Informer
Platinum Member
- Jul 29, 2006
- 1,629
- 6,812
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kimejipanga kuhakikisha wanarejesha majimbo yote kiliyoyapoteza katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015 kwa kuwa kimeshabaini sababu za kupoteza majimbo na kata katika uchaguzi uliopita.
Hayo yalibainishwa juzi na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, Mwigulu Nchemba, wakati akizungumza kwenye kikao maalumu cha Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Ilemela, jijini hapa.
Tumeshagundua sababu za kupoteza baadhi ya maeneo ni ugomvi tu baina yetu. Sasa tumekuja na kaulimbiu mpya ya Umoja ni Ushindi, anayesubiri CCM ishindwe atazeeka sana bila kuona hivyo, alisema.
Kwa kuwa kikao hicho kiliwashirikisha watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ilemela, Mwigulu alisema wapo watu wanaoacha kuitumikia Serikali iliyopo madarakani wakidhani kuwa kuna Serikali nyingine itaingia madarakani hivi karibuni.
Aliwataka viongozi wa CCM wasisite kuchukua hatua na kukemea kwa kile wanachotaka kitekelezwe na watendaji kwa mujibu wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
Waliopo Serikalini wanatekeleza mkataba wa Serikali inayoongoza nchi, tukifuata hilo Tanzania tutapiga hatua na tunapoisimamia Serikali hatupaswi kulaumiwa na mtu, kwani tunaisimamia ilani ya CCM itekelezwe, alisema Naibu Katibu Mkuu huyo wa CCM.
Nchemba alisema kinachoigharimu Tanzania ni baada ya uchaguzi kumalizika, halafu watu kuanza uchaguzi mwingine badala ya kuchapa kazi ya kuwatumikia wananchi.
Uchaguzi ukiisha tujenge kasumba ya kuacha kampeni na maandamano ya kila siku na kuingia kazini kuwatumikia wananchi, si mmeona wenyewe baada ya uchaguzi wa Marekani kumalizika watu wanafanya kazi na sio kuzungumzia uchaguzi tena, alisema.
Haiwezekani siku zote ziwe za kampeni. Tutafanya lini kazi, siku zote kuwa za kampeni zinawafanya watumishi wa serikali kushindwa kugawa muda wa kuwatumikia wananchi? Alihoji.
Katika kikao hicho maalumu, Nchemba aliwagawia wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya makabrasha ya maazimio ya Mkutano Mkuu wa Nane wa Taifa na Hotuba ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Jakaya Kikwete, kama vitendea kazi vyao.
Chanzo: HabariLeo | Imeandikwa na Grace Chilongola, Mwanza | Jumapili, 23 Desemba 2012