CHADEMA baada ya miaka 28 hatimaye leo imekufa rasmi

CHADEMA baada ya miaka 28 hatimaye leo imekufa rasmi

Unajua kuna kitu watu hawajajua bado na wanaamini vyengine. Ukweli utawaweka huru.

Zisome vizuri zile kauli za jumuiya za kimataifa. Utaona kuwa Jumuiya zote zinaitambua serikali ya JPM mpya. Hakuna budi wapinzani nao wakaitambua tu, maana huko ICC hamna kitu nimetoka kutembelea website yao kuona kama kuna habari ya shauri kutoka TZ hamna kitu.

Mabeberu hawajawahi kusaidia wananchi ikiwa wananchi wenyewe wamekaa ndani tu badala ya kutoka nje kupambana damu ikamwagika. Hio kafara lazima iwepo ndio hawa jamaa wajue kuwa watu wapo serious na mabadiliko. Mkaambiwa na viongozi wenu maandamano kila mtu kakaa ndani. Nimegundua kuwa wenzetu upande wa pili wamekuwa wakitegemea damu za Wazanzibari zimwagike ndio wapate ukombozi wao, watu huku wakapambana na askari mwishowe wakauliwe, wakatekwa na kuteswa lakini upande wa pili wapinzani wapo JF wakisikiliza mshindo tu.
 
Kama kuna aliefungwa kwa ajili ya chadema leo ameambiwa "kilikuwa kiherehere chako"
 
Mbowe anaonesha dalili za uoga sna.CDM haipaswi kuendelea na watu wa dizaini hii
Wafute uanachama, anza kutengeneza wengine

CDM ni chama cha wananchi
Kumtengeneza mwanasiasa sio jambo jepesi...

Mwanasiasa amefuzu vitu vingi haiwezekani kufukuzwa kirahisi huko ni kukibomoa chama
 
Siasa bana kila mtu kachanguka kivyake kudadeki nani hataki "mambo ni mengi muda hautoshi"
 
Wakati CUF na NCCR Mageuzi vinakufa, zilifia ICU, lakini CHADEMA inakufa kama mtu aliyefia USINGIZINI. CHADEMA inakufa kama mtu ambaye hajauguzwa. Binafsi ninatamani CHADEMA yenye nguvu itakayoipa changamoto CCM, na sitaki kuiona CHADEMA ambayo imechakachuliwa Na kuharibu misingi Yao ya awali. CCM haiwezi kuondolewa na vyama dhaifu vinavyoamini kuwa Mabeberu ndio watashiriki kuiondoa CCM.
 
Wamesaliti kwa lipi ? Wameshindwa uchaguzi kwa halali na wewe unajitoa unafahamu kuliko wao waligombea. Watanzania tumechgua kwa hiari yetu bila kulazimishwa leo unajitoa ufahamu kwamba uchaguzi haukuwa wa haki ? Endelea kuamini hivyo na kupteza muda wako bure. Sisi ni CCM kwa mbele mpaka ichoke yenyewe kutawala.
Kuna ka msemo ka Kiswahili kanasema
"Hakunaga Umoja kwenye Njaa akitokea mwenye chakula "

Ni dhahiri shahiri huu msemo unatumika sasa kwa kile ambacho kinatokea na kinachoendelea kutokea ndani ya CHADEMA

Ni ujinga mkubwa kiasi gani kuona usaliti wa namna hii unatokea. Watu wamefungwa gerezani, kupigwa, kujinyima ili tu wapate haki yao halafu anatokea mtu ambaye alikua anawahimiza wananchi kujitolea anawasaliti mbele yao tena dakika za lala salama kabisa. Ina maana hawa wabunge wa CHADEMA walioapa kama Wabunge wateule wa viti maalumu hawajaona AIBU kabisa kwa usaliti wao huu!! Huku si kuwasaliti wanachama tu yaani umesaliti hata Nchi yao Mama.

Watu wanasaliti ilihali MAPAMBANO ya kutafuta haki bado yanaendelea. Inasikitisha sana

Halima Mdee na kikundi chake wamesaliti Nchi.Hawafai kufumbiwa macho kabisa.Wanafaa kuondolewa uanachama

Alamsiki
 
Huna lolote ukiona mshiko unachukua tu. Usitudanganye humu.
Kwa kuwa hunijui sitakulau. Ni kweli, ni watu wengi hawawezi kukataa ulaji kama huu. Lakini siyo mimi! Katu! Yaani niwe nimefanyiwa kama huyo dada aliyekaa rumande muda wote bila kosa halafu nije nitupiwe ''nyama'' kama mbwa ili kunipoza? Au niwe nimefanyiwa kama Halima Mdee, kura ziporwe kwa nguvu mchana kweupe halafu nije nitupiwe posho kama mbwa? Au kiongozi wangu niliyeshirikiana naye kupambana apigwe risasi kwa lengo la kuuawa kama Lissu halafu nije nitupiwe bakshishi nimsaliti? Du... acha nife na umaskini wangu kama ambavyo siwezi kuua ili nipate fedha.
 
Kuna ka msemo ka Kiswahili kanasema
"Hakunaga Umoja kwenye Njaa akitokea mwenye chakula "

Ni dhahiri shahiri huu msemo unatumika sasa kwa kile ambacho kinatokea na kinachoendelea kutokea ndani ya CHADEMA

Ni ujinga mkubwa kiasi gani kuona usaliti wa namna hii unatokea. Watu wamefungwa gerezani, kupigwa, kujinyima ili tu wapate haki yao halafu anatokea mtu ambaye alikua anawahimiza wananchi kujitolea anawasaliti mbele yao tena dakika za lala salama kabisa. Ina maana hawa wabunge wa CHADEMA walioapa kama Wabunge wateule wa viti maalumu hawajaona AIBU kabisa kwa usaliti wao huu!! Huku si kuwasaliti wanachama tu yaani umesaliti hata Nchi yao Mama.

Watu wanasaliti ilihali MAPAMBANO ya kutafuta haki bado yanaendelea. Inasikitisha sana

Halima Mdee na kikundi chake wamesaliti Nchi.Hawafai kufumbiwa macho kabisa.Wanafaa kuondolewa uanachama

Alamsiki
Sasa we bwege unasema mapambano yanaendelea ilhali ulipotakiwa kuandamana kupinga matokeo ukajiharishia. Leo umeamua kuandamana JF. Hopeless kabisa
 
Back
Top Bottom