CCM yawataka Maaskofu wavue majoho...

CCM yawataka Maaskofu wavue majoho...

Nawashauri CCM wampe Ulinzi huyo Mama maana mimi watu wa Arusha na wajua sana namna wanavyowathaimini Viongozi wao wa Dini halafu mtu mwingine tu anakuja na kuwabeza hadharani itakula kwake. Na zaidi watu wa Arusha ni wacha Mungu na wapole sana lakini wakigeuka hawasikiagila mnadi swala wala la Mhadhini Huyo Mama akae akijua hilo.
Lakini hebu wan JF nipeni CV ya huyo Mama tusijekuwa tunmhukumu bure kumbe sio yeye.

CV namba moja....1. Chakula ya wazee.
 
nadhani haya mauaji ya arusha ni malipo ya ile dhambi ya chadema kuuwa mtu pale maswa kipindi cha kampeni. Twende mbele turudi nyuma ukweli ndio huo.

maaskofu wanaendelea kujiumbua - kanisa = chadema = mauaji ya kimbari.

kama unayoyaandika ndio unayo yaamini heri iwe pamoja nawe, lakini kama ni ujasiri unaoupata kupita mavazi ya kijani siku yaja hambayo utotaka kukumbuka uliandika nini humu jf
 
Jukumu la Viongozi wa Dini ni kukemea maovu na uovu siyo zinaa na ulevi tu,ni pamoja na uporaji wa madaraka kwa kuchakachua uchaguzi na kuiba kura katika kuteua Meya, ni uhuni wa hali ya juu na lazima wahuni wakemewe na wasitambuliwe na viongozi wa dini
 
Nimemuona yule mama akiongea na press..kwa hakika ni ZERO brain,to be honest ajiuzulu kabisa ili uchunguzi wa kisheria ufanyike sio kubwabwaja pumba..These are the type of ppl CCM they want,just wapigadebe wasiojua wakifanyacho wao bora mkono uende kinywani na misifa....hafai,hafai..i daught mwisho wake utakuwaje!
 
Ni kweliChama chake CCM kimempangia Arusha au kakaa huko ili iwe rahisi kuchakachuliwa na waliompatia madaraka huku mumewe akiwa Iringa. Hili ni tatizo la aina ya viongozi wanaopewa kwa kuvua ........aibu na kichefuchefu. Pamoja na jamii kumwona EL hafai angalu kwa hili aliliona na kulikemea mapema Kichaa Makamba akaona heri damu imwagike iwe kafara za uongozi wao wanng'arishe nyota zinazonukua maana watalaamu wote ufundi umepungua mkulu nyota haing'ai tena
 
We need 2 tight nuts a little more on ccm. they have done enough stupid stuffs. we should pull them out!
 
Adhabu ya anayeuwa mtu mmoja na aliyeuwa mia au zaidi uzito wake ni ule ule duniani na hata kwa Mungu......sijui inakuwaje wewe unabeza vifo vya wanaadamu wenzako [eti wawili]....bila kuongelea wale 40 ambao wanaendelea kuugulia na risasi kwenye miili yao.........unasema ni kelele!!!!!
unaonaje ungekufa wewe......au angekufa mtu wako wa karibu kabisa ....pia bado ingemfaa mtu kubeza.......!!!...usishangilie kifo cha mwanaadamu hata akiwa mmoja

Au angekufa mwanawe wa kwanza
au Mke wake wa kitandani
au mama yake mzazi

Watu kama hawa ni kuwaombea nao wapatwe angalau kidogo halafu wanaone uchungu ni kitu gani!!!
 
kama unayoyaandika ndio unayo yaamini heri iwe pamoja nawe, lakini kama ni ujasiri unaoupata kupita mavazi ya kijani siku yaja hambayo utotaka kukumbuka uliandika nini humu jf

sijawahi kuvaa nguo ya kijani hata siku moja. hilo ni jicho langu la ndani. Nimechelea pasije kusemwa "Hawakuwepo watu wa kutuonya na kutukumbusha"
 
Mary Chatanda + Yusuf Makamba = TRUE CCM which think from the bottom
 
Tuzingatie maneno ya busara hapa chini kabla ya kutoa misimamo yetu. nimenukuu ktk thread ya jana.
Kadogoo said
Re: Maaskofu watoa tamko la kumkataa meya Arusha
Kanisa heri linyamaze na kufunga mdomo maana kila nikikumbuka mauaji ya kimbari Rwanda huwa nasikitika sana Kanisa linapoongelea juu ya haki! kila nikikumbuka mauaji ya Mwembechai Dar, na kauli alieitoa Padri Lwambano kuwa Serikali iwashugulikie Waislamu wa Msikiti wa Mwembechai na siku ya pili Polisi waliitikia wito huo na kuuwa wananchi wenzetu! nasikitika tena Kanisa kuhubiri haki!

Kila nikikumbuka mauaji ya raia huko visiwani na kauli ya Muadhama Kardinali
Pengo kuwa waliouliwa na Polisi huko Zenji ndio wabebe lawama kwa kutokutii amri ya Serikali ya kutokuandamana!!

Sasa, leo Kanisa na Baraza la Maaskofu watakuwa na ubavu gani wa kujitokeza na kulaani mauaji ya Arusha?

Kuna watu wengine wapumbavu watakao fikiri kuwa mimi nafurahia mauaji ya Arusha lakini kwa hakika kila binaadamu mwenye hisia hatafurahia kitendo hicho cha Askari wetu kufyatua risasi za moto na kuua wananchi! ni tendo la kulaaniwa lakini sio Maaskofu wajitokeze leo ghafla na kutoa kilio cha kinafiki! kwanza waombe msamaha kwa maovu waliofanya huko nyuma kwa kuunga mkono maamuzi ya Serikali ya Benjamin Mkapa ya kuuwa raia wa nchi hii na ndipo wafungue ukurasa mpya wa kudai haki za wananchi kinyume chake itakuwa vigumu kuelewa lengo la Kanisa ni nini!

Anko Sam said
Re: maaskofu watoa tamko la kumkataa meya Arusha
Originally Posted by zomba https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ya-wa-ccm-arusha-post1460753.html#post1460753
Hawa maaskofu ndio kiini cha chokochoko, fitna na uzabizabina. Kuna zaidi wanachokijuwa?

Haya, wamkatae meya, sasa wamkatae ana chaguo la mungu. Si walioteshwa?
"Zomba mimi nakushangaa sana, maana siku hizi UMEHARIBIKA KABISA, kwani huko nyuma haukuwa hivyo"
George Jinasa said
Re: Maaskofu wamkataa meya wa CCM Arusha
kwa kulaani vurugu na mauwaji yaliyotokea Arusha mimi ninawapongeza mababa Askofu kwa dhati. Ili hili la kutomtambua Meya mimi nakuwa mgumu kukubaliana nao kwa sababu nyingi. Kwanza, ninauhakika kwamba Maaskofu hawakushiriki katika uchaguzi wa Meya. CCM wanadai Meya wao alishinda. Chadema wanadai Kura zilichakachuliwa. Msimamizi wa uchaguzi alimtangaza mgombea wa CCM kuwa mshindi. Sasa kama Chadema anasema ukweli au CCM anasema ukweli sijua Maaskofu wametumia kigezo gani kubaini. Naamini hawawezi kusema kwa mgombea wa Chaedema alipata kura ngapi na wa CCM alipata kura ngapi tofauti na alivyotangaza msimamizi. Maana, kumbukumbu za kura bado ziko mikononi mwa msimamizi wa uchaguzi.Sababu ya pili ni kwamba usahihi na uhalali wa matekeo umezua mgogoro kati ya CCM na CHADEMA. Maaskofu ni wetu sote. Wanasikiliza maungamo kwa waumini wao walio CCM, CHADEMA, CUF na vyama vingine. Ingekuwa ni busara zaidi kwao kama wangetaka uhalali wa matokeo hayo uchunguzwe na vyombo venye mamlaka ya kufanya hivyo kuliko kuunga mkono upande mmoja kati ya pande zinazogombana.

Makanisa na taasisi nyingine katika sehemu nyingine duniani zinachukua nafasi ya usuluhishi, Kristo anasema "Heri wapatanishi maana hao wataitwa wana wa Mungu". Kanisa linapoteza sifa hii ya upatanishi kwa kuchukua nafasi katika pande zinazogombana. Tunaelewa pia kwamba taasisi za kidini ni kama wazazi. Wanaweza mara nyingine kutoa sauti ya kukosoa. Lakini hilo linahitaji kufanyika kwa hekima na busara sana hasa pale pana pande mbili zenye ushawishi mkubwa zinapovutana.
Ningewashauri mababa Askofu na viongozi wa dini zingine siku nyingine tujitahidi kuepuka kuchukua nafasi fulani katika pande zinazovutana. Safari bado ni ndefu kwa hali inavyoonesha na mchango wa taasisi za dini unategemewa sana katika kuiweka nchi yetu katika amani. Watanzania bado tunaheshimu sana dini zetu na viongozi wetu wa dini.

kagumyamuheto said
Re: Maaskofu wamkataa meya wa CCM Arusha
Pengine ile dhana ya UDINI ndipo inapoonekana hapa. Mbuni kaficha kichwa kwa muda mrefu huku kiwiliwili chote kikiwa nje sasa kaamua kutokeza kichwa hadharani. Mbona hawakutoa tamko pale dereva wa ccm pale maswa alipouawa na chadema?? Au pale hakuna haki ya kuishi?? Na je, uchaguzi wa meya umefanyika januari??? Why now??
Nasikia harufu ya kumwagika damu kama ile ya rwanda!! Unapoona maaskofu nao wanachanganya dini na siasa ujue ni hatari. Kwani nafasi ya umeya ni ya kuhubiri kanisani???. Au kuwa meya lazima uthibitishwe na kanisa??. Ni kweli taratibu zilikiukwa katika kumpata meya kwani mahakama hazipo?? Taratibu zipi zimefuatwa??
Nasikia harufu ya damu!. Jk andaa jeshi liwe tayari tayari! Nasi pia tupo tayari.

MSAUZI said
Re: Maaskofu wamkataa meya wa CCM Arusha
Hawa Maaskofu wenu ni wanafiki,si ndo hawa waliowahi kusema Kikwete kachaguliwa na Mungu?
Anonymous said
Re: Maaskofu watoa tamko la kumkataa meya Arusha
Originally Posted by Kadogoo https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...amkataa-meya-wa-ccm-arusha-4.html#post1462746
“Kanisa heri linyamaze na kufunga mdomo maana kila nikikumbuka mauaji ya kimbari Rwanda huwa nasikitika sana Kanisa linapoongelea juu ya haki! kila nikikumbuka mauaji ya Mwembechai Dar, na kauli alieitoa Padri Lwambano kuwa Serikali iwashugulikie Waislamu wa Msikiti wa Mwembechai na siku ya pili Polisi waliitikia wito huo na kuuwa wananchi wenzetu! nasikitika tena Kanisa kuhubiri haki!
Kila nikikumbuka mauaji ya raia huko visiwani na kauli ya Muadhama Kardinali Pengo kuwa waliouliwa na Polisi huko Zenji ndio wabebe lawama kwa kutokutii amri ya Serikali ya kutokuandamana!!
Sasa, leo Kanisa na Baraza la Maaskofu watakuwa na ubavu gani wa kujitokeza na kulaani mauaji ya Arusha?

Kuna watu wengine wapumbavu watakao fikiri kuwa mimi nafurahia mauaji ya Arusha lakini kwa hakika kila binaadamu mwenye hisia hatafurahia kitendo hicho cha Askari wetu kufyatua risasi za moto na kuua wananchi! ni tendo la kulaaniwa lakini sio Maaskofu wajitokeze leo ghafla na kutoa kilio cha kinafiki! kwanza waombe msamaha kwa maovu waliofanya huko nyuma kwa kuunga mkono maamuzi ya Serikali ya Benjamin Mkapa ya kuuwa raia wa nchi hii na ndipo wafungue ukurasa mpya wa kudai haki za wananchi kinyume chake itakuwa vigumu kuelewa lengo la Kanisa ni nini!”

Mkuu asante sana namie nakumbuka hilo tamko na siku mauaji ya mwembechai yalipotokea hakuna Tamko hata moja la maaskofu lilitokea kulaani leo hii wanaleta unafiki wao wa kulaani mauaji ya Arusha. Hakuna mtu anayeyafurahia haya ila tunakemea unafiki wa maaskofu kwa vile kuna muislamu pale juu leo wanajitia vimbembele kukosoa wajiangalie kwanza kabla ya kusema otherwise jamii hasa ya waislamu haijasahau makovu waliyoyaacha kipindi kile cha mwembechai.....

kagumyamuheto ahsante kwa kutukumbusha na posts hizo hapo juu, kama utafuatilia hoja zilizotolewa hapo juu na wahusika utagundua kwamba ni kweli wakati mwingine viongozi wa dini ni wachochezi wa migogoro mingi ya kisiasa na wanatenda bila kuchunguza mambo kwa makini. Wao walipaswa kuwa wasuluhishi wa pande zote, wakijua wana waumini wa pande zote lakini utaona wakati mwingine walishabikia upande mmoja, hiyo ni hatari sana na hayo ndiyo yaliyosababisha hata yale mauaji ya kimbari yaliyotokea Rwanda... Hawa walikuwa washawishi nambari one. Mimi naona viongozi hawa wajitahidi kufanya kazi zao za upatanishi hata kama wanajua pande moja inamakosa badala ya kushabikia upande mmoja... That's very dangerous!!! ndio maana kila wakati wanaambiwa wasiingilie masuala ya kisasa, hii ikimaanisha kwamba wanaongoza waumini wa vyama vyote vinavyoshindana, hivyo wakiingilia wataleta hata mgawanyiko katika kanisa. Vyanzo vya madhehebu ni hivyo lakini madhehebu hayakubaliki mbele za Mungu. Mungu alitazamia kuwepo na Dini moja, Imani moja (Waefeso 4:4-6).
 
katumwa na mbakaji makamba huyo wala msimlaumu
 
Kwa nini CCM hawamwambii Gertrude Rwakatare naye kuvua joho? Very stupid -- CCM leaders!!!
 
CCM: Maaskofu vueni majoho

Imeandikwa na Mwandishi Wetu,
Arusha;
Tarehe: 8th January 2011

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Arusha kimewataka maaskofu wote na viongozi wengine wa dini mkoani hapa, kuvua majoho ya kazi yao na kutangaza kuingia katika siasa.

Katibu wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda alisema hayo jana mbele ya waandishi wa habari wa Jiji la Arusha na kuwataka maaskofu hao kuacha kuingilia mambo ya siasa yasiyowahusu ya Meya wa Jiji la Arusha.

Chatanda alisema, kitendo cha maaskofu kusema hawamtambui Meya wa CCM Arusha, Gaudence Lyimo kimewashtua na hakiwezi kuachwa hivi hivi.

Alisema viongozi wa dini wanapoingilia masuala ya siasa ni ukiukwaji wa majukumu yao hivyo bora wavue majoho yao na kuingia kwenye ulingo wa siasa kama alivyofanya Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa.

Chatanda ambaye ndiye anatajwa kuwa chanzo cha mgogoro wa uchaguzi wa umeya wa Arusha, hasa kutokana na kupiga kura kama diwani wa Arusha, ilhali alichaguliwa kama Mbunge mkoani Tanga, alisema masuala ya kisiasa waachiwe wanasiasa wenyewe.

Chatanda ambaye alikuwa pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Onesmo Ole Nangole alisema kazi ya maaskofu ni kuelekeza njia za imani na kuwataka waumini kuwa wacha Mungu na si kushabikia siasa.

“Sisi kama viongozi wa CCM wa Mkoa wa Arusha tumesikitishwa na kauli za maaskofu hao na tulitegemea kabla ya kutoa tamko lao wangetuita sote na tukatoa maelezo yetu na hapo ukweli wangeupata lakini kusema uchaguzi haukuwa halali si sawa.”

Hata hivyo, alisema yeye kama Mbunge, alipangiwa na chama chake kuwa Arusha na hivyo, ataendelea kuwa diwani wa CCM Arusha hadi hapo itakapoamuliwa vinginevyo na chama chake.

Akizungumzia makundi ndani ya CCM ambayo pia yanampinga hasa kutokana na kumtuhumu kusababisha CCM kushindwa Jimbo la Arusha, alisema wanaCCM hao hawajui wanalosema hivyo wanapaswa kusamehewa.

Juzi Maaskofu wa Makanisa ya Kikristo mkoani Arusha walitoa tamko la pamoja la kutomtambua Meya wa Jiji la Arusha aliyeteuliwa na CCM na kuweka bayana kwamba hawatampa ushirikiano meya huyo.

Walitoa tamko hilo wakati walipokuwa wanalaani hatua ya Polisi mkoani Arusha, kutumia nguvu kupita kiasi katika kuvunja maandamano ya amani ya Chadema na hivyo kusababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi wengine zaidi ya 20.

Well said Mary waache unafiki maaskofu kama wanataka siasa tunawakaribisha ila wasiingilie fani zisizowahusu. Hawa ndio wachochezi wa vita vingi barani afrika hatutaki litokee Tanzania.
 
Mary chatanda shut up,,,,,,,,,,,,,,,,,,wewe ni mamluki ulisababisha vifo vya wasiokuwa na hatia,,,ndiwe ulieharibu uchaguzi,na damu zote ziwe juu ya kichwa chako

Wanahatia kwa sababu walikiuka amri ya polisi kutokuandamana!
 
CCM: Maaskofu vueni majoho

Imeandikwa na Mwandishi Wetu,
Arusha;
Tarehe: 8th January 2011

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Arusha kimewataka maaskofu wote na viongozi wengine wa dini mkoani hapa, kuvua majoho ya kazi yao na kutangaza kuingia katika siasa.

Katibu wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda alisema hayo jana mbele ya waandishi wa habari wa Jiji la Arusha na kuwataka maaskofu hao kuacha kuingilia mambo ya siasa yasiyowahusu ya Meya wa Jiji la Arusha.

Chatanda alisema, kitendo cha maaskofu kusema hawamtambui Meya wa CCM Arusha, Gaudence Lyimo kimewashtua na hakiwezi kuachwa hivi hivi.

Alisema viongozi wa dini wanapoingilia masuala ya siasa ni ukiukwaji wa majukumu yao hivyo bora wavue majoho yao na kuingia kwenye ulingo wa siasa kama alivyofanya Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa.

Chatanda ambaye ndiye anatajwa kuwa chanzo cha mgogoro wa uchaguzi wa umeya wa Arusha, hasa kutokana na kupiga kura kama diwani wa Arusha, ilhali alichaguliwa kama Mbunge mkoani Tanga, alisema masuala ya kisiasa waachiwe wanasiasa wenyewe.

Chatanda ambaye alikuwa pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, Onesmo Ole Nangole alisema kazi ya maaskofu ni kuelekeza njia za imani na kuwataka waumini kuwa wacha Mungu na si kushabikia siasa.

“Sisi kama viongozi wa CCM wa Mkoa wa Arusha tumesikitishwa na kauli za maaskofu hao na tulitegemea kabla ya kutoa tamko lao wangetuita sote na tukatoa maelezo yetu na hapo ukweli wangeupata lakini kusema uchaguzi haukuwa halali si sawa.”

Hata hivyo, alisema yeye kama Mbunge, alipangiwa na chama chake kuwa Arusha na hivyo, ataendelea kuwa diwani wa CCM Arusha hadi hapo itakapoamuliwa vinginevyo na chama chake.

Akizungumzia makundi ndani ya CCM ambayo pia yanampinga hasa kutokana na kumtuhumu kusababisha CCM kushindwa Jimbo la Arusha, alisema wanaCCM hao hawajui wanalosema hivyo wanapaswa kusamehewa.

Juzi Maaskofu wa Makanisa ya Kikristo mkoani Arusha walitoa tamko la pamoja la kutomtambua Meya wa Jiji la Arusha aliyeteuliwa na CCM na kuweka bayana kwamba hawatampa ushirikiano meya huyo.

Walitoa tamko hilo wakati walipokuwa wanalaani hatua ya Polisi mkoani Arusha, kutumia nguvu kupita kiasi katika kuvunja maandamano ya amani ya Chadema na hivyo kusababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi wengine zaidi ya 20.

Huyo Chatanda anafikiri?
 
kwani viongozi wa dini hawana haki yakutoa maoni yao
 
Aaaash,wamesahau hao hao ndo huwa wana wapamba mda wa kampeni ukifika?
 
Hayawahusu vipi wakati nao ni wananchi?Ina maana wao hawana haki ya kumkubali au kumkataa mtu anaetaka awaongoze??Nashawishika kuamini kwamba uwezo wa makuruta wa CCM wa kufikiri hautofautiani na wale wanaoambiwa wana upungufu wa akili maana maoni yao hua yanashangaza kweli!
 
Tuache udinimktk hili,Kuhusu mauji ya kimbari Rwanda historia yake sidhani kama maaskofu ndo walihusika,nikiangalia movie zote mbili zinazo onyesha mauaji ya Kimbari,kwa mfano some times in april maaskari waliwafuata wanafunzi kwenye shule ya m,asista na kuwaua,na ile ya Hotel Rwanda pia wanajeshi waliwafuata wananchi na kuwaua kanisani,ile vita ilikuwa ya kikabila zaidi(HutusVsTutsi's)any ways labda mimi uelewa wangu ni mdogo naweza kosolewa kwa hilo,kuhusu pale Maswa msafara wa CCM ulivamia mkutano wa chadema,Kuhusu Mwembe yanga ndugu zangu Kwenye misikiti mingi ya kiislamu udini unahubiriwa waziwazi nenda pale kwenye msikiti wa kariakoo na mmoja kwa mfano tu utakuja niambia.TUJENGE NCHI KWA MISINGI WALIOTUACHIA WAASISI WA NCHI HII HUKU TUNAPOELEKEA SIO
 
Back
Top Bottom