CHADEMA ijibu hoja ya msingi ya Peter Lijualikali

CHADEMA ijibu hoja ya msingi ya Peter Lijualikali

Tokea Lijuakali atoe hoja yake juu ya chama chake Cha Chadema baadhi ya wafuasi wa Chadema wametokea kupotosha hoja ya msingi ya Bwana Lijualikali sijajua ni kwasababu ya uchama wao au kukwepa kwa makusudi hoja ya Lijuakali.

Lijuakali ajalalamika kuhusu kuchangishwa pesa Kama wanavyodai wapenzi wa Chadema Bali anahoji matumizi ya michango ya pesa wanayochangishwa nanukuu " Tuliambiwa fedha zetu zitawekwa kwenye fixed account kwa ajili ya uchaguzi huu lakini tukahoji mbona mpaka sasa mjaweka wakasema zimeisha tukawauliza hamjengi ofisi za chama, hakuna shughuli yoyote ya siasa inayoendelea hizo hela zimeishaje wakatujibu hatutakiwi kuhoji chama"

Kwa sisi ambao hatuna itikadi ya hivi vyama au kuwa wapenzi wa vyama hivi Tanzania tungependa Chadema wajibu hoja ya msingi ya Peter Lijualikali kuliko kukwepa

#Tanzaniabilaushabikiwavyamainawezekana

IMG_3556.JPG
mengine akamuulize mteule wa rais CAG atamweleza



Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hujaelewa kabisaa msingi wa hoja

Nataka uniambie kisheria na kikatiba nani anamamlaka ya kukaguwa na kutoa majibu sahihi ya matumizi ya fedha za umma?

1. Lijuwalikali?
2. CAG ?

Ukinijibu jiandae na maswali yatakayofata
Nilitaka kuandika jambo kumbe umeshaandika, kuna viumbe wanapenda sana kujidanganya, yani CAG yupo, anakagua, na majibu anatoa ya kuridhisha, lakini bado kuna vipofu wengine watakwambia viongozi CDM wajitokeze kuzungumzia hii issue, wajitokeze ili iweje kama CAG tayari keshawapa majibu!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usimlishe huyo zumbukuku maneno,alichojibiwa na akatamka ni kwamba aliambiwa uchaguzi ni mchakato,kama hujui na yeye hajui wote ni mazumbukuku mzungu wa reli,uchaguzi si kampeni,kampeni ni matokeo ya mchakato,ndio maana mshindi kura za maoni anaweza achwa akateuliwa aliyefuatia,upo?,mpo,?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa ahamie ccm ambako mpaka leo
Deep green
Kagoda
Epa
Escrow
1.5t
Gas
Makinikia
Nk vimetumika vizuri zaidi

Nchambi na meno ya tembo yupo nje

Mdogo wake rostam na meno ya tembo yupo nje

Kama wizi wa ccm unajustify wizi wa chadema mnapigaga kelele za nini?
Maana hata mchungaji Leo anakiri alimsingizia kinana hajaiba sasa unaiminije huo wizi wa 1.5?
 
Umenijibu au unaendeleza hoja niliyotoa?
Ukimsikiliza vizuri Peter Lijuakali amesema hiv akihojiwa na global online tv amesema Kuna michango ipo ndani ya katiba ila Kuna michango mengine wameambiwa wachangie Ni nje ya katiba ambayo ndo yeye na baadhi ya wabunge wa Chadema ndo wanaoihoji kuhusu matumizi yake na Wana haki hiyo kwasababu ipo nje ya kikatiba na lengo la kuhoji Ni baada hela zinazochangishwa kuona zinaisha haraka bila wao kuona matumizi yake yakoje
 
Huwa wanapotuhumu nakuhoji haipiti kirahisi tuuu bila sheria kufatwa.

Je unafahamu taratibu zinazofuatwa na hatua zinazochukuliwa kisheria?

1. Mbunge huwajibika kutoa ushahidi wa kisheria kuthibitisha madai yake. Akishindwa hupewa adhabu na wengi wamekubwa na uropokaji wakashindwa kuthibitisha. Lijuwalikali anaweza kuwa mmoja wao

2. Kamati huundwa ya kibunge kuchunguza na kukusanya ushahidi kisheria nakuuleta bungeni kuthibitisha au kukanusha

3. Riport za ukaguzi hususani CAG hutumika kuthibisha tuhuma.

Swali

Katika madai yenu mmetumia utaratibu upi?

Kukusaidia hapo kwa CAG, ni kwamba CAG anakagua pesa za uma.

Kwa hiyo akienda kufanya ukaguzi CDM anaenda kukagua matumizi yanayotokana na fedha za ruzuku.

Kuhusu vyanzo vingine vya fedha ni uamuzi wa chama kutafuta mkaguzi kwa ajili ya kujiridhisha.
 
Kukusaidia hapo kwa CAG, ni kwamba CAG anakagua pesa za uma.

Kwa hiyo akienda kufanya ukaguzi CDM anaenda kukagua matumizi yanayotokana na fedha za ruzuku.

Kuhusu vyanzo vingine vya fedha ni uamuzi wa chama kutafuta mkaguzi kwa ajili ya kujiridhisha.

Tundu Lissu

Hili la CHADEMA na tuhuma dhidi ya Mwenyekiti Mbowe jibu lake hili hapa:

Haya malalamiko sio ya jana na sio ya juzi; na sio ya mwaka jana wala mwaka juzi. Tangu nimeingia CHADEMA mwaka 2004, kila kiongozi ambaye ameondoka CHADEMA na kujiunga na CCM amehalalisha kuondoka kwake kwa kutoa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za chama.

Sio Lijualikali na Silinde na Mwambe wa leo tu. Kila kiongozi - kuanzia marehemu Amani Walid Kabourou na Chacha Wangwe na kuendelea - amelalamikia matumizi mabaya ya fedha za chama pale anapoondoka kwenye Chama. Na mgomvi wao wa miaka yote ni Mwenyekiti Mbowe, sio Dr Slaa au Dr Mashinji waliokuwa Makatibu Wakuu wa Chama wa hivi karibuni.

Cha ajabu ni kwamba hakuna hata mmoja ambaye amewahi kuthibitisha madai yao haya. Ajabu nyingine ni kwamba wanatoa tuhuma wakati wa kuondoka kwenye Chama tu. Wakati wakiwa ndani hakuna shida.

Fedha za chama cha siasa ni fedha za umma; ndio maana hukaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kila mwaka. Ndio maana hukaguliwa pia na wahasibu huru na mahesabu hayo hupelekwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kwa ukaguzi zaidi.

Ubadhirifu au matumizi mabaya ya fedha hizo ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria za nchi yetu. Mwenye kutenda makosa hayo alipaswa na anapaswa kuchukuliwa hatua za kijinai kwa mujibu wa sheria za nchi yetu.

Sasa kama Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu na Msajili wa Vyama vya Siasa na wahasibu wa kujitegemea hawajawahi kuona huo ubadhirifu au matumizi mabaya fedha, hawa wanaolalamikia jambo hili, hasa wanapoelezea sababu za kuondoka kwenye Chama na kujiunga na CCM wanawezaje kuwa taken seriously???

Kwa nini hamuwaulizi hata uthibitisho wa tuhuma hizo, kama sio kujaribu kuficha sababu halisi za kukimbia kwao kwenye Chama???

Kwa jinsi ambavyo mamlaka za Serikali ya Magufuli na ya Kikwete kabla yake ambavyo zimekuwa zinatuchukia, kama kweli kungekuwa na ubadhirifu tunaotukanwa nao miaka yote hii, tungeshafungwa wote zamani. Huyu Mbowe si angeshaozea gerezani???

Badala yake, tumekuwa Chama Kikuu cha Upinzani katika nchi yetu licha ya matusi yote haya na licha ya uonevu mkubwa ambao tumeendelea kufanyiwa. Tunasonga mbele.

Kuhusu Wabunge kuchangishwa michango mbali mbali. Tofauti na CCM ambayo huchotewa pesa za serikali na za wafanya biashara wanaohitaji tender au leseni mbali mbali, CHADEMA imejengwa kwa michango ya wanachama, hasa Wabunge.

Wabunge wa CHADEMA miaka yote wamechangia fedha, magari na muda wao kwa ajili ya shughuli za Chama. Ndio maana tumeweza kupata Wabunge, madiwani na Wenyeviti wa Vijiji na Mitaa wengi. Hawa akina Lijualikali na wenzake wanaolalamika sasa hivi, walipatikana kutokana na michango ya Wabunge waliokuwapo kabla yao.

Nimemsikia akidai kwamba alichangiwa na wananchi wake tu. Ni mwongo. Mimi mwenyewe nimemchangia kwa fedha, mali na muda wangu. Nimekwenda kumfanyia kampeni za uchaguzi wa Diwani wa Kata ya Ifakara mwaka '13 kwa gharama zangu mwenyewe.

Nimemsaidia kesi ya Ubunge wakati hawa maswahiba zake wa sasa walipojaribu kumvua Ubunge wake kihuni. Nimemsikia akilia Bungeni kwamba alifungwa jela miezi sita kwa uonevu kwa ajili ya CHADEMA.

Hakusema ukweli wote. Hakusema nani aliyemhangaikia Mahakama Kuu kwenye rufaa mpaka akatoka gerezani. Mimi sio tu nilimtetea mahakamani; nilienda kumwona gerezani Ukonga na kumfariji. Baba yake mzazi ni shahidi yangu.

Hakusema kama alisaidiwa na chama au na sisi wanachama wenzake. Hawezi kusema amewahi kutulipa au kuwalipa hao waliomsaidia kiasi gani cha pesa. Hakusema na hatasema kwa sababu anajua jinsi ambavyo Chama chake na wanachama wenzake walivyombeba.

Sasa amepanda bei anaomba CCM wampe kazi. Wale wale waliomfunga na kumnyanyasa na kumdhalilisha mara nyingi, sasa ndio maswahiba zake. Sisi tuliomsaidia kwenye shida yake hatuna maana tena. Hamna shida. Tunasonga mbele.

Nilichokisema kuhusu Lijualikali linawahusu Wills Lwakatare na Cecil Mwambe na David Silinde. Wamebebwa na chama na viongozi na wanachama. Sasa Chama hakiwababaishi tena.

Siwezi kuwaambia wakumbuke walikotoka, maana hawatakumbuka. Nawasihi wajiulize walikoishia waunga juhudi za Rais wengine wote wa miaka ya nyuma.8
 
Mke ulieishi naye miaka kadhaa ukazaa naye watoto ikatokea hitirafu akajipendekeza kwa danga, kabla ya kupokelewa na hilo danga jipya akatangaza kuwa hudindishi na hapo bado hata hajalala na hilo danga sasa wewe kama mwanaume unaejitambua mtu katoka kwako unamjua inside out inamaana nawewe utakuja hadharani uudindishie umma kwamba anachokisema huyo mwanamke ni uongo?
 
Back
Top Bottom