Mwizukulu wa Buganda
JF-Expert Member
- Nov 19, 2024
- 638
- 1,771
Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina, ameendelea na mikutano ya hadhara jimboni humo, akihutubia wananchi wa Kijiji cha Mwabusalu, Juni 13, 2025.
Katika mkutano huo, wanachama na Viongozi wa vyama vya upinzani, akiwemo Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Kisesa, Tekla James, na mwanachama wa CHADEMA, Fabian Sai Masunga, walijitokeza kumuunga mkono Mbunge Mpina.
“Mpina hana shida, ila CCM ndicho chenye shida. Mtu mwema ni mwema tu, hata porini,” amesema Tekla James.
Naye Fabian Masunga amewataka wana-CCM waendelee kumuunga mkono Mpina, kwani anajua kazi na ana uchungu na wananchi.