Katika hali ya kushangaza chama cha CCM kimeshindwa kuzindua kampeni zake katika jimbo la Kalenga leo kama walivyotangaza awali.
Badala yake wamesema uzinduzi utafanyika siku nyingine itakayotangazwa.
Inadaiwa mbali na sababu nyingine mojawapo ni kutokana na mgombea wake kutokukubalika jimboni humo.Mgombea huyo wa CCM Godfrey Mgimwa alikuwa akiishi Uingereza na ameoa mke wake Mzungu raia wa huko huko.Pia wananchi wa Kalenga wanadai walimfahamu siku ya mazishi ya baba yake.
Inawezekana pia Ahirisho hilo linatokana na Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa kuzindua kwa kishindo kikubwa kampeni za chama chake hapo jana Jumamosi huku akisindikizwa na Chief wa Kabila la Wahehe Abdu Sapi Mkwawa.