CCM walitumia Pengo la Katiba na Sheria nyingine mbovu za Nchi Kwa ajili ya kushinda uchaguzi 2005
CCM walitumia Pengo la Katiba na Sheria nyingine mbovu za Nchi Kwa ajili ya kushinda uchaguzi 2005
CCM wanapoteza mwelekeo wake
Hakuna mtu yoyote asiyejua kuwa CCM wanatumia Rasilimali za Tanzania kwa ajili yao, yaani watu, Magari hata Fedha za Taifa, Tazama Kagoda na mengine jinsi yalivyoweza kufanikisha ushinda wa CCM mwaka 2005, nani asiyejua kuwa mambo ya ajabu hata mikakati ya Wanamtandao jinsi walivyopiga kampeni hata vyombo ya habari?? Je wapinzani walipewa fursa sawa katika vyombo vya habari Tanzania?? Je Tume huru ya Uchaguzi inawasikiliza Wapinzani?? Wewe Kaka yangu Mkandala unajua vizuri sana jinsi na sheria gani?? Kulikuwa na Sheria mbaya sana hata zile za Takrima?? Na Sheria za MWaka 1977 ya uchaguziHakuna cha pengo wala mjomba wake.. Unganeni, ondoeni tofauti zenu mtaishinda CCM hata wakileta mchawi toka Sumbawanga..hawawezi kuiba kura zote, watajaribu lakini Umati utawasuta.. wataiba ngapi jamani wakati hesabu ya watu waliojiandikisha inajulikana na wapiga kura watajua walichagua chama gani.. Sidhani kama CCM inaomba ya Zimbabwe, Kenya au Iran yatokee..
Jipangeni acheni tofauti zetu za kulilia ruzuku hamjengi kitu... Asiyetaka kujiunga atolewe akapange jiwe lake CCM..
Ni fedha zetu ndio zilizoanzisha CCM na pia kuna haja ya kurudisha mali zote wanaodhi CCM na kurudisha serikalini na kufanya uwanja uwe sawa na watu wote na vyama vyote
Siasa ni kila siku hata kama CCM watakuja na mbinu nyingi sasa watu wanaanza kuelewa kabisa na pia itafika kipindi watu wataona ukweli, Ni kwamba Chadema wasiache kujenga watu wapya na sio masalio toka CCM na Kufanya kiwe makini na endelevu, You know Tatizo kubwa ni vyama vyetu vinabebwa na watu, Hata CCM kwa kiasi fulani walitumia mbinu ya Mafiga matatu na kuchagua Wabunge wengi toka CCM, Hivyo utaona haya Mwakani maana kati yao wanaweza wasirudi Bungeni, Hivyo nilikuwa nasema kuwa wengi katika vyama hivi hakuna Progressive plans na kufanya kiwe hai na sio mtu baada ya uchaguzi, Tazama hali ya uzalendo kati yao kaka yangu Mkandala, utaona na kujiuliza kuwa Chadema wanajitahidi kufanya hivyo. Kuna kila dalili za kufanya vizuri, then NCCR ya wakati ule ilikosa sustainable ya kuendelea kwasababu ni kwamba walikuwa wanafocus uchaguzi tu na vyama husika, Kuna haja ya kuwa na vyama kuwa tayari ya uchaguzi, Kwa kipindi chote hiki tuona na tumepima vyama vytu, tunawajua mamluki na hatimaye watapoteza au kufa natural Death kama vile vyama vingine, Lazima hata sio leo basi ni siku zizajo tuone au kupata vyama kama 2 vyenye nguvu Tanzania.
Watu wanaogopa na Watu makini wanaogopa kuingia kwenye Siasa kwa ajili ya kuogopa Watu toka CCm, Siku inakuja na saa inakuja CCM utafika mwisho wao na wizi wa mali za umma, Kagoda, EPA, na Meremeta itakuwa mwisho wake. Mafisadi watakuwa mwisho wake
Hapana Siasa zinawahusu maisha yao kila siku, Hali ngumu ni kwasababu ya wanasiasa wetu, Kila kitu kina connection za tabia hizi na kwasababu hiyo ndio maana CCM wanatumia mianya kama hii kubana demokrasiaSiyo kuogopa mkuu. Kuna watu hawapendi siasa. Ujue kwamba siasa ni interest kama interest zingine. Na kwa wale ambao wanapenda siasa CCM ndiyo imefanya kazi kubwa zaidi ya kuwa shawishi wajiunge na vyama vyao. Je recruiting system ya Chadema ikoje? Hatua gani wanazo chukua kuhakikisha wana nyakua vichwa vinavyo weza kusaidia chama chao? Au ni mpaka hao vichwa wenyewe waamue kuwafuata na kuomba wajiunge? Siasa na kama mchezo. Wachezaji nyota na chipukizi ndiyo wana paswa kutafutwa kwa udi na uvumba. Siyo kuchukua has beens wa vyama vingine au kuchukua watu ambao obviously hawata kisaidia chama kwa lolote.
Kwani CCM wapo vipi?? Mbona kuna Ndoa kibao kule Bungeni?? Mbona kuna watoto kibao wa vigogo, Sio sababu hiyo bwana mzee, the Tazama miundombinu ya Tanzania na tena utagemea nini?? Mbona SITTA ni SPIKA, MKEWE ni WAZIRI?? Mbona kuna ndoa kibao CCM??