Juliana Shonza
JF-Expert Member
- Dec 19, 2012
- 2,009
- 1,607
Kwa muda mrefu tumekuwa tukieleza hapa jamvini na hata kwenye majukwaa ya kisiasa kuwa wapo viongozi wakubwa ndani ya vyama vya siasa ambao wanafanya ubadhirifu na kutumia pesa ya ruzuku kwa manufaa binafsi, lakini kama ilivyo kawaida ya waliofunga masikio na mioyo yao tukaambulia matusi na hata ban hapa jamvini. Lakini waswahili wanasema "sikio la kufa halisikii dawa" kama tungelisikilizwa kipindi kile na watu wale wakajirekebisha na kuacha tabia ya kugeuza chama cha siasa kuwa SACCOS yao binafsi basi hatari inayowakabili sasa isingelikuwa mbele yao.
Taarifa zilizopo mtaani na kila kwenye chombo cha habari ni juu ya Mwenyekiti wa PAC na Naibu katibu mkuu wa Chadema ndugu Zitto Kabwe kuahidi kuwapeleka mahakamani wale wote watakaodhihirika kuwa wamefisidi na kutumia pesa ya ruzuku ya chama kwa maslahi binafsi, baada tu ya kufanya ukaguzi kwenye vyama husika. Kwa wale tunaofahamu ukweli ni kuwa ukaguzi huo hautakiacha salama chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kwa maana yupo babu mtu mzima na kiongozi mkubwa wa Chadema ambae tunao ushahidi wa maandiko lakini pia ushahidi wa kauli yake kuwa amejikopesha pesa za ruzuku ya Chama. Sasa ataeleza kama lengo na matumizi ya ruzuku ni kukopeshana..? na kwa bahati mbaya maelezo haya ataenda kuyanyoosha vizuri akiwa kisutu.
Kimsingi ni lazima kila mtanzania regardless chama anachotokea, dini anayoiamini ama itikadi anayosimamia ni LAZIMA awe mstari wa mbele kuhakikisha kuwa anaitetea na kuilinda TANZANIA, kwa maana anaonyesha uzalendo na upendo wa kweli kwa TAIFA kwa kuwataja hadharani na hata kupeleka vielelezo mahakamani juu ya wale wote wanaofisidi na kula mali ya umma kwa vigezo na trick mbalimbali.
Nakuunga mkono zitto na natuma salamu kwa Babu ajiandae kukabiliana na PILATO wa Kisutu.