Kichaka cha Hayati Magufuli kitawatokea puani viongozi wa CHADEMA

Kulwa Jilala

JF-Expert Member
Sep 6, 2022
3,510
7,755
Hivi karibuni imezuka tabia ya kukwepa majukumu ambayo inapaswa kupingwa kwa hali na mali ndani ya nchi yetu.

Vyama vya upinzani hasa Chadema kila wanapopata matatizo kisingizio chao ni hayati rais Magufuli,!

Chadema wamesambaza mitandaoni vijana wa kumtetea Mbowe.

Kazi yao ni kuwapumbaza wanachama na wananchi kwa ujumla waone tatizo la chadema ni Magufuli wakati Magufuli hayupo na hakuwahi kuongoza CHADEMA. Kila uzi humu Jamii forum lazima vijana wa Mbowe wataje na kutukana mwendazake!

Mwenyekiti na aliyekabidhiwa usukani wa kuiongoza CHADEMA ni Mbowe lakini hawataki aulizwe chochote.!!!

Kutokana na Chadema kufa kila mahali kwa kupoteza mvuto na kukimbiwa na madiwani na wabunge ,viongozi wamebuni mbinu ya kukwepa aibu hii kwa kujificha kwa hayati rais Magufuli!

Viongozi wa Chadema wakihojiwa kwa nini chama hakina ofisi watakujibu tatizo ni Magufuli.

Tundu Lisu akiulizwa kuwa yeye ni makamu mwenyekiti wa CHADEMA lakini kwa nini hafanyi kazi za Chadema? Bavichaa watakujibu chanzo ni Magufuli!

Bavicha ukiwauliza kwa nini kamati kuu ya CHADEMA wanafanyia vikao vyao kwenye hoteli za kitalii na kuacha ukumbi wa ufipa ? Utajibiwa tatizo ni hayati Magufuli!

Chadema wakiulizwa kwa nini kwenye uchaguzi mliwatosa makada wenu waliokipigania chama ,mkabadili gia angani na kutuletea mgombea urais ambaye yupo kwenye list of shame(orodha ya chadema ya mafisadi wakuu wa nchi )? Utajibiwa tatizo ni mwendazake!

Bavicha na vijana wote mliosambazwa mitandaoni kumtetea Mbowe ,tambueni anayepaswa kuulizwa kuhusiana na mabaya na mazuri ya Chadema ni Mbowe na Tundu Lisu hao ndio viongozi wenu mliowapa ridhaa ya kuwaongoza kwa sasa.

Hayati Rais Magufuli hakuwahi kuwa kiongozi wa chadema ,hivyo kukaa mnamhusisha na kuporomoka kwa chama chenu ni kupoteza muda na kuonyesha uzwazwa wa hali ya juu.

Kuporomoka kwa CCM wataulizwa SAMIA na Dr Nchongolo na lazima watoe majibu kwa sababu wao ndiyo viongozi wa ccm kwa sasa.

Kwa nini nyinyi hamtaki kupata majibu kwa Mbowe badala yake mnataka majibu yatoke kwa Magufuli
 
Mtu mwenye akili timamu anataka jifu ( mfu mwovu ) JPM aendelee na urais akiwa kuzimu
MAGUFULI is dead, just for good reason.

Kwa nin inalazimishwa MBOWE amkosoe SAMIA hata kwenye mambo yaliyo njee ya uwezo wa SAMUA?

Mafuta na chakula bei dunia nzima yamepanda....

Kw nin wewe usimkosoe SAMIA?
 
He was kinda evil. Ni ukweli huo, mnanpenda mtaumia sana roho! Lakini mashambulizi ndio kwanza yanaanza. Mtapigwa na CCM mtapigwa na wapinzani.

Mbaya zaidi kesi zikianza kwenda mahakamani mtapata taabu sana.
Bila shaka wewe ni mmoja ya waliosambazwa na Mbowe
 
Na wakitaka wafanikiwe wasimwongelee kwenye majukwaa wataishia kuzomewa.
 
Vile mwendakuzimu amefurahia uzi wako huu kutokea huko kuzimu😁😁😁
downloadfile-4(1).jpg
 
Magufuli alisema msaliti wa nchi hatakiwi kuishi na baada ya masaa machache nikapigwa risasi ~~~~~ Lisu.

Kumbe anajijua kabisa ni msaliti
 
Chadema wasingechagua kumtukana mwendazake wangekuwa na nguvu ya kutisha sasa hivi
Wanachadema hakuna mahala maekua na agenda ya kumtukana mwenda zake! Sema hukujachorwa mstari sahihi unatenganisha kinachodhaniwa Ni matusi na kisichokua Tusi!
Tukikuomba ulete angalau matusi matatu yaliyotolewa Rasmi kwenye vikao rasmi au mikutano rasmi ya CHADEMA au press release yoyote iliyosheheni matusi sidhani Kama utaweza kuleta!

Sidhani kabisa kwa sababu kuna maneno ambayo alijitungiaa yeye akiamini kwamba yatambemba na kuvifanya jumuiya ya watanzania imuogope, ikawa kinyume chake! Mfano: Jiwe, Bulldozer, Jembe, Mwamba , Kichaa! Na Mambo Kama hayo! Sasa kwakua Yana Image mbaya inabidi CDM walamiwe na CCM juu ya majina hayo! Na kuyatafsiri Kama matusi.
 
Bora umepigwa ban, unalidhalilisha sana jukwa hili kwa mada zako za kipumbavu. Mods mungepiga life ban kwa Ids zake zote kwani ziinafahamika kwa uchafuzi wa mazingira hapa jukwaani
Wapi nimepigwa ban?, Utakuwa umeni quote kwa makosa, sio mleta mada.
 
Back
Top Bottom