CHADEMA hawana chao utawala wa Rais Magufuli

CHADEMA hawana chao utawala wa Rais Magufuli

Kiumweli Lizaboni sijaelewa. Chadema kwa sasa inaweza kuja na sera gani maana sera zile na ajenda zile muhimu zote Magufuli ndio anazisimamia na kwa nguvu zote. Hatari ninayoiona ni kwa vyama hivi sasa kuyumba na hata kufa. naomba ushauri wa kizalendo kabisa kabisa. Mparaganyiko unaousema ni kweli bila kuficha. Ni heri Dr Slaa angekuwepo kusukuma gurudumu hili. Sasa hivi baada ya kuwapokea na kuwasafisha wale watuhumiwa wa ufisadi, tulilazimishwa kuua zile ajenda na kuambiwa Shut-up!

Kama hawana Sera kwa nini mnatumia bunduki,mabomu na magari ya deraya kuwazuia wasiongee na wananchi? Waoga wakubwa nyie.
 
Kama hawana Sera kwa nini mnatumia bunduki,mabomu na magari ya deraya kuwazuia wasiongee na wananchi? Waoga wakubwa nyie.
Tunatumia hivyo kwa sababu wanafanya matendo yanayopingana na misingi ya kidemokrasia. Huwezi kuhamasisha vurugu then ukategemea ubaki salama
 
ru
CHADEMA kwa sasa wamepoteana.

Hakuna cha Mwenyekiti wala Katibu Mkuu.

Makamanda wao kwa sasa wamefarakana.

Wale nguli wa sheria waliokuwa wanawategemea kwa sasa hawana lolote. Ni baada ya Kisutu Kufumuliwa

Utawala wa Magufuli waliuchukulia poa sana na sasa unawatokea puani.

Mijadala mingi ya wafuasi wa CHADEMA mitandaoni ni ya malalamiko. Hata wale waliokuwa wanajenga hoja kama Malisa Godlisten, Ben Saanane na wengineo wamekata tamaa na sasa wamejiweka pembeni.

Ufipa hakukaliki tena. Kumekuwa ni hame la watoto wa jandoni.

Kelele nyingi kuhusu udikteta wa Rais Magufuli zimezimika mithili ya moto wa njiti ya kiberiti.

Asiyechaguliwa na wanachama na ambaye hakijui chama ndiye anayesimamia harakati za chama kwa sasa

Wale waliokuwa wanajiita CHADEMA Diaspora kwa sasa wameamua kususia chama. Hata yale matawi ya DMV na London kwa sasa yamebaki makumbusho tu.

Yule cha Mdomo na mtukanaji wao Mange Kimambi kwa sasa ameamua kujiweka pembeni kwa kisingizio eti bwana wake kamnyang'anya simu. Wanaona aibu

Ni mwaka mmoja tu wa Magufuli CHADEMA wapo hoi bin taaban. Wapo nyaka nyaka. Hawajiwezi.

Niwakumbushe tu kuwa siasa si mihemko. Siasa ni mikakati na mbinu za medani. CCM tuna mbinu zaidi ya 2000 za kutuwezesha kufanya siasa. Hata hii mbinu ya kuwaacha mjazane mitandaoni nayo ni mbinu. Kupitia humu kila mnachotema kinakuwa na tija kwetu.

Tukutane 2020
rudisheni rambirambi matapeli wakubwa
 
One man show is a big problem. Watz hatuna wengine wenye mawazo na michango bora kwa taifa lao zaidi ya huyo. Lets be serious. Watz tunahitaji mawazo n michango ya kila mtu kuivusha nchi ng'ambo ya pili.
Ilishatabiriwa kwa Magufuli kila goti litapigwa.

Mimba za ufipa zinachoropoka zenyewe moja baada ya nyingine.

Mwishoni kwenye hilo pagale atabaki Mbowe tu na mkwe wake
 
Yaani mwaka mmoja tu CHADEMA wapo nyang'anyang'a. Hiyo miaka mingine ndo watazidi kupotea. Ninachokiona hapa ni siasa za chadema Kufanywa na akina Bashe
Hivi mazoezi yale yote jeshi la polisi ni kupambana na chama kilichokufa?Kuzuiliwa mikutano ya kisiasa ni dalili tosha kuwa dikteta anajihami.Huwezi kujihami na mdhaifu,kama mwelewa utaelewa.Bunge mmeweka kwapani,yote haya kujihami,shame.
 
next time jifunze ku argue kwa hoja sio mipasho haisaidii kuondoa ukweli kuwa katiba mnaiburuza sasa bila shughuli za kisiasa vyama vinapataje wafuasi na vinauzaje sera zao kwa wananchi. alafu pia unaposema tumeshindwa unatumia muktadha upi zile kura ambazo dunia nzima inajua mlichakachua mkaona haitoshi zenji mkafuta kabisa the mnajisifu mmeshinda sasa kama mnajiamini mmeshinda kwanni hamjiamini sasa mkaacha tufanye siasa zetu bila bugudha?? kwa kweli watu kama nyie mnasikitish sana mnaturudisha nyuma enzi za chama kimoja ambapo fikra za mtu mmoja ndio zinatawala na sio mawazo mbadala.

Kuna mambo mawili mkiambiwa hayo mnaleta stories nyiiingi! Leta kifungu cha katiba na leta cheti cha kidato cha nne. Hivi kwa nini lakini. Naweza kuelewa hili la cheti kuwa kinaweza kuwa mbali, lakini hili la kifungu cha katiba kinachovunjwa nawaona mnafuata mkumbo tu kama Manyumbu. Katiba ipo hewani tena ya Kiswahili ni kiasi cha kukopi na ku paste humu jf tu basi. Mngetaka kufanya siasa bila bughudha mngeshinda, mbona mnaruhusiwa kufanya katika majimbo yenu mlioshinda? Mtafanyaje siasa sehemu mlizokataliwa? Kama uchaguzi uliibiwa, nitajie angalau wabunge watano unaodhani walishinda lakini waliibiwa kura
 
One man show is a big problem. Watz hatuna wengine wenye mawazo na michango bora kwa taifa lao zaidi ya huyo. Lets be serious. Watz tunahitaji mawazo n michango ya kila mtu kuivusha nchi ng'ambo ya pili.

Kwa taarifa yao dunianimipango iliyofanikiwa na kuleta tija mpaka leo ni ile ya one man show ndio maana hata sinema nyingi duniani zime adapt hiyo. Hakuna dunia yenye 'stering' wawili. Michangoyenu hiyo peleka kijijini kwenu kwenye umasikini wa kutupa, mbona huko hupeleki mawazo? Porojo tu, sema kwenye hayo majimbo ambayo kuna demokrasia na ushirikishwaji kukoje?
 
Tunatumia hivyo kwa sababu wanafanya matendo yanayopingana na misingi ya kidemokrasia. Huwezi kuhamasisha vurugu then ukategemea ubaki salama

Mnatumia wewe na nani? Wewe subiri tu utupiwe vipeperushi walivyoaanda wengine huko ndani utabaki kwenye korido mpaka unaingia kaburi, uwezo wako ni wa kulamba viatu vya wenye chama, size yako bk7 tu si zaidi ya hapo.
 
Hahahahahahaaaaaa! Mwaka huu umeuza korosho kwa shilingi 4000 kwa kilo. Mwaka jana uliuza kwa shilingi 1200. Hapo vipi?
Korosho ndio zao la biashara Tanzania, mbona sielewi? Hivi linalimwa Mwanza, Kagera, Morogoro, Dodoma, Iringa, Sumbawanga, Manyala, Njombe, Songwe au!! Mbona mmeishiwa hoja, Mnaacha kubadilisha mikataba ya madini, Gas, Mafuta na vitu vya maana, mnaingia kwenye vocha!!! Duh, kweli wakati ni ukuta.
 
Kitengo cha IT Lumumba kiko busy kweli lakini ukweli hujitenga na uongo uongo.
 
Kuna mambo mawili mkiambiwa hayo mnaleta stories nyiiingi! Leta kifungu cha katiba na leta cheti cha kidato cha nne. Hivi kwa nini lakini. Naweza kuelewa hili la cheti kuwa kinaweza kuwa mbali, lakini hili la kifungu cha katiba kinachovunjwa nawaona mnafuata mkumbo tu kama Manyumbu. Katiba ipo hewani tena ya Kiswahili ni kiasi cha kukopi na ku paste humu jf tu basi. Mngetaka kufanya siasa bila bughudha mngeshinda, mbona mnaruhusiwa kufanya katika majimbo yenu mlioshinda? Mtafanyaje siasa sehemu mlizokataliwa? Kama uchaguzi uliibiwa, nitajie angalau wabunge watano unaodhani walishinda lakini waliibiwa kura
SHERIA YA VYAMA VYA SIASA

SEHEMU YA PILI
HAKI YA CHAMA
4.–(1) Kila chama cha siasa kitakuwa na haki zifuatazo-
(a) Kutoa elimu ya uraia na elimu ya uchaguzi kwa wananchi kwa
kufuata sheria na kanuni za nchi;
(b) Kutoa maoni ya kisiasa kadri itakavyoona inafaa ili kutekeleza sera
zake, kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Katiba ya Zanzibar;
(c) Kujadili na kushindanisha sera zake na zile za chama cha siasa
kingine kwa lengo la kutaka kukubalika na wananchi;
(d) Kuwa na uhuru wa kutafuta kuungwa mkono na wapiga kura; na
(e) Kila Chama cha siasa kitakuwa na haki ya kufanya mikutano ya
kisiasa na maandamano kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa;
 
hapo juu nmekuwekea kipande cha sheria ya vyama vya siasa pia kasome katiba ibara ya 18 inatoa uhuru wa maoni bila kuingiliwa na mtu yeyote. pia umeongelea kuhusu kuibiwa kura majimbo ni mengi mkuranga,mbagala,kigoma kusini,nyamagana,kyerwa,kwela kwa naftali n.k mifano iko mingi ambapo mlitumia nguvu ya dola kuwabana wapinzani na hata kuingilia mchakato wa kuhesabu kura hadi mkatangaza wagombea wa ccm kwa nguvu na mabavu.
kuhusu swala la kufanya siasa majimboni hivi kweli imefikia stage tunapangiwa limits ya kufanya shughuli za kisiasa kutokana na kauli ya mtu mmoja tu wakati sheria ya vyama vya siasa imeruhusu kufanya mikutano ya kisiasa na kuuza sera kwa wananchi bila kuingiliwa as long as umepata kibali kwenye eneo husika. kma magufuli alitaka kuzuia siasa aende bungeni wafanyie amendment hiyo sheria na waseme siasa mpka 2020 kuliko kwa sasa ambapo mnataka kutuburuza kwa kauli ya mtu mmoja anayehisi yupo juu ya katiba na sheria za hii nchi. au kama anaona sisi tunambugudhi kwa kudai haki yetu then aende bungeni alete mswada wa kuwa na chama kimoja tu kuliko sasa ambako ccm pekee inapewa platform kwa mgongo wa serikali afu wapinzani mnatubana kwa kweli inakera sana. i rest my case
 
Umetenda vyema, na hapa ndipo nilipokuwa napataka.Katiba imeelekeza kufuata sharia ya vyama vya siasa. Katiba pia imetuelekeza kufuata sharia na kanuni za nchi. Je hizo sharia tunazifahamu? Hizo kanuni za nchi zinapatikana vipi? Lengo la kukuuliza kuhusu wabunge ni kutaka wewe uone uongo unaolishwa kuhusu kuipiwa kura. Wingi wa wabunge angalau unge reflect kama kweli mliibiwa kura. Hebu ongeza wabunge ishirini wa kuchaguliwa na rais vipi mngeweza kuongoza nchi kwa mujibu wa katiba? Mlikuwa uwezo wa kupata wabunge wengine ishirini? Huko mlipoibiwa kwa nini msiende mahakamani?
 
SHERIA YA VYAMA VYA SIASA

SEHEMU YA PILI
HAKI YA CHAMA
4.–(1) Kila chama cha siasa kitakuwa na haki zifuatazo-
(a) Kutoa elimu ya uraia na elimu ya uchaguzi kwa wananchi kwa
kufuata sheria na kanuni za nchi;
(b) Kutoa maoni ya kisiasa kadri itakavyoona inafaa ili kutekeleza sera
zake, kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Katiba ya Zanzibar;
(c) Kujadili na kushindanisha sera zake na zile za chama cha siasa
kingine kwa lengo la kutaka kukubalika na wananchi;
(d) Kuwa na uhuru wa kutafuta kuungwa mkono na wapiga kura; na
(e) Kila Chama cha siasa kitakuwa na haki ya kufanya mikutano ya
kisiasa na maandamano kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa;

20.-(1) Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheria za nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.
(2) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (1) haitakuwa halali kwa chombo chochote cha siasa kuandikishwa ambacho kutokana na Katiba au sera yake-
(a) kinakusudia kukuza au kupigania maslahi ya- (i) imani au kundi lolote la dini;
(ii) kundi lolote la kikabila pahala watu watokeapo, rangi au jinsia;
(iii) eneo fulani tu katika sehemu yoyote ya Jamhuri ya Muungano;

(b) kinapigania kuvunjwa kwa Jamhuri ya Muungano:

(c) kinakubali au kupigania matumizi ya nguvu au mapambano kama njia za kufikia malengo yake ya kisiasa;

(d) kinapigania au kinakusudia kuendesha shughuli zake za kisiasa katika sehemu moja tu ya Jamhuri ya Muungano;

(e) hakiruhusu uongozi wake kuchaguliwa kwa vipindi na kwa njia za kidemokrasia.

(3) Bunge laweza kutunga sheria inayoweka masharti yatakayohakikisha kuwa vyama vya siasa vinazingatia mipaka na vigezo vilivyowekwa na masharti ya ibara ndogo ya (2) kuhusu uhuru na haki ya watu kushirikiana na kujumuika.

(4) Bila ya kuathiri sheria za nchi zinazohusika ni marufuku kwa mtu yeyote kulazimishwa kujiunga na chama chochote au shirika lolote, au kwa chama chochote au cha siasa kukataliwa kusajiliwa kwa sababu tu ya itikadi au falsafa.
 
SHERIA YA VYAMA VYA SIASA

SEHEMU YA PILI
HAKI YA CHAMA
4.–(1) Kila chama cha siasa kitakuwa na haki zifuatazo-
(a) Kutoa elimu ya uraia na elimu ya uchaguzi kwa wananchi kwa
kufuata sheria na kanuni za nchi;
(b) Kutoa maoni ya kisiasa kadri itakavyoona inafaa ili kutekeleza sera
zake, kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Katiba ya Zanzibar;
(c) Kujadili na kushindanisha sera zake na zile za chama cha siasa
kingine kwa lengo la kutaka kukubalika na wananchi;
(d) Kuwa na uhuru wa kutafuta kuungwa mkono na wapiga kura; na
(e) Kila Chama cha siasa kitakuwa na haki ya kufanya mikutano ya
kisiasa na maandamano kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa;

SEHEMU YA KWANZA RAIS

Rais wa Jamhuri ya Muungano Sheria ya 1984 Na.15 ib.9

33.-(1) Kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano.
(2) Rais atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano na mamlaka yake Sheria ya 1984 Na.15 ib.9

34.-(1) Kutakuwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ambayo itakuwa na mamlaka juu ya mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano, na pia juu ya mambo mengine yote yahusuyo Tanzania Bara.
(2) Mamlaka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatahusu utekelezaji na hifadhi ya Katiba hii na pia mambo mengineyo yote ambayo Bunge lina mamlaka ya kuyatungia sheria.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania _________________________________________________________________
28
(3) Mamlaka yote ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano juu ya mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano, na pia juu ya mambo mengineyo yote yahusuyo Tanzania Bara, yatakuwa mikononi mwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
(4) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, madaraka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatatekelezwa ama na Rais mwenyewe moja kwa moja au kwa kukasimu madaraka hayo kwa watu wengine wenye madaraka katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(5) Ifahamike kwamba masharti yaliyomo katika ibara hii hayatahesabiwa kwamba-
(a) yanahamishia kwa Rais madaraka yoyote ya kisheria yaliyowekwa na sheria mikononi mwa mtu au mamlaka yoyote ambayo si Rais; au
(b) yanalizuia Bunge kukabidhi madaraka yoyote ya kisheria mikononi mwa mtu au watu au mamlaka yoyote ambayo si Rais.
 
Back
Top Bottom