CHADEMA Iitishe Maandamano dhidi ya Jeshi la Polisi?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
POLISI%2B2.JPG

Kwa miaka sasa CDM wamekuwa wakionewa, kunyanyaswa na kukandamizwa na jeshi la polisi la Tanzania linaloongozawa na IGP Said Mwema. Na kwa miaka sasa CDM imekuwa ikitoa hutuba za motomoto kilaa wanachama au mashabiki wake wanapouawa na jeshi hilo huku viongozi wake wakinyanyaswa (mnakumbuka Mbowe alivyobebwa kwa ndege ya jeshi kupelekwa Arusha?). Sasa imekuwa ni tabia kuwa CDM hawawezi kufanya maandamano au mkutano wowote wa kisiasa bila kufikiria polisi watafanya nini 'this time'.

Jeshi la Polisi (kuanzia juu hadi chini) limeendelea kuwachukulia CDM with contempt; haliamini wana haki yakupinga serikali na kwa hakika linaamini linaweza kuwanyamazisha ilimradi tu. Matokeo yake CDM wako chini ya huruma ya jeshi la polisi. Makala hii ya Februari 2012 iligusia kitu hicho hicho: Bwagamoyo: Polisi wataendelea kutuua mpaka lini? Kuna haja ya kufanyika kitu.

a. CDM iache kulionea aibu jeshi la polisi na mchezo wao huu wa kuwahutubia polisi kwenye mkutano yao. Wakati umefika wa kuanzisha maandamano dhidi ya jeshi la polisi na uongozi wake wa juu ili kutaka kina Mwema, Chagonja na wenzake waondolewe kwani ni watuhumiwa nambari moja hawa wa uvunjaji wa haki za msingi za raia!

b. Maandamano haya yawe na lengo la kuonesha dunia juu ya ukatili wa jeshi letu la polisi kwa raia.

c. CDM waliambie taifa mapema kabisa na viongozi wote wa polisi wajue kuwa itakapoingia madarakani kazi ya kwanza itakuwa ni kulivunja jeshi la polisi na kuliunda upya. Katika kulivinja kuna viongozi ambao watashtakiwa kwa yale anbayo wanayafanya sasa dhidi ya raia. Viongozi wa polisi wajue kabisa kuwa "nilikuwa nafuata amri" siyo utetezi pale maisha ya wananchi yanatoweshwa. Watanzania wajue kabisa kuwa jeshi lao la polisi linahitaji kuvunjwa siyo kufanyiwa tu marekebisho. CDM angalieni ilani yenu inasema nini kuhusu jeshi la polisi!!!

Ikumbukwe kuwa wafadhili wamekuwa wakitoa misaada mingi kwa jeshi la polisi vikiwemo vile vya mafunzo, silaha na vifaa. CDM imulike wafadhili hawa vile vile!! Iweje waendelee kufadhili jeshi linalokandamiza upinzani wa kisiasa nchini.

Nitadharau nikisikia tena viongozi wa CDM wanazungumzia mambo yale yale, kuhusu jeshi lile lile na kwa namna ile ile!! hawatokuwa tofauti na watawala wa sasa!
 
napita naweza fungiwa maisha nina hasira hawa police dawa yao ipi jikoni wewe subri

Napita Thanks MMJ
 
Mi sioni haja ya CDM kuwaambia yote hayo polisi maana itakuwa kama ni mkwara.
Dawa ni kufanya vitendo. CDM iwe na subira mpaka hapo itakapoingia madarakani kisha iwashughulikie vibaraka wote wa polisi wanaotumiwa kwa maslahi ya watu wachache.
Waanze na shemeji yake rais (Said Mwema) kisha ma'RPC na wengine wa chini yao.
 
Bwagamoyo:polisi wataendelea kutuua mpaka lini?

Saturday, 25 February 2012 18:05

Na. L. W. Nzela

KWA mara nyingine raia wasio na silaha wameuawa mikononi mwa Polisi na kwa mara nyingine ni wao wanalaumiwa kwa vifo vyao.

Kwa mara nyingine jeshi hili chini ya Said Mwema, limeendelea kuona uhai wa Watanzania kuwa ni kitu cha kuzima kama utani bila ya kuwajibishwa yeyote.

Kwa mara nyingine makala hii itaonekana ni ya kupandikiza chuki kwa sababu inanyoshea kidole moja kwa moja Jeshi la Polisi kuwa kwa ujumla wake limepoteza weledi wake, halijali haki za raia wala haki za binadamu. Lina maofisa ambao vidole vyao vinawashwa kuua!

Yaliyotokea Songea siku ya Jumatano hayawezi kutetewa kwa namna yoyote ile. Kwamba, wananchi wanaoandamana kupinga mauaji ya wananchi katika mazingira ya kishirikina wao wenyewe wanauawa ni kashfa ndani ya kashfa.

Naweza kusema pasi ya shaka kuwa watu wengi wanaouawa kwa kutumia silaha za moto (bunduki) nchini, wanakufa kwenye mikono ya polisi au vyombo vya usalama.

Ni mara chache sana kuwaona raia wanauana kwa kutumia bunduki. Hii ni kinyume na nchi kama Afrika ya Kusini, Honduras, Jamaica au hata Marekani ambapo mauaji ya silaha za moto, hutokea mikononi mwa raia wenyewe.

Tatizo ni fikra za kikoloni

Napendekeza kwamba, mojawapo ya makosa makubwa ya nchi yetu ni kupokea Jeshi la Polisi lililoundwa kulinda utawala wa kikoloni na kulifanya kuwa jeshi la polisi la kuwalinda wananchi.

Jeshi la Polisi la mkoloni lilikuwa na jukumu la kuhakikisha wakoloni wanaishi katika hali ya utulivu na amani na raia wao nchini hawabughudhiwi na wenyeji. Wananchi wetu walikuwa wakiliogopa jeshi hilo kwani halikuwa la kwao na halikuwa rafiki kwao.

Profesa Issa Shivji akiandika katika kazi yake mojawapo ya A Study of Police Powers and Political Expression (REDETt, 2001) anasema kwa Kiingereza kuwa, "The police force in Tanzania is the creation of the colonial period, particularly of the British". Yaani "Jeshi la Polisi la Tanzania limetoana na enzi za wakoloni, hususan Waingereza".

Akielezea sifa za jeshi la mkoloni Shivji anasema kuwa lilikuwa na sifa zifuatazo
• Linawajibika kwa mtawala;
• Limepangwa kwa vyeo;
• Lenye silaha na la kiuanamgambo;
• Likiwa limejitenga na jumuiya likiwa na lengo la uwatia hofu wananchi wahofie wenye mamlaka.

Akielezea historia fupi ya jeshi letu hili kutoka katika fikra za wakoloni Shivji anatudokeza kuwa ni mwaka 1950 kikosi cha polisi cha magari kiliundwa ambacho ndio mwanzo wa ‘Field Force Unit' (FFU). Anasema (kumbuka ni miaka kumi iliyopita akiandika haya); "Hadi leo hii FFU inaendelea kuweka hofu ndani ya wananchi na inajulikana kwa ukatili wake kama ambavyo tumeshuhudia mara kwa mara kwenye TV".

Ni kikosi hiki ndicho kilichoenda kuzima mgomo wa makuli mwaka 1950 ambapo watu wawili waliuawa, tuhuma zikiwa ni zile zile ambazo tumezisikia Songea – kukusanyika pasipo kibali.

Ni kikosi hiki hiki kilichotumika kuzima mgomo wa kiwanda cha Kilombero mwaka 1986 ambapo raia 4 waliuawa. Kwa ufupi tulichonacho leo hii ni mazao ya ukoloni na hatujaweza kubadilisha.

Ni jeshi la polisi la kisiasa
Sijapata muda wa kusoma matokeo ya utafiti wake wote (Shivji) kuhusu hali ya jeshi letu la Polisi kwa msingi wa kazi yake hiyo hapo juu. Lakini matukio mbalimbali ambayo yametokea kuanzia 1995 hadi sasa yamenifanya niamini kuwa jeshi letu halijawa chini ya raia kama inavyopaswa na limekuwa ni jeshi la kisiasa. Lina malengo ya kulinda na kuwanufaisha wanasiasa walioko madarakani na linadharau ya moja kwa moja dhidi ya wananchi. Bado linajiona ni jeshi la watawala na siyo wananchi.

Hii ni hatari katika mazingira ya demokrasia. Wananchi wanapojitokea – kwa haki waliyonayo kama chanzo cha utawala – na kusema tunaandamana kupinga au kuunga mkono jambo fulani mwitikio wa kwanza wa polisi haupaswi kuwa - wataifanya CCM ionekane vibaya!

Mwitikio wao ulipaswa kuwa hivi; "Tufanye nini ili wananchi waweze kuelezea hisia zao za kisiasa katika mazingira ya amani na utulivu – hata kama yatakuwa na maneno makali ya kisiasa?" Bahati mbaya jeshi hili chini ya IGP Mwema limepoteza uwezo huo.

Kuliunda upya
Binafsi ninaamini hakuna namna ya kulibadilisha jeshi letu isipokuwa kwa kuliunda upya ikiwa ni pamoja na maafisa wote kupewa mafunzo ya kuelewa haki za raia na haki za binadamu. Haitoshi kutoa mafunzo ya juu juu tu kuna tatizo la msingi katika jeshi hili na ipo haja ya baadhi ya maafisa kuondolewa warudi uraiani.

Tatizo hili la msingi litaendelea kutusumbua kwa muda mrefu. Watanzania waliochoshwa na vitendo vya ukatili na ukiukaji mkubwa wa haki za raia na za binadamu unaofanywa na baadhi ya polisi, wanalo jukumu la kutafuta chama kingine ambacho kitaweka wazi lengo na sera ya kulivunja jeshi hili.

Tusipofanya hivyo, tutaendelea kufa mikononi mwa polisi kama mbu anavyokufa mikononi mwa mtu. Jeshi hili hili ambalo linalindwa na kutetewa na wanasiasa hawa hawa litaendelea kupiga risasi watu mgongoni huku viongozi wake wakitumia mistari ile ile tuliyoisikia miaka hamsini iliyopita! Na kama hatutaonesha hasira ya kutosha na kutaka kina Mwema wawajibike tutaendelea kukodolea televisheni zetu kila baada ya miezi michache tukishuhudia watu wakipopolewa kwa risasi kama swala msituni.

Ndugu zangu, Jeshi la Polisi linatakiwa kuwa ni mlinzi wa wananchi na rafiki wa jumuiya. Lakini historia inavyojirudia mara kwa mara inatuonesha kuwa ni jeshi lenyewe ndilo limetengeneza uadui wa kudumu na wananchi wake.

Kuanzia Mererani, Nyamongo, Mwembe Chai, Pemba, Tanga, Mwanza, Mbeya n.k, jeshi hili limekuwa likiwashambulia wananchi bila kukemewa.

Si Rais wala Waziri Mkuu ambaye amewahi kuonesha kuguswa na hili; si Spika wa Bunge wala wabunge wa CCM wamewahi kuzungumzia hili. Lakini tunashuhudia hoja za ajabu ajabu zinaletwa bungeni kwa mbwembwe, isipokuwa hoja ya kukemea ukatili wa Polisi!

Mpaka auawe nani ndio tutakasirika?

Niandikie: lulawanzela@yahoo.co.uk

Source:http://www.mwananchi.co.tz/mwananchi-jumapili/43-uchambuzi-na-maoni-mwananchi-jumapili/20558-bwagamoyopolisi-wataendelea-kutuua-mpaka-lini.html
 
Mzee Mwanakijiji,kwanza pole kwa kupoteza ndugu yako katika tasnia ya habari,ndugu yetu,mwananchi mwenzetu...nashukuru kwa bandiko hili pia,pengine tutapata maoni ya wananchi nini kifanyike.Nilianzisha thread ambayo nilitaka wananchi watoe maoni yao ni kivipi wanaweza kujilinda.

Ni wazi hatuwezi tena kutegemea ulinzi wa polisi.Polisi walikuwa wakiwauwa raia wema toka kitambo tu,sema hii ni kwasababu wameanza kuuwa kwasababu za kisiasa wazi wazi!

Maandamano ya kulilaani jeshi la polisi ni mwanzo tu.Lakini siyo solution ya tatizo.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mzee Mwanakijii pole kwa kuandika hii thread ambayo inanizidishia uchungu jinsi hii nchi inavyoendeshwa kibabe wamemaliza kuuza rasilimali sasa za nchi sasa wameanza kututoa uhai
 
Jamani tujiulize ni kifungu gani cha sheria kinachowapa polisi mamlaka ya kutoa vibali vya kuandamana? Maana tumezoea kufanya vitu mechanically.
 
POLISI%2B2.JPG

Kwa miaka sasa CDM wamekuwa wakionewa, kunyanyaswa na kukandamizwa na jeshi la polisi la Tanzania linaloongozawa na IGP Said Mwema. Na kwa miaka sasa CDM imekuwa ikitoa hutuba za motomoto kilaa wanachama au mashabiki wake wanapouawa na jeshi hilo huku viongozi wake wakinyanyaswa (mnakumbuka Mbowe alivyobebwa kwa ndege ya jeshi kupelekwa Arusha?). Sasa imekuwa ni tabia kuwa CDM hawawezi kufanya maandamano au mkutano wowote wa kisiasa bila kufikiria polisi watafanya nini 'this time'.

Jeshi la Polisi (kuanzia juu hadi chini) limeendelea kuwachukulia CDM with contempt; haliamini wana haki yakupinga serikali na kwa hakika linaamini linaweza kuwanyamazisha ilimradi tu. Matokeo yake CDM wako chini ya huruma ya jeshi la polisi. Makala hii ya Februari 2012 iligusia kitu hicho hicho: Bwagamoyo: Polisi wataendelea kutuua mpaka lini? Kuna haja ya kufanyika kitu.

a. CDM iache kulionea aibu jeshi la polisi na mchezo wao huu wa kuwahutubia polisi kwenye mkutano yao. Wakati umefika wa kuanzisha maandamano dhidi ya jeshi la polisi na uongozi wake wa juu ili kutaka kina Mwema, Chagonja na wenzake waondolewe kwani ni watuhumiwa nambari moja hawa wa uvunjaji wa haki za msingi za raia!

b. Maandamano haya yawe na lengo la kuonesha dunia juu ya ukatili wa jeshi letu la polisi kwa raia.

c. CDM waliambie taifa mapema kabisa na viongozi wote wa polisi wajue kuwa itakapoingia madarakani kazi ya kwanza itakuwa ni kulivunja jeshi la polisi na kuliunda upya. Katika kulivinja kuna viongozi ambao watashtakiwa kwa yale anbayo wanayafanya sasa dhidi ya raia. Viongozi wa polisi wajue kabisa kuwa "nilikuwa nafuata amri" siyo utetezi pale maisha ya wananchi yanatoweshwa. Watanzania wajue kabisa kuwa jeshi lao la polisi linahitaji kuvunjwa siyo kufanyiwa tu marekebisho. CDM angalieni ilani yenu inasema nini kuhusu jeshi la polisi!!!

Ikumbukwe kuwa wafadhili wamekuwa wakitoa misaada mingi kwa jeshi la polisi vikiwemo vile vya mafunzo, silaha na vifaa. CDM imulike wafadhili hawa vile vile!! Iweje waendelee kufadhili jeshi linalokandamiza upinzani wa kisiasa nchini.

Nitadharau nikisikia tena viongozi wa CDM wanazungumzia mambo yale yale, kuhusu jeshi lile lile na kwa namna ile ile!! hawatokuwa tofauti na watawala wa sasa!

Tatizo hili naona ni kubwa kwa cdm.Pia hawajui matokeo halisi ya hicho wafanyacho.Haya hata kama cdm wakajua kwa asilimia mia kuwa it is a well planned stratregy to kick their ass,cdm watafanya nini
What cdm is prepared to do,say if their party is deregesterd.To me it looks cdm is short of stratergies.
 
Mi sioni haja ya CDM kuwaambia yote hayo polisi maana itakuwa kama ni mkwara.
Dawa ni kufanya vitendo. CDM iwe na subira mpaka hapo itakapoingia madarakani kisha iwashughulikie vibaraka wote wa polisi wanaotumiwa kwa maslahi ya watu wachache.
Waanze na shemeji yake rais (Said Mwema) kisha ma'RPC na wengine wa chini yao.

Ni vizuri wawaambie na wajue kuwa kila wanalofanya linawekwa kwenye record. Tena ningependa CDM waanzishe Tume ya Haki za Raia na za Binadamu ambayo itakuwa na kazi ya kurekodi vitendo vyote (na wanaoviteda) vya kuvunja haki hizo.
 
POLISI%2B2.JPG

Kwa miaka sasa CDM wamekuwa wakionewa, kunyanyaswa na kukandamizwa na jeshi la polisi la Tanzania linaloongozawa na IGP Said Mwema. Na kwa miaka sasa CDM imekuwa ikitoa hutuba za motomoto kilaa wanachama au mashabiki wake wanapouawa na jeshi hilo huku viongozi wake wakinyanyaswa (mnakumbuka Mbowe alivyobebwa kwa ndege ya jeshi kupelekwa Arusha?). Sasa imekuwa ni tabia kuwa CDM hawawezi kufanya maandamano au mkutano wowote wa kisiasa bila kufikiria polisi watafanya nini 'this time'.

Jeshi la Polisi (kuanzia juu hadi chini) limeendelea kuwachukulia CDM with contempt; haliamini wana haki yakupinga serikali na kwa hakika linaamini linaweza kuwanyamazisha ilimradi tu. Matokeo yake CDM wako chini ya huruma ya jeshi la polisi. Makala hii ya Februari 2012 iligusia kitu hicho hicho: Bwagamoyo: Polisi wataendelea kutuua mpaka lini? Kuna haja ya kufanyika kitu.

a. CDM iache kulionea aibu jeshi la polisi na mchezo wao huu wa kuwahutubia polisi kwenye mkutano yao. Wakati umefika wa kuanzisha maandamano dhidi ya jeshi la polisi na uongozi wake wa juu ili kutaka kina Mwema, Chagonja na wenzake waondolewe kwani ni watuhumiwa nambari moja hawa wa uvunjaji wa haki za msingi za raia!

b. Maandamano haya yawe na lengo la kuonesha dunia juu ya ukatili wa jeshi letu la polisi kwa raia.

c. CDM waliambie taifa mapema kabisa na viongozi wote wa polisi wajue kuwa itakapoingia madarakani kazi ya kwanza itakuwa ni kulivunja jeshi la polisi na kuliunda upya. Katika kulivinja kuna viongozi ambao watashtakiwa kwa yale anbayo wanayafanya sasa dhidi ya raia. Viongozi wa polisi wajue kabisa kuwa "nilikuwa nafuata amri" siyo utetezi pale maisha ya wananchi yanatoweshwa. Watanzania wajue kabisa kuwa jeshi lao la polisi linahitaji kuvunjwa siyo kufanyiwa tu marekebisho. CDM angalieni ilani yenu inasema nini kuhusu jeshi la polisi!!!

Ikumbukwe kuwa wafadhili wamekuwa wakitoa misaada mingi kwa jeshi la polisi vikiwemo vile vya mafunzo, silaha na vifaa. CDM imulike wafadhili hawa vile vile!! Iweje waendelee kufadhili jeshi linalokandamiza upinzani wa kisiasa nchini.

Nitadharau nikisikia tena viongozi wa CDM wanazungumzia mambo yale yale, kuhusu jeshi lile lile na kwa namna ile ile!! hawatokuwa tofauti na watawala wa sasa!

Nakubaliana na wewe karibu kila kitu ulichoandika hapo juu isipokuwa hapo kwenye wafadhili tu kwa maana mimi siamini kabisa kama mtu wa nje anaweza kutusaidia na hao wafadhili (wazungu) hata kama Polisi wakiua watu 200 cold blood kwa mara moja hawawezi kusema chochote wala kuweka pressure yoyote kwa Serikali kwa maana Serikali yetu inawatimizia yote wanayoyahitaji kwa maana nyingine Serikali yetu ina manufaa kwao na ndio maana tunasifika kwa amani na wazungu hawaingilii sehemu yoyote ambayo hawana maslahi.

Mfano haya matukio yangetokea Rwanda au Kenya au Uganda ungesikia breaking News Dunia nzima, na hii yote ni sababu ya interest, Tanzania bado hatujakuwa na maslahi makubwa kwa wazungu kuweza kuwafanya waingilie kinachoendelea hapa.

Hapa cha kufanya ni kujipanga sisi wenyewe na kuangalia jinsi tunavyoweza kutatua matatizo yetu, tusikimbilie kwa watu wa nje!

Chairman Mao katika harakati zake za mapinduzi alipewa scholarship kwenda kusoma Ufaransa lakini alikuwa too clever akaikataa akasema Mapinduzi ya kweli yanatoka ndani ya China yenyewe na si vinginevyo si ajabu angekubali leo hii China ingekuwa tu kama India au Afrika!
 
This is the climax huwezi kuwa unaua watu kama zama za ukoloni!
Ivi hawa polisi hawajui kuwa we are customers to them
 
They are killing us, they fear us, they know how bitterly we are...ooh God may let me live to see when those fascists face trials at the Hague and some in our reborn courts..Amen
 
Hili jeshi limekuwa kipofu na linaniudhi kwa kujiingiza kwenye mauaji. Limepoteza mwelekeo kabisa
 
muda wa mabadiliko ya haki ndio huu! Haiwezi kuendelea hivi tena.....
 
Back
Top Bottom