PreGE2025 CCM yapata aibu tena Sumbawanga

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Leo ilikuwa zamu ya wilaya za Kalambo na Sumbawanga kutembelewa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema Mh. Tundu Lissu ambaye ameendeleza kampeni yake ya No Reforms No Election.

Katika jambo la kusikitisha na aibu kubwa tangu jana CCM walizuia magari yote ya matangazo kwa kuwalipa wamiliki wake ili yasikodishwe na Chadema kwa ajili ya kutangaza na kuhamasisha wananchi kuhudhuria mkutano mkubwa wa hadhara mjini Sumbawanga.

Lakini katika hali iliyowaacha midomo wazi viongozi wa CCM ni mafuriko makubwa ya watu waliohudhuria mkutano huo pamoja na hujuma kubwa ya kuandaa Bonanza katika uwanja wa Mandela na tamasha la ngoma katika kiwanja cha Sabato.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mkutano huo mkubwa pia ulihudhuria na RPC wa Rukwa aliyekuwa amejificha ndani ya gari yake iliyokuwa imeegeshwa kwenye miti pembeni mwa uwanja wa mkutano.

View: https://twitter.com/OleMtetezi/status/1904950670773346380?t=6hCRQj8ixPrNZrNNI9ugnQ&s=19

Hivi hawa watu wakati wa kupiga kura huwa wanatokomea wapi 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣. Bongo unafiki ni maisha ya kawaida kabisa
 
Tatizo siyo wapiga kura (watu) kutokupiga kura bali wanaotangaza matokeo ya kura ni makada wa CCM ndiyo sababu ya no reforms no election. Kupata Katiba Mpya na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi!
 
Leo ilikuwa zamu ya wilaya za Kalambo na Sumbawanga kutembelewa na Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema Mh. Tundu Lissu ambaye ameendeleza kampeni yake ya No Reforms No Election.

Katika jambo la kusikitisha na aibu kubwa tangu jana CCM walizuia magari yote ya matangazo kwa kuwalipa wamiliki wake ili yasikodishwe na Chadema kwa ajili ya kutangaza na kuhamasisha wananchi kuhudhuria mkutano mkubwa wa hadhara mjini Sumbawanga.

Lakini katika hali iliyowaacha midomo wazi viongozi wa CCM ni mafuriko makubwa ya watu waliohudhuria mkutano huo pamoja na hujuma kubwa ya kuandaa Bonanza katika uwanja wa Mandela na tamasha la ngoma katika kiwanja cha Sabato.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mkutano huo mkubwa pia ulihudhuria na RPC wa Rukwa aliyekuwa amejificha ndani ya gari yake iliyokuwa imeegeshwa kwenye miti pembeni mwa uwanja wa mkutano.

View: https://twitter.com/OleMtetezi/status/1904950670773346380?t=6hCRQj8ixPrNZrNNI9ugnQ&s=19

Kwa staili hii CCM twafwa
 
RPC anakubali kimya kimya

RPC ni lazima ahudhurie hata mkuu wa usalama mkoa na wilaya ili wajiandae kwa nguvu kubwa kulingana na ukubwa na nguvu ya Chadema .

Ila Chadema na ACT awamu hii wasiwe wapumbavu kwenye kuandaa maandamano .

Maandamano yanapaswa yawe nchi nzima . Kila mahali kwenye mikusanyiko mikubwa Kama masoko ,biashara ndogo ngogo na stendi.
 
Maandamano inategemea na wananchi wa eneo husika
 
Back
Top Bottom