CECAFA: Yanga yavuliwa Ubingwa - Kombe la Kagame

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,222
1,667
"Mabingwa watetezi wa Kombe la Kagame"

"Ni kwa kuwa hali ya Darfur siyo nzuri kiusalama."

Yanga yavuliwa ubingwa
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imesema kuwa haiwezi kuziruhusu timu za Tanzania kushiriki katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati...

Yanga ndiyo mabingwa watetezi wa kombe la Kagame
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imesema kuwa haiwezi kuziruhusu timu za Tanzania kushiriki katika mashindano ya Klabu Bingwa Afrika
Mashariki na Kati kutokana na hali ya usalama ya Darfur.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri, Amos Makalla baada ya gazeti hili kutaka kujua hatima ya timu za ushiriki wa timu za Tanzania katika mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika wiki ijayo.
“Nipo kwenye kikao cha baraza la mawaziri, hata hivyo hatuwezi kuziruhusu timu zetu kwenda eneo ambao si salama, pamoja na kusubiri taarifa rasmi kutoka kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,” alisema Makalla.
Kauli hiyo inaifanya timuza Yanga kupoteza ubingwa wake, huku Simba na Super Falcon kuachana na mashindano hayo kutokana na sababu hiyomuhimu. Timu hizo pamoja na Shirikisho la Soka nchini, TFF lilikuwa linasubiri taarifa rasmi kutoka serikalini.
Awali, Rais wa Shirikisho la Kandanda nchini, TFF, Leodegar Tenga alisema kuwa wao hawana taarifa zozote kuhusiana na uamuzi waSerikali zaidi ya kauli yaoya kwanza.
“Sina taarifa, labda wewe una taarifa rasmi kuhusiana na uamuzi wowote kuhusiana na hatima ya timu za Tanzania
katika mashindano hayo,” alisema Tenga ambaye pia ni Rais wa Cecafa.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe alisema kuwa hali ya usalama wa Darfur si nzuri na kuiomba TFF ifikirie upyauamuzi wa upeleka timu Darfur kwani kuna ushahidi kuwa hali ya usalama si nzuri.
“Tuna ushahidi kuwa hali ya Darfur siyo nzuri kiusalama, tumewaandikia TFF kuwaeleza hayo na kuwaomba wafikirie upya ushiriki wa Tanzania katika mashindano hayo,” alisema Membe.

CHANZO: MWANANCHI
 
da we jamaa ni aje mbona unatujazia jukwaa na habari isiyokuwa na kichwa wala miguu??hebu rudi kwa mwalimu wako wa imla ujifunze alafu uje kupost hapa
 
Kama hujashiriki na ni bingwa mtetezi,ukweli ni kuwa unakuwa umeutema ubingwa.
 
Yanga waache uoga!mbona timu zingine zinaenda kucheza huko darfur?wao wanasikiliza maneno ya media za ulaya na marekani kuwa sudan sii salama huku wanamezea mate mafuta.Waende waache upuuzi
 
Yanga waache uoga!mbona timu zingine zinaenda kucheza huko darfur?wao wanasikiliza maneno ya media za ulaya na marekani kuwa sudan sii salama huku wanamezea mate mafuta.Waende waache upuuzi
Serikali ndio imesema SUDAN sio salama(Benard Membe waziri wa mambo ya nje) kwa hiyo timu zake (Simba na Yanga ) zisiende
 
..afu mzigo wenyewe ni wa kucopy na kupest tu, anaweweseka...

...Una jambo umeliona kutoka chanzo
chochote cha habari? Hoja binafsi?
Usisite, liweke hapa uwahabarishe
wenzako...
 
waliwahi kuchomoa kwa Simba mshindi wa tatu

Moyoni mwako unajua fika kwamba Yanga hawawezi kuikimbia Simba Koko. Kilichotokea ni kwamba Yanga na Simba Koko walikaa kwa pamoja na kukubaliana kutopeleka timu uwanjani. Yanga, kwa kudhania kuwa wameongea na wanaume wenzao, kweli hawakupeleka timu uwanjani. Upande wa pili, jopo la wakuna nazi likaamua kwenda uwanjani kuchukua ujiko. Matokeo yake Yanga ikafungiwa kushiriki Kagame kwa miaka 3, jambo ambalo CECAFA wenyewe walijiiona wamechemka na kuamua kuifungulia Yanga mwaka juzi.

Kudhihirisha Yanga ni timu mume, taarifa za kufunguliwa zilikuja just one week kabla ya mashindano. Lakini kwa kuwa Yanga haiogopi vita, vijana wakazama ndani na kubeba ndoo. Msimu uliofuata (uliopita) Yanga tena wakabeba ndoo. Baada ya kuona Yanga anabeba ndoo mfululizo, CECAFA ikahofia Yanga italibeba tena na kulichukua moja kwa moja. Musonye akatumia janja ya kupeleka michuano Darfur.

Ukiwa na akili timamu, Darfur haiingii akilini kwanza hata watazamaji hakuna. Hii ni janja ya CECAFA ili isilazimike kununua kombe lingine. Na wanaogopa kulihamishia sehemu nyingine kwa kuwa wanajua Yanga wanayo jeuri ya kulichukua hata likichezwa Rwanda kwani Yanga imeshafanya hivyo mara mbili tofauti na Simba Koko ambaye yeye ni kama mbwa koko, yaani anabweka nyumbani tu, akiwa ugenini ni kama kondoo mgeni.

Ama kuhusu kukimbia uwanjani, yawezekana umri wako ndio tatizo. Ni Simba Koko ndio iliwahi kukimbia uwanjani mwaka 1993 (kama sikosei). Ilikuwa mapumziko na 3 zilikuwa zimeshapigwa ndio vijamaa vikaamua kubanisha kwenye vyumba vya kubadilishia nguo pale shamba la bibi. Baada ya refarii kuvisubiri kwa muda mrefu, aliamua kuvifuata huko ndani 'vikamjibu kuwa havitarudi uwanjani ng'o mpaka vipewe bagia na Dewji'

Kimahesabu Simba Koko wali-win. Enzi hizo ukiweka mpira kwapani mpinzani wako anapewa points 2 na magoli mawili, sasa wao ilikuwa mapumziko na tayari wameshalamba 3, kwa hiyo nitakuwa mchoyo kutowapongeza, ama hakika walitumia akili kupunguza idadi ya magoli.
 
Yanga waache uoga!mbona timu zingine zinaenda kucheza huko darfur?wao wanasikiliza maneno ya media za ulaya na marekani kuwa sudan sii salama huku wanamezea mate mafuta.Waende waache upuuzi

Mpuuzi ni wewe unayefikiri Yanga inajiongoza. Kwenda katika nchi ya watu huendi tu kama unavyoenda bar au bafuni, lazima serikali yako ikuruhusu na serikali ya unakoenda ikupokee.

Usiwe mpuuzi uliyepitiliza kiasi cha kuropokaropoka kama juha. Aliyesema Darfur sio salama ni Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa Bernard Membe (ama sijui kwa akili yako huyo ni media za Ulaya na marekani?!) na amesema hayo bungeni.

Na mbona uiseme Yanga tu, kwani uliambiwa Simba inaenda?

Ndio shida ya wanaume kuishia kusoma magazeti ya udaku badala ya kusoma magazeti yenye habari. Mambo aliyoyaongea Waziri Membe bungeni, mwingine anasema 'media za marekani'. Umeenda hadi kwenye mafuta
 
...Una jambo umeliona kutoka chanzo
chochote cha habari? Hoja binafsi?
Usisite, liweke hapa uwahabarishe
wenzako...
...yaaap yap..! mkuu lakini ili tuhabarike lazima habari iwe habari na si mhtasari wa habari,hususan kwenye forums kama hizi zinazosomeka kudunia kote, kwa mfano stori hii ulikuwa na kila sababu ya kutuliaaa kama unanyolewa na kuleta fulu story,ingetufaa wengi....
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom