Chadema Digital yatikisa Mbarali, CCM yaanza kupagawa

Tulionya mapema sana kwamba , huu mpango wa Chadema wa kusajili watu nyumba kwa nyumba , na huku wengine wakifuatwa hadi mashambani utakuja kuleta mtikisiko , hiki ndicho kilichotokea huko Mbarali .

Kipo chama kinaanza kuweweseka kwamba Chadema Digital isifanyike wakati wa kazi au Week end , sasa wanataka tufanye lini ?View attachment 2831380View attachment 2831381View attachment 2831382View attachment 2831383View attachment 2831384View attachment 2831385View attachment 2831386
Hongereni.Lakini sisi CCM huwa hatutishiki na hatua za namna hiyo kwa sababu CCM ina mabalozi wa nyumba kumi,viongozi wa tawi na kata ambao wapo hapo hapo.
Nyinyi mtu anaenda kijijini akitokea mjini anasajili wanachama halafu anaondola kurudi mjini.Baada ya siku mbili waliosajiliwa wote wanarudi nyumbani.
 
Chadema kuna sehemu mnapwaya ziara ya wiki moja tu ya Mwenezi iliwafuta kwenye uwanja wa siasa mkaishia kumzungumzia Mwenezi kila alikokuwa anapita.

Mtatoboa kweli 2025?
 
Kanda hii ya Mbeya, Iringa, Njombe, Sumbawanga ni maeneo yetu mengine CHADEMA ipo imara.

Juzi juzi kasi ya CHADEMA imesababisha CCM kuitisha uchaguzi wa kumtafuta mwenyekiti wa mkoa wa Mbeya baada za taarifa ya kisiasa na kijamii kuonesha hali ni mbaya kwa chama dola kongwe hivyo wameamua kubadili uongozi pengine wanaamini itaweza kuzuia wimbi hili la CHADEMA kukubalika nyanda hizi.

Toka maktaba :

TOKA MAKTABA

2 Julai 2023
Mbeya, Tanzania

"HIZI SIO KAULI ZA MWENYEKITI WA CCM" - DR MPANGO AKASIRIKA AMVAA MWENYEKITI WA CCM MBEYA
Miradi mingi imekwama asema mwenyekiti wa CCM mkoa na kauli hiyo kumstua makamu wa rais

View: https://m.youtube.com/watch?v=u_plPg33ltk


Kuhusu bandari, mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya alisema haya :

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya ajitosa sakata la Bandari, na uwezekano wa CCM kuanguka kisiasa. Asisitiza Uhuru wa Kusema na kukosoa una manufaa



Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya Dr. Stephen Mwakajumilo aliye mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa NEC anajibu swali kuhusu sakata la bandari na uwezekano wa CCM kuanguka kisiasa kwa kukosa ushawishi na mvuto kwa wananchi.

Dr. Stephen Mwakajumilo asisitiza umuhimu wa utamaduni wa kusema kweli na kukosoa ni mzuri ili kuweza kurekebisha pale serikali ilipoishindwa ....

Noma sana
 
Hongereni.Lakini sisi CCM huwa hatutishiki na hatua za namna hiyo kwa sababu CCM ina mabalozi wa nyumba kumi,viongozi wa tawi na kata ambao wapo hapo hapo.
Nyinyi mtu anaenda kijijini akitokea mjini anasajili wanachama halafu anaondola kurudi mjini.Baada ya siku mbili waliosajiliwa wote wanarudi nyumbani.
Hujui kitu
 
Back
Top Bottom