Kwenye vitabu vyote vitakatifu Mwovu Shetani ametajwa kama adui wa hatari ambaye anapaswa kupigwa vita muda wote na kila mtu mwenye kumheshimu Mungu .
Baada ya kupata Msamaha wa Rais kutoka kwenye kifungo cha milele Ndugu Nguza Vicking akajisahau na kudhani kwamba msamaha ule ulikuwa umeletwa na wanadamu kiasi cha kumsahau Mungu wake na kuanza kuabudu chama cha siasa kiitwacho ccm , akajimilikisha uanachama na kuchukua nafasi ya Marehemu Komba ya kuburudisha wanachama , ( AMELAANIWA MTU YULE AMTEGEMEAYE MWANADAMU )
Uchunguzi nilioufanya ni kwamba Nguza sasa amesahaulika kwenye ulimwengu wa Music hata afanyeje , kitendo cha kujiegemeza ccm iwe kwa kulazimishwa au kwa hiyari yake , chama kinacholaaniwa kwa kila hujuma na dhuluma dhidi ya binadamu ni sawa na kujirudisha jela kimuziki .
Kabla ya uamuzi wake Nguza na wanawe walitakiwa kufikiria na kujiuliza mahali ikopotelea Bendi ya TOT , Kwa msanii yeyote kuiunga mkono ccm ni sawa na kuunga mkono dhuluma na unyama unaotendwa , haina tofauti na kujizika ukiwa hai .