CHADEMA chama Mbadala kwa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA chama Mbadala kwa CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Josh Michael, Jun 27, 2009.

 1. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Baada ya Kupita kwa Miaka kama 4 hivi chama Cha Demokrasia na Maendelea CHADEMA, Kimeonyesha kuwa kipo makini sana katika kutoa motisha kubwa sana kwa Serikali na hata kufanya mambo makubwa sana katika Siasa za Tanzania.

  Mwaka 2007 Chini ya Dr.Slaa, Tindu Lissu, Na Vijana weingine wa CHADEMa waliweza kuja na List ya Mafisadi iliyotolewa Kule Mwembe Yanga Dar-Es-Salaam, Katika Orodha hiyo kulikuwa na Watu kama 11 hivi, Kati yao karibu wote wamefikishwa Mahakamani au kuanza kuchunguzwa na vyombo vya Dola, Kutokea Kipindi Hicho Katika Siasa za Tanzania Kulibadilika Sana na Kufanya hata CCM kuanza Kusema na Kuiga Lugha Za Upinzani na Kama vile nao ni Wapinzani.

  Kwa Miaka yote toka Uchaguzi uishe CHADEMA wamesimama Kidete Sana kusema Kuhusu Ufisadi na hata Kusababisha Serikali Kuanguka na Kuanda Serikali mpya, Yaani EL na timu yake kuacha Madaraka na Kuteuliwa Mtoto wa Mkulima Pinda, Hiyo yote ni Kazi ya CHADEMA na Watu makini sana katika kutetea maslai ya Taifa Letu la Tanzania.

  Chadema Mara zote wanakuwa wanapendekeza mapendekezo kadhaa katika maboresho kadhaa na hata CCM kuweza kuiga hata kuazima sera hizo.

  Leo hii Lugha za Wakina Selelii, Ole Sendeka, Dr.Mwakyembe Na Mama Kilango wasingeweza kusema hivyo kama Siyo CHADEMA,

  Buzwagi, Leo Katika Taifa la Tanzania kuna mambo mengi yaliyokuwa yanafanya kinyume cha Sheria na hata ukiukaji mkubwa sana wa haki za Binadamu, Tazama Mgodi wa North Mara na jinsi watoto, Wakimama Wanavyoteseka?? Utashangaa sana kusikia kuwa CCM kuwa Hawajui, Watu tuliwapa Dhamana ya uongozi wetu na kufanya watu kuwa wakimbizi.

  Bunge la Tanzania Leo Nimebadika kwa kiasi fulani kutokana na wabunge Kadhaa wa Upinzania na Hasa CHADEMA, Wakiongozwa na Rashid Mohamedi wa CUF.

  Leo Kila Sehemu kuna hali ya Mwamko hasa baada ya CHADEMA kuanzisha Kampeni Sangara na kufanya hata CCM kuanza kujibu mapigo.

  Leo Madudu yote ya Kagoda, EPA, ANBEN, Ufisadi mwingine usingeweza kusikika kama siyo CHADEMA. Kwa sababu hiyo CHADEMA wamejaribiwa kwa madogo na makubwa watayaweza pia!! Kuna kila Dalili za Kuona Chadema ni Chama Cha Upinzania makini Tanzania na Pia CCM wanajibu kujua wanapofanya au kufinya Demokrasia Tanzania ni kujitumbukiza katika Kaburi na kufanya kinyume cha matakwa ya kisiasa Tanzania.
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Jun 27, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Josh Michael,

  Mkuu Chadema bila kuunganisha vyama hakiwezi kuwa chama Mbadala..Ndicho pekee kilichobakia kwani wameisha jaribu sana miaka yote..

  Kila mtu alifikiria Chadema ni chama Mbadala toka mwaka 1994 lakini walivunjwa nguvu kabla ya uchaguzi na ujio wa Mrema na chama chake cha NCCR -Mageuzi, Kwa kutumia jina la Mrema CCM walifanikiwa kupandikiza mbegu chafu kuvunja nguvu ya Chadema na hakika waligawana Kura - Mshindi akawa CCM.

  Kabla ya Uchaguzi wa mwaka 2005 kila mtu alisema, Chama Mbadala ni Chadema. Na hakuna wakati Mbowe ameweza kutingisha nchi kama kuelekea uchaguzi wa mwaka huo.. Lakini, Chadema na uongozi wake wakashindwa kuelewa kwamba Umaarufu wa mtu kama Kikwete ndilo pingamizi kubwa ktk ushindi wao, Ujio wa Mbowe alikuja wakati mbaya kwani CCM walikuwa wakikata makali ya CUF.. Kikwete aliuzika kuliko Mbowe na Lipumba..

  Sasa pamoja na kwamba Kikwete anapungua umaarufu wake tusisahau kwamba CCM hawachoki kutafuta Fitna na mbinu za kisiasa kurudisha umaarufu wao ama kumwondolea mtu umaarufu kujaza kikombe chao..

  Wananchi hawatazami chama na sera zake..hawajui sera ni kitu gani zaidi ya ahadi za kisiasa hivyo wanachotazama ni MTU/WATU kwa bei ya mali sokoni..meaning ktk mazingira yetu samaki wazuri hawapatikani Shoppersrite, ila pale Kivukoni kwenye harufu na kila ghasia, ndiko utakuta watu wamejazana ktk mazingira ambayo wameyazoea hayawapi taabu.

  Soko la Kariakoo linavuta wateja wengi kuliko maduka yote ya mjini pamoja na kwamba ni chafu na halina mvuto..Na ndio maana kodi za nyumba na thamani ya eneo hilo nmi kubwa kuliko maeneo yote mjini Dar..

  Kwa mifano hii miwili nadhani utanielewa kwamba ni muhimu kwa Chadema kujifunza WATU na MAZINGIRA kuweza kujipanga vizuri na sio kufikiria mapenzi yao wao.. DJ mzuri ktk upangaji muziki ni yule anayeweka mashuzi yanayopendwa na wateja wake sio kile anachofikiria yeye kuwa ni baaabu kubwa!
   
 3. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #3
  Jun 27, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Ahhhggh!
   
 4. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #4
  Jun 27, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Siasa ni kila siku hata kama CCM watakuja na mbinu nyingi sasa watu wanaanza kuelewa kabisa na pia itafika kipindi watu wataona ukweli.

  Ni kwamba Chadema wasiache kujenga watu wapya na sio masalio toka CCM na Kufanya kiwe makini na endelevu, You know Tatizo kubwa ni vyama vyetu vinabebwa na watu, Hata CCM kwa kiasi fulani walitumia mbinu ya Mafiga matatu na kuchagua Wabunge wengi toka CCM, Hivyo utaona haya Mwakani maana kati yao wanaweza wasirudi Bungeni, Hivyo nilikuwa nasema kuwa wengi katika vyama hivi hakuna Progressive plans na kufanya kiwe hai na sio mtu baada ya uchaguzi, Tazama hali ya uzalendo kati yao kaka yangu Mkandala, utaona na kujiuliza kuwa Chadema wanajitahidi kufanya hivyo.

  Kuna kila dalili za kufanya vizuri, then NCCR ya wakati ule ilikosa sustainable ya kuendelea kwasababu ni kwamba walikuwa wanafocus uchaguzi tu na vyama husika, Kuna haja ya kuwa na vyama kuwa tayari ya uchaguzi, Kwa kipindi chote hiki tuona na tumepima vyama vytu, tunawajua mamluki na hatimaye watapoteza au kufa natural Death kama vile vyama vingine, Lazima hata sio leo basi ni siku zizajo tuone au kupata vyama kama 2 vyenye nguvu Tanzania.
   
 5. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #5
  Jun 27, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  CCM iko ngangari mkuu.
  Kuing'oa lazima upinzani uache ubinafsi na kutafuta umoja wa wapinzani kwanza.
   
 6. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #6
  Jun 27, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Watu wanaweza kufanya maajabu sana, na pia kwanini dhana ya unganisha vyama wakati kila chama kina sera zake na mambo yake?? Hakuna shaka kuwa lazima watu wajue kuwa chama gani kinatakiwa na hivi vingine vitakufa natural death tu,Watu wanaweza kufany maajabu sana. Hawa Watanzania mzee wangu
   
 7. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #7
  Jun 27, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  swali sio upinzani baali wanachi wa TZ kubadilika kiakili, na kadri siku zinavyoenda ccm wanaonyesha kuwadumaza kiakili
   
 8. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #8
  Jun 27, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Nyie huko dar hangaikeni kuungana, huku wilayani wanaungana. Muungano mpaka Poor Lipumba na Mbowe waungane?
   
 9. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #9
  Jun 27, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Na ndio maana nasema kuja haja na kuwa makini sana na wakati huu maana kuna kila dalili za kampeni kuanza na kuanza kuwadumaza Watanzania tena na kuwazuga tena, lakini wakati umefika kwa watu kusema sasa basi inatosha,
   
 10. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #10
  Jun 27, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Mkuu Josh heshima mbele.

  Ni mapema mno kubashiri kwamba CHADEMA ni chama mbadala kwa CCM katika muda mfupi ujao kwa kweli safari bado ni ndefu kuliko tunavyowaza.

  Zipo sababu kuu tatu zinazozinifanya niamini kwamba bado CCM itaendelea kushika dola kwa muda mrefu ujao hata kama hatupendi lakini ndiyo hali yenyewe ilivyo.

  Sababu ya kwanza ni katiba ya Tanzania bado inatoa mwanya kwa CCM kuendelea kugandamiza upinzani.Katiba ya Tanzania inatoa madaraka makubwa kwa rais wa JMT na mara zote CCM wamekuwa wakifaidika na madaraka ya rais.

  Rais anayo madaraka ya kumteua mwenyekiti wa tume ya uchaguzi pamoja na wajumbe wake wote.Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi akishatangaza mshindi wa uchaguzi kwa nafasi ya rais mahakama zetu hazina mamlaka ya kusikiliza wachilia mbali kutengua.

  Wasimamizi wa uchaguzi kwa nafasi za ubunge na madiwani ni wakurugenzi wa halmashauri wa wilaya. Kuwepo, kutokuwepo, kupanda cheo au kushushwa cheo kunategemea sana watawala ambao ni CCM. Wakurugenzi wengi wa halmashauri wamepanda vyeo hadi kuwa makatibu wakuu,mabalozi si kwasababu ya utendaji kazi mzuri bali hasa kwa wale walioweza kucheza karata zao vyema kama wakubwa waliowaweka madarakani walivyotaka.

  Vyombo vya ulinzi na usalama [polisi & UWT] wamekuwa wakitumika kuhakikisha CCM inabaki madarakani. Wakuu wa mikoa ambao ni wenyeviti wa vikao vya ulinzi na usalama katika mikoa yao mara vyingi utumia kofia zao za ulinzi na usalama kwa kulielekeza jeshi la polisi kuisaidia CCM hasa katika sehemu ambazo wapinzani wataonekana kuwa tishio kwa chama tawala. Wakuu wa mikoa tusisahau nao ni wateule wa rais hivyo niwajibu wao kuhakikisha aliyewaweka madarakani anaendelea kutawala.

  Sababu ya pili ni uelewa mdogo na umaskini uliopindukia wa wananchi/wapiga kura wengi wa Tanzania. Elimu ya uraia kwa wananchi wengi bado ni tatizo kubwa na pengine ni eneo ambalo vyama vya upinzani watatakiwa kulifanyia kazi kama watataka kuja kushika dola. Vyama vya upinzani vimejikita sana katika kampeni hasa kipindi cha uchaguzi kinapokaribia kitu ambacho si kizuri hasa tukizingatia aina ya watu tunaowalenga. Siasa za vyama karibu vyote vya upinzani ziko zaidi Dar na kwenye vyombo vya habari. Chama kikifanikiwa kuanzisha gazeti au kuwaweka watu wa kukipigia debe katika mitandao mbali mbali hasa Jamiiforums kinadhani kinaweza kuwa mbadala wa CCM.

  Umasikini wa wapiga kura na wananchi wengi ni mtaji mzuri kwa mafisadi ambao wengi wako CCM na wanazo fedha nyingi walizotuibia, mara nyingi uzitumia sehemu ya hizo fedha kuwahonga wananchi masikini ili kuendelea kulinda nafasi zao za kisiasa.Tumeshuhudua wenyewe jinsi mafisadi waliosababisha hasara kubwa kwa taifa namna walivyopokelewa kwa mbwembwe waliporudi kwenye majimbo yao ya uchaguzi.

  Sababu ya tatu ni CCM yenyewe bado iko imara kuliko tunavyodhani,bado ni chama ambacho kina mtandao ulioenea nchi nzima. CCM ina uwezo mkubwa wa fedha ukilinganisha na vyama vya upinzani. CCM ilifanikiwa kupora assets kama viwanja vya mpira kirumba Mwanza, Shekh Amri abed Arusha. Mkwakwani Tanga, Dodoma, Tabora na vingine vingi ambavyo vyanzo muhimu kwa mapata ya chama, wapinzani kwa kiasi kikubwa wanategemea mapato kutokana na mauzo ya kadi. CCM ina mtandao wa ofisi ulioenea Tanzania nzima kuanzia Kata mpaka taifa, vyama vya upinzani karibu vyote wana ofisi Dar na pengine kwenye miji ya kibiashara tu.

  CCM ina uwezo mkubwa wa kutatua migogoro yake ya ndani,hali ni tofauti ndani ya vyama vya upinzani. Vyama vyote vya upinzani havina uwezo wa kutatua migogoro yao ya ndani.Tumeshuhudia mgogoro wa uchaguzi TLP ulivyokididimiza.Tumeshuhudia mgogoro wa CHADEMA na Chacha Wangwe ulivyokisumbua chama.Tumeshuhudia mgogoro wa kugombea madaraka CUF uliosababisha Bwana Lwakatare kutimkia CHADEMA na bado itakuja mingi na tutashuhudia jinsi vyama vya upinzani vitakavyoshindwa kuhimili dhoruba za migogoro.

  Mwisho bado ninaamini ushirikiano baina ya vyama vya upinzani ni suluhisho sahihi kwa mustakabali wa maendeleo ya vyama vya upinzani.Leo hii CHADEMA inachekelea sana kwa kufanikiwa kumpata Bwana Lwakatare wa CUF kwangu mimi bado nawashangaa laiti Bwana Lwakatare angekuwa ametoka CCM hata mimi ningekuwa na sababu ya kufurahi lakini huyu Bwana Lwakatare katoka chama cha upinzani kunatofauti gani kuchukua fedha yako kutoka mfuko wa shati na kuziweka kwenye mfuko wa suruali. Viongozi wa juu CHADEMA wote wamehamia Bukoba kumpokea mpinzani mwenzao !!!!.

  Ndani ya bunge CHADEMA na CUF vinaunda muungano mzuri uliofanikiwa kwa kiasi kikubwa kuitikisa CCM nje ya bunge hawana ushirikiano ???????????. Wapinzani wanawachanganya wananchi kwa kukubali wao wenyewe kuparurana.

  Naomba kuwasilisha.
   
 11. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #11
  Jun 27, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  Hakuna Ajira, Watanzania tukale wapi?
  1. Watanzania wengi wanaishi kwa kubahatisha – Asilimia 28 ya vijana wanaoishi mjini hawana ajira.
  2. Wafanyakazi wanakandamizwa – mifumo ya ajira ya soko holela inawaminya.
  3. Wafanyakazi wanazidi kupunguzwa bila maslahi yao kuzingatiwa.
  4. Wafanyakazi wa Kitanzania wanalipwa mishahara midogo kuliko wa kigeni kwa kazi ileile.
  5. Mishahara na mazingira ya kazi bado ni duni.
  6. Hakuna juhudi mahususi za kutengeneza ajira kwa Watanzania.
  7. Hakuna takwimu sahihi za masuala ya ajira.
  8. Wawekezaji wanaajiri wageni hata kwa kazi ambazo kuna Watanzania wengi wanaweza kuzifanya.


  Serikali ya CHADEMA itatengezena ajiri nyingi na hasa kwa vijana, kivipi?
  1. Tutaweka kipaumbele kuweka mazingira ya kuongezeka fursa za ajira
  2. Tutatengeneza ajira milioni moja ndani ya mwaka mmoja wa utawala wa CHADEMA kwa kuimarisha sekta za ujenzi, madini, kilimo, utalii na huduma za jamii (walimu, madaktari na manesi)
  3. Tutakomesha ubaguzi wa ajira kwa watu wenye ulemavu na tutatoa motisha kwa mashirika yatakayoajiri watu wenye ulemavu na kuwaendeleza kitaaluma.
  4. Tutaweka sheria kali kulinda haki za ajira kwa wanawake na mashirika na makampuni yatakayo ajiri wanawake zaidi yatapewa motisha katika kodi na hata zabuni za serikali.
  5. Tutaweka mifumo yenye kulinda haki na maslahi ya wafanyakazi.
  6. Vyama vya wafanyakazi vitalindwa kisheria na kupewa nafasi kubwa katika kulinda maslahi ya wafanyakazi.
  7. Vyama vya wafanyakazi vitakuwa huru kweli kweli na itakuwa ni marufuku kwa serikali kuingilia utendaji wa vyama vya wafanya kazi.
  8. Tutasimamia wazawa na wageni wenye ujuzi unaolingana kulipwa sawasawa.
  9. Tutatunga sheria itakayohakikisha kuwa Wageni wataajiriwa pale tu hakuna mtanzania anayemudu kazi husika na kwamba Wawekezaji watafanya juhudi kufundisha Watanzania kumudu kazi hizo siku za mbeleni.
  10. Tutatoa msamaha wa kodi wa kiasi kwa kila atakaye ajiri mhitimu wa chuo mara baada ya masomo.
  11. Tutaweka kipaumbele umuhimu wa kurekebisha ajira na maslahi ya wafanyakazi
  [​IMG]
  Hali ya Elimu yetu Tanzania ikoje?
  1. Elimu bado ni ya kikoloni inayozalisha watwana.
  2. Mitaala haiendani na hali halisi ya kidunia.
  3. Wanafunzi wanalazimishwa kusoma kila somo kupata vyeti wakati vipaji haviendelezwi.
  4. Mpango wa Elimu ya Msingi wa kudandia uliyogubikwa na rushwa – Maandalizi ya walimu ni duni na rasilimali hazifikii walengwa.
  5. Bajeti ya elimu finyu sana – asilimia 9 tu!
  6. Tanzania ni nchi ya tatu kutoka mwisho duniani ambayo kiuwiano na idadi yake ya watu, ina idadi ndogo ya wasomi wa sekondari na vyuo.
  7. Elimu inawezeshwa kwa fedha za mikopo na misaada ya wahisani wakati fedha itokanayo na kodi atozwayo mwananchi inafanyiwa anasa tu.
  8. Gharama za elimu bado ni mzigo mkubwa kwa familia masikini.
  9. Mazingira ya elimu ni duni – madarasa, nyumba za walimu, maabara na vitabu.
  10. Mfumo wa Elimu hauna mtazamo wa Kijinsia hivyo hauweki mazingira mazuri ya kupata maarifa kwa wanafunzi wa kike na pia wanafunzi wenye ulemavu.
  11. Mazingira ya shule haya kidhi haja na sio rafiki kwa watoto wenye ulemavu wa viungo,wasioona na viziwi.
  12. Elimu ya teknohama hususan sayansi ya kompyuta haijaanzishwa.
  13. Mfumo wa elimu unaochelewesha kuhitimu – kuchelewa kuanza (miaka 7+) na kuchelewa kumaliza (2,7,6,3+)
  14. Elimu ya Uraia ni finyu na potofu.
  15. Michezo mashuleni imefutwa na hivyo kuziba vipaji vya watoto mfano UMITASHUMTA na UMISETA.


  Serikali ya CHADEMA itafanyaje ili kuboresha Elimu ya Tanzania?
  1. Itabadili mitaala ya elimu – Italenga mahitaji na maslahi ya Taifa, mitaala itakayochochea fikra, udadisi, ugunduzi na kuendeleza vipaji.
  2. Itatenga kwa sekta ya Elimu na Elimu ya Uraia asilimia 35% ya bajeti yote ya Serikali – italenga kuboresha mazingira ya elimu, ya ufundishaji na uboreshaji wa maslahi ya Waalimu na kuweka mazingira mazuri kwa wanafunzi wenye ulemavu kupata elimu bila vikwazo
  3. Kamwe elimu haitategemea misaada ya wafadhili na hatutakopa ili kusomesha Watanzania. Elimu italipiwa na fedha za ndani kutokana na makusanyo ya mapato ya kodi na pia mkakati utawekwa ili mapato yote yanayotokana na uchimbaji wa madini yalipie elimu ya watoto wa Tanzania.
  4. Tutajali walimu kwa kuboresha kipato, makazi na mafunzo yao.
  5. Mfumo wa elimu utarekebishwa kwa kiasi kikubwa na utakuwa na mtazamo wa kijinsia ili tuoe fursa sawa kwa wananfunzi wa kike na wenye ulemavu katika kujifunza.
  6. Elimu itatolewa bure kutoka CHEKECHEA mpaka SEKONDARI.
  7. Tutashirikisha wadau wote muhimu kuweka mfumo wa elimu unaowahisha kuhitimu – kuwahi kuanza (miaka 5) na kuwahi kumaliza (2,6,4,3+)
  8. Elimu ya msingi itakuwa mpaka darasa na tisa (Kidato cha Pili) na itakuwa ni lazima kwa kila mtoto anaeishi Tanzania.
  9. Ushirikishwaji wa jamii na wanafunzi katika uendeshaji wa shule utaimarika ili kuboresha ufundishaji na uwazi katika matumizi ya pato la shule.
  10. Elimu sahihi ya Uraia inayochochea kujitambua na uzalendo itafundishwa katika ngazi zote.
  11. Kila mwanafunzi wa sekondari atafundishwa somo la sayansi ya kompyuta na utumiaji wa kompyuta.
  12. Tutageuza majengo yote ya Serikali Dodoma kuwa vyuo vikuu na vyuo vya ufundi kwa kuendelea na azma yetu ya kuachilia mbali mpango wa kuhamishia makao makuu kwenda Dodoma. Dodoma itakuwa ni jiji la vyuo na kitovu cha elimu cha nchi.
  13. Uendeshaji wa shule za msingi na sekondari itakuwa ni jukumu la Serikali za Mitaa na Serikali kuu itatunga sera, kusimamia utekelezajiwa sera na kugawa rasilimali kama fedha.
  14. Tutaelekeza kila halmashauri kwa kutumia rasilimali zao kuanzisha vyuo vya ufundi katika kila wilaya.
  15. Tutatoa kipaumbele katika elimu ya ujasiriamali ili Watanzania waweze kujiajiri baada ya masomo.
  16. Tutarejesha masomo ya biashara katika shule za sekondari ili kuwajenga vijana wa Kitanzania waweze kujiajiri.
  17. Tutao ruzuku kwa shule za sekondari na vyuo vya elimu ya juu. Tutabadili shule za serikali kuwa ni vituo vya ubora wa elimu ili kuondoa matabaka.
   
 12. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #12
  Jun 27, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  Hali ya afya Tanzania ikoje?
  1. Serikali imekwepa jukumu lake la kutoa huduma za afya kwa wananchi, imelifanya kuwa la kibiashara kuliko huduma.
  2. Huduma za afya nchini zimezidi kupororoka siku hadi siku.
  3. Bajeti ya Wizara ya Afya haina mtazamo wa kijinsia kwani madawa mengi yanayoagizwa nchini ni ya magonjwa ya jumla.
  4. Mpango wa afya ya msingi umeshindikana – wananchi wenye uwezo wanatibiwa na wasio na uwezo wanakufa kwa magonjwa yanayotibika kama malaria na kipindupindu.
  5. Wanawake wajawazito hawana uhakika wa maisha yao wakati wa kujifungua kwani katika kila wanawake elfu moja wanaojifungua sita hupoteza maisha yao kwa sababu ya mfumo mbaya wa afya usiojali kazi muhimu ya kuzaa.
  6. Ni wanawake 47 tu kati ya wanawake mia moja wanajifungulia hospitalini. Mafunzo kwa wakunga wa jadi hayatoshi na hakuna juhudi za kutatua tatizo hili.
  7. Maslahi ya wafanyakazi wa sekta ya afya ni finyu.
  8. Pesa za vita dhidi ya ukimwi zinaishia mifukoni mwa wajanja wachache.
  9. Upanuzi wa sekta ya afya haulingani na ongezeko la watu – Daktari mmoja anahudumia wagonjwa.
  10. Wagonjwa wachache sana wa Ukimwi wanapata madawa ya kurefusha maisha – madawa mengi yaliyotolewa kwa msaada yanaporwa na vigogo.
  11. Gharama za afya bado ni mzigo mkubwa kwa wananchi wa kawaida kiasi cha kupelekea kujitibu kwa matabibu wasiyofuzu ilhali viongozi wakitibiwa nje kwa kodi ya wananchi.
  12. Mzigo wa kulea wagonjwa wa Ukimwi limeachwa kwa akina mama majumbani peke yao bila msaada wowote wa serikali (serikali kuu na serikali za mitaa).


  Serikali ya CHADEMA itafanya nini ili kuboresha huduma za Afya?
  1. Kupanua mpango wa bima ya afya kumshirikisha kila Mtanzania. Mkazo utawekwa katika kusisitiza ‘lishe bora' na siyo ‘bora lishe' – miongoni mwa wananchi Mamlaka za serikali za Mitaa zitaunda mfuko wa Hifadhi ya jamii kwa wananchi ili kuweka bima ya Afya kwa wananchi wengi vijijini.
  2. Mfumo wa Afya utajengwa kuanzia ngazi ya kijiji ili kupata mahitaji halisi ya madawa kutoka na historia ya magonjwa katika maeneo husika.
  3. Tutahakikisha bajeti ya wizara ya afya inakuwa na mtazamo wa kijinsia kwa kujali sana madawa muhimu kwa akina mama kufuatia masuala ya kimaumbile.
  4. Nguo za watoto wachanga kama nepi n.k hazitatozwa kodi VAT.
  5. Madawa yote muhimu kwa akina mama wajawazito na watoto hayatakuwa na kodi ya forodha na pia VAT.
  6. Ushuru wa forodha na VAT kwa vifaa vya hedhi utakuwa sifuri.
  7. Hamasa itatolewa kwenye utafiti, utumiaji na uboreshaji wa tiba zetu za asili.
  8. Elimu ya afya itatolewa ikiwemo kuhusu lishe ili kurekebisha mila na desturi ambazo zinaathiri afya ya jamii.
  9. Huduma zitakazolipiwa na serikali nje ya nchi ni zile tu zisizopatikana nchini na kwamba wananchi wote watapewa haki sawa ya kupata nafasi hizo.
  10. Vituo vya afya vitaanzishwa vijijini kuwapunguzia wananchi umbali wa kutembea kutafuta huduma za msingi.
  11. Itawajali na kuwahudumia Watanzania wenye kuishi na virusi vya ukimwi kwa kuweka mfumo bora utakaosimamiwa na serikali za Mitaa ili kuondoa mzigo wa kuhudumia wagonjwa kwa akina mama peke yao.
  12. Watanzania wote wenye kuishi na virusi vya ukimwi watapatiwa madawa {bure} na jamii kupitia serikali za vijiji na Mitaa na pia kupitia Asasi zisizo za kiserikali zitabeba jukumu la kuhudumia wagonjwa bila ubaguzi wa kijinsia.
  13. Tutatangaza malaria kuwa janga la kitaifa na tutoa huduma za afya kwa malaria bure.
  14. Huduma za afya zitatolewa bure kwa makundi maalum – waja wazito, vikongwe, wanafunzi, wenye kuishi na virusi vya ukimwi, watoto wachanga na walemavu

  [​IMG]
  Uchumi wa Takwimu, Umasikini kibao, kwa nini?
  1. Uchumi umekuwa kwa matajiri na wageni. Kwa Watanzania walio wengi uchumi unazidi kudorora.
  2. Bei za bidhaa zinapanda kifalaki kila mwaka-Petroli ilikuwa shilingi 450 mwaka 1995, mwaka 2005 imefikia shilingi 1,100 na inazidi kupanda.
  3. Pesa imepotea mifukoni mwa wananchi wakati maisha yanazidi kuwa ghali.
  4. Sekta zinazokuwa kwa kasi ni madini, utalii na utoaji huduma ambazo zinamilikiwa kwa kiasi kikubwa na wageni - ugenishaji
  5. Umaskini umezidi kuongezeka - asilimia 60 ya Watanzania wote maisha yao ya kiuchumi ni duni kuliko 1992.
  6. Kati ya Watanzania mia moja ni arobaini na nne tu wana uhakika wa mlo MMOJA kwa siku.
  7. Tofauti kati ya wenye kipato na wasicho nacho inazidi kuwa kubwa.
  8. Tumegeuzwa soko (dampo) la bidhaa hafifu za nje.
  9. Gharama ya kulipia mikopo holela kutoka nje inazidi kuwa kubwa – mikopo ya miradi isiyotekelezeka na miradi hewa iliyotafunwa na wajanja.
  10. Serikali ya awamu ya tatu imesambaratisha thamani ya shilingi ya Tanzania - Shilingi 575 iliweza kununua dola moja mwaka 1995, mwaka huu utahitaji takriban shilingi 1,200.
  11. Uchumi wa nchi unashikiliwa na wanaume wachache na wanawake kuwekwa pembezoni kabisa katika umiliki wa uchumi. Walio masikini zaidi katika Tanzania ni wanawake na hasa wa vijijini.
  12. Mchango wa wanawake wa Tanzania katika kukuza uchumi hauthaminishwi, mfano mchango wa kukaa nyumbani na kulea watoto na kutunza nyumba haupewi thamani ya kifedha katika kukokotoa pato la Taifa.
  13. Uchumi unakua mjini ilhali vijijini unazidi kuzorota. Umasikini wa Tanzania una sura ya Kijiji.
  14. Masharti ya mikopo ya mabenki kwa wanawake ni magumu sana.
  15. Serikali imepuuza kilimo ilihali kinachangia asilimia 44% ya pato la Taifa na 80% ya ajira.
  16. Bajeti zinapendelea walionacho - mfano kufutiwa kodi mafuta ya ndege


  CHADEMA itafanyaje WATANZANIA WOTE wafaidi matunda ya kukua kwa uchumi?
  1. Tutatunga na kutekeleza sera za uchumi zinazojali watu maskini (pro-poor economic policies).
  2. Tutahakikisha kuwa tunatoa kipaumbele kwa sekta zinazotengeneza ajira kwa watu wengi mfano kilimo.
  3. Tutatunga na kutekeleza sera ambazo zitaweka mazingira bora kwa Watanzania kufanya biashara na hasa biashara ya kimataifa ili kuongeza ajira na kukuza pato la mtu binafsi na pato la Taifa.
  4. Tutaweka mazingira ya Watanzania kumiliki uchumi wao wenyewe na kuwezesha wanawake kushiriki katika kumiliki uchumi wa nchi yao kwa kuwapa fursa zaidi na mafunzo bora na ya kisasa zaidi.
  5. Tutafuta misamaha ya kodi kwa wawekezaji wageni isipokuwa kwenye sekta ya kilimo na mifugo tu.
  6. Tutaimarisha benki ya rasilimali (Tanzania Investment Bank) ili itoe mikopo kwa Watanzania kwa masharti na gharama nafuu na hasa kuzingatia umuhimu wa mikopo kwa wanawake ili masharti yalingane na uwezo wa wanawake na vijana katika kulipa.
  7. Tutajenga miundo mbinu ya barabara ili kurahisisha kukua kwa uchumi kwa mikoa ya pembezoni. Barabara za kuunganisha mikoa ya Rukwa, Mbeya, Tabora, Shinyanga na Kigoma zitajengwa ili kuunganisha mikoa hii na nchi nzima.
  8. Tutaelekeza halmashauri za wilaya kuanzisha benki za jumuiya pamoja vikundi vya kuweka na kukopa.
  9. Mikopo ya nje itakuwa ni kwa ruhusa ya Bunge ili kuthibiti ukopaji usio wa lazima.
  10. Kuanzisha mfumo utakaomwezesha kila Mtanzania kumiliki mali bila mizengwe- ikiwamo mali za vipaji.
  11. Sheria zote za umiliki wa mali ikiwemo ardhi zitapitiwa kwa lengo la kuhakikisha haki ya kumiliki mali hasa kwa wanawake na vijana inalindwa kisheria na kufuta sheria au kanuni zote za ubaguzi katika kumiliki mali.
  12. Tutathamini mchango wa Wanawake katika kukuza uchumi kwa kutoa vipaumbele kwa wanawake katika elimu na nafasi za kazi kama ujira wa kazi wasiolipwa ya kulea Taifa.
  [​IMG]

  Hali katika sekta ya ardhi ikoje?
  1. Watanzania wote ni wapangaji katika ardhi yao – sheria za ardhi hazitoi mamlaka ya kumiliki ardhi kama mtu binafsi ama vikundi.
  2. Sheria hizi zinampa mgeni mamlaka makubwa juu ya ardhi kuliko mwananchi.
  3. Mfumo dume umetawala katika kumiliki ardhi – wanawake na vijana hawajapata fursa ya kumiliki au ‘kukodisha' ardhi.
  4. Wageni wanauziwa ardhi kama khanga.
  5. Mfumo mbaya wa ugawaji na umiliki wa ardhi pamoja na rushwa imesababisha utitiri wa migogoro ya ardhi.
  6. Wananchi wanaporwa ardhi zao kwa visingizio vya kuendeleza maslahi ya Taifa.
  7. Utaratibu uliyopo wa milki ya ardhi hautoi uhakika kwa wanyonge na maskini kumiliki ardhi yao.
  8. Kuna urasimu mkubwa unaoshawishi rushwa katika kutoa haki za kumiliki ardhi.


  Serikali ya CHADEMA itafanya nini ili kumilikisha Ardhi kwa Watanzania?
  1. Tutarejesha mamlaka ya asili ya wananchi kumiliki ardhi.
  2. Hatima ya ardhi ya kijiji itaachwa mikononi wa mamlaka ya Serikali ya kijiji.
  3. Rais hatokuwa na mamlaka ya kuhamisha ardhi kutoka kundi moja hadi jingine.
  4. Wageni watapatiwa ardhi kwa masharti yafuatayo - kutoimiliki, kutoiuza, kutoipora rasilimali na kutoitumia kwa namna itakayoharibu mazingira.
  5. Umilikaji wa ardhi kwa wanawake haitakuwa suala la mjadala tena. Mfumo dume wa kumiliki ardhi utatokomezwa na kufanywa historia.
  6. Utawekwa utaratibu wa kisheria utakaowawezesha wanawake kumiliki ardhi bila bughudha wala hofu ya kuporwa.
  7. Itaimarisha mabaraza ya ardhi ya vijiji na wilaya na kuhakikisha yanatoa haki kwa wananchi.
  8. Utawekwa utaratibu wa serikali kuwawekea mawakili wananchi wasio na uwezo katika mashauri ya ardhi katika ngazi ya mahakama kuu na mahakama ya rufaa.
  9. Tutatunga na kusimamia sheria zitakazo shughulikia uvamizi na ujenzi holela.
  10. Itatoa maelekezo kwa halmashauri kuendesha mipango ya ujenzi wa nyumba za bei nafuu za wananchi.
  11. Itarejesha nyumba zote za serikali zilizouzwa kwa upendeleo.
  12. Tutaunda baraza la Taifa la ardhi litakalowajibika kwa Bunge.
  13. Mahitaji ya ardhi kwa jamii za vijijini yatapewa kipaumbele kuliko mahitaji ya wengine.
  14. Tutalinda ardhi za vijiji dhini ya umegaji mkubwa ili kuepuka matatizo ya kijamii.
  15. Itahakikisha vijiji vinakuwa ni vitengo vinavyojiendesha na kujitawala vyenyewe na tutawezesha wanavijiji kushiriki kikamilifu kuendesha masuala yote ya ardhi kupitia vikao vya mkutano mkuu wa kijiji.
  16. Tutahakikisha wanyonge na maskini wanamiliki ardhi ya nchi yao bila ubaguzi wa jinsi wala umri.
  17. Madaraka ya kutoa haki za kumiliki ardhi yatakuwa chini ya mikoa (majimbo).
  [​IMG]

  Kilimo chetu kidemorora, kwa nini?
  1. Watanzania wengi bado wanalima kwa kutumia jembe la mkono.
  2. Kilimo bado kinategemea huruma ya mwenyezi Mungu kupata mvua.
  3. Soko finyu la mazao ya kilimo – Mengi yanaozea shambani, au kuuzwa kwa bei ya kutupa.
  4. Mifumo mibovu ya kuhifadhi na kusindika mazao ya kilimo.
  5. Sera potofu za soko holela zimeua kabisa motisha ya wakulima wa mazao ya chakula na yale ya biashara.
  6. Bado tunategemea mazao ya biashara tuliyorithi kutoka kwa wakoloni.
  7. Barabara hazifiki vijijini na hivyo mazao ya wakulima kuoza kabla ya kufika sokoni.


  Serikali ya CHADEMA itafanya nini kurejesha hadhi ya kilimo na Wakulima?
  1. Kodi zote za pembejeo za kilimo zitafutwa ikiwemo VAT.
  2. Itatilia mkazo wa kipekee barabara zingiazo vijijini.
  3. Tutatumia mabonde yote, mito na maziwa katika kilimo cha umwagiliaji maji.
  4. Tutarejesha vyama huru vya ushirika na mali zake.
  5. Serikali itadhibiti ya soko holela ya mazao ya kilimo.
  6. Tutatoa ruzuku kwa wakulima wetu ili wazalishe chakula cha kutosha na pia kupambana na ushindani wa bidhaa hafifu kutoka nje.
  7. Tutatoa motisha kwa wakulima kuzalisha mazao mbadala ya biashara km maua, viungo, mboga.
  8. Tutatoa motisha katika sekta ya usindikaji ya mazao ya kilimo – maelekezo kwa halmashauri ya wilaya kuweka mazingira ya uwekezaji katika usindikaji wa mazao yapatikanayo ndani ya wilaya.
  9. Serikali itashirikiana na nchi zingine zinazoendelea kushinikiza nchi zilizoendelea kulegeza masharti ya kuuza bidha zetu za kilimo katika masoko yao.
  10. Tutalinda soko la ndani la bidha zetu.
  11. Tutatafsiri kilimo sio tu kuishia katika kulima na kuvuna bali kwenye kuzindika na kuongeza thamani ya bidhaa.
   
 13. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #13
  Jun 27, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Tanzania hakuna chama mbadala mpaka sasa.

  CCM imeingiliwa na kirusi cha ufisadi na viongozi wanaojiona kuwa wananchi ni watumishi wao badala ya wao kuwa watumishi wa wananchi.

  Chadema wana baadhi ya viongozi ni wazuri ila inaelekea wana lack short & long term goals.

  CUF ndiyo kilikuwa chama cha upinzani chenye nguvu lakini wao naona kila siku ni kulalamikia tu CCM lakini sioni wakionyesha kuwa they can do better wakipewa usukani. Nawaona kama chama cha walalamishi tu.

  Vyama vingine they are not even worth mentioning maana ni vipo vipo tu.

  Haya maoni yangu tu wakuu.
   
 14. M

  Mkandara Verified User

  #14
  Jun 27, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Josh Michael,

  Tatizo letu sisi Wadanganyika ni kujidanganya.. kila siku tunarudia somo lilelile kwamba huwezi kumwondoa CCM bila muungano wa watu hasa vyama vya Upinzani kwa sababu nyingi sana za kimsingi ikiwa ni pamoja na katiba..huwezi kuleta mabadiliko ya aina yoyote ikiwa hujakaa IKULU wala kupata wabunge wengi bungeni zaidi ua chama hicho.

  Watazame CCM pamoja na mapungufu yao, pamoja na migogoro yote waliyokuwa nayo iwe kisera au mtazamo bado wanasimama pamoja inapofikia swala la Uchaguzi..

  Swala la sera hata watu wihtin one party wanatofautiana . TYumeyaona kwa Obama na Mama Clinton isipokuwa msisitizo ni mrengo. tanzania hakjuna chama chenye mrengo hivi sasa Chadema wenyewe wametoka kati Kulia na kuingia kati yaani Liberal..Ni Watanzania wangapi wanajua Liberal inasimamia sera zipi?

  Mkuu huu ni wakati wa kumwondoa CCM, Chadema TLP, NCCR na CUf inabidi waondoe tofauti zao kwa maslahi ya Taifa na sii ya vyama vyao. Ugonvhi kati yao unatokana na maslahi binafsi.. Nani hapatani na nani au nani mbihsi hawezi kuaminika au kueleweka.. forget all that, kwanza ingia Ikulu.

  Mbona Kikwete ameweza kufanya mabadiliko baada ya kuingia Ikulu.. waache wananchi wakupeni list ya viongozi wabovu mkisha ingia Ikulu kisha mfanye marekebisho.. hata yule mpuuzi Mrema anaweza kuwa mbora kati yenu nyote inapofikia swala la kuongoza kwani mawazo ya jukwaani hayaongozi nchi ila ni kifra mbadala zinapofanya kazi na kuleta mafanikio.

  Tumeyaona Kenya na sasa hivi Zimbabwe kwani huyo Morgan na Mugabe wana sera sawasawa..Leo hii Zimbabwe watu wanpumua kidogo na misaada inaanza kumiminika..

  Acheni ubinafsi na mpango wa kugombea majimbo haiwezi kuwasaidia kitu jamani mweee huu ni wakti wa kujipanga laa sivyo hata hayo majimbo mtayapoteza kwani kati yetu kuna siri nyingi zimekwisha sambaa na mtajiua wenyewe kusafisha njia ya CCM..

  take my word kwa mwendo huu sii Chadema wala CUF watakuwa pingamizi la CCM isipokuwa kama mtajipanga hata iwe nyuma ya Dr. Slaa kwa miaka mitano tu ya mwanzo..basi ushindi wenu..Kisha baada ya Ushindi ndipo mnaweza kupanga tofauti zetu kama Kenya walivyofanya..By 2015 CCM wamekimbia wote...
   
 15. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #15
  Jun 27, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Umesema ukweli lakini jua kuwa mambo haya yana mwisho wake, Kwa sasa hivi kwamba watu wanatafuta watu wa kuwapa dhamana ya uongozi lakini hakuna, Je kati yao hakuna hata mmoja ambaye anaweza kufanya au kuwa Mbadala ya CCM, Siamini kuwa CCM wanatatua migogoro yao ndani kwa ndani, but ni kwamba vyama vya Upinzania huwa wanajitangaza sana na watu kati yao kuna mamluki Kibao.

  Kuna wakweli kati yao na wengine sio. Na kama ulivyosema kuwa Katiba ndio inatoa madaraka makubwa sana, Je kuna Haja ya Kutokuwa na Uchaguzi kabla ya kudai katiba mpya. Je kama Chama kingine kikishinda Katiba ya leo itakuwa kama inahodhi kila kitu, Mambo kama haya yametokea Kenya ambapo Vyama vya upinzania vilikuwa vinadai katiba Mpya na Baada ya kushinda walianza kusema kuwa hawawezi kubadilisha katiba.

  Kuna haja ya kuwa na Katiba Mpya, na watu wafundishe jinsi gani ya kufanya Demokrasia ya Kweli. Kama kweli tunataka kujenga Tanzania ya Kweli
   
 16. M

  Masatu JF-Expert Member

  #16
  Jun 27, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Unacheza wewe!
   
 17. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #17
  Jun 27, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mimi nasema kuwa kuna Kizazi ambacho hata kama wakiwazuga hawezi kuzugika hata kidogo, Tazama yale ya Iran leo?? Mbona Kulikuwa na mapinduzi kwanini leo wamegawanyika?? Kipo Kizazi ambacho kitakuja na hawezi kuwazuga wa kununua maana wao sio Bei poa kama wakini Akwilombe na wengine walio kwenda huko, Nasema kuwa saa haja tena Haraka sana
   
 18. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #18
  Jun 27, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Si utoe basi na maoni yako na wewe mkuu? At least mwenzio anasema anachoona ni alternative basi na wewe sema chako. You can't simply disagree with a person you must show why.
   
 19. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #19
  Jun 27, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Maana Watanzania kama tuna vyama mfu nani anayepewa afadhali?? Je ni CHADEMA, TLP, CUF ni nani?? Maana vyama vyote ni mahututi au
   
 20. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #20
  Jun 27, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Nina imani kubwa kuwa pole pole mambo yanabadilika - miaka 40 na ushee ina madhara yake na inachukua muda kudadilisha mtazamo katika jamii. Ni kweli muumgano wa vyama vya upinzani hauwezi kuwa rahisi kwani viongozi wake wengi ni uzao wa ukiritimba wa chama kimoja. Hata hivyo naanza kuona dalili za kizazi kipya kinaanza kupenya kwenye hizi anga na wazee pole pole wanawekwa kando. Muda si mrefu kuna vyama itabidi vife "natural death".

  Chadema imeweza kufanikiwa kwa kiasi fulani katika hili wimbi hili la mabadiliko ya fikra. Tunaanza kuona viongozi wa vyama vingine wakitofautiana wazi wazi na wanachama wao kwenye uchaguzi kama wa Tarime. Tulishuhudia kwa mfano wanachama wa NCCR wakitofautiana na viongozi wao na kushirikiana na Chadema licha ya maelekezo kutoka makao makuu kuwa wasitoe ushirikiano. Pia katika uchaguzi wa Busanda nina hakika wanachama wa CUF waliipigia kura Chadema.

  Kuhusu Biharamulo pamoja na CUF kupoteza kada wake maarufu kwa Chadema, ni wazi waliokuwa wanachama wa CUF watakuwa nyuma ya mgombea wa Chadema na hivyo hivyo NCCR. Ni ukweli ulio wazi kuwa Chadema hivi sasa inaanza kuwa tishio kwa vyama kamaa NCCR, CUF, UDP, na vyama vingine vya upinzani na viongozi wake wanaanza kuinyooshea vidole Chadema badala ya CCM. Hili ni thibisho kuwa Chadema ina kila sababu ya kujiita chama mbadala.

  Wazo la kutaka vyama viungane hivi sasa vina lengo la kuidhoofisha Chadema na mimi ningewashauri wawe waangalifu sana kwenye hili. Kuna kila dalili kuwa hivi vyama tayari vinachungulia kaburi na vina hatari ya kutumiwa - ushauri wangu ni kuwa kama chombo kinazama, wakati wa kutoka ni sasa kama alivyofanya Lwakatare. Wale wasioipenda Chadema wanaweza kurejea CCM lakini wale walio na nia ya kweli ya kulikomboa taifa mikononi mwa mafisadi, wajiunge na Chadema.
  Kama kawaida woga unawaingia CCM
  Homa ya Chadema imelitikisa Bunge
  Mwaka 2010 wengi wataachwa kwenye mataa.
  Labda Tume ya Uchaguzi na Jeshi la Polisi
  ziipakate CCM - kama kawaida yao.
   
Loading...