Josh Michael
JF-Expert Member
- Jun 12, 2009
- 2,523
- 77
- Thread starter
- #21
Napenda sana kwa vyama hivi vife kipo cha natural death ili tupate watu makini na walio na uchungu wa Kweli na Taifa letu Tanzania. Na pia kuna kila Dalili kwa CHADEMA kupewa au kusurvival katika mabadiliko haya, na pia hata haya ya CUF ni mtikisiko ambao utavikumba vyama karibu vyote, Kizazi cha Dot.com kinakuja na wala hawawezi kuzugwa na mambo ya CCM. Sisi tunasema kuwa mwanga wa Kweli upo mlangoni ni vyama husika kuona vinajitayarisha kukubali matokea haya. Chadema Kina Kizazi ambacho wao wanaweza kujua na kutambua na pengine hata CCM watashindwa kujua alama hizi na kutojua miiko yao ya uongozi na ndio maana unaona more contradicts za ajabu kati yao kuhusu ufisadi.Nina imani kubwa kuwa pole pole mambo yanabadilika - miaka 40 na ushee ina madhara yake na inachukua muda kudadilisha mtazamo katika jamii. Ni kweli muumgano wa vyama vya upinzani hauwezi kuwa rahisi kwani viongozi wake wengi ni uzao wa ukiritimba wa chama kimoja. Hata hivyo naanza kuona dalili za kizazi kipya kinaanza kupenya kwenye hizi anga na wazee pole pole wanawekwa kando. Muda si mrefu kuna vyama itabidi vife "natural death".
Chadema imeweza kufanikiwa kwa kiasi fulani katika hili wimbi hili la mabadiliko ya fikra. Tunaanza kuona viongozi wa vyama wakitofautiana wazi wazi na wanachama wao kwenye uchaguzi kama wa Tarime. Tulishuhudia kwa mfano wanachama wa NCCR wakitofautiana na viongozi wao na kushirikiana na Chadema licha ya maelekezo kutoka makao makuu kuwa wasitoe ushirikiano. Pia katika uchaguzi wa Busanda nina hakika wanachama wa CUF waliipigia kura Chadema.
Kuhusu Biharamulo pamoja na CUF kupoteza kada wake maarufu kwa Chadema, ni wazi waliokuwa wanachama wa CUF watakuwa nyuma ya mgombea wa Chadema na hivyo hivyo NCCR. Ni ukweli ulio wazi kuwa Chadema hivi sasa inaanza kuwa tishio kwa vyama kamaa NCCR, CUF, UDP, na vyama vingine vya upinzani na viongozi wake wanaanza kuinyooshea vidole Chadema badala ya CCM. Hili ni thibisho kuwa Chadema ina kila sababu ya kujiita chama mbadala.
Wazo la kutaka vyama viungane hivi sasa vina lengo la kuidhoofisha Chadema na mimi ningewashauri wawe waangalifu sana kwenye hili. Kuna kila dalili kuwa hivi vyama tayari vinachungulia kaburi na vina hatari ya kutumiwa - ushauri wangu ni kuwa kama chombo kinazama, wakati wa kutoka ni sasa kama alivyofanya Lwakatare. Wale wasioipenda Chadema wanaweza kurejea CCM lakini wale walio na nia ya kweli ya kulikomboa taifa mikononi mwa mafisadi, wajiunge na Chadema.
Kama kawaida woga unawaingia CCM
Homa ya Chadema umelitikisa Bunge
Mwaka 2010 wengi wataachwa kwenye mataa.
Labda Tume ya Uchaguzi na Jeshi la Polisi
ziipakate CCM - kama kawaida yao.