CHADEMA baada ya miaka 28 hatimaye leo imekufa rasmi

CHADEMA baada ya miaka 28 hatimaye leo imekufa rasmi

Chademax2 pipozi pawa
Tanzaniax2 pipozi pawa
Tumia akili mtanzania
Chadema sio mali ya mtanzania
Tutawavuruga mkijivunia
Tukiteuliwa bungeni tunaingia
Hata mtuseme hatutosikia
Watoto ada tunalipia

Wimbo mpya wa mtoto wa kawe
 
KWA adabu na unyenyekevu naona speaker anatoa tabasamu mwanana la ushindi,sauti ya zege njaa ya week 3 keshalainika
MDEE.JPG
 
Kweli siasa kitu cha ajabu Leo hii Halima Mdee Hana tofauti na Paulina Gekul?.
 
Mkuu uko kama miye. Na mijitu mingine mpaka inauliwa ikiwa mbele kwenye maandamano. Ukiiuliza unapigania nini hasa hata haijui. Halafu kesho na kesho kutwa hao hao unaowapigania mpaka kuhatarisha maisha yako unawakuta wako pamoja wanafakamia keki ya taifa. Utopolo mtupu na kamwe sitakaa nishabikie mwanasiasa !
In one way or another siasa ni part kubwa sana maishani mwako. Ukitaka kushiriki ni juu yako lakini hata ulisema hushabikii itakugusa tu.

You can not run away from politics.
 
Kuna ka msemo ka Kiswahili kanasema
"Hakunaga Umoja kwenye Njaa akitokea mwenye chakula "

Ni dhahiri shahiri huu msemo unatumika sasa kwa kile ambacho kinatokea na kinachoendelea kutokea ndani ya CHADEMA

Ni ujinga mkubwa kiasi gani kuona usaliti wa namna hii unatokea. Watu wamefungwa gerezani, kupigwa, kujinyima ili tu wapate haki yao halafu anatokea mtu ambaye alikua anawahimiza wananchi kujitolea anawasaliti mbele yao tena dakika za lala salama kabisa. Ina maana hawa wabunge wa CHADEMA walioapa kama Wabunge wateule wa viti maalumu hawajaona AIBU kabisa kwa usaliti wao huu!! Huku si kuwasaliti wanachama tu yaani umesaliti hata Nchi yao Mama.

Watu wanasaliti ilihali MAPAMBANO ya kutafuta haki bado yanaendelea. Inasikitisha sana

Halima Mdee na kikundi chake wamesaliti Nchi.Hawafai kufumbiwa macho kabisa.Wanafaa kuondolewa uanachama

Alamsiki
Chadema haiwezi kufa kwa sababu ya Halima Mdee na kikundi chake , Jiwe kanunua wabunge wangapi na hakijafa? Jiwe ana dola katumia mbinu haramu na halali , zinazoonekana na zisizoonekana kwa miaka mitano lakina Chadema haijafa , Leo ndio ife , jambo Bora Ni kuwa sisi wanachadema tunajielewa Sana , yaani tunajitambua , intelijensia ya chama inajua walivyotishwa hao wanawake . Tutawafukuza watsbakizwa na Ndugai lakini tutaandika barua barua jamani hata mkiwapa uenyekiti wa wa kamati za PAC na LAAC bado hela hamtapata .
 
Hatuitaki ccm, na wala haimaanishi cdm wakiamua kusaliti misimamo ya kidemokrasia ndio tutaikubali ccm.
 
Kuna ka msemo ka Kiswahili kanasema
"Hakunaga Umoja kwenye Njaa akitokea mwenye chakula "

Ni dhahiri shahiri huu msemo unatumika sasa kwa kile ambacho kinatokea na kinachoendelea kutokea ndani ya CHADEMA

Ni ujinga mkubwa kiasi gani kuona usaliti wa namna hii unatokea. Watu wamefungwa gerezani, kupigwa, kujinyima ili tu wapate haki yao halafu anatokea mtu ambaye alikua anawahimiza wananchi kujitolea anawasaliti mbele yao tena dakika za lala salama kabisa. Ina maana hawa wabunge wa CHADEMA walioapa kama Wabunge wateule wa viti maalumu hawajaona AIBU kabisa kwa usaliti wao huu!! Huku si kuwasaliti wanachama tu yaani umesaliti hata Nchi yao Mama.

Watu wanasaliti ilihali MAPAMBANO ya kutafuta haki bado yanaendelea. Inasikitisha sana

Halima Mdee na kikundi chake wamesaliti Nchi.Hawafai kufumbiwa macho kabisa.Wanafaa kuondolewa uanachama

Alamsiki
Chadema ni itikadi, Chadema sio watu. Hata Lissu akifikia bei bado nitaamini kuwa Chadema ndo Chama chenye itikadi bora katika kuijenga Tanzania bora
 
Nadhani CHADEMA imetumia busara kubwa hadi kuwaruhusu wabunge wa upinzani. CHADEMA wametumia akili kubwa. Kwa sitiation iliyopo, muingie bungeni ama msiingie bungeni kila kitu kitaendelea kama kawaida. Mkiwa na msemaji mmoja tu bungeni anaweza kubadilisha upepo ambavyo isivyotarajiwa. Ingawa Mataga wanaweza kuona kwamba CHADEMA wamejimaliza ukweli ni kwamba chadema imepata pumzi mpya. Wamepata uwanja wa kuongelea...wamepata uwanja wa kusikaka midomoni mwa watu.

Sasa wawakilishi wachache waliopo bungeni wanaenda kutikisa bunge. Wanaenda kusikika kitaifa na kimataifa.

Mapambano ni mbinu. Na wakati mwingine mbinu zinaweza kuonekana za kijinga lakini ndizo zinazoleta mageuzi. Vuteni subira muone.

Mkuu Mandela aliwasumbua wazungu bila kuwa bungeni. Kwenye hilo bunge kibogoyo nani atawasikiliza? Hata waongee point vipi huko bungeni, rasmi tumepoteza imani na wao.
 
Fikra potofu alizonazo Magufuli na genge lake la akina Ndugai na Polepole ni kufikiri kuwa CDM ni Mbowe, Mdee, Lema, Sugu nk, nk..
Wanajitoa ufahamu na kujisahaulisha kuwa Upinzani uko ndani ya mioyo ya watanzania.

Kimsingi watanzania hawaitaki wala kuiamini tena CCM na ndo maana walinunua wabunge wa CDM wakadhani Chama kimekufa matokeo yake mziki waliuona ile 28 oktoba 20.

Mpumbavu atashangilia kufa CDM akiamini kura zote sasa itakuwa Kwa CCM, nasema huyo awazae hivyo ni Chizi na inabidi afuatilie enzi ya NCCR (Bara) na CUF (Zenji) ndo atajua wananchi wameichoka CCM..
 
Mkuu uko kama miye. Na mijitu mingine mpaka inauliwa ikiwa mbele kwenye maandamano. Ukiiuliza unapigania nini hasa hata haijui. Halafu kesho na kesho kutwa hao hao unaowapigania mpaka kuhatarisha maisha yako unawakuta wako pamoja wanafakamia keki ya taifa. Utopolo mtupu na kamwe sitakaa nishabikie mwanasiasa !
Wasaliti hata wakati wa Yesu walikuwepo
 
Fikra potofu alizonazo Magufuli na genge lake la akina Ndugai na Polepole ni kufikiri kuwa CDM ni Mbowe, Mdee, Lema, Sugu nk, nk..
Wanajitoa ufahamu na kujisahaulisha kuwa Upinzani uko ndani ya mioyo ya watanzania.

Kimsingi watanzania hawaitaki wala kuiamini tena CCM na ndo maana walinunua wabunge wa CDM wakadhani Chama kimekufa matokeo yake mziki waliuona ile 28 oktoba 20.

Mpumbavu atashangilia kufa CDM akiamini kura zote sasa itakuwa Kwa CCM, nasema huyo awazae hivyo ni Chizi na inabidi afuatilie enzi ya NCCR (Bara) na CUF (Zenji) ndo atajua wananchi wameichoka CCM..
Point tupu mkuu
 
Back
Top Bottom