ndicho pekee chafaa kuungwa mkono katika kuiangusha CCM. Tunaambiwa vyama vingine viungane nacho kwa sababu kimeonesha uongozi na kuwa ndiyo "upinzani" wa kweli. Wapo watu wanaoamini kabisa jambo hili. Wanaamini kuwa CHADEMA ndicho chama hasa mbadala kinachoweza kuchukua uongozi wa taifa letu toka mikononi mwa CCM.
Kama nilivyouliza huko nyuma ni mambo gani Chadema wamefanya kustahili kuongoza leo naomba nidokeza swali hili ambalo ni muhimu.
Je Chadema ilivyo sasa iko tayari kuongoza taifa la watu milioni 40 kwa ubora na kwa maono bora zaidi na mfano mzuri wa kiuongozi katika ngazi zote kuliko CCM? Ni nini msingi wa imani ya wale wanaoona kuwa iko tayari?
Mwenyewe ni na maoni yangu.. naomba nisikie ya kwenu.
Ukiwa makini utaona swali linahusu Chadema na utayari wao kuongoza.. nje ya hapo ni red herring.
Hakuna chama cha upinzani ambacho kipo tayari kuongoza iwe Chadema, CUF au hata CCJ. Upinzania haipo tayari kuongoza si kwa sababu hawana viongozi wazalendo wenyewe uwezo na nia ya dhati bali kutokana na mfumo uliopo. Kabla upinzani haijaweza kuongoza nchi ni lazima wawe wame jijengea nguvu Bungeni kiasi cha kupata wabunge wa kutosha. Hamna chama Tanzania kinacho weza kuongoza kikamilifu bila majority bungeni.
Kufafanua zaidi hoja yangu ngoja ngoja nitoa statistics na mifano. Katika Bunge la sasa CCM ina viti 206 wakati CUF ina 19, Chadema 5, kimoja kwa TLP na UDP(IPU PARLINE database: UNITED REPUBLIC OF TANZANIA (Bunge ), Full text). Ina maana hakuna chama cha upinzani chochote chenye hata "strong minority" na leo hii hata vyama vya upinzani vyenye wabunge viungane watakua na wabunge 26 tu dhidi ya 206 ya CCM. Hii ndiyo composition ya Bunge letu kwa sasa na sidhani kama 2010 composition hii ita badilika sana......
Sasa nitoe mfano wangu. Tuassume Chadema ina baki na wabunge wake watano na tuassume mgombea wao wa uraisi anashinda. Je raisi huyo wa Chadema ata ongozaje na wabunge watano tu Bungeni? Kwa vile raisi anaweza kuteua wabunge wachache tuseme idadi hiyo ina panda mpaka 10. Ata pitishaje sheria na mabadiliko anayo taka? Hata awe na coalition ya wabunge wapinzani bado hana asilimia ya kufanya chochote Bungeni. Pia kwa sheria za Tanzania mawaziri tu wa serikali lazima watoke bungeni. Je raisi huyo ataweza hata kuunda baraza la mawaziri na kuteua wasaidizi kutoka chama chake? Waziri mkuu ni lazima atoke kwenye chama chenye majority bungeni kwa hiyo waziri mkuu ambae ndiyo msaidizi mkuu wa raisi na kiongozi wa serikali bungeni hata kua wa chama chake. Barabara zote katika mfano huu zinaelekea kwa Chadema kuomba msaada kutoka chama kitakacho kua na nguvu bungeni na chama hicho kwa hali ya sasa inaelekea kuwa ni CCM. Kwa hiyo utawala utabaki wa CCM, serikali itabaki ya CCM, Bunge litabaki chini ya CCM.
Nime tolea mfano Chadema kwa vile mada ni kuhusu Chadema lakini ukweli una baki pale pale kwa hata iwe CUF, CCJ, TLP, UDP nk wata kumbana na hali hiyo hiyo. Kabla chama hakija wazia kutoa raisi ni lazima wajiimarishe bungeni. Rasilimali na nguvu nyingi za upinzani zinge wekezwa katika kuimarisha idadi ya wabunge wa upinzani. Kama chama haki wezi kufikisha hata asilimia 25 bungeni ita kuaje na umaarufu wa kutosha wwa kutoa raisi? Vyama vyote vya upinzani pamoja na "die hard" fans wao na uongozi wenyewe wana kosea katika priorities zao. Chama cha upinzani kwa sasa kina hitaji kiongozi ambae atajua njia na jinsi ya kweli ya kuimarisha chama kwa siku za mbeleni na si viongozi wa sasa ambao wao wana wazia kugombea uraisi tu, uraisi ambao hawawezi kupata, uraisi ambao hawata weza kutumia kikamilifu hata washinde.