CHADEMA haya ya Morogoro nyie hayawahusu?

CHADEMA haya ya Morogoro nyie hayawahusu?

Lilambo

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2013
Posts
2,523
Reaction score
208
Kwa wakati mmoja nimesikia habari mbili tofauti ambazo zimetikisa kwa kiasi fulani nchi yetu.

1. Ni operation mpya iliyoanzishwa na chadema katika mikoa tofauti hapa Tz kwa kutumia chopa 3.

2. Ni suala la mafuriko kule morogoro na sehemu za dom. Mafuriko haya yamepelekea vifo na hali ngumu ya wananchi wa maeneo hayo.

LAKINI jambo la kushangaza ni wenzetu kuendelea na operation zenu ambazo mnadai ni kuwatafutia maisha bora watz kwann tusiungane na hawa watz wenzetu wa morogoro kwanza kisha kuendelea na operation zenu? Rejea bomu la Arusha; Wabunge wa cdm mliondoka bungeni vikao vikiendelea kwenda Arusha.

Lakini je hili la Morogor vp? Wenzetu hayawahusu? Kama lengo ni kuwasaidia watz kwa sababu uokozi wa serikali ya ccm ni mdogo. Na nyie wenzetu mko chopa tatu tusaidieni wala kuokoa watz wenzetu kule Mvomero na Kilosa+Dodoma. Kwa sababu ya Arusha hayana tofauti na haya.

Ni kipindi kigumu tuungane pamoja..... Mkinitusi poa tu tushazoea
 
Kwa wakati mmoja nimesikia habari mbili tofauti ambazo zimetikisa kwa kiasi fulani nchi yetu. 1. Ni operation mpya iliyoanzishwa na chadema katika mikoa tofauti hapa Tz kwa kutumia chopa 3. 2. Ni suala la mafuriko kule morogoro na sehemu za dom. Mafuriko haya yamepelekea vifo na hali ngumu ya wananchi wa maeneo hayo. LAKINI jambo la kushangaza ni wenzetu kuendelea na operation zenu ambazo mnadai ni kuwatafutia maisha bora watz kwann tusiungane na hawa watz wenzetu wa morogoro kwanza kisha kuendelea na operation zenu? Rejea bomu la Arusha; Wabunge wa cdm mliondoka bungeni vikao vikiendelea kwenda Arusha. Lakini je hili la Morogor vp? Wenzetu hayawahusu? Kama lengo ni kuwasaidia watz kwa sababu uokozi wa serikali ya ccm ni mdogo. Na nyie wenzetu mko chopa tatu tusaidieni wala kuokoa watz wenzetu kule Mvomero na Kilosa+Dodoma. Kwa sababu ya Arusha hayana tofauti na haya. Ni kipindi kigumu tuungane pamoja..... Mkinitusi poa tu tushazoea

Umeona Chadema pekee mbona Rais yuko nje na hajarudi kwa ajili ya hao wahanga ? Unataka Chadema ifanyeje sasa kwa mfano wakae tu ?
 
Waulizeni wanaokusanya kodi zenu nakama wameshindwa wakiri kushindwa na kuomba msaada.
 
Uliza swali Hilo kitengo cha Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu. ChADEMA sio Serikali Ndugu na sijui wanahusikaje!
 
Nyumba zenyewe za tembe elkopta 1 tu ya polisi imeshindwa kusogea chini ili iwaokoe, unadhani zikija nyingi si ndiyo zitabomoka kabisa? Hafu nikushauri siyo kila elkopta inaweza kuokoa ktk mazingira hayo hapo miti mingi nyumba haziko imara, Waulizeni JWTZ je hawana zile za kutolea misaada? ie kama za amarekani, waingereza, south Africa, German etc.?
 
Nadhani mafuriko ya Morogoro yanahitaji wataalam zaidi na sio siasa jamani. kama ni vifo Singida kwenye Noah na Kiteto ni wengi zaidi, maana mpaka sasa kifo kimeripotiwa kimoja. Pole sana kwa wote walioathriwa na mafuriko
 
Mbona mada yako iko out of context, wakati wa Bomu la Arusha CCM waliahirisha shughuli za Bunge, Je walienda hata kwenye mazishi??
Kwa nini sio CUF, TLP, UMD, NCCR, PPT MAENDELEO na unawakomalia CHADEMA tu?
 
Uloi nga mâché68;8481555 said:
Uliza swali Hilo kitengo cha Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu. ChADEMA sio Serikali Ndugu na sijui wanahusikaje!

kwamba mafuriko ni problem ya CCM?!!!
 
Mbona Rais amekwenda uswizi si bora ma-cdm yako kwa wananchi
 
Mbona mada yako iko out of context, wakati wa Bomu la Arusha CCM waliahirisha shughuli za Bunge, Je walienda hata kwenye mazishi??
Kwa nini sio CUF, TLP, UMD, NCCR, PPT MAENDELEO na unawakomalia CHADEMA tu?

Mtoa hoja anasema Chadema ina Chopa zenye kuweza kusaidia kusambaza misaada ya dharura, haya mjibu sasa.
 
watanzania wakipata tabu chadema ndiyo furaha kwao tena wanaomba na lingine lisombwe na maji.
 
Ushauri mzuri sana, nianze kukupa pole kwa matusi watakayokushushia.

P1010338.JPG
 
Mbona mada yako iko out of context, wakati wa Bomu la Arusha CCM waliahirisha shughuli za Bunge, Je walienda hata kwenye mazishi??
Kwa nini sio CUF, TLP, UMD, NCCR, PPT MAENDELEO na una
Mbona mada yako iko out of context, wakati wa Bomu la Arusha CCM waliahirisha shughuli za Bunge, Je walienda hata kwenye mazishi??
Kwa nini sio CUF, TLP, UMD, NCCR, PPT MAENDELEO na
unawakomalia CHADEMA
tu?
wakomalia CHADEMA

Mkuu si unajua mti wenye matunda? CHADEMA inaongoza wengine wamekalia viti ndo maana mlipa kodi anaona amdai hudumuma anaye ongoza!
 
Yaani unategemea shetani akuonee huruma?

Chadema wanadai kuwa mafuriko yamesababishwa na CCM

Kwanza hawataenda huko mpaka mafuriko yaishe
 
Back
Top Bottom