JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,460
====
"Wanaojaribu kufanya propaganda huko (Sakata la kina Mdee), suala hili limekwenda mahakamani, tuko tayari na mahakamani wametupeleka eneo ambalo kwetu ni kanda ya faraja, ni eneo tunalomudu. Sidhani kama kuna kesi ambayo Chadema ilishindwa mahakaamni, rekodi bazipo," - John Mrema.
"Fomu za kudhaminiwa kwa hawa wabunge 19, zilitoka wapi na zilikuwa za chama gani? Maana fomu za kudhaminiwa za CHADEMA hadi leo zipo. Katibu Mkuu aliyepeleka majina alikuwa ni wa chama gani kwa kuwa Katibu Mkuu John Mnyika hakuwahi kupeleka majina Tume ya Uchaguzi," - Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara
"Sasa tunakwenda kuwahoji (kina Halima Mdee), nani alisaini barua zao? Nchi hii ingekuwa inafuata sheria, wangekuwa na kesi ya jinai ya kughushi nyaraka na kujipatia fedha za walipa kodi kinyune cha sheria," - John Mrema.
"Ili mtu yeyote awe mbunge wa CHADEMA ni lazima ateuliwa ha kamati kuu ya CHADEMA kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA na mamlaka ambao kamati kuu imepewa," - Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara.
"Walipoitwa (Wabunge 19) kujieleza kamati kuu walisema wanahofia usalama wao na wakaomba wapangiwe siku nyingine. Katibu Mkuu John Mnyika aliwajibu kuwa wenye mamlaka hayo ni Kamati Kuu, hawakutokea. Hivi Mahakamani mshtakiwa asipotokea shauri haliendelei kusikilizwa?" - Benson Kigaila
Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Benson Kigaila amesema Chama hicho hakitaingilia taratibu zinazoendelea mahakamani kuhusu wabunge 19 waliofutiwa uanachama, huku akisisitiza kuwa hawakuwahi kumteua mtu kuwa mbunge wa viti maalum na hawautambui uchaguzi wa mwaka 2020 wala matunda yoyote ya uchaguzi huo