Chama, Mwangos ni mwandishi wa habari. Kazi ya uandishi wa habari pamoja na nyingine ni kuripoti matukio. Narudia ni kuripoti matukio. Kwa maana hiyo Mwangos akiwa mwananchi mwajiriwa alikuwepo kazini kama mtumishi mwingine akitafuta mkate wa siku kwa njia halali kama mtu mwingine.
Hakukuwa na kosa yeye kuwepo katika 'mkusanyiko' usio halali kwasababu kazi yake ni kuelezea umma kuhusu kukosekana kwa uhalali wa mkutano nani amefanya nini n.k.
Kusema angekaa nyumbani yasingemkuta nadhani ni kumdhalilisha na kuudhalilisha utu wa mwadamu kiwango dah..
Ukiangalia picha, hivi Chama unaweza kuamini kuwa Polisi sita wenye silaha wameshindwa kumdhibiti Mwangos na kumfungulia mashtaka hadi wamuue kwa kitu cha namna ile!
Mkuu Nguruvi3
Labda nikuulize Mwangoso (R.I.P) alikuwa pale kama kamanda na mwanaharakati au kama mwandishi wa habari? Ukinijibu ndio nitakupa majibu majibu yako
Chama
Gongo la mboto DSM