WAKATI Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kupitia kwa Msimamizi wa uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki, Trasias Kagenzi, ikisema kuwa itakuwa tayari kutoa majibu ya rufaa ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) juu ya utata wa Sioi Sumari ndani ya siku saba, chama hicho kikuu cha upinzani kimesema kuwa kimepata taarifa za uhakika kuwapo kwa mpango wa kumsafisha mgombea huyo wa CCM.
Rufaa hiyo ilikatwa NEC baada ya Kagenzi kutupilia mbali pingamizi la mgombea wa CHADEMA, Joshua Nassari, alilomwekea mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuhusiana na uraia wake.
Akizungumza jana katika mikutano ya kampeni ya chama hicho iliyofanyika katika eneo la Imbaseni, Kata ya Maji ya Chai, Meneja Kampeni wa CHADEMA, Israel Natse, alisema kuwa chama hicho kimepata taarifa za uhakika kutoka vyanzo vyake kuwa baadhi ya maofisa wa NEC walikwenda kuomba ushauri wa kisheria makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, jijini Arusha, wakitafuta namna ya kumsafisha Sioi.
Alisema kuwa taarifa za ‘kumsafisha' walianza kuzipata tangu juzi usiku, lakini jana wakapata taarifa nyingine zikisema kuwa maofisa wa NEC (hakuwataja majina) walikwenda EAC kutafuta ushauri wa kisheria, wakitaka ufafanuzi juu ya utata wa Sioi kwa kuangalia sheria za Kenya na Tanzania wakati mgombea huyo wa CCM alipozaliwa nchini Kenya, zilikuwa zinasemaje juu ya suala la uhamiaji, ambapo imedaiwa kuwa walipata ‘mwanya' katika sheria hizo.
"Tunataka kumwambia Mwenyekiti wa Tume, Jaji Lubuva, kuwa tunazo taarifa za uhakika juu ya kuwepo kwa mpango wa kumsafisha Sioi kuhusiana na rufaa yetu tuliyokata kutokana na utata wa uraia wa Sioi, tunaomba ajue tunajua mpango huo, tunamtaka yeye na tume yake watende haki," alisema Natse, ambaye ni Mbunge wa Karatu (CHADEMA).
Source:Tanzania Daima