CCM yamponza Babu Seya

CCM yamponza Babu Seya

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
143,344
Reaction score
289,404
Kwenye vitabu vyote vitakatifu Mwovu Shetani ametajwa kama adui wa hatari ambaye anapaswa kupigwa vita muda wote na kila mtu mwenye kumheshimu Mungu .

Baada ya kupata Msamaha wa Rais kutoka kwenye kifungo cha milele Ndugu Nguza Vicking akajisahau na kudhani kwamba msamaha ule ulikuwa umeletwa na wanadamu kiasi cha kumsahau Mungu wake na kuanza kuabudu chama cha siasa kiitwacho ccm , akajimilikisha uanachama na kuchukua nafasi ya Marehemu Komba ya kuburudisha wanachama , ( AMELAANIWA MTU YULE AMTEGEMEAYE MWANADAMU )

Uchunguzi nilioufanya ni kwamba Nguza sasa amesahaulika kwenye ulimwengu wa Music hata afanyeje , kitendo cha kujiegemeza ccm iwe kwa kulazimishwa au kwa hiyari yake , chama kinacholaaniwa kwa kila hujuma na dhuluma dhidi ya binadamu ni sawa na kujirudisha jela kimuziki .

Kabla ya uamuzi wake Nguza na wanawe walitakiwa kufikiria na kujiuliza mahali ilikopotelea Bendi ya TOT , Kwa msanii yeyote kuiunga mkono ccm ni sawa na kuunga mkono dhuluma na unyama unaotendwa , haina tofauti na kujizika ukiwa hai .
 
Kwenye vitabu vyote vitakatifu Mwovu Shetani ametajwa kama adui wa hatari ambaye anapaswa kupigwa vita muda wote na kila mtu mwenye kumheshimu Mungu .

Baada ya kupata Msamaha wa Rais kutoka kwenye kifungo cha milele Ndugu Nguza Vicking akajisahau na kudhani kwamba msamaha ule ulikuwa umeletwa na wanadamu kiasi cha kumsahau Mungu wake na kuanza kuabudu chama cha siasa kiitwacho ccm , akajimilikisha uanachama na kuchukua nafasi ya Marehemu Komba ya kuburudisha wanachama , ( AMELAANIWA MTU YULE AMTEGEMEAYE MWANADAMU )

Uchunguzi nilioufanya ni kwamba Nguza sasa amesahaulika kwenye ulimwengu wa Music hata afanyeje , kitendo cha kujiegemeza ccm iwe kwa kulazimishwa au kwa hiyari yake , chama kinacholaaniwa kwa kila hujuma na dhuluma dhidi ya binadamu ni sawa na kujirudisha jela kimuziki .

Kabla ya uamuzi wake Nguza na wanawe walitakiwa kufikiria na kujiuliza mahali ikopotelea Bendi ya TOT , Kwa msanii yeyote kuiunga mkono ccm ni sawa na kuunga mkono dhuluma na unyama unaotendwa , haina tofauti na kujizika ukiwa hai .
Labda pia si laana, bali umri umemtupa mkono na ushindani mkubwa na kupotea kwa muziki wa dansi nchini akaamua ajiegeme CCM kama mwanamuziki wa chama ili mkono uende kinywani!

Hata ningekuwa mie, kutoka kifungo cha maisha mpaka kuachiwa huru uraiani inadhani sitamtumikia aliyenitoa gerezani kwa moyo wangu wote katika siku chache nilizobakiza duniani?
 
Badala ya kumchunguza mbowe kwa kuwa mwenyekiti wa kwanza kufiwa na chama mkononi unaenda kumchunguza mzee Nguza Vicking??

Ama kweli we ni bavichaaaaa
 
si lazima kutunga hata show ya zile za zamani hawezi kupata watu hata akipiga bure .
Wamerekodi nyimbo mbili chini ya WANENE ENTERTAINMENT na iliyotoka ni moja ikapewa promo na serikari kupitia naibu waziri juliana shonza haikufanya vizuri kabisa
Jamani gemu ya muziki kwa sasa ni ngumu sana ukilinganisha na miaka ile kabla hawajafungwa. Sasa hivi ili watoboe inawabidi wafanye kitu cha ziada vinginevyo watapotea kabisa kwenye tasnia hii ya muziki!
 
Back
Top Bottom