Nimesoma michango ya Mheshimiwa Josh Michael ktk thread hii, na nataka kumshukuru kwa analysis ya Chadema na maendeleo yake. Ni zaidi ya miaka 17 sasa tangu nilipokaa na wale Watanzania wazalendo tukaandika malengo na madhumuni ya chama hiki. Tangu mwanzo tuliamini kwamba ni lazima Chadema kiepuke kung'ang'ania viongozi wazee. Kauli Mbiu zetu:-
VIJANA: TAIFA LA LEO!
WATOTO: TAIFA LA KESHO!
KINA MAMA :WALEZI!
WAZEE: DHAMANA.
Najisikia vizuri sana kwamba vijana wazalendo, jasiri, wabunifu, wengi wao wakiwa wasomi wenye huruma na umma wa Watanzania wanaotumbukia deeper and deeper katika lindi la umaskini kila kukicha kwa sababu ya ufisadi, wanaongoza CHADEMA sasa. Uongozi unaoona uchungu kwamba maliasili zetu zinaporwa na wageni wakishirikiana na chama cha mafisadi kupitia serikali yao.
Licha ya kwamba kuna wanaosita kwamba hatuwezi kuchukua dola mwakani, ni tumaini langu kwamba Watanzania wataonyesha kuchukia kwao ufisadi kwa kutuunga mkono ili tuikomboe Tanzania. Mafisadi kwetu iwe ni mwiko.
Nimewashauri vijana waendelee na "OPERESHENI SANGARA" kila mkoa, ili kusimika chama na kusambaza ujumbe kwamba vita dhidi ya ufisadi itaweza kufanikiwa tu pale kizazi kipya kitakapotwaa dola. Na katika vita hii, hata ongezeko la Wabunge wenye msimamo huo ni kuimarisha wapiganaji. Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke.