CCM yatamba kuzoa majimbo, kata 2015

CCM yatamba kuzoa majimbo, kata 2015

Wana jamvi ni ukweli usiopingika kwamba chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kitapoteza majimbo mengi kiliyoyapata 2010 kutokana na misuguano ndani y chama hiko ambayo inazidi kukibomoa chama hiko.

You never know. Sometimes you have to let things go so as better things can unfold. And problems sometimes are opportunity for growth
 
Hongera kwa kujaribu, its a wishful thinking that will never happen, sor maana utakuwa disappointed
 
Ritz,mkiendelea na ubishi wa aina hiyo majimbo ya Mtwara utayakuta kwenye orodha hiyo yameongezwa.Nikufanya kazi kwa bidii na kuacha ufisadi pekee ndio tiba ya kuiponya CCM isipoteze viti.Ila haya ya kuwapa vyeo wauza pembe za ndovu Na mnajifanya Hamuoni wakati watu wanaona!haya

sio kuacha ufisadi! Tunahitaji manyan'gau yote ya sisiem waliojimegea keki ya taifa kwa maslai binafsi wafungwe maisha ndipo sisiem ianze kujikosha vinginevyo huruma hakuna! Wacha mchezo kabisa!
 
Kuna watu wengine bila kuitaja CDM wanawashwa mwili mzima.
 
Wana jamvi ni ukweli usiopingika kwamba chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kitapoteza majimbo mengi kiliyoyapata 2010 kutokana na misuguano ndani y chama hiko ambayo inazidi kukibomoa chama hiko.

Tofauti ndogondogo ktk mkusanyiko wa watu ni kitu cha kawaida sana,sijaona kama ni tatizo kubwa kama unavyolielezea hapa.Mbona CCM kuna makundi kibao na tunayajua,why usiwwonee wasiwasi hawa kupoteza majimbo mengi kwa msingi huo??????
 
CCM iko level ipi ya KTUIBIA RASILIMALI na kuiba kura kwenye uchaguzi? 2015 tutabaki na pua ya gamba yyte atakayejaribu kuiba kura.
 
Kwa nini iwe majimbo na si kata?Misuguano ndiyo itakayopitisha CHADEMA katika TANURU la moto.Hoja yako haijasimama na hujatueleza ni kwa namna gani umefikia hitimisho hilo.Usijenge hoja nje ya mantiki

Jamani ebu muwe mnajishauri thread za kujibu. Maana watu wako kazini kuchokonoa na kuchokoza na nyinyi mnaanika mawazo yenu kuwasaadia walipofikia ukomo wa kufikiri. Kuna issues za CDM za kujadili si za CCM take it from me.
 
pro-chadema watakuwashia moto! haya! wakati wao wanadhani watapata urais wewe unawatabiria kupoteza majimbo? sasa hivi watakuambia wewe uko nyuma ya mgogoro unaofukuta ndani ya chama.ngoja waje!

Mkuu Betlehem htuwezi kuogopa kusema kama mtu amekosea,huu ni uoga ambao unapaswa kukemewa kwa nguvu zote,ni ukweli usiopingika kwamba CHADEMA wamefanya kosa kubwa sana la kuiga misuguano na minyukano iliyokuwa ikiafanywa na CCM ambayo ilifika sehemu ambayo imewagharimu kwa kiwango kikuba,lakini kwa sababu wao wamewahi kulitambua hilo unaona hivi sasa wamekaa chini na wamejiapanga upya,cha ajabu ni kwamba chama ambacho kinategemewa sana na watanzania alio wengi kamba kingewea kupamba na CCM na kuiondoa madarakani kimeanza nacho migogoro tena isiyokuwa na maana yoyote.

Watapotea majimbo mengi tu mojawapo ni Nyamagana,Ilemela,Bukombe,Musoma mjini,Biharamulo,Meatu,Maswa Mashariki na Magharibi,na mengine kama kuna mtu anayejua aendelee hapo.
 
Wana jamvi ni ukweli usiopingika kwamba chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kitapoteza majimbo mengi kiliyoyapata 2010 kutokana na misuguano ndani y chama hiko ambayo inazidi kukibomoa chama hiko.

Itayapoteza kwa chama gani? CCM, kwa akili yako kuna msuguano CHADEMA wa kusababisha tupoteze majimbo! Acha kuwa mtumwa wa magamba! Unafikiri watanzania bado wajinga siyo!
 
Itayapoteza kwa chama gani? CCM, kwa akili yako kuna msuguano CHADEMA wa kusababisha tupoteze majimbo! Acha kuwa mtumwa wa magagamba! U afikiri watanzania bado wajinga siyo!

Usimshambulie sana huyu Bwana wewe jibu hoja kwa hoja na utoe sababu ni kwa nini hawatapoteza kwa sababu yeye amesema watapotea kwa sababu ya msuguano unaondelea,au unakataa kwamba hakuna msuguano,pili yeye hajasem kwamba Itapotea kwa CCM isipokuwa wewe ndiye umesema hivyo,hebu nenda kwenye hoja usitutoe kwenye hoja,watu wa taipu yenu ndio siku zote mnatutoa kwenye hoja mpaka mnasababisha watu wanakuwa BAN,kwa sababu mnachakachua Thred na kuingiza Interest zenu.
 
Ritz jibu hoja kwanini hujaona hayo majimbo yako wazi haufanyi uchunguzi wewe usitoe majibu marahisi.

Majanikv,
Hakuna hoja hapo ulichofanya umeweka hiyo orodha ambayo umeipenda.

Kumbuka Chadema majimbo kama ya Kawe, Ubungo, Nyamagana, Ilemela, Ukerewe, na mingineyo lazima watayapoteza.
 
Last edited by a moderator:
Wana jamvi ni ukweli usiopingika kwamba chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kitapoteza majimbo mengi kiliyoyapata 2010 kutokana na misuguano ndani y chama hiko ambayo inazidi kukibomoa chama hiko.
bila shaka hizi ni stori za kwenye kahawa
 
wanawaza kuzaa wakati uzazi hawana.... Ni zitto na mbowe ndio ambao watatea majimbo yao.

Zitto ameshatangaza kutokugombea mwaka 2015 kwa hiyo nalo wamepoteza,labda Mboe ka ababu yeye anajua kula Kipofu.
 
Majanikv,
Hakuna hoja hapo ulichofanya umeweka hiyo orodha ambayo umeipenda.

Kumbuka Chadema majimbo kama ya Kawe, Ubungo, Nyamagana, Ilemela, Ukerewe, na mingineyo lazima watayapoteza.

Sasa wewe umefanya nini hapo na wewe si umeweka list unayopenda je ulifanya uchunguzi gani hayo majimbo tutapoteza.

Kwanini ubungo na kawe unaona tutapoteza nipe sababu?

Kutokana na upepo wa kisiasa mfano ukiangalia kisarawe bado kuna mahitaji mengi sana elimu duni,maji bado shida,barabara tatizo sana,ajira ngumu mbunge mpaka sasa hivi hajayatatua hata kuuliza maswali pia kwenye suala la afya.
 
Last edited by a moderator:
Majanikv,
Hakuna hoja hapo ulichofanya umeweka hiyo orodha ambayo umeipenda.

Kumbuka Chadema majimbo kama ya Kawe, Ubungo, Nyamagana, Ilemela, Ukerewe, na mingineyo lazima watayapoteza.

Kuna Meatu,Biharamulo,Kigoma Kaskazini lile la Zitto alilotangaza kutokugombea tena,Musoma Mjini,na Bukombe.
 
Ni mafisadi na watoto wao tu ndio wanaojiaminisha ushindi wa CCM 2015.Kama si uchakachuaji wa kura 2010,Rais alikuwa Dr Slaa.Tunawashukuru usalama wa taifa na tume ya taifa ya uchaguzi kwa kazi nzuri mliowatendea Watanzania.
 
Back
Top Bottom