CHADEMA Arusha yatoa mkono wa pole kwa jeshi la polisi Arusha

Mwan mpambanaji

JF-Expert Member
Apr 3, 2008
482
131
Baada ya kufanya mkutano mkubwa wa kumbukumbu ya Jan 5, na wanachi kuchangia Laki nane kwa ajili ya wahanga, leo viongozi wa wilaya wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti wa wilaya ambaye pia ni Diwani wa Levolosi Nanyaro, wametoa mkono wa pole kwa Askari aliyeuwawa na majambazi,habari kutoka ndani ya CHADEMA zinasema kuwa huo ni mchango wa wananchi wa Arusha chini ya mpango wa CHADEMA wa "they give us bullet we give them love".

Sambamba na hilo pia familia za wahanga zimekabidhiwa rasimi fedha zilizochangwa uwanjani juzi.

Nawasilisha

JESHI la Polisi nchini limekipongeza Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa kuonyesha ukomavu wake kisiasa kulikodhihirishwa na kitendo chake cha mchango wa sh 200,000 za rambirambi kwa ajili ya askari Kijanda Mwandu mwanzoni mwa wiki iliyopita mkoani Arusha.

Akipokea mchango huo wa rambirambi kutoka kwa viongozi wa CHADEMA, mkoa wa Arusha, jana, kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi hilo, Saidi Mwema, Kamanda wa Polisi wa mkoa, Thobias Andengenye, alisema kitendo cha CHADEMA kujitokeza na kushiriki nao katika msiba wa askari wake, kitafungua upya ukurasa wa mshikamano baina ya pande hizo mbili.

Kamanda Andengenye alisema pamoja na polisi kufarijika kwa kitendo cha CHADEMA kuungana na familia, ndugu na jamaa wa marehemu, hatua hiyo imedhihirisha kuwa jeshi hilo na marehemu Mwandu wanajituma kuwatumikia wananchi kwa moyo na kwamba hakuna chuki baina ya pande hizo mbili.

"Licha ya tukio hilo kudhihirisha kuwa makundi mbalimbali ya kijamii yanatambua na kuthamini mchango na umahiri wa marehemu kiutendaji wakati wa uhai wake, jambo kubwa ambalo litafungua ukurasa mpya kati ya polisi na CHADEMA ni kwamba mchango huu umedhihirisha kwamba hakuna chuki wala uhasama kati ya jeshi letu na chama hiki kikuu cha upinzani kama watu wengine wanavyofikiri," alisema Kamanda Andengenye.

Alifafanua kuwa wakati mwingine polisi na CHADEMA wamekuwa wakihitilafiana katika utekelezaji wa harakati, shughuli zao za kila siku na usimamizi wa sheria ambapo wakati mwingine hujikuta wakikabiliana bila kukusudia.

Kamanda Andengenye alisema fedha hizo zitaandikiwa taarifa na kuwasilishwa kwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Saidi Mwema, ambaye atapanga utaratibu wa kuzifikisha kwa familia ya marehemu Kijanda Mwandu aliyezikwa nyumbani kwao Magu, mkoani Mwanza, wiki iliyopita.

Msafara wa viongozi wanne wa CHADEMA waliokabidhi ubani huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Wilaya ya Arusha, Ephata Nanyaro, aliyeongozana na Mwenyekiti wa Madiwani wa CHADEMA katika Baraza la Madiwani Manispaa ya Arusha, Isaya Doita; Mwenyekiti wa Baraza la wanawake (Bawacha), wilaya ya Arusha, Gloria Shio; na mjumbe wa Kamati ya Utendaji wilaya, Sarah Fundikira ambao kwa pamoja walielezea kusikitishwa na kifo cha askari huyo aliyejitolea maisha yake kupambana na kudhibiti uhalifu.

Nanyaro ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Levolosi alisema CHADEMA kama wadau wa amani, utulivu na ulinzi wa raia na mali zao mkoani Arusha, wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha askari huyo pamoja na kujeruhiwa kwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Faustine Mafwele, katika tukio lililotokea Januari 3, mwaka huu, eneo la Shangarai, wilayani Arumeru.

"Fedha hizi kidogo ni mchango wa viongozi, wanachama, wapenzi wa CHADEMA na wananchi waliohudhuria mkutano wetu wa hadhara kuadhimisha kumbukumbu ya waliouawa na kujeruhiwa katika tukio la maandamano ya Januari 5, mwaka jana," alisema Nanyaro.


SOURCE:TANZANIA DAIMA
 
Good! Mnafanya vizuri sana kujitofautisha na wale wapenda shari ambao hitma yao kisiasa imefanyika hivi karibuni. By the way, wapi Nape? Au hili la askari kuuwawa na jambazi halikihusu chama chake?
 
Mbona inasemekana wale Polisi walifuata mgao! Inafahamika wazi kuwa lile eneo, vijana wengi wanajihusisha na uhalifu na Polisi huwa wanavamia na kuchukua mgao. Inasemekana kuwa Wahalifu walipata habari kuwa kuna mkakati wa Polisi na dola kuwaua Majambazi na ndio maana yule Jambazi alichukua hatua ya kuwafyatulia risasi zilizoua na kujeruhi Polisi.
 
Ndipo lile neno la wahenga linakamilika. USILIPIZE BAYA KWA BAYA.

Viva Chadema!!
Maandiko matakatifu yanasema hivyo!
 
Mbona inasemekana wale Polisi walifuata mgao! Inafahamika wazi kuwa lile eneo, vijana wengi wanajihusisha na uhalifu na Polisi huwa wanavamia na kuchukua mgao. Inasemekana kuwa Wahalifu walipata habari kuwa kuna mkakati wa Polisi na dola kuwaua Majambazi na ndio maana yule Jambazi alichukua hatua ya kuwafyatulia risasi zilizoua na kujeruhi Polisi.
Kweli hilo eneo wakazi wake wengi ni mabedui na polisi wanawajua hapo ukipata tatizo usiku usimwamini mtu awe mtoto au mwanamke wote nyan'gau
 
Ndugu zangu wana CHADEMA Arusha nawapongeza sana kwa moyo huo mliouonesha kwa hao police na mmewaachia funzo kubwa sana
 
Baada ya kufanya mkutano mkubwa wa kumbukumbu ya Jan 5,na wanachi kuchangia Laki nane kwa ajili ya wahanga,leo viongozi wa wilaya wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti wa wilaya ambaye pia ni Diwani wa Levolosi Nanyaro,wametoa mkono wa pole kwa Askari aliyeuwawa na majambazi,habari kutoka ndani ya CHADEMA zinasema kuwa huo ni mchango wa wananchi wa Arusha chini ya mpango wa CHADEMA wa "they give us bullet we give them love".Sambamba na hilo pia familia za wahanga zimekabidhiwa rasimi fedha zilizochangwa uwanjani juzi.
Nawasilisha

Safi sana, Mngewaachia na walaka wa samsoni mwigamba wabaki wanausoma.
 
Baada ya kufanya mkutano mkubwa wa kumbukumbu ya Jan 5,na wanachi kuchangia Laki nane kwa ajili ya wahanga,leo viongozi wa wilaya wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti wa wilaya ambaye pia ni Diwani wa Levolosi Nanyaro,wametoa mkono wa pole kwa Askari aliyeuwawa na majambazi,habari kutoka ndani ya CHADEMA zinasema kuwa huo ni mchango wa wananchi wa Arusha chini ya mpango wa CHADEMA wa "they give us bullet we give them love".Sambamba na hilo pia familia za wahanga zimekabidhiwa rasimi fedha zilizochangwa uwanjani juzi.
Nawasilisha

Ngongo uko wapi?
 
Na wasivyo na haya wamepokea ama kweli wamemeza ndoano ya chadema maana kwa waliyowafanyia CDM kama ni binadam wenye utashi na akili timamu wangejipotezea tu wasingepokea maana polisi wetu wanatia aibu kwa unyama wanaowafanyia wananchi na viongozi wa CDM kwa ujumla.
 
Safi sanaaaaaaaa!!!!!! Ukifanya afanyavyo MJINGA watu hawatakutofautisha nae Polisi wa nchi hii ni wajinga sana kwasababu nao pia ni wanasiasa.
 
Back
Top Bottom