Kuna nini kimejificha nyuma ya Babu Seya na Papii Kocha kutafutiwa studio ya kurekodia muziki !?

justin mwanshinga

Senior Member
May 22, 2014
179
619
Serikali imesema iko kwenye mpango wa kuwatafutia studio wanamuziki Nguza Vicking (Babu Seya) na mwanae Johnson Nguza (Papii Kocha) ili waweze kurekodi na kurudi tena katika tasnia ya muziki. Hayo yameelezwa baada ya Naibu Waziri Shonza kukutana nao jana na kujadiliana nao jinsi serikali inavyoweza kuwasaidia.

Kwa maoni yangu hiki ni kitendo cha HOVYO kabisa kuwahi kufanywa na serikali tangu mwaka huu uanze. Sioni sababu ya serikali kuhangaika na suala hili kwa kiwango hiki unless kuna agenda ya siri nyuma ya pazia.

Babu Seya na mwanae Papii walishitakiwa kwa makosa ya ubakaji na ulawiti. Mahakama ikawakuta na hatia. Hata walipojaribu kukata rufaa mara kadhaa na kuomba judicial review bado walionekana kuwa na hatia. Francis Nguza na Nguza Mbangu waliachiwa kwa kukosekana ushahidi, lakini Babu Seya na Papii waliendelea kuonekana wana hatia.

Rais aliwaachia kwa msamaha alioutoa siku ya uhuru December 09, mwaka 2017, kwa kutumia mamlaka yake kikatiba (ibara ya 45). Well.! Ni jambo jema alilofanya Rais. Binafsi nilimpongeza kwa kuwaachia kina babu Seya na wafungwa wengine zaidi ya 40 waliokuwa wamehukumiwa adhabu ya kifo lakini walizeekea magereza bila adhabu zao kutekelezwa.

So far Rais alifanya jambo jema linalostahili pongezi (kwa maoni yangu). Lakini ikumbukwe Rais hakuwaondolea HATIA akina babu Seya. Aliwaondolea ADHABU. Watu wengi wanaonekana kuchanganya dhana hizi mbili. Wanadhani kitendo cha Rais kuwasamehe basi ina maana hawakubaka. No. Bado ni WABAKAKI lakini WABAKAJI WALIOSAMEHEWA.

Kwahiyo Mheshimiwa Rais aliwaondolea KIFUNGO si HATIA. Bado wataendelea kubaki na hatia ya kile mahakama ilichowahukumu nacho kwa ushahidi usio na shaka.

Kwa hiyo kitendo cha Rais kuwaondolea adhabu was more than enough. Serikali ingeishia hapo, kisha iwaache waendelee na maisha yao wenyewe kama wale wengine waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa wanavyopambana na hali zao huko mtaani.

Lakini kitendo cha serikali kuanza kuhangaika na kina Babu Seya, mara kuwaita Ikulu, mara Waziri Shonza kukutana nao, mara kuwatafutia studio ya kurekodi kwa gharama ya serikali ni mambo yanayoleta ukakasi kwenye suala hili la kuachiwa kwa kina Babu Seya. Ni kama vile waliachiwa ili waje watumike kisiasa.

Kuna watanzania wangapi wanaofanya muziki hawajawahi kukutana hata na wakuu wa wilaya achilia mbali kuitwa Ikulu. Nadhani Waziri Shonza angekutana na wanamuziki wote na kujadili nao namna serikali inavyoweza kusaidia kukuza muziki wao, sio anakaa na kupoteza siku nzima kujadili namna serikali inavyoweza kukuza mziki wa Babu Seya. Serikali yenye vission ingesaidia sekta nzima ya muziki, sio mtu mmoja mmoja.

Pia kuhusu Babu Seya kutafutiwa studio ya kurekodi kwa gharama za serikali hiki ni kituko kingine cha kufungua mwaka. Kazi hii haikupaswa kufanywa na serikali. Wapo wadau wengi sana wa muziki wangeweza kuona fursa hiyo na kuitumia. Mathalani Clouds Media Group wamekuwa nguzo muhimu sana ya kukuza muziki wa Tanzania kwa miaka mingi sasa. Wangeweza kukaa na kina babu Seya na kuona namna ya kuwasaidia kurudi tena kwenye industry ya muziki.

Na ukweli ni kwamba nguvu ya CMG kwenye muziki wa kitanzania ni kubwa mara milioni ya nguvu ya Shonza and Mwakyembe united. Clouds waliomfufua Saida Karoli kutoka kule Mwabuki alikokua akipiga nyimbo kwenye sherehe za kipaimara hadi kumrudisha tena kwenye kilele cha mafanikio, huwezi kuwalinganisha na Shonza ambaye tukio kubwa analokumbukwa nalo kwenye sekta ya habari ni kugombana na Saed Kubenea.

Shonza kama Waziri hakupaswa kabisa kufikiria kumpeleka Babu Seya studio. Hiyo sio kazi ya waziri. Alitakiwa kuwafikiria wanamuziki wa Tanzania kwa ujumla wao. Yeye ni Waziri wa Sanaa sulio waziri wa Babu Seya. Badala ya kutatua matatizo ya mtu mmoja mmoja, angetatua matatizo ya sekta ya sanaa kwa ujumla wake.

Then Babu Seya angetaka support as individual angeweza kuwasiliana na CMG or wadau wengine wakamuandalia tamasha kubwa pale uwanja wa taifa. Kutokana na ushawishi mkubwa walionao CMG nina uhakika ule uwanja ungejaa. Kila mtu angelipa just 10K mara watu 60K ingepatikana pesa taslimu TZS Milioni 600. Wangetoa gharama za uandaaji, akina Babu Seya wasingekosa milioni 200 za kwenda kuanzia maisha.

Lakini hii ya kuitwa Ikulu, mara kuitwa na Waziri Shonza, mara kutafutiwa studio ya kurekodi kwa gharama za serikali ni kupoteza muda tu.

Industry ya sanaa ina matatizo mengi, serikali iache kushughulikia matatizo ya mtu mmoja mmoja ishughulikie matatizo ya tasnia nzima ya sanaa. Leo Babu Seya anarekodi kwa gharama za serikali, hivi kesho Harmorapa akiomba serikali imgharamie kurekodi itakubali? Shonza must think beyond that.!

Malisa GJ
 
tatizo sio serikali! ila baadhi ya watendaji wa serikali! Naibu wazi hakupaswa kuendelea na hili kuna mambo mengi sana ya kufanya! la babu seya ilitakiwa liishe pale pale dodoma! watolewe na waendelee na mambo yao!

kwenda ikulu, as long as hawakualikwa its very okey, hata wengine wanaweza fanya hivyo
 
naona na wewe unapongeza kitendo cha kina babu seya ila ungetaka kitendo hicho kifanye na taasisi nyingine ila sio serikali kwa kifupi sio serikali watanzania wengi uwezo wetu wa kufikiri ni kidogo ndio maana hatuoni athari yoyote kwa kitendo walichofanya wakina babu seya
 
Ulitakiwa uudhibiti mapema mdomo wa lowasa kipindi kule ulipokuwa unakaa nae jukwaa moja..ungeonekana smart sana..leo huna uhalali wa kuzungumzia chochote kuhusu kuachiwa na shughuli zozozte za babu seya kinyume na kukubaliana na kilichotokea..maana ni wazi ulishabariki kabla jpm hajalitazama
 
Serikali imesema iko kwenye mpango wa kuwatafutia studio wanamuziki Nguza Vicking (Babu Seya) na mwanae Johnson Nguza (Papii Kocha) ili waweze kurekodi na kurudi tena katika tasnia ya muziki. Hayo yameelezwa baada ya Naibu Waziri Shonza kukutana nao jana na kujadiliana nao jinsi serikali inavyoweza kuwasaidia.

Kwa maoni yangu hiki ni kitendo cha HOVYO kabisa kuwahi kufanywa na serikali tangu mwaka huu uanze. Sioni sababu ya serikali kuhangaika na suala hili kwa kiwango hiki unless kuna agenda ya siri nyuma ya pazia.

Babu Seya na mwanae Papii walishitakiwa kwa makosa ya ubakaji na ulawiti. Mahakama ikawakuta na hatia. Hata walipojaribu kukata rufaa mara kadhaa na kuomba judicial review bado walionekana kuwa na hatia. Francis Nguza na Nguza Mbangu waliachiwa kwa kukosekana ushahidi, lakini Babu Seya na Papii waliendelea kuonekana wana hatia.

Rais aliwaachia kwa msamaha alioutoa siku ya uhuru December 09, mwaka 2017, kwa kutumia mamlaka yake kikatiba (ibara ya 45). Well.! Ni jambo jema alilofanya Rais. Binafsi nilimpongeza kwa kuwaachia kina babu Seya na wafungwa wengine zaidi ya 40 waliokuwa wamehukumiwa adhabu ya kifo lakini walizeekea magereza bila adhabu zao kutekelezwa.

So far Rais alifanya jambo jema linalostahili pongezi (kwa maoni yangu). Lakini ikumbukwe Rais hakuwaondolea HATIA akina babu Seya. Aliwaondolea ADHABU. Watu wengi wanaonekana kuchanganya dhana hizi mbili. Wanadhani kitendo cha Rais kuwasamehe basi ina maana hawakubaka. No. Bado ni WABAKAKI lakini WABAKAJI WALIOSAMEHEWA.

Kwahiyo Mheshimiwa Rais aliwaondolea KIFUNGO si HATIA. Bado wataendelea kubaki na hatia ya kile mahakama ilichowahukumu nacho kwa ushahidi usio na shaka.

Kwa hiyo kitendo cha Rais kuwaondolea adhabu was more than enough. Serikali ingeishia hapo, kisha iwaache waendelee na maisha yao wenyewe kama wale wengine waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa wanavyopambana na hali zao huko mtaani.

Lakini kitendo cha serikali kuanza kuhangaika na kina Babu Seya, mara kuwaita Ikulu, mara Waziri Shonza kukutana nao, mara kuwatafutia studio ya kurekodi kwa gharama ya serikali ni mambo yanayoleta ukakasi kwenye suala hili la kuachiwa kwa kina Babu Seya. Ni kama vile waliachiwa ili waje watumike kisiasa.

Kama lengo ni kuwastabilize kiuchumi wafungwa waliopewa msamaha wa Rais mbona hakuna jitihada zozote za kuwawezesha kimaisha wale wafungwa wengine waliosamehewa pamoja nao? Na wengine wamekaa gerezani muda mrefu zaidi kuliko kina Babu Seya. Na kama lengo ni kusaidia wanamuziki wetu, je kuna watanzania wangapi wanaofanya muziki lakini hawajawahi kukutana hata na wakuu wa wilaya achilia mbali kuitwa Ikulu.

Nadhani Waziri Shonza angekutana na wanamuziki wote na kujadili nao namna serikali inavyoweza kusaidia kukuza muziki wao, sio anakaa na kupoteza siku nzima kujadili namna serikali inavyoweza kukuza mziki wa Babu Seya. Serikali yenye vission ingesaidia sekta nzima ya muziki, sio mtu mmoja mmoja.

Pia kuhusu Babu Seya kutafutiwa studio ya kurekodi kwa gharama za serikali hiki ni kituko kingine cha kufungua mwaka. Kazi hii haikupaswa kufanywa na serikali. Wapo wadau wengi sana wa muziki wangeweza kuona fursa hiyo na kuitumia. Mathalani Clouds Media Group wamekuwa nguzo muhimu sana ya kukuza muziki wa Tanzania kwa miaka mingi sasa. Wangeweza kukaa na kina babu Seya na kuona namna ya kuwasaidia kurudi tena kwenye industry ya muziki.

Na ukweli ni kwamba nguvu ya CMG kwenye muziki wa kitanzania ni kubwa mara milioni ya nguvu ya Shonza and Mwakyembe united. Clouds waliomfufua Saida Karoli kutoka kule Mwabuki alikokua akipiga nyimbo kwenye sherehe za kipaimara hadi kumrudisha tena kwenye kilele cha mafanikio, huwezi kuwalinganisha na Shonza ambaye tukio kubwa analokumbukwa nalo kwenye sekta ya habari ni kugombana na Saed Kubenea.

Shonza kama Waziri hakupaswa kabisa kufikiria kumpeleka Babu Seya studio. Hiyo sio kazi ya waziri. Alitakiwa kuwafikiria wanamuziki wa Tanzania kwa ujumla wao. Yeye ni Waziri wa Sanaa sio waziri wa Babu Seya. Badala ya kutatua matatizo ya mtu mmoja mmoja, angetatua matatizo ya sekta ya sanaa kwa ujumla wake.

Then Babu Seya angetaka support as individual angeweza kuwasiliana na CMG or wadau wengine wakamuandalia tamasha kubwa pale uwanja wa taifa. Kutokana na ushawishi mkubwa walionao CMG nina uhakika ule uwanja ungejaa. Kila mtu angelipa just 10K mara watu 60K ingepatikana pesa taslimu TZS Milioni 600. Wangetoa gharama za uandaaji, akina Babu Seya wasingekosa milioni 200 za kwenda kuanzia maisha.

Lakini hii ya kuitwa Ikulu, mara kuitwa na Waziri Shonza, mara kutafutiwa studio ya kurekodi kwa gharama za serikali ni kupoteza muda tu.

Industry ya sanaa ina matatizo mengi, serikali iache kushughulikia matatizo ya mtu mmoja mmoja ishughulikie matatizo ya tasnia nzima ya sanaa. Leo Babu Seya anarekodi kwa gharama za serikali, hivi kesho Harmorapa akiomba serikali imgharamie kurekodi itakubali? Shonza must think beyond that.!
 
Kwa maoni yangu hiki ni kitendo cha HOVYO kabisa kuwahi kufanywa na serikali tangu mwaka huu uanze. Sioni sababu ya serikali kuhangaika na suala hili kwa kiwango hiki unless kuna agenda ya siri nyuma ya pazia.
 
Kwanza hawa nao bado wanasubiri nini TZ wasirudi makwao huko!
 
Watatoka na nyimbo za kuabudu, kumpamba na kumsifu tu, na labda pia hiyo studio ni maandalizi ya 2020.
 
Itabidi namimi nimbake jesca yohana makomeo bila shaka ntapewa uwaziri kabisa
 
"Magu wa Mivaloooo"

Kumbuka Kapteni Komba hatupo naye tena kwahiyo hawakua Na mtu wa kutengeza "wacha waisome namba" party 2.
 
Back
Top Bottom