CHADEMA haya ya Morogoro nyie hayawahusu?

CHADEMA haya ya Morogoro nyie hayawahusu?

Nna uhakika CDM wakienda huko mtasema wanatafuta sifa...tumeshawazoea mbowe akienda pale hamtakosa chakuongea pigeni domo CDM inapiga kazi period
 
Serikali ya ccm ndiyo iliyojenga barabara hiyo na daraja hilo. Wao ndio wanapaswa kuwajibika na tatizo hilo. Chadema haikusanyi kodi kwa wananchi ili kutoa huduma serikali ya ccm ndiyo ina fedha zetu ambazo zinatakiwa kutumika kwenye maafa sio chadema. CCm hawajaenda kule kwa sababu hawajali. Chagua CDM 2015 uone itakufanyia nini ikiongoza serikali9.
 
Ni sehemu ya majukumu yake lazima ahamie huko na pia hilo daraja lilijengwa chini ya kiwango in the first place otherwise tusingekuwa tunapoteza pesa again....

Ndo maana mi nasema kuwa mpinzani ni kuwa MWENDAWAZIMU!
 
Mbona JK amekwea pipa na yupo Davos, Pinda nakagua mradi wa gesi! Kwani wao hawaguswi na hayo mafuriko?

Yaani unategemea shetani akuonee huruma?

Chadema wanadai kuwa mafuriko yamesababishwa na CCM

Kwanza hawataenda huko mpaka mafuriko yaishe
 
kwa hyo tuseme kama Chadema wasingekua kwenye operation ungewaita waende kwenye tukio? au ndo kuonesha unawajali sana watu wa Moro?mbona sijasikia ukipiga mbiu wanajeshi kambi ya moro wawahi eneo la tukio na isitoshe wao wanambinu na ukakamavu wa kupambana na majanga? acha kuchonganisha wananchi na chama lao kipenzi

Mkuu sichonganishi, nimeuliza tu maana kuna wakati watu walisitisha vikao vya bunge kwa sbb ya maafa... Tungeungana pamoja katika hili.
 
Duh hapa naona jamaa anataka washuushe daraja lingine kuonyesha CCM wameshindwa!
 
Nimepita eneo ya vijiji vya
Magole na Dakawa mchana huu hali kwakweli ni mbaya sana nimeona makada wa ssm wakigeuza eneo hilo kama show room ya V8 na sikuona lolote la maana wanalofanya-Ingawa naamini chadema wakienda hapo ssm wataamuaka na hatimaye wananchi wale kupata msaada unaositahili.

Wewe umenena la maana. Na hii ilikuwa ni bonge la kete kwao. Kama ccm wamelala cdm wangeonesha kitu kwa wananchi.
 
Mwenyewe mkuu wa nchi kasepa nje unataka Chadema wafanye nini au CCM mmefanya nini. Unafiki unakusumbua

Kumbe mmemuiga huyo... Sioni tofauti sasa ya waliopo na wanaotaka kuja.
 
Rais ana wawakilishi wake pale.
Kumbe hapo hakuna hata kiongozi mmoja wa Chadema awe diwani,mwenyekiti wa kijiji hata wanachama watakuwa wanamwakilisha Chadema na viongozi wake amka wewe uliyelala unashindwa hata kufikiri??Acha ujinga na uvivu wa kufikiri.
 
CHADEMA hawatengewi bajeti ya maafa wala ya barabara, waambie wenye hela zetu waende huko

Sawa Jabulani ball.... Kwa hiyo msaada huwa ni pesa tu? Arusha walienda kwani walitengewa bajeti ya maafa?
 
Yanatokea mafuriko., mbunge wa maccm anafariki mwenyekiti wa chama amaenda ulaya tuanze na hapa.

Kanumba na Mh. Bwanamdogo yupi rais alopaswa kuhudhuria msiba?

Mnajiita wakombozi alafu mnaiga ubovu za upande wa pili. Ipi tofauti yenu na hawa jirani zenu.
 
Mbona unataka kuwalaumu sana CHADEMA mbona Pinda anafanya ziara ya kukagua mabomba ya gesi, JK amepaa kwenda Vados unasemaje kuhusu viongozi wa kitaifa mbona wahajajumuika?

Kumbe mmewaiga hawa? Kisa hawajenda na nyinyi hamna time? Safi
 
kitengo cha maafa kinapo serikalini au chadema? Hatuna bajeti ya maafa mpaka tushike dola. Halafu sijui unatumia akili gani kuanzisha topic na sijui unategemea nini.

Sijui unatumia akili gani kuchangia uzi ambao unaulaum!
 
Kama mtanzania hauhitaji kuwa na fungu la maafa ili kumsaidia mtz mwenzio. Cdm n taasisi tena inayojipambanua wazi kwa watz kama wakombozi. Lakini katika hili kutokana na comment zenu wengi bado mmemisi. Wengi mnajikita et ccm, rais, w/mkuu hawapo. Kwa hiyo na nyinyi....
 
Yaani unategemea shetani akuonee huruma?

Chadema wanadai kuwa mafuriko yamesababishwa na CCM

Kwanza hawataenda huko mpaka mafuriko yaishe

nikweli shetani hana huruma kama anakula mpaka rambirambi za yatima na wajane,,,,,,
 
Back
Top Bottom