Cha bure hata siku moja hakitokuja kukutosha

AbuuMaryam

JF-Expert Member
Dec 26, 2015
2,537
4,517
Wanatumia jina la sheria wakijitungia wenyewe.

Wanawapora watu mali zao kwa kuhalalisha uporaji wao kwa neno sheria na kanuni, wanaita kodi.

Sasa hivi ni rasmi KUTOKA SH 1000/- MPAKA 1500/- Kwa jina la kodi. Ila pesa ya bure huwa haitoshi, mwakani watatamani kuongeza tena.

Vitu vingi vinapanda bei na bei ya vitu haishuki hata kama gharama zipo chini au bei katika soko la dunia lipo chini, ila Tanzania bei itabaki juu na itazidi kupanda kwa hiki kinachoitwa kodi. Pesa ya bure. Hizi sababu zingine sijui dola imeadimika ni uongo, wao wanachotaka ni kodi tu, hawajali.

Ambayo kiuhalisia. Sehemu kubwa ya mapato inaenda kuwalipa wanasiasa. Na asilimia kidogo inaenda kwenye maendeleo. Ambayo ndio tunaambiwa "Kodi kwa maendeleo".

Ukisikia matumizi ya kawaida 60% UJUE NI MISHAHARA NA POSHO ZA WANASIASA, HALAFU 40% ZA MAENDELEO (Hapo ndipo kuna miradi ya maendeleo na mishahara ya wafanyakazi wengine kama walimu)

Wanahangaishwa machinga kwa ajili ya kodi.

Mishahara na viinua mgongo vya wafanyakazi wa umma kupanda haitungiwi sheria haraka haraka kama wanavyotunga sheria za kodi, na ikiongezwa mshahara wa wafanyakazi, mpaka ije kuonekana kwenye account yako, mtasubiri sana, ila kodi na mishahara ya wanasiasa ni haraka sana.

Ila sheria za mishahara yao WANASIASA WABUNGE. Sheria inatungwa kila mwaka tena kimya kimya.

Hii kodi inayotozwa kwenye umeme itaongezeka kila mwaka. Haitokuja kutosha pesa ya bure.

Hivi ninyi wanasiasa mbona mnajidanganya sana. Laiti ingekuwa kadiri pesa unavyokusanya ndivyo unavyozidi kuongeza umri wa kuishi hapa duniani. Ningewaunga mkono. Ibeni mtakavyoiba. Lakini pesa mnayokusanya haizuii kufa na kuiacha ili waliobaki wazifuje.

Kwani ukiwa na mabilioni kwenye account yako itakufanya uwe unakula kiroba cha mchele kwa siku...? Hii tamaa tu...Ila maisha yako hayatobadilika kwa kuwa na pesa nyingi.
 
Back
Top Bottom