CHADEMA Iitishe Maandamano dhidi ya Jeshi la Polisi?

Ni vizuri wawaambie na wajue kuwa kila wanalofanya linawekwa kwenye record. Tena ningependa CDM waanzishe Tume ya Haki za Raia na za Binadamu ambayo itakuwa na kazi ya kurekodi vitendo vyote (na wanaoviteda) vya kuvunja haki hizo.

Hili ndio bandiko bora kwa mwaka huu 2012!!!!
 
Tatizo la polisi na askari ni ujinga, utafikiri watoto wa shule za msingi. Kufurahia mwezako akichanwa viboko na mwalimu. Hii ndo tabia ya polisi.

Unaweza kuta hawa jamaa wala sio pro wa mtu, ila wanaujinga fulani. Polisi wa tz akikukamata eti anafurahi jinsi alivyokupa kibano wana ujinga fulani, ni wajinga. Huwa hawa reason, bali reasoning yao ni kama sungusungu ya enzi za sokoine, ama waluga luga wa mtemi mirambo.

Sisi secondari walikuwa wanatuchalaza kwa malungu yao, provided ya kwamba hata vurugu za uanafunzi hazipo tena, wanafunzi wamekimbilia mlimani lakini polisi bado wanakupa kibano hata wakikuta umejifungia kabatini kama mende. sijui hizo vurugu unaweza zifanya umejifungia kabatini. Labda vurugu za mende.
 
Mzee mwanakijiji kwanza nimekugongea like! Pili nasikitika kusema kwamba ulichosema ndicho kilichotokea kwa CDM kukaa meza moja na policcm Leo na kukubaliana kusitisha shuhuli za CDM kwa Siku 3/4 swali la kujiuliza je walishindwa mini kukutana na kumaliza tofauti zao CDM na policcm kabla maafa Haya yote kutokea?

Kwanini CDM wanashindwa kuwa na misimamo kwenye maamuzi Yao? Ni damu ipi hasa wanayoogopa kumwagika zaidi ya hii? Kwa nini wasiseme Kama ccm au polisi liwalo na liwe? Dr slaa ni u padri na huruma zimemzidi au ni nidhamu ya uoga? Naanza kupoteza Imani na CDM Kama nilivopoteza kwa ccm na serikali kwa ujumla Kama ataweka mikono juu na Kama yasemwayo ni kweli kwamba kasalimu kwa IGP




POLISI%2B2.JPG

Kwa miaka sasa CDM wamekuwa wakionewa, kunyanyaswa na kukandamizwa na jeshi la polisi la Tanzania linaloongozawa na IGP Said Mwema. Na kwa miaka sasa CDM imekuwa ikitoa hutuba za motomoto kilaa wanachama au mashabiki wake wanapouawa na jeshi hilo huku viongozi wake wakinyanyaswa (mnakumbuka Mbowe alivyobebwa kwa ndege ya jeshi kupelekwa Arusha?). Sasa imekuwa ni tabia kuwa CDM hawawezi kufanya maandamano au mkutano wowote wa kisiasa bila kufikiria polisi watafanya nini 'this time'.

Jeshi la Polisi (kuanzia juu hadi chini) limeendelea kuwachukulia CDM with contempt; haliamini wana haki yakupinga serikali na kwa hakika linaamini linaweza kuwanyamazisha ilimradi tu. Matokeo yake CDM wako chini ya huruma ya jeshi la polisi. Makala hii ya Februari 2012 iligusia kitu hicho hicho: Bwagamoyo: Polisi wataendelea kutuua mpaka lini? Kuna haja ya kufanyika kitu.

a. CDM iache kulionea aibu jeshi la polisi na mchezo wao huu wa kuwahutubia polisi kwenye mkutano yao. Wakati umefika wa kuanzisha maandamano dhidi ya jeshi la polisi na uongozi wake wa juu ili kutaka kina Mwema, Chagonja na wenzake waondolewe kwani ni watuhumiwa nambari moja hawa wa uvunjaji wa haki za msingi za raia!

b. Maandamano haya yawe na lengo la kuonesha dunia juu ya ukatili wa jeshi letu la polisi kwa raia.

c. CDM waliambie taifa mapema kabisa na viongozi wote wa polisi wajue kuwa itakapoingia madarakani kazi ya kwanza itakuwa ni kulivunja jeshi la polisi na kuliunda upya. Katika kulivinja kuna viongozi ambao watashtakiwa kwa yale anbayo wanayafanya sasa dhidi ya raia. Viongozi wa polisi wajue kabisa kuwa "nilikuwa nafuata amri" siyo utetezi pale maisha ya wananchi yanatoweshwa. Watanzania wajue kabisa kuwa jeshi lao la polisi linahitaji kuvunjwa siyo kufanyiwa tu marekebisho. CDM angalieni ilani yenu inasema nini kuhusu jeshi la polisi!!!

Ikumbukwe kuwa wafadhili wamekuwa wakitoa misaada mingi kwa jeshi la polisi vikiwemo vile vya mafunzo, silaha na vifaa. CDM imulike wafadhili hawa vile vile!! Iweje waendelee kufadhili jeshi linalokandamiza upinzani wa kisiasa nchini.



Nitadharau nikisikia tena viongozi wa CDM wanazungumzia mambo yale yale, kuhusu jeshi lile lile na kwa namna ile ile!! hawatokuwa tofauti na watawala wa sasa!
 
Naunga mkono hoja yako, wakibaki salama mpaka 2015, tutawawajibisha kwa uhalifu huu dhidi ya Binadamu.
Kama na wewe kiongozi unasubiria mpaka 2015 watu waendelee kufa basi tz hatuna viongozi! Kama dhamira ya CDM ni kusubiria. 2015 watu waendelee kufa basi Mimi narudisha kadi ya CDM na sitotaka chama chochote ntampigia kura mtikila mgombea binafsi na si vinginevo. Na Kama kweli ndivo CDM wanavotaka kusubiria mpaka 2015 kwa nini msisimamishe shughuli zote za CDM mpaka Iyo 2015 kupunguza mauaji Haya? Kesho akiuliwa Mbowe au slaa mtasubiria tuu mpaka 2015? Mna uhakika gani wa kushinda serikali hii dhalimu Iyo 2015? Kama huu ni msimamo wako basi hustahili kuwa mwanamapinduzi na Kama ndio msimamo wa CDM basi ukombozi ni ngozi za mchana.,..samahani Kama kuna mahali nimekukwaza nimetumia uhuru wangu kutoa maoni yangu be blessed...
 
Umenena vyema mkuu MM..Nadhani si wakati wa kulalamika sasa, kama ambavyo CHADEMA wamechukua maamuzi magumu kuingia kata mpaka kata, kijiji mpaka kijiji, wilaya mpaka wilaya, jimbo mpaka jimbo, mkoa mpaka mkoa. Sasa uwe ni wakati wa kwenda Taifa mpaka Taifa kulisemea hili la JESHI LA POLISI linaloongoza kuua watu. Maana sasa tutaonekana wa kutoa matamko sana. Nimefurahi leo Mkuu wa kituo cha haki za binadamu Dr Hellen Kijo Bisimba amesema kuwa wameacha kutoa matamko sasa, wana-mpango wa kwenda kuishitaki serikali kwenye ngazi za kimataifa. Si wakati wa matamko sasa.
 
gt natoa wito kwa wale wote ambao hatukupitia jeshi, tuhudhurie mafunzo ya mgambo hata ya jeshi, tukimaliza mafunzo tunaacha na kuingia kufanya kazi mitaani. ili risasi zikipigwa tuwe tunajua ni silaha ya aina gani inapigwa na jinsi ya kukwepa na ikibidi tuichukue nchi yetu ambayo wahuni wa ccm kama akina ncemba, shigela, nape wasira na ccm wanaona ni ya kwao peke yao, wakati ni yetu sote

vijana wanatucheka eti hata mgambo hatujaenda hivyo hatujui mbinu za mapambano, ebu shime twendeni ili tukihitimu mafunzo tukomeshe udhalimu huu
 
gt natoa wito kwa wale wote ambao hatukupitia jeshi, tuhudhurie mafunzo ya mgambo hata ya jeshi, tukimaliza mafunzo tunaacha na kuingia kufanya kazi mitaani. ili risasi zikipigwa tuwe tunajua ni silaha ya aina gani inapigwa na jinsi ya kukwepa na ikibidi tuichukue nchi yetu ambayo wahuni wa ccm kama akina ncemba, shigela, nape wasira na ccm wanaona ni ya kwao peke yao, wakati ni yetu sote

vijana wanatucheka eti hata mgambo hatujaenda hivyo hatujui mbinu za mapambano, ebu shime twendeni ili tukihitimu mafunzo tukomeshe udhalimu huu
Nashukuru kwa bandiko hili,ni mawazo mazuri tu ya namna ya kujilinda dhidi ya udhalimu.Kitu cha kwanza kwa mwananchi wa nchi yoyote ile,ni security.

Kama hakuna security kwa wananchi,nothing is well.
 
Mkuu chama,

Hakuna uhuru usiokuwa na mipaka huwezi kuiapa amri serikali iliyowekwa madarakani na raia kwa sababu wewe ni Dr.Slaa wa Chadema? Vyombo vya dola vina utaratibu wake hata Dr.Slaa angekuwa yeye rais sidhani kama angekubali kupangiwa...Dr.Slaa anaimbia serikali ana muda tena wa kusubiri watafanya mkutano kwa nguvu..

Mkuu Ritz;
Porojo za wanasiasa uchwala kama Slaa lazima uzielewe; jamaa alishakuwa mwajiriwa wa serikali ya muungano ya Tanzania anajua fika utaratibu wa serikali, mbona kwenye hizo vurugu hapeleki ndugu yake au ndugu wa Josephine? Anajua serikali itafanya kweli, ni kawaida ya wapinzani kulalama kuhusu polisi lakini wao wakishika dola ndio wanageuka wabaya hawana mfano si unakumbuka Kibaki Kenya kabla hajashika uraisi alivyokuwa akilalama kuhusu prezdee Moi? Je alivyoshika madaraka moto anaouwasha ni zaidi ya Moi; juzi tu kampa shekhe wa watu kitu na box hakuna serikali inayotaka kuchezewa hasa serikali halali ilioyoingia madarakani kwa nguvu za wananchi.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
gt natoa wito kwa wale wote ambao hatukupitia jeshi, tuhudhurie mafunzo ya mgambo hata ya jeshi, tukimaliza mafunzo tunaacha na kuingia kufanya kazi mitaani. ili risasi zikipigwa tuwe tunajua ni silaha ya aina gani inapigwa na jinsi ya kukwepa na ikibidi tuichukue nchi yetu ambayo wahuni wa ccm kama akina ncemba, shigela, nape wasira na ccm wanaona ni ya kwao peke yao, wakati ni yetu sote

vijana wanatucheka eti hata mgambo hatujaenda hivyo hatujui mbinu za mapambano, ebu shime twendeni ili tukihitimu mafunzo tukomeshe udhalimu huu

Hivi ni kitu gani kinachoishinda chadema kuwa na jeshi lake, manake ndicho chama chenye wafuasi wengi. Kwani what is so is special about jeshi zaidi ya kuwa na silaaa, ambazo unawezakutumia njia nyingi tu kuzipata, ikiwezekana hata kutengeneza (kwa nini nani hajue kutengenza mabomu na bunduku au mnatake tuanze kuweka recipes huku?). Siamini hata kwa mtutu kwamba cdm itakuja kuchukua nchi bila jeshi au kwa kutegemea jeshi hilihili la ccm. Hiyo ni ndoto. Dawa ya ccm ni kichapo tu. Vinginevyo atawakatambike hakunamabadiliko katika haka kanchi, kenye viongozi miungu mtu, vichwa maji, wenye visions za panzi (Slaa anaweza kukosea but he is the greatest leader than anyone in ccm at the moment). Kamuulizeni Kagame au Mseveni au Kibaki. ....hii trend ya kuua raia haita stop, yanni hapa bado hatujaona kitu, Nyerere alisema ni kama kula nyama ya mtu...
 
.....

a. CDM iache kulionea aibu jeshi la polisi na mchezo wao huu wa kuwahutubia polisi kwenye mkutano yao. Wakati umefika wa kuanzisha maandamano dhidi ya jeshi la polisi na uongozi wake wa juu ili kutaka kina Mwema, Chagonja na wenzake waondolewe kwani ni watuhumiwa nambari moja hawa wa uvunjaji wa haki za msingi za raia!

b. Maandamano haya yawe na lengo la kuonesha dunia juu ya ukatili wa jeshi letu la polisi kwa raia.

c. CDM waliambie taifa mapema kabisa na viongozi wote wa polisi wajue kuwa itakapoingia madarakani kazi ya kwanza itakuwa ni kulivunja jeshi la polisi na kuliunda upya. Katika kulivinja kuna viongozi ambao watashtakiwa kwa yale anbayo wanayafanya sasa dhidi ya raia. Viongozi wa polisi wajue kabisa kuwa "nilikuwa nafuata amri" siyo utetezi pale maisha ya wananchi yanatoweshwa. Watanzania wajue kabisa kuwa jeshi lao la polisi linahitaji kuvunjwa siyo kufanyiwa tu marekebisho. CDM angalieni ilani yenu inasema nini kuhusu jeshi la polisi!!!

Ikumbukwe kuwa wafadhili wamekuwa wakitoa misaada mingi kwa jeshi la polisi vikiwemo vile vya mafunzo, silaha na vifaa. CDM imulike wafadhili hawa vile vile!! Iweje waendelee kufadhili jeshi linalokandamiza upinzani wa kisiasa nchini....

Mzee mwanavillage I greet you!
pamoja na hasira juu ya polisi hapo kwenye blue, i beg to differ with you sir! kumbuka polisi wengi ni vijana na wengi ni CDM ila kiapo ndio issue! Wianza kuchagua watimize amri ipi na ipi wasiitii hakutakuwapo jeshi tena!

Halafu issue ya kulivunja baada ya CDM kuingia madarakani hautakua solution kwani askari alieachishwa kazi bila ridhaa yake ni hatari sana kuliko majambazi wote waliopo mtaani!

I would like kuwashauri CDM hasa Slaa akumbuke kale la methali ka: Never argue with a fool!!, CDM wanajua type za askari wetu, yaani juzi tu Moro kafa mtu, a week later mwingine! bado Dr. Slaa anaendelea ku-argue with fools! till when?
I am out.
 
CCM na Nape wameshindwa kulaani au hata kukemea mauaji haya? Tena Nape alikuwa huko Iringa jana kwenye mazishi ya yule Katibu wao wa CCM.
 
CDM haiwezi kuwa na jeshi lake kwasababu ni kosa kisheria, ndiyo maana ni vigumu wao kuwa na jeshi. Wakijidanganya wakaanzisha jeshi, watafunguliwa kesi ya jinai na jinsi wanavyowatamani itakuwa kesi ya uhaini, ambayo adhabu yake mara nyingi ni kifo.

Mimi nadhani ni watz tukiwa na mafunzo ya jeshi, huu woga tulio nao tunaodhani dola ya ccm hauwezi kushindana nayo itaondoka, then, tutakisambaratisha kama chama cha Mubarak wa misri na kuwashitaki mafisadi wote na kutaifisha mali zote na kufanya mali za serikali
 
Umenena vyema mkuu MM..Nadhani si wakati wa kulalamika sasa, kama ambavyo CHADEMA wamechukua maamuzi magumu kuingia kata mpaka kata, kijiji mpaka kijiji, wilaya mpaka wilaya, jimbo mpaka jimbo, mkoa mpaka mkoa. Sasa uwe ni wakati wa kwenda Taifa mpaka Taifa kulisemea hili la JESHI LA POLISI linaloongoza kuua watu. Maana sasa tutaonekana wa kutoa matamko sana. Nimefurahi leo Mkuu wa kituo cha haki za binadamu Dr Hellen Kijo Bisimba amesema kuwa wameacha kutoa matamko sasa, wana-mpango wa kwenda kuishitaki serikali kwenye ngazi za kimataifa. Si wakati wa matamko sasa.
Huyo Dr.Bisimbi mwenyewe ni njaa tu, amekosa kazi ya kufanya ameamua na yeye kujitafutia umaarufu. Tanzania ina rekodi nzuri sana ukifananisha na nchi zingine duniani. Hayo mashitaka yake yatatupiliwa mbali.
 
Mkuu Ritz;
Porojo za wanasiasa uchwala kama Slaa lazima uzielewe; jamaa alishakuwa mwajiriwa wa serikali ya muungano ya Tanzania anajua fika utaratibu wa serikali, mbona kwenye hizo vurugu hapeleki ndugu yake au ndugu wa Josephine? Anajua serikali itafanya kweli, ni kawaida ya wapinzani kulalama kuhusu polisi lakini wao wakishika dola ndio wanageuka wabaya hawana mfano si unakumbuka Kibaki Kenya kabla hajashika uraisi alivyokuwa akilalama kuhusu prezdee Moi? Je alivyoshika madaraka moto anaouwasha ni zaidi ya Moi; juzi tu kampa shekhe wa watu kitu na box hakuna serikali inayotaka kuchezewa hasa serikali halali ilioyoingia madarakani kwa nguvu za wananchi.

Chama
Gongo la mboto DSM
..................
 
SEPTEMBA 2, 2012, polisi waliua kikatili mwandishi wa habari wa kituo cha Channel TEN, Daudi Mwangosi, katika Kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa. Alikufa mbele ya Kamanda wa Polisi mkoani humo, Michael Kamuhanda, wakati polisi hao walipovamia ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ili kuwatawanya wasifungue tawi la chama chao katika kijiji hicho.

Mmoja wa watu walioshuhudia tukio zima, ni mwandishi wa Tanzania Daima, Abdallah Khamis. Ifuatayo ni simulizi ya kile alichokiona wakati polisi wanaondoa uhai wa Mwangosi.

SIKU hiyo asubuhi tulipata taarifa kuwa Kamanda wa Polisi mkoani humo (RPC), Michael Kamuhanda, alipanga kukutana na waandishi wa habari majira ya saa 2.30 ambapo waandishi walifika akiwemo Daudi Mwangosi.

Tukiwa katika chumba cha mikutano katika jengo la polisi Mkoa wa Iringa, Kamanda wa mkoa huo, alifika akiongozana na maafisa wake wawili na kuanza kutusomea taarifa ya zuio la mikutano ya CHADEMA iliyokuwa iendelee siku hiyo baada ya kupisha zoezi la awali la sensa.

Alitusomea zuio hilo na kutuambia hata viongozi wa CHADEMA wameshataarifiwa usiku wa Septemba Mosi. Tukamuuliza mbona taarifa za sensa zinaeleza kuwa kuna mafanikio kwa asilimia 95 na waliobaki wanatakiwa waende kwa viongozi wao? Akatujibu kuwa hilo ni agizo na linapaswa litekelezwe na CHADEMA.

Waandishi hawakuchoka kumuuliza maswali RPC na moja ya maswali yaliyoonekana kumkera kamanda huyo ni lile lililotoka kwa Daudi Mwangosi kuwa mbona wakati wa mwanzo walipozuia mikutano ya CHADEMA mkoani humo mikutano mingine ya CCM ndani ya mkoa huo na sehemu nyingine nchini ilikuwa inaendelea.

Swali lingine la Mwangosi lilimtaka kamanda huyo kutumia busara katika hali iliyopo kwa lengo la kuepusha maafa yanayoweza kutokea endapo angeendelea kushikilia msimamo wake kuwa hakuna mkutano wa aina yoyote utakaofanyika.

Baada ya maswali hayo, tulimuona Kamanda Kamhanda akiwa amekunja sura kama ishara ya kuchukizwa na maswali ya Mwangosi ambaye aliongeza swali lingine kwamba, "inaonekana Kamanda umechukia kutoka ndani ya moyo wako" na kamanda akajibu "ni lazima nichukie na nawachukia hawa CHADEMA kwa kuwa ninaipenda kazi yangu na pia ninakaribia kustaafu na sitaki kustaafu vibaya."

Baada ya hapo maafisa waliokuwa na RPC waliandika ujumbe kwenye karatasi na wakamfikishia mkuu wao, na baada ya muda mkutano huo ulimalizika huku kukiwa na kauli za utani wa hapa na pale kati ya waandishi wa habari na baadhi ya askari juu ya kwenda kuripoti matukio ya siku hiyo.

Tulipokuwa nje ya jengo, Mwangosi, kwa kuwa ni mwenyeji wa mkoa huo, alikuwa akitaniana na mmoja wa askari aliyevaa kiraia, ambaye alimwambia kuwa, "huko hakutakuwa na kujuana na kuna uwezekano wa watu kufa."
Mwangosi alijibu papo hapo kuwa hilo haliogopi kwa kuwa kifo ni ada ya mja yeyote na kwamba ataogopa kama mtu atamuahidi kuishi milele.

Baada ya hapo, kila mmoja alitawanyika katika eneo lake, na majira ya saa saba mchana baadhi ya waandishi walikutana ili kuanza safari katika Wilaya ya Mufindi kwa ajili ya kuripoti mkutano wa ndani wa CHADEMA na ufunguzi wa matawi.

Waandishi wa habari hao pamoja na mimi ni Godfrey Mushi (Nipashe), Olver Motto (Star Tv), Renatus Mutabuzi (ITV), Clement Sanga (Mwananchi), Joseph Senga (Tanzania Daima) na Tumaini Makene (Ofisa Habari wa CHADEMA).

Tulipofika katika mji wa Mafinga, tulipata chakula cha mchana kabla ya kwenda katika Kijiji cha Nyololo, na muda wote huo Mwangosi alikuwa hajaungana nasi.

Tuliondoka Mafinga kuelekea Nyololo huku mwenzetu Clement Sanga akiwasiliana na Mwangosi aliyesema yuko katika basi na angeungana nasi tukiwa Nyololo. Tulipofika pale tuliona askari wachache wakiwa wamesimama barabarani huku gari lao moja likiwa linajaza mafuta katika kituo cha mafuta kilichopo eneo hilo.

Tukiwa njia ya kwenda Mbeya, mita kama 100 kutoka katika mji wa Nyololo, kushoto kwetu tuliziona ofisi za CHADEMA zikiwa zimepambwa kwa bendera nyingi, na kulia kwake tuliona magari manne ya askari waliokuwa na silaha.

Baada ya kupita eneo hilo, gari moja la polisi lilikuwa likitufuata, na hapo tulishauriana kugeuza gari kurudi katika eneo la mji. Tulipofanya hivyo, na gari la polisi lilisimama.

Wakati tunarudi katika eneo la mji, tuliegesha gari pembeni. Baadhi ya waandishi wa habari waliingia mitaani kwa makubaliano kuwa baada ya dakika 10 tuwe tumerejea kwa ajili shughuli iliyotuleta – kushuhudia ufunguzi wa tawi hilo jipya la CHADEMA.

Muda huo ulipofika, tulirejea, lakini Mwangosi alikuwa hajaungana nasi. Baadaye tulianza kuona baadhi ya magari yakiwa na bendera ya CHADEMA yakipita moja baada ya jingine.

Kuwasili kwa Mwangosi eneo la Nyololo
Saa 10.22 Mwangosi aliwasili kwa basi ambalo sikumbuki kama ni Hood au Abood; na muda huo huo tukawaona askari wakiyatoa magari yao kutoka mafichoni na kuingia upande wa kulia wa mji wa Nyololo kwenye ofisi za kata za CHADEMA.

Wakati askari wakiwa wanapita walikuwa wakisema Dk. Slaa anatokea eneo la Wami. Waandishi wa habari wakawa wamejiandaa kwenda kwa kufuata njia hiyo.

Tuliegesha gari letu mbali. Mwangosi ambaye hakuwepo awali, akataka kuchukua pikipiki ili awahi. Kwa kuwa muda huo nilikuwa naye, nikamsihi kuwa hana haja ya kuingia gharama kwa kuwa gari la waandishi wa habari lipo. Akanielewa, na tukaingia katika gari hilo, huku akiwa amempakata Oliver Motto wa Star Tv.

Tulipoenda kama mita 50 hivi, tulikutana na msafara wa CHADEMA ukiwa unaelekea tunakotoka. Gari la waandishi wa habari na magari ya polisi yakalazimika kukaa pembeni kuyapisha, kisha wakaungana nao kuelekea katika ofisi za tawi za chama hicho.

Ofisi za tawi za CHADEMA katika mji huo wa Nyololo zipo mita zaidi ya 100 upande wa kushoto wa bararara ya kuelekea Mbeya. Awali polisi walikuwa wameegesha magari yao barabarani wakati CHADEMA wakielekea katika ofisi zao.

Hakukuwa na vurugu yoyote. Ghafla kiongozi wa polisi ambaye alikuwepo pale – tulimtambua kwa jina la Mnunka – aliwaamuru askari wake watoe ilani kwa kunyoosha bendera kubwa nyekundu juu na kuwataka CHADEMA waondoke katika ofisi zao. Tukapiga picha tukio hilo.

Wakati askari wakijiandaa kuwafuata wana CHADEMA katika ofisi zao, alitokea mtu aliyevaa shuka na kujifunga kitambaa kichwani ambaye baadaye alijitambulisha kama mkuu wa upelezi mkoa (RCO), akawaamuru wenzake waende katika ‘target' lakini wasithubutu kutumia nguvu bila amri.

Hapa ndipo tulipoanza kupata wasiwasi ni nani anatoa amri kwa kuwa yule wa mwanzo, Mnunka alijiapiza kuwa wamechoka kuvumilia, na kwamba siku hiyo CHADEMA watawatambua. Hata tulipomuuliza maana ya kauli ile, hakutupa jibu la kueleweka.

Katika hali hiyo, mtu aliyejitambulisha kama ndie RCO alizungumza na viongozi wa CHADEMA, wao wakamwambia wako katika kikao cha ndani. Yeye akasema jukumu lake ni kuhakikisha usalama unakuwepo, na kwamba kama ni suala la kikao cha ndani hawawezi kuzuia.

Tulitaka kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali kutoka kwa RCO ambaye alikuwa akizungumza kwa simu na mtu ambaye baadaye ilikuja kubainika kuwa ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC), akawa anamueleza kuwa hali ni salama. Alituahidi waandishi wa habari tuvute subira "kwa kuwa mwenye mkoa amewasili."

Baada ya kuwasili kwa RPC Kamuhanda, Kamanda wa FFU, Mnunka alienda akamnong'oneza jambo. Pale pale, Kamuhanda akaonekana kukasirika. Akaagiza CHADEMA wasimamishe shughuli yao mara moja.

Tulitaka kujua tafsiri ya mkutano wa ndani kwa Jeshi la Polisi ni ipi, ni kwa wahusika kukaa ndani au ni ule mkutano utakaowahusisha wanachama peke yao kama ambavyo CHADEMA walikuwa wanasema pale. RPC akatujibu kuwa hilo halielewi na yeye si mwanasiasa.

Baada ya maelezo hayo, waandishi wa habari tulimbana RPC kwa maswali hata ikafikia hatua ya kamanda huyo kuanza kuwanyooshea vidole baadhi yetu, huku alimlalamikia Mwangosi kwamba kwanini hakushiba na majibu aliyopewa tangu asubuhi.

RPC akaniambia mimi kwamba nauliza maswali yanayopingana na mtazamo wa jeshi hilo; akamwambia Mutabuzi kuwa anamfahamu.

Baada ya hali hiyo, CHADEMA walimaliza mkutano wao katika ofisi za tawi na wakawa wanaelekea katika ofisi za kata. Gari lililotubeba lilikuwa nyuma ya gari la RPC ambaye baadaye dereva wake aliendesha kwa kasi kwenda mbele kutaka kuzuia msafara wa CHADEMA.

Lakini viongozi wa CHADEMA walikuwa wameshafika katika ofisi yao ya kata na tukashuka kwenda kushuhudia kinachoendelea. Hapo ndipo tulimkuta Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zanzibar, Hamad Yusuph na viongozi wengine wakisaini katika kitabu cha wageni.

Ghafla, RPC akatoa amri ya kuwakamata viongozi wa CHADEMA waliokuwa katika ofisi yao. Baada ya amri hiyo, wanachama wa CHADEMA waliokuwa pale wote walikaa chini wakinyoosha mikono juu.


Balaa linaanza kwa amri ya RPC Kamuhanda
Baada ya RPC kutoa amri hiyo, polisi walioipokea walianza kurusha mabomu ya machozi kuelekea sehemu waliyokaa wanachama wa CHADEMA. Mabomu hayo yalirushwa na kuumiza wengi, wakiwamo waandishi wa habari. Mimi nilipigwa na kitu chenye kishindo, nikajeruhiwa mkono wa kushoto na sehemu ya paja la mguu wa kulia.

Jitihada za polisi kuwatawanya wafuasi wa CHADEMA zilifanikiwa. Baadhi ya watu na viongozi waliwekwa chini ya ulinzi, sisi tukiwa tunaendelea kufanya kazi yetu ya kukusanya taarifa ili kuhabarisha umma juu ya kile kinachoendelea katika eneo hilo.

Wakati hali hiyo ikiendelea, ofisi za kata za CHADEMA hazikuwa na mtu. Askari wakawa wanapiga mabomu kuelekea ndani ya ofisi hiyo tupu.

Tuliendelea kupiga picha tukio hilo. Ghafla askari mmoja akamgeukia mwandishi wa gazeti la Nipashe, Godfrey Mushi, akaanza kumpiga.

Baada ya kuona mwandishi huyo anapigwa, Mwangosi aliwasogelea askari akitaka kujua sababu za kumshambulia mwandishi wakati yupo kazini kama ambavyo askari hao walivyokuwa wakiwajibika.

Swali la Mwangosi likavuta askari wengine. Wakamzunguka na kuanza kumpiga kwa marungu, mateke na ngumi. Wakati hayo yakifanyika, RPC alikuwa pale anashuhudia.

Baada ya kuona kipigo kimekuwa kikali, Mkuu wa Kituo cha Polisi (OCS) cha Mafinga aliingilia kati kutaka kumnusuru Mwangosi.

Wakati Mwangosi akiwa anashambuliwa, mpiga picha wa gazeti la Tanzania Daima, Joseph Senga, naye alikuwa katika wakati mgumu baada ya askari kumdhibiti na kuanza kumpekua mifukoni, huku mwenyewe akijitahidi kujinasua mikononi mwao.

Mbali na mimi na Senga, muda huo hakukuwa na raia yeyote katika eneo lile, isipokuwa Godfrey Mushi wa Nipashe ambaye sina hakika kama alikuwa anafahamu kinachoendelea maana alikuwa amepigwa sana, yuko hoi.

Baada ya kuona kipigo kinazidi kwa Mwangosi huku Senga akiendelea kupiga picha, uzalendo ulinishinda, nikaamua kumfuata Kamanda wa Polisi mkoani humo aliyekuwa mita zisizozidi kumi ndani ya gari lake, akishuhudia tukio lile. Nikamuomba asaidie kumnusuru Mwangosi na kipigo kile.

RPC alishusha kioo cha gari lake, akaniangalia, kisha akafunga kioo, huku dereva wake akawa anapiga honi. Sikujua maana ya honi hiyo.

Baada ya kuona hakuna msaada wowote kutoka kwa RPC, nilisogea karibu kwa ajili ya kuendelea kupata picha ya tukio, ili umma ujue juu ya madhila yanayowapata waandishi wa habari mikononi mwa polisi.

Wakati nikiwa naendelea kuchukua picha, nilimwona askari mmoja akinyoosha mkono juu na mwingine aliyevaa kiraia akiwa ameshika bastola yake kuelekeza juu, huku wengine wakiwa wanaendelea kumpiga Mwangosi aliyekuwa anajitahidi kuinuka kwa kumshika mmoja wa askari wale.

Katika harakati za Mwangosi kujinasua, nilimshuhudia mmoja wa wale askari akiwa kama anainama akaelekeza mtutu wa bunduki usawa wa tumbo la Mwangosi aliyekuwa katika hali ya kutaka kusimama huku akipiga kelele "msiniuee, msiniuee…"

Mara nikasikia mlipuko mkubwa pale pale walipo; baadhi ya nyama zikarushwa na kutapakaa, nyingine zikanirukia mimi na kuchafua fulana yangu.

Kumbe walikuwa wamemlipua Mwangosi! Nikapiga picha ya mwili uliosambaratika na kukatika vipande vipande. Nikaona askari wale wanambeba askari ambaye naye alijeruhiwa na mlipuko uliomuua Mwangosi. Nikakimbia kujinusuru na askari wale.

Sikuona tena usalama wangu mbele ya polisi wake. Sikumwamini tena RPC kama angeweza kulinda maisha yangu. Nikatimua mbio kuelekea nisipopajua.

Nikiwa nakimbia nilichomoa kadi ya kamera kutoka katika kamera yangu ili nisipokonywe. Hapo ndipo nilipokutana na mwandishi mwingine, Francis Godwin, nikamwambia asielekee nilikokuwa natoka mimi – ambako ndiko alikuwa anataka kwenda – kwa kuwa Mwangosi ameshauawa na polisi!

Wakati naachana na Godwin, nilichukua simu yangu na kumpigia Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda, ambaye ndiye Mhariri Mtendaji wa gazeti hili kwa ajili ya kumpa taarifa. Bahati mbaya simu yake haikupokelewa.

Nikamfuata Makene (Tumaini, afisa habari wa CHADEMA) aliyekuwa amejikinga katika gogo, alikokuwa pamoja na Oliver Motto, nikawaambia eneo hili halitufai watatuua. Ndipo nikampigia simu Bakari Kimwanga, mwandishi wa gazeti la Mtanzania, nikamfahamisha kuwa Mwangosi ameuawa na polisi. Tukakimbilia porini kujificha, kila mtu akiwa analia kivyake.

Baada ya kukaa porini kwa muda, tuliamua kubadilisha nguo zetu ili tusitambulike kirahisi. Tukatoka mafichoni kuangalia hali ya usalama. Tukaanza kuwatafuta wenzetu ambao tulipoteana nao. Baadaye tulikodi teksi kuwafuata wenzetu ambao wakati huo walishakimbia kutoka eneo hilo la hatari.

Tukiwa katika hoteli ya MR mkoani Iringa, mwananchi mmoja alikuja kutueleza kuwa alifanikiwa kukusanya sehemu ya mwili wa marehemu Mwangosi pamoja na mabomu yaliyoachwa katika eneo la tukio na walipoangalia wakaona ni sehemu ya nyama ya utumbo iliyowekwa katika mfuko pamoja na mabomu ya machozi na kuyapanga yale mabomu juu ya meza ya hoteli hiyo na kuyapiga picha huku utumbo wa Mwangosi ukiendelea kuwa katika mfuko uliowekwa.

Hadi sasa sijajua endapo sehemu hiyo ya utumbo ilizikwa usiku ule mkoani Iringa au uliunganishwa na sehemu nyingine ya mwili wake uliotawanywa na bomu hilo kiasi cha kushindwa kujua kama ni mwili wa binadamu au ni ng'ombe aliyechinjwa tayari kwa mauzo.
Hivi ndivyo tulivyompoteza mwandishi mwenzetu, Daudi Mwangosi, akiwa mikononi mwa polisi.
Tumeambiwa Mwangos(R.I.P) hakuwa mwandishi wa habari ! Tumesikia ikihojiwa aliwezaje kufika mufindi kwasababu ni mbali saana! n.k.
Unaweza kuandika kitu au kutetea jambo baada ya muda ukajiuliza kama ulipokuwa unaandika ulikuwa mzima au vipi.
Habari hii imeletwa na mtu aliyekuwepo katika tukiio kuanzia A-Z.

Mafundi wa spinning wakati wenu sasa m-challenge first hand information kama hii.
 
Hakuna haki wala haki haitatendeka iwapo wafuatao hawatajiuzulu au kuchomolewa na Kikwete kupisha uchunguzi:1. Waziri Nchimbi;2. Mkuu wa mkoa wa IRINGA; 3. RPC;4. Mkuu wa wilaya;5. OCD; na 6. mkuu wa upelezi mkoa (RCO), 7. Chagonja.
 
Back
Top Bottom