CHADEMA ijibu hoja ya msingi ya Peter Lijualikali

CHADEMA ijibu hoja ya msingi ya Peter Lijualikali

Watamwita msaliti
Hawataki Kabisa kuangalia mapungufu ya chama

Haiwezekani wabunge zaidi ya 20 wakukimbie uwaite Wasaliti lazima kuna tatizo
Sure mkuu,

Mi nadhani ni wakati wa CHADEMA kuja na majibu sahihi. Waache kukwepa kwepa. Kama wamekosea waseme tu. Watajijengea credibility kubwa kuliko kumwita kila anayehama msaliti
 
Naona umerukia kwingine tena. Mf Bungeni, wabunge wanapohoji matumizi ya fedha za walipa kodi, huwa wanasubiri reports za CAG?
Kwenye vikao vya chama, wabunge/wanachama kuhoji matumizi ya fedha zao mbali na ruzuku ya chama ni kosa kiasi wasubiri report ya CAG? Jaribu kufikiria kidogo hapa.

Nakumbuka report ya CAG 2017/2018 kwa Chadema ilionyesha upotevu wa fedha, karibu billions kadhaa (sina kumbukumbu vizuri). Unataka kunambia baada ya hiyo report, wao kama wabunge na wanachama wa Chadema hawakupaswa kuhoji huo upotevu wa pesa?.
Hitimisho langu:
Chadema kama chama kama kinashindwa kujiwajibisha chenyewe sababu ya udikiteta uliokithiri, basi watulie tu kuliko kutumia nguvu kubwa kumuona Lijuakali na wabunge wengine wa Chadema kuwa ni wabaya nk kwa kuonyesha madhaifu ya chama chao.

Sent using Jamii Forums mobile app

Huwa wanapotuhumu nakuhoji haipiti kirahisi tuuu bila sheria kufatwa.

Je unafahamu taratibu zinazofuatwa na hatua zinazochukuliwa kisheria?

1. Mbunge huwajibika kutoa ushahidi wa kisheria kuthibitisha madai yake. Akishindwa hupewa adhabu na wengi wamekubwa na uropokaji wakashindwa kuthibitisha. Lijuwalikali anaweza kuwa mmoja wao

2. Kamati huundwa ya kibunge kuchunguza na kukusanya ushahidi kisheria nakuuleta bungeni kuthibitisha au kukanusha

3. Riport za ukaguzi hususani CAG hutumika kuthibisha tuhuma.

Swali

Katika madai yenu mmetumia utaratibu upi?
 
Uzuri tu ni kwamba hao watetezi wa leo ndo waombolezaji wa kesho.

Kipindi Wangwe anahoji haya akina Zito walikuwa wapiga "zumali" wa Mbowe,leo wapo wapi?

Kipindi Zitto yupo kibra baada ya kuhoji vifungu vya sheria kuondolewa kihuni kina Slaa walidhani hayawahusu,leo wapo wapi?

Kina Lijuakali,Silinde ni sehemu tu ya chain hii na hata hawa wapiga vinubi na mapambio wa leo mtakuja kutubania pua wenyewe bila hata kuwauliza.

I HATE DEADLINES!!
 
500,000 kwa mbunge kila mwezi

500,000 x 71MPs x 12months x 5yrs =2.13Billion

Nauliza tu ni hiyo laki 5 tu mlikuwa mnakatwa kila mwezi au kuna michango zaidi ya hapo?

Nimesikia ilifikia 8 billion!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunaomba nakala za barua ya Mh. Lijualikali za malalamiko yake kwa chama ili zitumike kama Ushahidi.

Tutaomba pia nakala ya majibu ya Chama kwenda kwa Mhe. Lijualikali ili yadhibitishe uhalali wa alichosema Mhe. Lijualikali
 
Kuna maswali ambayo kiuhalisia CHADEMA wanatakiwa kuyajibu na sio kukimbia kimbia. Hili suala la Lijualikali CHADEMA watoke hadharani walijibu na sio kujificha kwenye kichaka cha wasaliti
 
Kuna maswali ambayo kiuhalisia CHADEMA wanatakiwa kuyajibu na sio kukimbia kimbia. Hili suala la Lijualikali CHADEMA watoke hadharani walijibu na sio kujificha kwenye kichaka cha wasaliti

Tangu lini umbeya ukajibiwa?

Yaani unamjibu mzushi asie na reference yoyote? Utakuwa mwehu.
 
Ila mwanaume kulia huku kwetu Ukuriani ni umama kweli ..... yaani kalia kweli au alikuwa anaekti kama marehemu mzee Majuto
 
Tokea Lijuakali atoe hoja yake juu ya chama chake Cha Chadema baadhi ya wafuasi wa Chadema wametokea kupotosha hoja ya msingi ya Bwana Lijualikali sijajua ni kwasababu ya uchama wao au kukwepa kwa makusudi hoja ya Lijuakali.

Lijuakali ajalalamika kuhusu kuchangishwa pesa Kama wanavyodai wapenzi wa Chadema Bali anahoji matumizi ya michango ya pesa wanayochangishwa nanukuu " Tuliambiwa fedha zetu zitawekwa kwenye fixed account kwa ajili ya uchaguzi huu lakini tukahoji mbona mpaka sasa mjaweka wakasema zimeisha tukawauliza hamjengi ofisi za chama, hakuna shughuli yoyote ya siasa inayoendelea hizo hela zimeishaje wakatujibu hatutakiwi kuhoji chama"

Kwa sisi ambao hatuna itikadi ya hivi vyama au kuwa wapenzi wa vyama hivi Tanzania tungependa Chadema wajibu hoja ya msingi ya Peter Lijualikali kuliko kukwepa

#Tanzaniabilaushabikiwavyamainawezekana
Yeye si mwanachama anahoji vipi? Na kama kulikuwa na makubaliano kwa maandishi atazipata hata kwa mahakamani ukiwa mroho usiwe mchoyo ukishatoka chama huwezi dai mchango uliochangoa chama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tokea Lijuakali atoe hoja yake juu ya chama chake Cha Chadema baadhi ya wafuasi wa Chadema wametokea kupotosha hoja ya msingi ya Bwana Lijualikali sijajua ni kwasababu ya uchama wao au kukwepa kwa makusudi hoja ya Lijuakali.

Lijuakali ajalalamika kuhusu kuchangishwa pesa Kama wanavyodai wapenzi wa Chadema Bali anahoji matumizi ya michango ya pesa wanayochangishwa nanukuu " Tuliambiwa fedha zetu zitawekwa kwenye fixed account kwa ajili ya uchaguzi huu lakini tukahoji mbona mpaka sasa mjaweka wakasema zimeisha tukawauliza hamjengi ofisi za chama, hakuna shughuli yoyote ya siasa inayoendelea hizo hela zimeishaje wakatujibu hatutakiwi kuhoji chama"

Kwa sisi ambao hatuna itikadi ya hivi vyama au kuwa wapenzi wa vyama hivi Tanzania tungependa Chadema wajibu hoja ya msingi ya Peter Lijualikali kuliko kukwepa

#Tanzaniabilaushabikiwavyamainawezekana
Chadema haiwezi kulazimishwa kujibu hoja lijua kwa shinikizo lako wewe maana CCM ya Chadema watamaliza wenyewe nilitegemea ulete hoja ya mwenzenu kukutwa na silaha kule Shinyanga
 
Hana reference . ? Yaani aliyekuwa akikatwa mshahara kwa ajili ya hitaji husika hana reference . ?

Jamani tuacheni shabiki. Vitu vingine viko wazi kabisa

Hebu tuwekee japo page moja ya ushaidi na uwe umethibitishwa na chombo chochote cha kisheria hapa Tanzania.
 
Hebu tuwekee japo page moja ya ushaidi na uwe umethibitishwa na chombo chochote cha kisheria hapa Tanzania.
Mkuu nina mashaka kama unaijua system of justice.

Tuhuma ikitolewa, anayekutuhumu anakuwa na reasonable doubt sasa ni jukumu la mtuhumiwa mwenyewe kuja na reasonable doubt yake kuipinga ile ya awali. Na hiki ndicho kinachopaswa kufanywa na chama smart na sio kuwatoa watu kwenye hoja eti weka ushahidi. CHADEMA ndio waje na ushahidi kwa sababu mtoa tuhuma alikuwa insider wao
 
Atajibiwa kama atafuata utaratibu mzuri was kuhoji. Bungeni sio sehemu ya kuhoji mapato na matumizi ya Chama. Ni nidhamiu ya wapi hiyo, hata CCM mnafundishwa hivyo? Kumhoji mwenyekiti mapato na matumizi ya Chama

Katika siasa busara inatakiwa itangulie unless unabaki kituko kwa wajuzi was siasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cdm haiwez kulazimishwa kujibu hoja lijua kwa shinikizo lako ww maana ccm ya cdm watamaliza wenyewe nilitegemea ulete hoja ya mwenzenu kukutwa na silaha kule shinyanga
Umenikumbusha kitu
FB_IMG_1588949324380.jpeg

In God we Trust
 
Back
Top Bottom