Hizi ndizo swali najiuliza. Kwa mijibu wa sheria hii lazima wakaguliwe na mkaguzi alie teuliwa na CAG. Kama wanajikagua wenyewe hakuna uhakika wowote. Sio kwamba nawadhania vibaya, ila one never knows. Na ndio maana sheria inataka wapangiwe mkaguzi.
Haya tukija swali la pili nalo, hizo hesabu zilipokewaje na msajili? Je msajili alizipokea kama just for his information au alizipokea kama audited report?
Narudia tena: kwa mujibu wa sheria ya vyama Chadema haijakaguliwa.
Ninatumaini mwisho wa yote tutaupata ukweli. Hivi CAG na Msajiri walikuwa hawaijui sheria hii. Kwa nini hawakuitekeleza mpaka Kamati ya Bunge ipige kelele. Kwa maelezo ya Zitto wawili hawa walikuwa na woga, je wafikiri walikuwa wakimwogopa nani hasa, ambaye ana nguvu juu yao?