CHADEMA haya mnayoyafanya ndio yalipelekea tukaletewa Hayati Magufuli

Katiba iliyopo inaeleweka kwa wananchi? Katiba ya chama chako si ndiyo hiyo mkiti wako ameichakachua aendelee kuongoza milele na milele, umeshawahi kulalamika humu jinsi katiba yako ilivyochakachuliwa?

Ww ni bendera fuata upepo ila huna lolote ujualo. Ni kipi kinachoeleweka na wananchi wote ndio kibadilishwe? Kila siku mitaala ya elimu huwa inabadilishwa na kikundi cha watu wachache, je huwa wananchi wote wanaelewa kwanini mitaala inafanyiwa mabadiliko? Mimi sio muumini wa kiongozi kukaa madarakani zaidi ya miaka 10, na post zangu kibao zimo humu ndani nikipinga hilo. Mimi sio bendera fuata upepo kama ww tafadhali.
 
Sorry Mkuu, but kuna mahali cdm wanakosea

Tuwekee sehemu ccm wanapatia tena kwenye mambo ya msingi kama yafuatayo. Ccm enzi za JK waliimba umeme wa Gas ndio muarobaini wa nishati, umeme wa maji ni tatizo kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, na kwenye gas tutapata 5,000m. Ccm ya Magufuli chini ya miaka mitano, umeme wa maji ni wa gharama nafuu, na tutapata 2,115m, umeme wa gas hapana maana gas sio yetu tumepigwa. Hebu nitolee ushahidi usioacha shaka wa hiyo ccm kwa mifano hiyo halisi.
 
Amani iwe nanyi nyote.

Naomba niwakumbushe udugu wangu chadema, awamu ya nne mlipiga sana kelele kuwa kuna ufisadi, nchi haikuwa na Rais tunahitaji Rais Dikteta naomba niseme ukweli niliungana na CHADEMA, na katika uchaguzi niliisaidia kweli kweli kwa mapenzi ya kutoka moyoni

Mungu si Athumani tukaletewa jiwe, mwamba kweli kweli, ghafla tukashuhudia hakuna uhuru wa habari! utekaji kila kona, watumishi wakapauka na nataka niseme ukweli kura nilimpa Lissu na nilimpambania hadi kwa ndugu zangu.

Ila Mungu si mzee Hassan katikati ya giza katuletea mama, msikivu ndani ya miezi mitatu nyoyo zimetua, matumaini yamefufuka.

Mama msema kweli katwambia uchumi wetu umeyumba tupige kazi tuukuze, leo mnataka kuleta ngebe, ndani ya miezi mitatu mnataka katiba, hii ni sawa na kuoa mke kisha ndani ya mwezi unamdai mtoto hata mimba huchukua miezi 9 kuzaliwa.

Hayo mnayoyafanya ndo yalisababisha tuletewe jiwe, safari hii hatukubali, tutaenda taratibu na mama.
We mama k" Kama kwa kelele za CDM aliletwa magufuli. basi kwa kelele hizo hizo italetwa katiba mpya ya wananchi.
endelea kuiamini nguvu ya ushawishi ya chadema
 
Duh masikini ya Mungu..hamjitambui kabisa
Umeandika kama Magufuli bado yupo hai..
Mtaji wa kumpinga Magufuli haupo..
Lissu umaarufu wake kwa kumpinga Magufuli umeshashuka...

Watu wanamsikiliza Samia kuliko Lissu

The sands has shifted beneath...eleweni
Kumbe nawe huna akili

Watu husikiliza mtu mwenye hoja zenye facts na za kushawishi

Ikitokea lisu ana hoja atasikilizwa na ikitokea Samia ana hoja atasikilizwa pia

Siasa ni Zina dynamics nyingi wiki moja ni ndefu Sana kwenye siasa
 
Kwa aina ya siasa hi ya CHADEMA waungwana watakaa pembeni waendelee na hawo watoto waropikaji., maana ni kuishiwa hoja na kubaki na matusi matokeo yake ni kuambulia jela na kuanza lawama kwa serikali ambayo kila moja anaona mama ana nia na katiba mpya na ni imani ya wengi mchakto utaanza kabla hajamaliza muda wake ila wajinga wachache wanataka kutuharibia.
 
Back
Top Bottom