CCM Yapandikiza Mamluki ndani ya CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Yapandikiza Mamluki ndani ya CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NyepesiNyepesi, Jul 2, 2011.

 1. N

  NyepesiNyepesi Member

  #1
  Jul 2, 2011
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ni tahadhari kwa viongozi na wanachama wa chadema.

  Baada ya tume ya uchaguzi kugawanya baadhi ya kata na majimbo ya uchaguzi mwaka jana, chama cha chadema kililazimika kuteua viongozi wa muda kukaimu nafasi za uongozi katika kata na majimbo mapya hadi hapo uchaguzi mkuu utakapokuwa umekwisha. Na baada ya kukamilika kwa zoezi la uchaguzi mkuu, uongozi wa chadema taifa umetoa maelekezo ya kufanyika kwa chaguzi za kidemokrasia ili kupata viongozi watakaoshikilia madaraka hadi 2014 utakapofanyika uchaguzi mkuu wa chama.

  Kutokana na mwitikio mkubwa wa wananchi kujiunga na chadema na kuiunga mkono, aidha kwa kuchukua kadi na kuwa wananchama ama kwa kuwaunga mkono kwa wingi sana wanapoitisha maandamano na mikutano katika maeneo mbalimbali ya nchi, chama tawala ccm kimeingiwa na uwoga wa kuondolewa madarakani mwaka 2015. Pamoja na mikakati mbalimbali wanayoipanga ili kuidhoofisha chadema, mojawapo ni kupandikiza watu wao ndani ya chadema ili iwe rahisi kwao kujua kwa undani mipango na mikakati ya chadema lakini pia wawatumie watu wao hao kujipenyeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kupitia chadema na hivyo kuisaidia ccm kushinda uchaguzi mkuu ujao kwa hao mapandikizi yao kufanya hujuma dhidi ya chadema.

  Sasahivi kuna wimbi kubwa sana la watu kumiminika ndani ya chadema kuchukua kadi za uanachama na moja kwa moja kugombea nafasi za uongozi, wengi wao ndio hao waliotumwa na ccm ili baadae wasaidie kuchafua hali ya hewa ndani ya chadema na kuihujumu. Kwahiyo nawatahadharisha wanachadema muwe makini sana mnapofanya uchaguzi. Kwa hapa Dar es salaam nimeambiwa kuna chaguzi ndogo katika majimbo ya ukonga na segerea pamoja na baadhi ya kata katika majimbo hayo.

  Katika jimbo la ukonga kwa mfano, kuna watu kadhaa ambao wamejiunga na chadema hivi karibuni na moja kwa moja wameingia kwenye kinyang'anyiro cha uongozi wa jimbo. Mojawapo ni Mchungaji mmoja(jina kapuni) aliyegombea ubunge jimbo la ubungo mwaka jana 2010 kwa tiketi ya chama cha UDP lakini sasahivi amehamia chadema na mojakwa moja amejitosa kuwania uongozi jimbo la ukonga. Uongozi wa chadema muwe macho na mchungaji huyo atawavuruga, taarifa zaidi ni kwamba mwaka jana alishiriki kumpigia kampeni mgombea ubunge jimbo la ukonga kwa tiketi ya CUF, sasa hayo mapenzi na chadema yametoka wapi ndani ya miezi michache?? huyu ni wa kuangaliwa sana atawavuruga. Mwingine ni kijana mmoja, mdogo wake na mbunge mmoja wa viti maalum ccm mkoa wa iringa, kabla ya hapo alikuwa diwani wa viti maalum ukonga. Huyu kijana amejiunga na chadema mwezi wa sita na moja kwa moja amejaza fomu ya kuwania uongozi wa bavicha jimbo la ukonga, huyu naye ni kuangaliwa sana asije akakihujumu chama. Kuna vijana wengine wawili mwanamke na mwanaume, mmoja wao mwanaume alijaribu kujipenyeza kugombea nafasi ya uongozi(ukatibu) bavicha taifa kutokea jimbo la ukonga lakini bado hakijaeleweka. Uongozi wa taifa uwe makini na kijana huyo, amejiunga na chadema wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu wa bavicha. Mwanamke bado hajaweka dhamira yake hadharani lakini ameanza kujipitisha kwa viongozi wa kata ambao ndio wapiga kura katika uchaguzi wa jimbo na pia anaonekana "kumteka" kiongozi mmoja wa jimbo.

  Mwisho kabisa namalizia kwa kuwataka tena wanachadema kuwa makini na mamluki wa ccm na vyama vingine wataivuruga chadema, kila mmoja anashuhudia jinsi shibuda anavyowakoroga, kila mmoja anakumbuka jinsi yule mamluki wa ccm alivyokihujumu chama kule singida kwenye uchaguzi mkuu mwaka jana,na mifano kwa kweli ni mingi sana kila mmoja mahali pake ana ushuhuda.

  Jambo la muhimu ni kujipa muda kwanza kuwapima hawa wanachama wapya hasa wanaotokea vyama vyengine ili kujiridhisha kama ni wa ukweli ama ni wa "kichina", nadhani mnanielewa vizuri. Kazi kwenu chadema. Hakuna chuki binafsi katika hili bali ni tahadhari kwa viongozi wa chama changu ili wawe makini na mamluki!!

  Nawasilisha na kuwatakia weekend njema.
   
 2. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Crackpot
   
 3. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  he!!! any proof, prove it.
   
 4. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Proof ni Shitambala na Shibuda! Haya ni magamba kwa 100%!
   
 5. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kakojoe ukalale, mtoto mzuri, ili uamke mapema kesho, uwahi shule!
   
 6. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #6
  Jul 2, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  wakina SHIBUDA!
   
 7. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #7
  Jul 2, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Kuwa makini ni jambo la lazima maaana msifikirie CCM imelala na haingaiki juu ya hilo jambo, la muhimu ni kama una ushahidi wa vitu kama hivi wafikishie viongozi wa CDM pamoja na ushahidi wake siyo kuyaweka hapa JF ambayo 99% ni mali ya CCM. Juwa kuwa adui yako akijuwa mbinu zako unajitia mashakani wewe mwenyewe.

  Husifikie kuwa JF founders na allied Big chaps wa JF ni Chadema au wanamapinduzi wa kweli hapa wanachofanya si kuipinga CCM bali kumpinga Kikwete basi, akirudi Mkapa utaona wote wanarudi kuitetea CCM! Hivyo hapa weka mambo ya Jamii siyo yanayohusu chama kama chama na maslahi binafsi juu ya kuijumu chama, wataitumia kujiweka sawa mapema wakati bado mnatafakari.
   
 8. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #8
  Jul 2, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,155
  Trophy Points: 280
  Mbona wengi tu, wa kwanza Mbowe, au hamjaona alivyo fanya muafaka na Pinda halafu wanawageuzia kibao madiwani, nashaka hata Slaa ni mtu wetu, maana naona anachosema haeleweki. Kaongelea ya madiwani ya Mwenyekiti na Pinda kabana.
   
 9. N

  NyepesiNyepesi Member

  #9
  Jul 2, 2011
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bwahahahaaa,
  Bila shaka wewe mdau wa ccm.

  Pole kama imeuma!
   
 10. N

  NyepesiNyepesi Member

  #10
  Jul 2, 2011
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Soma vizuri na kwa makini, utaona kuna mahali nimewataja baadhi ya mamluki, usiwe na haraka ya kujibu post bila kuisoma na kuielewa.
   
 11. N

  NyepesiNyepesi Member

  #11
  Jul 2, 2011
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ushauri wako ni mzuri, pamoja na mafounder hao uliowataja lakini usisahau kwamba viongozi wa chadema nao ni wadau wa JF. Kuna Dr.Slaa, Mnyika, Zitto, Dr. Kitila kwahiyo wanaweza wakaanzia hapa na kufanya uchunguzi wa kina, mimi nimewapa pa kuanzia.
   
 12. nditolo

  nditolo JF-Expert Member

  #12
  Jul 2, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 1,335
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Porojo
   
 13. M

  MKALIMOTTO Senior Member

  #13
  Oct 7, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Niliwahi kumnukuu Stephen M. Wassira akisema kuwa chadema ni cha msimu na kitakufa kabla ya 2015. Nilimwona huyu mzee amechanganyikiwa na anatapatapa kama mfamaji. Sasa naweza sema nakubaliana na Wassira na pengine kwa kauli yake hiyo alijua kinachofanyika kati ya CCM na baadhi ya wasaliti ndani ya chadema. Tangu leo tujue kuwa msaliti ndani ya cdm si zitto na shibuda tu bali kuna orodha ndefu ambayo kila kukicha inaongezeka. Inaandaliwa na ccm kwa umakini mkubwa na baadhi yao wameanza kuonesha utii kwa ccm kwa kutoa siri za chadema kwa ccm. Hivi juzi, niwaibie siri(kama si kweli Slaa aikanushe.) Slaa alihojiwa incamera na wazee wa system baada ya kupatikana kwa traces zinazomwonesha Slaa akiwa Italy mwezi Agost 2012 akizungumza na Italy Mafia Mob (ITAMM) ili iwafundishie snipers na sharpshooters kwaajili ya uchaguzi mkuu 2015. Mwanzoni alikataa japo alikuja kukubali baada ya kuoneshwa mkanda wa video Dr Slaa akiwa airport Dar, akiwa mapokezi uwanja wa ndege Rome na akiwa Foret de Mafia Italiano akizungumza na master wa Mafia d'Italiano. Slaa anadaiwa kuikataa sauti na kudai kuwa video ni fabricated. Hata hivyo Slaa anadaiwa kumlaumu askofu mmoja mwanza kuwa ndiye aliyevjisha siri hiyo kupitia kwa Halima mdee ambaye anadaiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na kigogo mmoja wa system. Inadaiwa askofu huyo haelewani na Slaa tangu akiwa katibu wa TEC hivyo amefanya hivyo kumkomoa Slaa baada ya Slaa kumtuhumu kuwa alihamishiwa hapo
  ili kuisaidia ccm. Katika Mazingira hayo ni wazi kuwa Wassira anajua jinsi watakavyoimaliza chadema, ana uhakika asilimia 100. Zaidi ya Zitto ambaye ndiye anaonekana msaliti, yeye ni kiongozi tu lakini nyuma yake kuna shibuda, shushushu mabere marando, halima mdee, sugu, wenje, mbunge ester, kasulumbai, selasini na vicent nyerere. Mkubali msikubali ukweli ndo huo ingawa ni mchungu.
   
 14. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #14
  Oct 7, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,769
  Likes Received: 6,098
  Trophy Points: 280
  Wacha wendawazimu wewe. Halafu mods, hebu ondoeni hii kitu fasta.
   
 15. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #15
  Oct 7, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  nguruwe wa iraq ww.
   
 16. M

  Molemo JF-Expert Member

  #16
  Oct 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Umeonyesha upeo wako wa kijinga kabisa.
   
 17. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #17
  Oct 7, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  najua kinachowafanya mropoke ni M4C. na bado mtaropoka mengi...

  makamanda 2.jpg
   
 18. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #18
  Oct 7, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Vitu ambavyo hauna uhakika navyo unaleta kwa great thinker ili iweje? Dr slaa? Mafia? Kuhojiwa na watu wa system? Askofu mwanza? Wapi na wapi!
   
 19. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #19
  Oct 7, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  Hebu tuhoji kwa hoja hivi bado tunahitaji snipers na sharpshooters kwenye democracy yetu?

  Ni utunzi gani huu umeshindwa hata kupima mazingira ya sasa?
   
 20. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #20
  Oct 7, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Dah!! mkuu yani muvi ndo linaanza halafu wewe unaleta za kuleta?
  Hili muvi limetulia, hebu acha watu waliangalie ....

  Halafu hapoo kwenye nyekundu, mbona mnapenda sana kuwaamrisha mods mkiona nanihii?
   
Loading...