CHADEMA chaishushia NEC tuhuma nzito Arumeru

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
WAKATI Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kupitia kwa Msimamizi wa uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki, Trasias Kagenzi, ikisema kuwa itakuwa tayari kutoa majibu ya rufaa ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) juu ya utata wa Sioi Sumari ndani ya siku saba, chama hicho kikuu cha upinzani kimesema kuwa kimepata taarifa za uhakika kuwapo kwa mpango wa kumsafisha mgombea huyo wa CCM.

Rufaa hiyo ilikatwa NEC baada ya Kagenzi kutupilia mbali pingamizi la mgombea wa CHADEMA, Joshua Nassari, alilomwekea mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuhusiana na uraia wake.

Akizungumza jana katika mikutano ya kampeni ya chama hicho iliyofanyika katika eneo la Imbaseni, Kata ya Maji ya Chai, Meneja Kampeni wa CHADEMA, Israel Natse, alisema kuwa chama hicho kimepata taarifa za uhakika kutoka vyanzo vyake kuwa baadhi ya maofisa wa NEC walikwenda kuomba ushauri wa kisheria makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, jijini Arusha, wakitafuta namna ya kumsafisha Sioi.

Alisema kuwa taarifa za ‘kumsafisha' walianza kuzipata tangu juzi usiku, lakini jana wakapata taarifa nyingine zikisema kuwa maofisa wa NEC (hakuwataja majina) walikwenda EAC kutafuta ushauri wa kisheria, wakitaka ufafanuzi juu ya utata wa Sioi kwa kuangalia sheria za Kenya na Tanzania wakati mgombea huyo wa CCM alipozaliwa nchini Kenya, zilikuwa zinasemaje juu ya suala la uhamiaji, ambapo imedaiwa kuwa walipata ‘mwanya' katika sheria hizo.

"Tunataka kumwambia Mwenyekiti wa Tume, Jaji Lubuva, kuwa tunazo taarifa za uhakika juu ya kuwepo kwa mpango wa kumsafisha Sioi kuhusiana na rufaa yetu tuliyokata kutokana na utata wa uraia wa Sioi, tunaomba ajue tunajua mpango huo, tunamtaka yeye na tume yake watende haki," alisema Natse, ambaye ni Mbunge wa Karatu (CHADEMA).

Source:Tanzania Daima
 
Sioni mantiki ya hiyo rufaa. Wameru wataamua kwenye box la kura.

Kwa kweli hekima na haki vinapaswa kutawala katika sakata la sioi pamoja na kuwaacha wana Arumeru waamue mbunge wanaye mtaka, bila hivyo watu wataumia sana.
 
Hivi nyie cdm kama sioyi wazazi wake wote ni watanzania tena wa kuzaliwa mnataka yeye aende wapi jamani acheni siasa za maji taka
 
Hivi nyie cdm kama sioyi wazazi wake wote ni watanzania tena wa kuzaliwa mnataka yeye aende wapi jamani acheni siasa za maji taka
akili zako ni kama JK kusamehe wezi wa EPA badala ya kutia ndani, huu ni utawala wa sheria
 
Hivi nyie cdm kama sioyi wazazi wake wote ni watanzania tena wa kuzaliwa mnataka yeye aende wapi jamani acheni siasa za maji taka

Kama wazazi wake ni Watanzania kuna taratibu zake. Kuna mke wangu wa rafiki yangu ambye wazazi wake ni watanzania na alikuwa akitumia passport ya TZ tangu utotoni. Lakini alipokwenda kubadilisha passport yake wakati akiwa above 18 alikataliwa mpaka atoe kiapo. Sasa kama Sioyi hakufanya hivyo then washa sheria ifanye kazi yake!!! Hatuko California ambako akina Arnold wanaweza kuwa magavana ingawa ni raia wa kuhamia.
 
Rufaa mkate nyie na majibu ya rufaa myajue nyie, kama mlikuwa hamna imani na NEC kwanini mlikata rufaa In the first place?
 
Hivi nyie cdm kama sioyi wazazi wake wote ni watanzania tena wa kuzaliwa mnataka yeye aende wapi jamani acheni siasa za maji taka
Angalia pia sheria zetu zinasemaje siyo kukimbilia kuwa wazazi wake wote ni wa Tanzania. Vinginevyo hakuna haja ya kuwapo hiyo sheria. Upo hapo?
 
Hivi nyie cdm kama sioyi wazazi wake wote ni watanzania tena wa kuzaliwa mnataka yeye aende wapi jamani acheni siasa za maji taka
sasa kama Sio ana pasi mbili za Kenya na Tanzania na umri wa kuukana uraia mmoja umeshapita sasa unategemea nini? Akiuza eneo huko Meru na kuwapa Wakenya si itakuwa too late???
 
sasa kama Sio ana pasi mbili za Kenya na Tanzania na umri wa kuukana uraia mmoja umeshapita sasa unategemea nini? Akiuza eneo huko Meru na kuwapa Wakenya si itakuwa too late???

Simamia kwenye sheria utajijibu na si mtazamo wako wa kiitikadi
 
Back
Top Bottom