Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,502
- 911,254
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Arusha kimewataka maaskofu wote na viongozi wengine wa dini mkoani hapa, kuvua majoho ya kazi yao na kutangaza kuingia katika siasa.
Katibu wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda alisema hayo jana mbele ya waandishi wa habari wa Jiji la Arusha na kuwataka maaskofu hao kuacha kuingilia mambo ya siasa yasiyowahusu ya Meya wa Jiji la Arusha.
Chatanda alisema, kitendo cha maaskofu kusema hawamtambui Meya wa CCM Arusha, Gaudence Lyimo kimewashtua na hakiwezi kuachwa hivi hivi.
Alisema viongozi wa dini wanapoingilia masuala ya siasa ni ukiukwaji wa majukumu yao hivyo bora wavue majoho yao na kuingia kwenye ulingo wa siasa kama alivyofanya Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa.
Chatanda ambaye ndiye anatajwa kuwa chanzo cha mgogoro wa uchaguzi wa umeya wa Arusha, hasa kutokana na kupiga kura kama diwani wa Arusha, ilhali alichaguliwa kama Mbunge mkoani Tanga, alisema masuala ya kisiasa waachiwe wanasiasa wenyewe.
Huyu Mama anajiona ana nguvu sana?
Anadhani kauli yake inatiliwa maanani na watu wangapi?...she is just a click, na sauti yake inaishia Magomeni!:-*.
Ni katika viumbe ambao Arusha inajutia kuwahi kuwapata!
maaaskofu wameingia hapo kwa kuwa kuna watu waliopoteza maisha..tulitegemea CCM mkoa iongelee namna ya kuzika wafu ...au kupekeka rambirambi na kuudumia majeruhi..........
Acheni upuuzi, kwani hii ni mara ya kwanza polisi kuuwa kwenye mitafaruku ya kisiasa hapa TZ? Hao watu wawili mlio watoa sadaka ni makelele chungu mzima! Mi naona CDM ni taasisi ya kanisa au vice-versa!(nilimskiliza uyo mama).
CCM wala hawana uzuni kuna watu wamekufa. wanachojua wao uchaguzi umekwisha anayeona kulikuwa na kasoro aende maakamani.
kwenye notebook yake akuna ata seemu aligusia abari za watu kupoteza maisha au ata kuonesha masikitiko kwamba kuna watu wamekufa. akili yake imajaa ccm = ulaji; ulaji = ccm.
Acheni upuuzi, kwani hii ni mara ya kwanza polisi kuuwa kwenye mitafaruku ya kisiasa hapa TZ? Hao watu wawili mlio watoa sadaka ni makelele chungu mzima! Mi naona CDM ni taasisi ya kanisa au vice-versa!
Adhabu ya anayeuwa mtu mmoja na aliyeuwa mia au zaidi uzito wake ni ule ule duniani na hata kwa Mungu......sijui inakuwaje wewe unabeza vifo vya wanaadamu wenzako [eti wawili]....bila kuongelea wale 40 ambao wanaendelea kuugulia na risasi kwenye miili yao.........unasema ni kelele!!!!!
unaonaje ungekufa wewe......au angekufa mtu wako wa karibu kabisa ....pia bado ingemfaa mtu kubeza.......!!!...usishangilie kifo cha mwanaadamu hata akiwa mmoja