waliwahi kuchomoa kwa Simba mshindi wa tatu
Moyoni mwako unajua fika kwamba Yanga hawawezi kuikimbia Simba Koko. Kilichotokea ni kwamba Yanga na Simba Koko walikaa kwa pamoja na kukubaliana kutopeleka timu uwanjani. Yanga, kwa kudhania kuwa wameongea na wanaume wenzao, kweli hawakupeleka timu uwanjani. Upande wa pili, jopo la wakuna nazi likaamua kwenda uwanjani kuchukua ujiko. Matokeo yake Yanga ikafungiwa kushiriki Kagame kwa miaka 3, jambo ambalo CECAFA wenyewe walijiiona wamechemka na kuamua kuifungulia Yanga mwaka juzi.
Kudhihirisha Yanga ni timu mume, taarifa za kufunguliwa zilikuja just one week kabla ya mashindano. Lakini kwa kuwa Yanga haiogopi vita, vijana wakazama ndani na kubeba ndoo. Msimu uliofuata (uliopita) Yanga tena wakabeba ndoo. Baada ya kuona Yanga anabeba ndoo mfululizo, CECAFA ikahofia Yanga italibeba tena na kulichukua moja kwa moja. Musonye akatumia janja ya kupeleka michuano Darfur.
Ukiwa na akili timamu, Darfur haiingii akilini kwanza hata watazamaji hakuna. Hii ni janja ya CECAFA ili isilazimike kununua kombe lingine. Na wanaogopa kulihamishia sehemu nyingine kwa kuwa wanajua Yanga wanayo jeuri ya kulichukua hata likichezwa Rwanda kwani Yanga imeshafanya hivyo mara mbili tofauti na Simba Koko ambaye yeye ni kama mbwa koko, yaani anabweka nyumbani tu, akiwa ugenini ni kama kondoo mgeni.
Ama kuhusu kukimbia uwanjani, yawezekana umri wako ndio tatizo. Ni Simba Koko ndio iliwahi kukimbia uwanjani mwaka 1993 (kama sikosei). Ilikuwa mapumziko na 3 zilikuwa zimeshapigwa ndio vijamaa vikaamua kubanisha kwenye vyumba vya kubadilishia nguo pale shamba la bibi. Baada ya refarii kuvisubiri kwa muda mrefu, aliamua kuvifuata huko ndani
'vikamjibu kuwa havitarudi uwanjani ng'o mpaka vipewe bagia na Dewji'
Kimahesabu Simba Koko wali-win. Enzi hizo ukiweka mpira kwapani mpinzani wako anapewa points 2 na magoli mawili, sasa wao ilikuwa mapumziko na tayari wameshalamba 3, kwa hiyo nitakuwa mchoyo kutowapongeza, ama hakika walitumia akili kupunguza idadi ya magoli.